Wananchi wa Magadu wapelekewa huduma ya maji

Oct 8, 2023
37
17
NEEMA YA MAJI KATA YA MAGADU

Wananchi wa mitaa ya Kidondolo, Forkolend na Kididimo Kata ya Magadu kwa nyakati tofauti tofauti wameongea na kuishukuru Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais. Samia S. Hassan kwa namna ambavyo imesikia kilio chao cha muda mrefu kuhusu maji. Akionge Ndg Paulo Joseph mkazi wa mtaa wa Kidondolo amesema kuwa "Anamshukuru sana Mhe Rais kwa kuwaletea maendeleo mengi na makubwa Katani mwao yakiwemo maji, aidha ndugu Paulo Joseph ameongeza kuwa atakuw
20240114_172203.jpg
a mnafiki kama akiacha kumshukuru pia Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe Abood amekuwa akiwakimbilia usiku na mchana pamoja na kuwasemea wananchi wake ili waletewe maendeleo.

MWENYEKITI WA CCM KATA
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Kata ya Magadu NDG JUMANNE HABIBU MKALI kwa upande wake amesema kuwa anampongeza Mhe. Rais. Samia Suluhu Hassan kazi kubwa za maendeleo zinaonekana, na wananchi wanaziona kwa macho yao hii ni heshima kubwa kwetu sisi wananchi wa Magadu. Sanjari na hayo Mwenyekiti wa Ccm Kata ameongeza kuwa anamshukuru sana MHE ABOOD hakika amekuwa mbunge wa vitendo na kimbilio la wananchi wa Morogoro mjini. Vilevile mwenyekiti ameongeza kuwa Morogoro imepata kiongozi mzuri na sahihi kwa upande wa maji, mamlaka ya maji safi na maji taka Morogoro (MORUWASSA) kumepita wakurugenzi wengi ila huyu wa sasa Eng Tamim Katakweba ni mtu na nusu amekuwa kiongozi wa mfano wa kuigwa na wengi hakika Morogoro tunajivunia Mkurugenzi huyu maana hapo zamani changamoto na malalamiko ya maji yalikuwa ni mengi kila sehemu ila sasa kukoswali.

ENG. TAMIM KATAKWEBA ATAO SHUKURANI KWA RAIS. MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAH, PAMOJA NA MHE. ABDULAZIZ M. ABOOD MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI

Akiongea na wanachi wa Kata ya Magadu, Mkurugenzi wa Moruwassa Eng Katakweba amesema kuwa maji haya yataongeza upatikanaji wa maji ya uhakika mitaa yote sita ya Kata ya Magadu pamoja na baadhi ya mitaa ya Kata ya Mafiga kama vile KIDONDOLO (A) na KIDONDOLO (B) takiribani wananchi elfu kumi na tatu watanufaika na maji haya. Maendeleo yote ya maji mnayoyaona pongezi kubwa na shukurani zimwendee Mhe. Rais. Samia S. Hassan kwa kuwaletea wananchi wa Morogoro maji, Eng Katakweba ameeleza kuwa nia ya Mhe Rais Samia S. Hassan ni kuhakikisha kila mwananchi mwenye uwezo wa kuvuta maji achote maji nyumbani kwake. Na kwa ambao hawana uwezo wa kuvuta maji wawekewe VIOSKI vya kuuza maji karibu na wananchi hao lakini pia maji yauzwe kwa bei ndogo na nafuu sana kwa wananchi hao. Vilevile Eng Katakweba ameongeza kuwa, anamshukuru sana MHE ABOOD Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini kwa namna ya kipekee amekuwa akimpa ushirikiano wa kutosha usiku na mchana.
20240114_172145.jpg
 
Back
Top Bottom