Mbunge CHADEMA atetea posho mpya

Mlikuwa mnafanya kazi gani kabla ya ubunge? Kama ilikuwa inalipa unafanya nini kwenye ubunge? temana nayo fasta mwingine ajaribu acheni kelele za kijinga nyie wabunge.. ninachojua ni kazi inayolipa kuliko yoyote kwa sasa Tanzania
 
Naona leo makamanda mmeloa kama mmemwagiwa cold water!

Mnyisanzu,

Mbona hakunaga shida mazee kuhusu habari kama hizi. Huyu Malack si wa kwanza kubwabwaja kuhusu posho za Wabunge. Tumeshamsikia John Shibuda Madale wa CDM na tamaa yake ya kuongezewa posho kutoka 70,000/= mpaka 500,000/= kwa siku! Sasa washangaa nini kuhusiana na huyu Malack?

Mimi nasema hawa Wabunge wa Tumbo ni bora wakahamia CCM kwenye chama cha Mafisadi na Majambazi wa Uchumi wa Nchi yetu. Watu wanaoji thamini wao badala ya kuwathamini watu waliowapa hiyo kazi ya Ubunge. Tunajua tayari Supuka wao Kigala Anne Makinda tayari alishawasilisha maombi kwa mkuu wa kaya kuomba ongezeko la kutoka 70,000/= mpaka 200,000/= kwa siku kama posho ya kikao mbali na 80,000/= ya perdiem na 50,000/= ya wese wanapokuwa mjengoni yote hii ikiwapa ulaji wa Tshs.330,000/= kwa siku moja!

Sasa hapa ndipo unaweza kugundua kuwa hatuna BUNGE MAKINI lenye kujali maslahi ya Watanzania na mstakabali wa Taifa letu. Kila Mtz kwa sasa anajua SERIKALI IKO HOI BIN TAABANI KIUCHUMI. The government coffers are empty, tunasikia Mkullo kwa sasa nahangaika kwenye Mabenki kutafuita mikopo ya Dharura angalao kuifanya SERIKALI YA KIWETE IWEZE KUMUDU KULIPA MISHAHARA YA WATUMISHI WA SERIKALI MAANA ILE BAJETI YA MWAKA 2011/12 WAMESHAIKOMBA YOTE WITHIN ONLY 4 MONTHS! maaana kama Bajeti ilisomwa June/July,2011 na tayari by Novemba,2011 SAERIKALI ILIKUWA TAYARI IMESHAMALIZA BAJETI YA MWAKA MZIMA!

Habari za kuaminika ni kuwa Uchaguzi wa Igunga,Sherehe za Miaka 50 ya UHURU na Kuporomoka kwa Thamani ya Fedha yetu ya madafu ndo zimevuruga Bajeti ya 2011/12.
 
PAMOJA na kusudio la kuongeza posho za wabunge kupingwa na vyama vya siasa, viongozi
wa dini na jamii, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) mkoani Rukwa, Anna Malack ameamua
kutetea kusudio hilo.

Mbunge huyo amesema kuwa wabunge walio wengi wanaishi maisha magumu kupindukia wanapohudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma kutokana na alichoita ukata mkali unaosababishwa na malipo duni wanayolipwa bungeni.


Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya
Mji wa Mpanda baada ya madiwani hao kutoa ombi kwa Serikali ifute kabisa posho mpya za vikao vya wabunge.

Madiwani hao katika ombi lao waliitaka Serikali, badala ya kuongeza posho za wabunge,
iboreshe posho za madiwani ambazo walidai ni duni na zimepitwa na wakati.

Wakati wa kujadili suala hilo, baadhi ya madiwani walilaani uamuzi wa wabunge kutaka kujiongezea posho ya vikao wawapo bungeni kutoka Sh 70,000 hadi Sh 200,000 wakidai kuwa ni uamuzi wa kilafi, tamaa na ubinafsi unaowasukuma wabunge hao.

Hata hivyo, baada ya madiwani hao kutoa ombi hilo na maneno ya kulaani kusudio hilo, Mbunge huyo aliamua kueleza alichoona kuwa ndiyo hali halisi.

“Kama si kulima vitunguu mie na mume wangu, ningetegemea mshahara wa bungeni, ningekuwa nimeadhirika ile mbaya… baadae mtu unajuta kwanini umeingia kwenye siasa.

“Mfano unaamka asubuhi unafungua mlango na kukuta watu zaidi ya hamsini wanakusubiri wakiomba uwasaidie… baadae unalazimika kuuza vitu vya ndani ili uwasaidie.

“Ukifika nyumbani kwangu sina lolote zaidi ya kukutana na harufu kali ya vitunguu, huwezi
kuamini kama ni nyumba ya mbunge wenu.

“Wabunge kwa hali hiyo tunaadhirika, kama huna miradi ya kujiongezea kipato ndio umekwisha,” alisema.

Alisema kutokana na ukata baadhi ya wabunge wamekuwa wakikacha kurejea kwenye majimbo
yao ya uchaguzi na badala yake wanaamua kukaa Dar es Salaam.

*Hajapokea lakini anazitamani
Mbunge huyo alisema kuwa yeye binafsi hajawahi kulipwa posho mpya ya vikao vya Bunge na
kuongeza kwamba ofisi ya Bunge imekuwa ikiwazungusha kuwalipa na kusababisha afulie ile mbaya.

“Nadhani watu hawaelezi ukweli, malipo ya posho hizo mpya ni blaa blaa tu kwani mie binafsi sijawahi kulipwa hata siku moja isitoshe nimekuwa nikisoma kwenye magazeti na kusikia kwenye vyombo vingine vya habari.

“Labda kama ofisi ya Bunge imebagua na kuwalipa wabunge wengine watueleze tujue,” alisema.

Alidai kutokana na kutolipwa hiyo posho mpya wamepigiana simu na wabunge wengine na wamekubaliana kufanya mgomo wa kutoingia bungeni katika mkutano ujao wa Bunge hadi wafahamu hatima ya malipo yao.

“Bila kuwataja kwa majina wapo baadhi ya wabunge kutokana na ukata wanashindwa
kulipia nyumba za kulala wageni, wanalazimika kulala kwenye magari yao huku suti zao zikiwa zimetundikwa kwenye kiti cha nyuma, amini usiamini wanalia kama watoto wadogo,” alisema.

Akiunyambulisho mshahara wake alisema kama Mbunge analipwa Sh 70,000 za posho na
mshahara wake ni Sh 2,500,000 lakini baada ya makato anasalia na Sh 800,000 tu.

“Makato hayo ni ya gari nililokopa na makato mengineyo hivyo nimefulia ile mbaya…nikisafiri na gari langu kutoka Mpanda hadi Dodoma natumia Sh 700,000 kwa mafuta tu,” alisema.

Madiwani wakaza uzi Hata hivyo madiwani hao bila kuuma uma maneno, walimtaka mbunge huyo akienda bungeni atoe shilingi kwenye mshahara wa waziri husika akishinikiza posho za madiwani ziboreshwe.
source : Habarileo.
my take SIJAMUELEWA MWANDISHI WA HABARI HII


Mchango wa wangu utazingia hizo red hapo juu kama ifuatavyo:

siyo sahihi kwamba maisha ni magumu Dodoma pekee. Kutokana na mfumuko wa bei kupanda kwa kasi zaidi, hali ya maisha imekuwa ngumu katika maeneo yote ya nchi yetu. Wabunge wanalipwa posho ya kujikimu sh. 80,000; fedha hizo zinatosha kujikimu wawapo Dodoma. Hakuna uhalali wa kulipwa sitting allowance wakati mbunge anakuwa ameshalipwa fedha za kujikimu. Ni jukumu(kazi) la mbunge kuhudhuria vikao vya bunge kwa mujibu wa Katiba ya JMT; na mbunge hulipwa mshahara kila mwisho wa mwezi kwa kazi hiyo.

Inaonekana wabunge wanafanya kazi isiyowahusu ya kugawa fedha kwa wapiga kura. Kwa mfano mbunge anasema "unaamka asubuhi unafungua mlango na kukuta watu zaidi ya hamsini wanakusubiri wakiomba uwasaidie" Kwa hiyo wabunge wanadai posho kubwa si kwa sababu posho wanayopewa haikidhi haja, bali wanataka fedha za kwenda kuwapa wapiga kura wenye shida. Hii ina maana kwamba wananchi wengi ni masikini kwa sababu serikali yao imeshindwa kuwawezesha kuondokana na umasikini; serikali imeshindwa kuweka mazingira mazuri ya kiuchumi, kijamii nk.
 
Mchango wa wangu utazingia hizo red hapo juu kama ifuatavyo:

siyo sahihi kwamba maisha ni magumu Dodoma pekee. Kutokana na mfumuko wa bei kupanda kwa kasi zaidi, hali ya maisha imekuwa ngumu katika maeneo yote ya nchi yetu. Wabunge wanalipwa posho ya kujikimu sh. 80,000; fedha hizo zinatosha kujikimu wawapo Dodoma. Hakuna uhalali wa kulipwa sitting allowance wakati mbunge anakuwa ameshalipwa fedha za kujikimu. Ni jukumu(kazi) la mbunge kuhudhuria vikao vya bunge kwa mujibu wa Katiba ya JMT; na mbunge hulipwa mshahara kila mwisho wa mwezi kwa kazi hiyo.

Inaonekana wabunge wanafanya kazi isiyowahusu ya kugawa fedha kwa wapiga kura. Kwa mfano mbunge anasema "unaamka asubuhi unafungua mlango na kukuta watu zaidi ya hamsini wanakusubiri wakiomba uwasaidie" Kwa hiyo wabunge wanadai posho kubwa si kwa sababu posho wanayopewa haikidhi haja, bali wanataka fedha za kwenda kuwapa wapiga kura wenye shida. Hii ina maana kwamba wananchi wengi ni masikini kwa sababu serikali yao imeshindwa kuwawezesha kuondokana na umasikini; serikali imeshindwa kuweka mazingira mazuri ya kiuchumi, kijamii nk.

Kwa akili zao wanadhani hao wanaokwenda kuwaomba msaada ndio watu pekee wenye shida katika majimbo yao! Hivi kila mwenye shida ya kifedha angeamka na kwenda kuomba msaada kwa mbunge wake hizo posho zao hata zingeongezwa kwa asilimia 300% zingetosha kweli! Mbunge wa CHADEMA akiongea upupu kama huo ananisikitisha sana! Hawakuchanguliwa ili wawe wanawasaidia wananchi pesa zao za posho!
 
Jibu hoja! Masaburi ndiyo nini.... Magwanda bwana... mkishikwa pabaya mnaleta matusi... mibunge yenu haitosheki?
Endeleeni kushikia hapo hapo maana mnafikiri hao wanaodai nyongeza ya posho ni saratani kama ya magamba, ukweli ni kwamba kutofautiana kimtazamo ni hulka ya mwanadamu na hata ndani ya cdm hilo lipo, ila saratani ya magamba ni ya kufisha ndugu yangu..! haina cha "mmeshikwa pabaya au mmeshika pabaya" hiyo mliyonayo nyie ninomaaa, inaua na imeanza kuwamaliza

Wenye mapenzi mema na nchi hii hawajali kama huyo mbunge ni wa cdm ila wanachofanya ni kusema ukweli daima mpaka watanzania wote waelewe mbivu na mbichi..
 
Mkuu, hata uandike maneno gani ukweli utabaki kuwa ukweli tu..

Mbunge wa Chadema posho mpya!
Unajua wewe Ritz unaushabiki fulani ambao sio mzuri,Hoja hapa ni Mbunge kukanusha au kukubali ,kam CDM wao walishasema hiyo ni sela ya chama ,kukataa posho na marupurupu mengine yasio na Tija hiyo ilikuwa manafesto yao. Kama ni manefesto yao usikatae kwa ushabiki wewe njega hoja then subiri watu nao watoe mawazo yaho.Unajua sasa hivi magazeti nayo yalishabebwa na wanasiasa kwahiyo ,tukikubali kwenda hivi tutafika pabaya sana ,maana hii ni nchi yetu tuijenge swala la posho ni kitu ambacho kinaitaji mjadala wa kitaifa kama hivi watu tutoe msimamo wala sio chama furani eti wao wakioneka wanatoa mawazo yao basi ndo samaki ameoza ,hili atutafika mbali.Natoa ushauri tu
 
Kama ubunge ni hali ngumu si ajiuzulu kwani ni lazima yeye tu? Halafu kila mtu anapaswa atafute vyanzo vya ziada vya mapato anataka matatizo yake yote yaishie kwa kuwa mbunge? Watu wanamuomba hela kwa vile aliwaahidi hela akipata ubunge analalamika nini?
 
Kumbe ni wa Viti Maalumu.. Basi haina haja ya kumdiscuss..siyo kosa lake.

malizia tu kuwa ni kosa la MBowe na huyo Padre mustaafu .

Na hao ni viti maalumu tu, atakapokalia kiti na kulazimika kuteua teuzi zote kwa mujibu wa nafasi yake , ataweka hadi ma beki tatu wa mizigo yake na jamaa zake.
 
Shibuda kazini siyo issue, kuta ni kitu yake shibuda bungeni. Ok yupo cdm kweli lakini jina lenyewe ndio leo nalisikia. Hivi huyu alishawahi hata kuuliza swali kweli? Mwenye picha yake aiweke tafadhali. Tuwajue hawa walafi.
Am with you mkuu wacha nione majibu yatakuwaje
 
Hatuna cha kushangilia hapo kwa maneno ya huyu kiruka njia. Hawa watu wanafiki sana. Wakikaa kwenye ule mjumba wanaongea pumba kwenda mbele wakisisitiza uzalendo kwa wataalam. Kila siku ni wataalam wanakimbilia nje kwa kukosa uzalendo, sasa wao nini wanadai? Kwanza ingekuwa vyema kupunguza wakinamama bungeni. Hata huyu she-budha ni type ya kutupa jalala la mbali.
 
Back
Top Bottom