Mbunge CHADEMA atetea posho mpya

Kwa akili zao wanadhani hao wanaokwenda kuwaomba msaada ndio watu pekee wenye shida katika majimbo yao! Hivi kila mwenye shida ya kifedha angeamka na kwenda kuomba msaada kwa mbunge wake hizo posho zao hata zingeongezwa kwa asilimia 300% zingetosha kweli! Mbunge wa CHADEMA akiongea upupu kama huo ananisikitisha sana! Hawakuchanguliwa ili wawe wanawasaidia wananchi pesa zao za posho!

Hawa wabunge wooote wenye ubunge wa kupewa akili zao zipo zaidi kwenye kuombaombana. Akili ya kusaidia mbegu hanayo, anayo ya kula mbegu
 
Kwani hawa wabunge wanalazimishwa kugombea kuchaguliwa au kuteuliwa? Wakiona hali ngumu si waache tu!!!
 
Hela yenyewe ya ubunge mbona sio ndefu kiivyo,labda kama una ishu zako zingine,...mshahara take home kilo 8!?
 
source: Habari leo.

Ukiisoma hiyo habari jinsi ilivyoandikwa na habari leo unaona kabisa kwamba imetiwa chumvi kwa malengo maalum.

Nilichokiona hapo ni kwamba mbunge alikuwa anajaribu kuwapooza madiwani ili wasione kama posho wanazolipwa ni kubwa sana ndipo akafikia hata kuelezea anavyoendesha maisha kwa kutegemea kilimo cha vitunguu badala ya malipo ya ubunge.

Lakini kwakuwa gazeti la serikali linapenda kuchonganisha wabunge wa chadema, basi wakaamua kutia chumvi.

Ninaweza kuiamini habari kama hii kama itakuwa imeripotiwa na gazeti jingine kabisa kama mwananchi ama kukiwepo na picha ya video. Kwakuwa hii habari bado ni tetesi basi kunahitajika ushahidi ili ithibitike na tuweze kumhukumu kwa haki mbunge!
 
Hela yenyewe ya ubunge mbona sio ndefu kiivyo,labda kama una ishu zako zingine,...mshahara take home kilo 8!?

Kuweni na huruma na waTz wenzenu,hyo unayoiona kidogo wengine hawapati kabisa kadhalika bado mna marupurupu ambayo wengine hawapati kwa hyo hyo ni kidogo? Kuweni na ubinadamu kwa kweli.
 
Ukiisoma hiyo habari jinsi ilivyoandikwa na habari leo unaona kabisa kwamba imetiwa chumvi kwa malengo maalum.

Nilichokiona hapo ni kwamba mbunge alikuwa anajaribu kuwapooza madiwani ili wasione kama posho wanazolipwa ni kubwa sana ndipo akafikia hata kuelezea anavyoendesha maisha kwa kutegemea kilimo cha vitunguu badala ya malipo ya ubunge.

Lakini kwakuwa gazeti la serikali linapenda kuchonganisha wabunge wa chadema, basi wakaamua kutia chumvi.

Ninaweza kuiamini habari kama hii kama itakuwa imeripotiwa na gazeti jingine kabisa kama mwananchi ama kukiwepo na picha ya video. Kwakuwa hii habari bado ni tetesi basi kunahitajika ushahidi ili ithibitike na tuweze kumhukumu kwa haki mbunge!

Nakubaliana nawe Mwita, nadhani kuna mahali ametwist hii habari kwa faida anazozijua yeye. Mwita uko rational sana, nasema hivi sababu ya post hii, na ile yangu kule kwingine. Unaangalia pande mbili za stori ndipo unapotoa conclusion
 
Hivi viti maalum si navyo hugombewa? Anaweza akajiuzuru tu na kurudia kazi yake itakayomfanya aishi maisha mepesi kuliko ya ubunge.
 
"Ukifika nyumbani kwangu sina lolote zaidi ya kukutana na harufu kali ya vitunguu, huwezi
kuamini kama ni nyumba ya mbunge wenu.

Kama aligombea ubunge kwasababu ya mshahara, then tatizo ni lake, maybe angeacha unbunge alime na nyanya kabisa.

Uongozi wa umma siyo pahala pa kwenda kujinufaisha, tena mbunge wa viti maalum ndo utajua wengine hawana clalibers za uongozi.

Inaonyesha aliutaka ubunge ili achume na kuachana na bisashara ya vitunguu!lol
 
Madiwani wakaza uzi Hata hivyo madiwani hao bila kuuma uma maneno, walimtaka mbunge huyo akienda bungeni atoe shilingi kwenye mshahara wa waziri husika akishinikiza posho za madiwani ziboreshwe
Kazi kweli kweli, siku hizi uongozi is all about posho tu, and not about what you do for the people who elected you to the office!
 
kwa siku kama posho ya kikao mbali na 80,000/= ya perdiem na 50,000/= ya wese wanapokuwa mjengoni yote hii ikiwapa ulaji wa Tshs.330,000/= kwa siku moja!

Watu wanalipwa $3000 kwa siku bado wanalalamika, only in TZ mambo kama haya ni ya kawaida!

Kama wabunge wangekuwa wanaombea kwa ajili ya kuwatumikia wananchi, the hili tatizo lisingekuwepo!

Na huu ubunge kapewa kwenye kisahani huyu...
 
Tsh 2,500,000 ni ndogo?? na Kuna aliyemlazimisha kukopa gari!!!
Mbona watumishi wengine wa serikali(tena wasomi kuliko yeye) wanatembea kwa mguu ktk kutekeleza majukumu yao ya kazi. Naona huyu Mbunge anaelekea kushindwa kazi bora aendelee kulima vitunguu..
 
Hee huyu nae mbunge wa wapi vile,au Shibuda kazini?lakini hofu yangu ni source ya habari,maana hilo gazeti wengine huwa hatulisomi hata kama ni bure,ila haka kabunge kapo kweli CDM? mbona hata sijakasikia?eeh basi kama huwa anapita humu atuweke vizuri alikuwa anamaanisha kama alivyonukuliwa au alikuwa anamaanisha kitu gani,maana hiyo hoja ya kusema eti ukiamka asubuhi unakuta kuna watu wanakusubiri uwasaidie,hili SIKUBALIANO NALO HATA KIDOGO.tena akome kuwapotosha wananchi wake kwa kuendekeza tabia ya kuwafanya tegemezi,hao si watoto,hilo ni jambo la kufanya ndio lakini sio frequently anachotakiwa kufanya kuwajengea uwezo ili wajitegemee,asiwafundishe kula samaki awafundishe kuvua samaki,huyu vipi kweli yuko CDM?
hebu mwenye picha atuwekee hapa nimufahamu.au ndo sampuli ya Shibuda tena?eeh hapa kuna kazi ya kuwachuja watu kama hawa.
 
Huu msimamo wa cdm kuhusu posho, unaonyesha c wabunge wa cdm wamekubalian nao! Utakuwa ni msimamo wa baadhi wa viongozi wa juu wa cdm. Wapo wengi wabunge ndan ya cdm wanapenda posho iongezwe, ila wanaogopa kuongea! Siasa bwama mhhh
 
Kama Source ni kutoka katika gazeti la Habari Leo, hapo kutakuwa na mashaka kidogo. Kinacho hitajika ni kusubiri
kauli ya Mh. Mbunge muhusika. Kwa sababu hii ni tetesi tu, na halafu gazeti la Habari Leo linajikita zaidi na habari za
uchonganishi na kujaribu kikibomoa chama Kikuu cha upinzani CDM. Bali ikiwa ni kweli kauli ya Mh. Mbunge ni ya kutetea
posho hapo tutaipinga, kwa sababu hatukubaliani na mawazo yanayokwenda kinyume na maslahi ya Wananchi
pamoja na chama chako CDM. Mh. Mbunge tunaomba ufafanuzi wako.
 
Huu msimamo wa cdm kuhusu posho, unaonyesha c wabunge wa cdm wamekubalian nao! Utakuwa ni msimamo wa baadhi wa viongozi wa juu wa cdm. Wapo wengi wabunge ndan ya cdm wanapenda posho iongezwe, ila wanaogopa kuongea! Siasa bwama mhhh

we ndio umenena,sidhani kama kweli kutoka moyoni kuna mbunge,au mtanzania mwingine yoyote angekuwa mbunge azitaki posho..sema ndio ivo politiki.
 
Back
Top Bottom