Mbunge Benaya Kapinga asisitiza Dawa na Vifaa Tiba vipelekwe kwa wakati sehemu za kutolea huduma za afya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
MBUNGE BENAYA KAPINGA ASISITIZA DAWA NA VIFAA TIBA VIPELEKWE KWA WAKATI SEHEMU ZA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA

Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini Mkoa wa Ruvuma Benaya Liuka Kapinga akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya Bungeni jijini Dodoma tarehe 12 Mei, 2023.

"Serikali katika Jimbo la Mbinga Vijijini imetoa Shilingi Milioni 400 za ukarabati wa kituo cha Afya cha Mapera na Shilingi Milioni 350 kwa ajili ya vifaa tiba. Pia, kupitia mradi wa Global Fund imetolewa ahadi ya kupewa Ambulance 🚑 na itakuwa na Ambulance 🚑 2 kutoka kwenye mradi wa UVIKO-19" - Benaya Kapinga

"Tumejenga na kukamilisha vituo vya afya Muungano, Matiri, Mkumbi na Magagula (Peramiho) kwa Mhe. Jenister Mhagama. Maeneo haya tupeleke vifaa tiba na madaktari wakafanye upasuaji" - Benaya Liuka Kapinga

"Nchi yetu kila mahali tuna majengo mazuri ya kutolea huduma za afya. Tuna Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, Hospitali za Rufaa (Mikoa) na Hospitali za Kanda. Niwapongeze madaktari, wanafanya kazi nzuri katika mazingira tuliyonayo. Waziri muwafanye wananchi waviamini vituo vya afya" - Mhe. Benaya Liuka Kapinga

"Uko ucheleweshaji sana wa fedha za dawa hasa pale kituo kinaposajiliwa. Inachukua muda mrefu sana kituo kikisajiliwa kuingia kwenye mfumo. Halmashauri/Mbinga imechukua miezi mitano mpaka sita kuingia kwenye mfumo. Tubadirishe huu utaratibu" - Benaya Liuka Kapinga

"Fedha za Basket Fund, Nadhani zinatoka Wizara ya Afya zinaenda TAMISEMI halafu ndiyo zinaenda eneo la kutolea huduma, lakini zinachukua muda mrefu sana. Fedha za mwezi wa saba zimekuja kutoka mwezi disemba mwishoni. Tuzitoe kwa wakati" - Benaya Liuka Kapinga

"Tumejenga vituo vya afya vingi sana. Eneo limejenga zahanati tano mpaka kumi lakini bajeti unakuta ni ya miaka 5 iliyopita. Hii hupelekea watu kupata mgao mdogo tofauti na uhalisia uliopo. Tupeleke dawa na Fedha kutokana na uhalisia uliopo" Benaya Liuka Kapinga.

WhatsApp Image 2023-05-15 at 14.40.30.jpeg
WhatsApp Image 2023-05-15 at 14.40.31(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-05-15 at 14.39.22.jpeg
 
Back
Top Bottom