Kisiwa cha Rukuba chafurahia kuanza kupokea vifaa tiba vya Kituo cha Afya Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
946
Kisiwa cha Rukuba kimekamilisha ujenzi wa Kituo chake cha Afya na tayari kimeanza kupokea vifaa tiba vya Kituo hicho.

Utoaji wa Huduma za Afya ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini unaendelea kuboreshwa na kuimarika. Kwa sasa tuna:

(i) Hospitali ya Halmashauri
Hii ina hadhi ya Hospitali ya Wilaya

(ii) Vituo vya Afya sita (6)
Murangi, Mugango, Bugwema, Makojo, Kiriba na Kisiwa cha Rukuba

(iii) Zahanati 42
*24 za Serikali
*4 za Binafsi
*14 zinajengwa

Maombi yaliyopelekwa Serikalini
*Wafanyakazi wa kutoa Huduma mbalimbali za Afya wapo wachache sana. Idadi iongezeke sana.

Tunaomba idadi iongezeke hasa kwenye Hospitali yetu mpya na kwenye Vituo vyote vya Afya.

*Vifaa tiba vinahitajika, ni pungufu sana.

*Wingi wa dawa za aina mbalimbali uongezeke sana.

Furaha & Shukrani
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO ya kutoka Kisiwani Rukuba iliyoambatanishwa hapa

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 28.9.2023

 
Back
Top Bottom