Mbunge aweka kando ubunge, afanya kazi ya kutoa `uchawi`

Ushirikina umekatazwa na dini zote kubwa (Christianity and Islam). Bila aibu watanzania tunauhalalisha kwa kuwatunuku wahusika ubunge. Halafu tunafungua bunge eti kwa sala inayomtaja MUNGU (Ile naona ni dhihaka).
Msiwalaumu waliomchagua, wamemchagua kwa ajili ya shida zao. Jamaa alianza kuwasaidia mambo mbalimbali kabla hajagombea ubunge. Mambo yenyewe ni mahitaji ya msingi ambayo kama kusingekuwa na ufisadi nadhani kila mtu angepata hayo mahitaji ya msingi.
JAMANI HII SYSTEM INAYOENDESHA NCHI YETU WAKATI WAKE WA KUITOA IMEFIKA.
Imezalisha maskini na wajinga wengi na wanatumia huo huo umaskini na ujinga katika kuzidi kujinufaisha.
 
kazi imeanza hata kule mjengoni asaidie inawezekana kuna wengine wana ntunguli viunoni nazo atoe.
 
sphen ngonyani ni kiboko alitaka kumzima zitto kabwe na hoja yake ya mikonge ikashindikana si unajua tena Zitto chuma cha reli kutoka kigoma kwa kumuonyesha jeuri bunge lilipoisha Zitto akaenda kufanya mikutani tanga bila kudhuriwa na kitu chochote kama asingekua mzitto zitto angebaki tanga kama msukule.na CCM watamtumia uyu jamaa kuwadhoofisha wapinzani wasiokua na kinga madhubuti.nina wasiwasi na Halima mdee maana huyu dada ndiye anayeonekana kuwadharau wazee wa CCM na kuwasemea mbovu kama anaongea na vijana wenzake na mwingine atakayewekwa sawa ni Tindu lissu nae anaongoza kwa dharau na kuwaona wenzake hawajui sheria.ata mimi ningependa hii mission ikamilike maana na mimi sipendi waha watu wanavyo endesha siasa zao bungeni
 
Majimarefu.jpg
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu, juzi aliweka ubunge wake kando na kurejea kazi yake ya uganga kwa kutoa ‘wachawi’ katika kijiji cha Kwemazandu.

Mbunge huyo alifanya kazi hiyo baada ya kuhudhuria mkutano wa kijiji uliopitisha maamuzi ya kumtimua mmoja wa wanakijiji wao kwa tuhuma za kishirikina.

Akizungumza na NIPASHE kwa simu kutoka Korogwe, alisema alilazimika kufanya kazi hiyo wakati wa mkutano wa halmashauri ya kijiji ambao pamoja na mambo mengine, ulijadili suala la kijiji hicho kukosa mvua kwa kipindi kirefu.

Kufuatia kutonyesha kwa mvua hiyo, wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakimtuhumu mkazi mwenzao, (jina limehifadhiwa) kwamba amekuwa akijigamba mitaani kuwa mvua kijijini hapo haitanyesha.

Baada ya wajumbe wa kijiji kuchangia kuhusu suala hilo, ndipo mbunge alipoondoka huku akiongozana na wajumbe hao pamoja na wananchi waliofurika kumwangalia, wakielekea katika nyumba ya mtuhumiwa huyo kwenye kitongoji cha Kimunyu.

“Jamani mnakumbuka kwenye kampeni nilivyosema, napenda niwakumbushe, nilisema kazi ya ubunge ni ya miaka mitano lakini kazi yangu ya uganga siwezi kuiacha nitaifanya hadi nitakapokufa," alisema Profesa Majimarefu.

Mbunge huyo baada ya kueleza hivyo aliongozana na mwenyekiti wa kijiji hicho, mtendaji wa kijiji na mwenye nyumba hizo kuingia nao ndani ya nyumba ya mtuhumiwa.

Baada ya kuingia katika nyumba hiyo, Profesa Maji Marefu alitoka akiwa na tunguri mbalimbali zilizodaiwa kumilikiwa na mtuhumiwa huyo.

CHANZO: NIPASHE
 
[h=2]Friday, March 9, 2012[/h][h=3][/h]

Majimarefu.jpg
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,
Stephen Ngonyani

Wabunge wetu hao waogopeni; kwanini wasiende kwake kabla ya kwenda India?
 
Back
Top Bottom