Juzi juzi nilisoma habari katika moja ya magazeti ya kila siku, likiripoti kwamba Mbunge wa Mvomero Mheshimiwa Amos Makalla ametoa msaada wa mipira 23 pamoja na seti za sare za michezo kwa vikundi vya vijana ambao ni wapiga kura wa jimboni kwake. Hili neno msaada lilinipa maswali kidogo hasa nikizingatia kwamba moja ya majukumu ya mbunge ni kutekeleza ahadi za chama chake kama zilivyoainishwa katika ilani yao ya uchaguzi, lakini vile vile kutekeleza ahadi zake mwenyewe. Mbunge pia ana wajibu wa kuhakikisha ustawi wa wananchi wa jimbo lake kwa kipindi chote cha ubunge wake. Sasa iweje kutekeleza majukumu haya kuwe ni msaada wakati aliomba kuchaguliwa na kuwaongoza wananchi wake ili atoe huduma hizo?
Hii ikanikumbusha hoja ambayo aliitoa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Africa Mashariki wa Uganda (wakati huo) Eliya Kategeya ambaye alisema kwamba wapiga kura wa Afrika wanahitaji kupewa elimu ya uraia ili wajue haki na wajibu wao na akatoa mfano wa wapiga kura wa huko Uganda ambavyo wanaandaa nyimbo na sherehe za kumpongeza na kumshukuru mbunge au waziri aliyefanikisha ujenzi wa barabara, bila kujua kwamba ujenzi huo umefanikishwa kwa kodi zao hao wananchi na kwamba sasa wanalipwa kutokana na kodi zao hizo. Kwa hakika elimu ya uraia inahitajika pia hata kwa waandishi wanaoripoti matukio ya namna hii.