Mbunge akerwa Zanzibar kufananishwa na wilaya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Godfrey Ismaely, Dodoma

MBUNGE wa Ole Rajab Mbarouk Mohammed (CUF), amemjia juu mbunge wa Geita, Bw. Donald Max (CCM) kwa kuifananisha Zanzibar na wilaya.Wakati akichangia
hotuba ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Max alisema kuwa wilaya ya Geita ina ofisa kilimo mmoja, wakati wilaya hiyo ni kubwa kuliko Kilwa na Zanzibar.

Baada ya mbunge kumaliza kuchangia hotuba hiyo, Bw. Mohammed, aliomba kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa bunge, Jenista Mhagama akisema kuwa mbunge aliyemaliza kuchangia ameitaja Zanzibar kama wilaya.

"Mheshimiwa Mwenyekiti naomba kutoa taarifa, mchangiaji aliyemaliza ameitaja Zanzibar kama wilaya.

"Naommba kumpa taarifa kuwa Zanzibar ni nchi, ina rais wake, katiba yake na bendera yake…tunataka hili suala likome," alisema Mohammed.

Akijibu hoja hiyo, Mhangama alisema kuwa taarifa hiyo imezingatiwa na itaingia kwenye hansard kwani inafahamika kuwa Zanzibar ni nchi.
 
Wabunge Wengine wa Bara lazima waende kwenye Darasa la Siasa, kama kweli tunataka Muungano wa hiari na sio kulazimishwa.

Hauwezi kulinganisha Nchi na Wilaya PERIOD.
 
Kama Mh Max alikuwa anamaanisha ukubwa wa eneo la wilaya Geita ni zaidi ya ule wa Kilwa na nchi ya Zanzibar (kwa pamoja!?) tatizo lipo wapi? Sula la ukubwa wa eneo ni factual. Inawezekana na 'inferiority complex' tu ndio tatizo hapa.
 
Aliyebuni muungano wa style hii japo huenda alikuwa na nia nzuri alikosea, kwa nini hakuivunja zanzibar na kuifanya mkoa/wilaya ya muungano?hatuwezi kufika kwa kuwa na muungano wa jinsi hii. Kuendelea na zanziba imekuwa issue kama kumbeba mtoto aliyeungua kwapani!Muungano urekebishwe, zanziba ifutwe na kuwa na serikali moja tu ya jamhuri au la kila nchi ichukue zake- suala la serikali tatu utakuwa ujinga wa kurudisha maendeleo yetu nyuma.
 
Zanzibar haina sifa ya nchi kama Zanzibar ni nchi mbona ilishindwa kujiunga OIC ?.Zanzibar haina tofauti na kata ya Kimandolu kuilinganisha na wilaya ya Geita ni makosa makubwa.Kama ni rais hata Yanga na TFF wana rais,kama ni bendera Simba,Yanga,Mtibwa wote wana bendera.
 
Wakubwa lazima tukubali kuwa hapa kuna tatizo,kama mbunge anaitolea zanzibar mfano kwa ukubwa wa eneo tu,mzanzibar anaomba mwongozo....hatari!!!..hivi anayejua aniambie hivi sababu kubwa ya Tanganyika na Zanzibar kuungana ni nini???..mara nyingi watu wanaungana ili wafaidi rasilimali kwa pamoja...lakini katika muungano huu utasikia..mafuta yasiyo ya Muungano...Hivi mnaweza kuoana halaf kila mtu akabaki na shuka lake???..samahani sikuwepo mwaka 1964..mtanisamehe
 
Zanzibar haina sifa ya nchi kama Zanzibar ni nchi mbona ilishindwa kujiunga OIC ?.Zanzibar haina tofauti na kata ya Kimandolu kuilinganisha na wilaya ya Geita ni makosa makubwa.Kama ni rais hata Yanga na TFF wana rais,kama ni bendera Simba,Yanga,Mtibwa wote wana bendera.
Kamani katiba....................
umesahau kumalizia.
 
Hao wabunge wa wilaya ya zanzibar wasitu.....nchi ni moja 2 TANZANIA period,mnawabembeleza nn?ujuha wa viongozi wa magamba kuogopa kuwaeleza ukweli eti kuwafurahisha kwa kuwambia znz ni nchi....hakuna mambo ya serkali 3 tuelekee 1
 
Changia basi wewe unayejua mbona unaishia kutukana? Issue ilikuwa ukubwa wa eneo sasa hawa jamaa wako so inferior ukiwagusa tu.....zanzibar ni nchi. Naushangaa sana huu muungano sijui una faida gani kwetu wabara zaidi ya kujaza wapemba huku kwetu na magavana wa kututawala hadi kwenye kata na tarafa wakati ni dhambi kwa Mtanganyika kuwa kiongozi zanzibar. Waitishe kura ya maoni waone. we are tired na hatuutaki muungano wa kinafiki.
 
Wabunge Wengine wa Bara lazima waende kwenye Darasa la Siasa, kama kweli tunataka Muungano wa hiari na sio kulazimishwa.Hauwezi kulinganisha Nchi na Wilaya PERIOD.
Mimi sioni kosa kulinganisha eneo moja na jingine hata kama eneo moja ni nchi na eneo jingine ni Wilaya! Hivi huyu mbunge anataka tuamini kwamba "kwa kuwa Zanzibar ni 'nchi' ina eneo kubwa kuliko Mkoa wa wote Morogoro?" Vitu vingine vinakuwa ni inferiority complex!
 
Changia basi wewe unayejua mbona unaishia kutukana? Issue ilikuwa ukubwa wa eneo sasa hawa jamaa wako so inferior ukiwagusa tu.....zanzibar ni nchi. Naushangaa sana huu muungano sijui una faida gani kwetu wabara zaidi ya kujaza wapemba huku kwetu na magavana wa kututawala hadi kwenye kata na tarafa wakati ni dhambi kwa Mtanganyika kuwa kiongozi zanzibar. Waitishe kura ya maoni waone. we are tired na hatuutaki muungano wa kinafiki.
Muungano umetuweka salama sana dhidi ya magaidi, otherwise Zanzibar/Pemba zingekuwa kama Somalia/Somaliland! Tuendelee kuuenzi Muungano huu wa kipekee duniani! Mungu uwaangamize wote wanaouonea kijicho Muungano wetu! Wote semeni Amen!
 
Kama Mh Max alikuwa anamaanisha ukubwa wa eneo la wilaya Geita ni zaidi ya ule wa Kilwa na nchi ya Zanzibar (kwa pamoja!?) tatizo lipo wapi? Sula la ukubwa wa eneo ni factual. Inawezekana na 'inferiority complex' tu ndio tatizo hapa.

hivi utajisikiaje kama rafiki yako anakuambia amemuona "changu doa", ambae amefanana na mama yako?
 
Back
Top Bottom