Mbowe, Seif na UKAWA kwanini mmekubali haya?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Habari wana jamiiforums,

Ni muda umepita, nilikuwa member humu ikiwa JamboForums na baadae Jamiiforums nakumbuka mwanzoni mwaka 2006 tulimpokea Ndg.Freeman A.Mbowe tulileta mijadala kuntu kuleta fikra mpya japo watu walijadili bila kuweka itikadi za vyama,ilikuwa ni mawazo ya kizalendo tu.

Niliondoka JF baada ya mlipuko wa vijana wa kundi liitwalo mtandao wa CCM ambao ni kama walimwagwa vijana humu JF kuhakikisha wanamtukana yeyote anayetowa hoja zenye mashiko kwa maendeleo ya nchi na mwenye kukemea nyendo za vigogo/mafisadi hao kutwaa ikulu kwa gharama yoyote.

Leo nimelazimika kuandika kuonyesha ni jinsi gani CHADEMA, CUF na UKAWA wamenasa kwenye nyavu za CCM na kufifisha harakati zao kisiasa, japo kuna ongezeko la uwakilishi bungeni na udiwani lazima nikiri tu katika sayansi ya siasa ni sawa na kupanda mbegu kwenye miiba, mmea utaota japo hautakuwa.

Lazima tukiri kwamba CCM inaimarika kuliko tulivyofikiria; kuanzia oganaizesheni, uongozi, wanachama,uibuaji wa kizazi kipya cha uongozi, nk. waliweza kwa mafanikio kuusambaratisha mtandao uliyoitafuna kwa miaka zaidi ya 20 kutaka madaraka. Inawezekana kwa kujuwa, kutokujua au tamaa ya pesa CHADEMA bila ya ajizi wakauchukuwa kama ulivyo na kuukabidhi chama kwa nia ya kushinda uraisi, 2015 kutokana na uzoefu na pesa za hili kundi. Madhara ya ujio huu ni makubwa kwa chadema na yanajitokeza;

Mosi; Ajizi nyumba ya njaa; kuondoka kwa Dr.Slaa na Prof Lipumba CHADEMA na CUF kwa kutokubali maamuzi ya kubadili gia angani imeleta madhara makubwa kwa vyama hivyo ki-oganaizesheni ni kama kumkata mbuzi miguu ya mbele. Mbowe anaendeleza makosa kwa kutumia gazeti lake kumchafua Dr.Slaa na familia yake ambaye kimsingi hafanyi siasa kwa sasa hivyo tabia hii haiongezi umaarufu wa CHADEMA bali inamnyima Mbowe na Chadema fursa ya mahusiano ya kibinadamu na Dr.Slaa (Akiba ya maneno), akumbuke madhila anayopitia Kubenea ambaye kwa mwaka mzima amemtukana Zitto ila uwezo wake finyu bungeni umemfundissha kwamba siasa sio ukanjanja, wiki 2 bungeni zimemtosha kuwa na akili kidogo na kuacha hekaya zake za uongo na chuki.Ni ngumu kupata mbadala anayeaminika.

Pili; EL ni kinyago kilichochongwa na CCM kwa hivyo hawezi kuwatisha wanajuwa kila mbinu zake, CCM wamefanikiwa kumkamua sumu yote na atawatumikia hana jinsi. Ameshaota mizizi ndani ya CHADEMA kiasi cha yeye kuhusishwa na ushindi wa madiwani na wabunge wote Ukawa, na hii mbinu aliitumia ndani ya CCM kuaminisha kwamba mkutano mzima ni ‘’watu wake’’.Vijana wake wametamalaki itakuwa shida kwa CHADEMA kupata wagombea ubunge na udIwani 2020 pale ambapo vijana wake watakapotaka kugombea huku CHADEMA wakiwaona sio wenzao, ikumbukwe tu kwamba ni vijana aliowatengenezea ukwasi na ushawishi hivyo kutachimbika na hii inaiweka CHADEMA katika hatari ya usaliti mkubwa ndani ya chama kwa miaka mingi ijayo kuliko kipindi kingine (Team Lowassa v CHADEMA).Tukumbuke EL na timu yake ni wakubwa kuliko CHADEMA na wamepewa utukufu kwamba bila yeye CHADEMA na UKAWA kwa ujumla wasingeshinda ubunge na udiwani, ikiwamo Tanzania bara na Zanzibar (rejea Magazeti ya desemba 2015; Lowassa awapa UKAWA wabunge 116, halmashauri nk), hataguswa na ataachiwa aamuwe nani anamtaka agombee wapi, kwani katika nafasi alizopewa kuteuwa viti maalum aliteuwa marafiki zake waliokuwa CCM, ofisi yake mikocheni ndio yenye maamuzi sio ufipa pale hapana hadhi yake.

Tatu; CCM wamefanikiwa kugeuza taswira na ni kama inawaeleza wananchi ambao ni wapiga kura kwamba kwa kuondoka kwa EL na gene lake kimepumua na sasa mzigo umehamia CHADEMA na kwa kweli hili wamefanikiwa ndio maana wakikosoa yeyote hujibiwa ‘’mbona CHADEMA mlimchukuwa EL kaeni kimya mafisadi nyinyi’’ nk. CCM imejivua gamba (mtandao) uliyowatesa na wanaonekana kuitumia hii fursa vyema ili kujenga taswira mpya huku CHADEMA wakitowa maelezo na utetezi (dodoki) ambao haueleweki vema, CCM kutumia fimbo hiyo kuwachapa, Kwa hali yoyote ile kataa kubali EL, Sumaye na wengine ni mradi mpya wa CCM upinzani kwa akili za kawaida itachukuchuwa miaka 20 kutambua kosa hili kama ilivyokuwa Mrema baada ya kushindwa uraisi mwaka 1995.Kibaya zaidi Maalim Seif kukubali EL awe bosi wake nayyeye maamuzi anafanyia Mikocheni bila kufahamu anatekeleza mipango isiyo ya CUF.

Nne; CHADEMA inafanya makosa makubwa kujaribu kupinga mabadiliko yanayofanywa na Raisi Dr.Magufuli, ambayo kwa pamoja na Kina Freeman Mbowe tuliyaongelea, kama kubana matumizi, safari za nje, utegemezi wa nje mbaya zaidi nimemsikia Mbowe akilalamikia viongozi na wafanayakazi wa Umma wanaowajibishwa kwa kuleta hasara bandarini, Nida, TRA, mahakama ya mafisadi, nk akisema ‘’wanaonewa’’ eti Raisi ‘’hafuati sheria ’’, EL analalamika ‘’marafiki zake’’ kutozwa kodi (japo yeye siwezi kumshangaa) kundi kutamani serikali ifanye makosa ili wapate cha kukosoa (siasa za fisi) kama ambavyo viongozi wa juu wanavyofanya. Badala ya kuboresha hoja chadema kimekuwa ni chama kinachopiga makelele.

Mwisho; Propaganda zisizo na mantiki kama ‘’kushitaki ICC & ICJ’’, ‘’TB Joshua kaja na ujumbe mzito’’!, ‘’Mkapa kafariki’’!,’’tumeibiwa kura’’ ambazo ni sawa na kujidanganya kwamba ‘’usiku hautakwisha”. Kinachoudhi zaidi ni Chadema kuacha kwenda kuishitaki serikali kwa wananchi na sasa wanakimbilia kwenye western media na mabalozi hizi ni dalili kwamba hoja zao haziaminiwi na wananchi. Kwangu mimi Dr.Slaa ni rasilimali muhimu tuliyotupa kwani hata angeshindwa uraisi bado angekuwa na uhalali wa hoja dhidi ya serikali. Mbowe kala matapishi yake na EL kamuumbua kwa kumbandika bei yake (price tag) mwaka 2013 alijitapa kwenye hana bei kipindi wanagombana na Zitto ni Kama namwona JK anamkejeli Mbowe ‘’Dogo mbowe bei yako ni chee mno!’ unakumbuka ulichosema mwaka, 2013? kwamba hauna bei, sasa vipi? Ni muda muafaka kwa Mbowe na Maalim kutafakari upya mustakabali wao kisiasa!

Nakaribisha hoja na si viroja
 
Hizo hoja zako hazina mantiki. Warudishie Lumumba. Nilipoanza kusoma nilijua umeleta ujumbe wenye mantiki kumbe umekuja kupigia kampeni ccm wakati uchaguzi ushamalizika.
 
Kijana huu ni uelekeo wa safari mbaya kwa chadema,usipende kusikia mema tu kuhusu chadema...weka akili yako huru kama vile sio msukule utaelewa,ila kwa akili ya kawaida itakuchukuwa miaka zaidi ya 10 kugundua hili jambo.
 
wemwenyewe lumumba,ndio zenu kujivika upinzani kupima upepo najua saivi mnaajira rasmi naposho itakuwa imependa maana JK alipendekeza mkumbukwe..asante kwamaneno yako mengi lakini nonsense
 
Kwa aina ya vijana watetezi wanaotetea haya ni dalili la bomu lililopo chadema,tuliongea mambo haya yalipokuwa CCM na sasa tutaongea chadema inapochuwa mrengo huu.Mwanzoni CCM ilijivunia kwa hili wimbi ila ilihangaika kulitowa kwa miaka 10 hadi 2015..walitetea uozo naona sasa wametamalaki ndani ya chadema tangia 29.7.2015...itasumbua!
 
wemwenyewe lumumba,ndio zenu kujivika upinzani kupima upepo najua saivi mnaajira rasmi naposho itakuwa imependa maana JK alipendekeza mkumbukwe..asante kwamaneno yako mengi lakini nonsense
Tulitukanwa hivi hivi..tatizo siasa zinafanywa utafikiri ibada za miujiza ili kuteka uelewa wa watu,ila ukitafakari kwa sauti ukiwa huru kwenye ubongo wako utajifunza...mambo haya yamefanywa kenya ambapo hadi leo upinzani haujawahi kuongoza nchi kivitendo bali ni kiini macho,uganda Mbabazi na Kiiza ni genge moja na M7.
 
Mkuu,

nNona kuna tatizo la objectivity kwenye bandiko lako;
1.CHADEMA Hawajawahi kumfukuza Dr slaa ameondoka kwa ridhaa yake mwenyewe

2.Lowasa ni mwanachama wa CHADEMA na mgombea Urais 2015....Ana hadhi yake.

3.Hizo ishu za ICJ hakujawahi kuwa na kauli yoyote kutoka CHADEMA Isipokuwa social media

4.Tanzania Daima haiandikwi na mbowe kuna waandishi na wahariri...so far ungekuja na specific case ambayo Tanzania daima wamemshambulia slaa.

5.CHADEMA Inaendelea kukua kutokana na mchango wa watu mbalimbali...kila mtu kwa wakati wake...Dr slaa amecheza nafasi yake tunamshukuru...ila no one is irreplaceable
 
CCM wanachofanya ni kusafiria nyota ya Magufuli,hakuna mabadiliko ki organzeshini wala ki uongozi.
Viongozi ni walewale akina Kinana,Mang'ula Nape,Mwigulu nk..hawana jipya
Historia itajirudia kama walivyosafiria nyota ya Kikwete 2005,sote tunajua ilipowafikisha
. Unknown factor ni iwapo Magufuli atakabidhiwa chama atafanya nini
 
CCM wamefanikiwa kugeuza taswira na ni kama inawaeleza wananchi ambao ni wapiga kura kwamba kwa kuondoka kwa EL na genge lake kimepumua na sasa mzigo umehamia CHADEMA

Mkuu uko sahihi zigo hilo wanalo CHADEMA hilo genge litawasumbua hasa.Ruzuku za CHAMA watazitaka na chama watataka wakishike Lowasa na GENGE LAKE.

Wale wote mliokuwa mkimtukana Lowasa na mafisadi wengine msidhani wamewasamehe.Time will tell.Hilo la kuingia huko ndani ya Chadema NI GEAR NAMBA MOJA ya kuingilia lakini wana viboko mikononi wanawalia timing.Hilo genge halina huruma japo ukiwatazama usoni waweza waona kama malaika.

KItakachowapata CHADEMA msije kulia nyau humu ndani
 
Niliondoka JF baada ya mlipuko wa vijana wa kundi liitwalo mtandao wa CCM ambao ni kama walimwagwa vijana humu JF kuhakikisha wanamtukana yeyote anayetowa hoja zenye mashiko kwa maendeleo ya nchi na mwenye kukemea nyendo za vigogo/mafisadi hao kutwaa ikulu kwa gharama yoyote.

Sasa umeshaambiwa kuwa hao vijana wameondoka?
 
Mkuu Freeland,
1.Akufukuzae akwambiitoka.
2. Tanzania Daima ni gazeti la propaganda la chadema linamilikiwa na Mbowe ndio maana sikuhizi linamchafua Dr.Slaa
3.Habari za ICC na ICJ,social media,EL,Mbowe wamekuwa wakiimba mahakama hizi kipindi chote cha kampeni hadi baada ya matokeo kutangazwa.
4.Nakubaliana na wewe kwamba mtapata mbadala ila naweka akiba ya maneno.
5.Siasa ni sayansi dogo...Mbowe anaelewa ninayosema wewe itakuchukuwa zaidi ya miaka 10 japo utakuwa umechanganyikiwa hadi upate ukweli.
mkuu,

naona kuna tatizo la objectivity kwenye bandiko lako;
1.CHADEMA Hawajawahi kumfukuza Dr slaa ameondoka kwa ridhaa yake mwenyewe

2.Lowasa ni mwanachama wa CHADEMA na mgombea Urais 2015....Ana hadhi yake.

3.Hizo ishu za ICJ hakujawahi kuwa na kauli yoyote kutoka CHADEMA Isipokuwa social media

4.Tanzania Daima haiandikwi na mbowe kuna waandishi na wahariri...so far ungekuja na specific case ambayo Tanzania daima wamemshambulia slaa.

5.CHADEMA Inaendelea kukua kutokana na mchango wa watu mbalimbali...kila mtu kwa wakati wake...Dr slaa amecheza nafasi yake tunamshukuru...ila no one is irreplaceable
 
Habari wana jamiiforums,

Ni muda umepita, nilikuwa member humu ikiwa JamboForums na baadae Jamiiforums nakumbuka mwanzoni mwaka 2006 tulimpokea Ndg.Freeman A.Mbowe tulileta mijadala kuntu kuleta fikra mpya japo watu walijadili bila kuweka itikadi za vyama,ilikuwa ni mawazo ya kizalendo tu.

Niliondoka JF baada ya mlipuko wa vijana wa kundi liitwalo mtandao wa CCM ambao ni kama walimwagwa vijana humu JF kuhakikisha wanamtukana yeyote anayetowa hoja zenye mashiko kwa maendeleo ya nchi na mwenye kukemea nyendo za vigogo/mafisadi hao kutwaa ikulu kwa gharama yoyote.

Leo nimelazimika kuandika kuonyesha ni jinsi gani CHADEMA, CUF na UKAWA wamenasa kwenye nyavu za CCM na kufifisha harakati zao kisiasa, japo kuna ongezeko la uwakilishi bungeni na udiwani lazima nikiri tu katika sayansi ya siasa ni sawa na kupanda mbegu kwenye miiba, mmea utaota japo hautakuwa.

Lazima tukiri kwamba CCM inaimarika kuliko tulivyofikiria; kuanzia oganaizesheni, uongozi, wanachama,uibuaji wa kizazi kipya cha uongozi, nk. waliweza kwa mafanikio kuusambaratisha mtandao uliyoitafuna kwa miaka zaidi ya 20 kutaka madaraka. Inawezekana kwa kujuwa, kutokujua au tamaa ya pesa CHADEMA bila ya ajizi wakauchukuwa kama ulivyo na kuukabidhi chama kwa nia ya kushinda uraisi, 2015 kutokana na uzoefu na pesa za hili kundi. Madhara ya ujio huu ni makubwa kwa chadema na yanajitokeza;

Mosi; Ajizi nyumba ya njaa; kuondoka kwa Dr.Slaa na Prof Lipumba CHADEMA na CUF kwa kutokubali maamuzi ya kubadili gia angani imeleta madhara makubwa kwa vyama hivyo ki-oganaizesheni ni kama kumkata mbuzi miguu ya mbele. Mbowe anaendeleza makosa kwa kutumia gazeti lake kumchafua Dr.Slaa na familia yake ambaye kimsingi hafanyi siasa kwa sasa hivyo tabia hii haiongezi umaarufu wa CHADEMA bali inamnyima Mbowe na Chadema fursa ya mahusiano ya kibinadamu na Dr.Slaa (Akiba ya maneno), akumbuke madhila anayopitia Kubenea ambaye kwa mwaka mzima amemtukana Zitto ila uwezo wake finyu bungeni umemfundissha kwamba siasa sio ukanjanja, wiki 2 bungeni zimemtosha kuwa na akili kidogo na kuacha hekaya zake za uongo na chuki.Ni ngumu kupata mbadala anayeaminika.

Pili; EL ni kinyago kilichochongwa na CCM kwa hivyo hawezi kuwatisha wanajuwa kila mbinu zake, CCM wamefanikiwa kumkamua sumu yote na atawatumikia hana jinsi. Ameshaota mizizi ndani ya CHADEMA kiasi cha yeye kuhusishwa na ushindi wa madiwani na wabunge wote Ukawa, na hii mbinu aliitumia ndani ya CCM kuaminisha kwamba mkutano mzima ni ‘’watu wake’’.Vijana wake wametamalaki itakuwa shida kwa CHADEMA kupata wagombea ubunge na udIwani 2020 pale ambapo vijana wake watakapotaka kugombea huku CHADEMA wakiwaona sio wenzao, ikumbukwe tu kwamba ni vijana aliowatengenezea ukwasi na ushawishi hivyo kutachimbika na hii inaiweka CHADEMA katika hatari ya usaliti mkubwa ndani ya chama kwa miaka mingi ijayo kuliko kipindi kingine (Team Lowassa v CHADEMA).Tukumbuke EL na timu yake ni wakubwa kuliko CHADEMA na wamepewa utukufu kwamba bila yeye CHADEMA na UKAWA kwa ujumla wasingeshinda ubunge na udiwani, ikiwamo Tanzania bara na Zanzibar (rejea Magazeti ya desemba 2015; Lowassa awapa UKAWA wabunge 116, halmashauri nk), hataguswa na ataachiwa aamuwe nani anamtaka agombee wapi, kwani katika nafasi alizopewa kuteuwa viti maalum aliteuwa marafiki zake waliokuwa CCM, ofisi yake mikocheni ndio yenye maamuzi sio ufipa pale hapana hadhi yake.

Tatu; CCM wamefanikiwa kugeuza taswira na ni kama inawaeleza wananchi ambao ni wapiga kura kwamba kwa kuondoka kwa EL na gene lake kimepumua na sasa mzigo umehamia CHADEMA na kwa kweli hili wamefanikiwa ndio maana wakikosoa yeyote hujibiwa ‘’mbona CHADEMA mlimchukuwa EL kaeni kimya mafisadi nyinyi’’ nk. CCM imejivua gamba (mtandao) uliyowatesa na wanaonekana kuitumia hii fursa vyema ili kujenga taswira mpya huku CHADEMA wakitowa maelezo na utetezi (dodoki) ambao haueleweki vema, CCM kutumia fimbo hiyo kuwachapa, Kwa hali yoyote ile kataa kubali EL, Sumaye na wengine ni mradi mpya wa CCM upinzani kwa akili za kawaida itachukuchuwa miaka 20 kutambua kosa hili kama ilivyokuwa Mrema baada ya kushindwa uraisi mwaka 1995.Kibaya zaidi Maalim Seif kukubali EL awe bosi wake nayyeye maamuzi anafanyia Mikocheni bila kufahamu anatekeleza mipango isiyo ya CUF.

Nne; CHADEMA inafanya makosa makubwa kujaribu kupinga mabadiliko yanayofanywa na Raisi Dr.Magufuli, ambayo kwa pamoja na Kina Freeman Mbowe tuliyaongelea, kama kubana matumizi, safari za nje, utegemezi wa nje mbaya zaidi nimemsikia Mbowe akilalamikia viongozi na wafanayakazi wa Umma wanaowajibishwa kwa kuleta hasara bandarini, Nida, TRA, mahakama ya mafisadi, nk akisema ‘’wanaonewa’’ eti Raisi ‘’hafuati sheria ’’, EL analalamika ‘’marafiki zake’’ kutozwa kodi (japo yeye siwezi kumshangaa) kundi kutamani serikali ifanye makosa ili wapate cha kukosoa (siasa za fisi) kama ambavyo viongozi wa juu wanavyofanya. Badala ya kuboresha hoja chadema kimekuwa ni chama kinachopiga makelele.

Mwisho; Propaganda zisizo na mantiki kama ‘’kushitaki ICC & ICJ’’, ‘’TB Joshua kaja na ujumbe mzito’’!, ‘’Mkapa kafariki’’!,’’tumeibiwa kura’’ ambazo ni sawa na kujidanganya kwamba ‘’usiku hautakwisha”. Kinachoudhi zaidi ni Chadema kuacha kwenda kuishitaki serikali kwa wananchi na sasa wanakimbilia kwenye western media na mabalozi hizi ni dalili kwamba hoja zao haziaminiwi na wananchi. Kwangu mimi Dr.Slaa ni rasilimali muhimu tuliyotupa kwani hata angeshindwa uraisi bado angekuwa na uhalali wa hoja dhidi ya serikali. Mbowe kala matapishi yake na EL kamuumbua kwa kumbandika bei yake (price tag) mwaka 2013 alijitapa kwenye hana bei kipindi wanagombana na Zitto ni Kama namwona JK anamkejeli Mbowe ‘’Dogo mbowe bei yako ni chee mno!’ unakumbuka ulichosema mwaka, 2013? kwamba hauna bei, sasa vipi? Ni muda muafaka kwa Mbowe na Maalim kutafakari upya mustakabali wao kisiasa!

Nakaribisha hoja na si viroja

Sasa we mzee umeandika nini? una tofauti gani na vijana
 
Sasa umeshaambiwa kuwa hao vijana wameondoka?
Wamekuja huko chadema na EL ,ndio wanaindesha bavicha kwa sasa jina lao maaruu ni 4U na TeamL....ni ngumu sana kuwadhibiti hasa ukizingatia chadema kwa sasa haina taasisi imara.
 
Kijana huu ni uelekeo wa safari mbaya kwa chadema,usipende kusikia mema tu kuhusu chadema...weka akili yako huru kama vile sio msukule utaelewa,ila kwa akili ya kawaida itakuchukuwa miaka zaidi ya 10 kugundua hili jambo.

Hivi kwa mfano ulitaka CDM wafanye nini kwa mazingira ya siasa za Africa. Siasa za mipasho isiyoheshimu upinzani huku dola ikifanya njama upinzani usisikike kwa wapiga kura na niseme wazi mtu yeyote anaeshabikia hali hiyo hawakomoi kina Mbowe na CDM yao bali tunajimaliza kwa kukumbatia mfumo mgando ulioshindwa kututoa kwenye lindi la
Umaskini huku raslimali zetu zikiuzwa kwa mrahaba wa 3percent.
 
Mkuu Freeland,
1.Akufukuzae akwambiitoka.
2. Tanzania Daima ni gazeti la propaganda la chadema linamilikiwa na Mbowe ndio maana sikuhizi linamchafua Dr.Slaa
3.Habari za ICC na ICJ,social media,EL,Mbowe wamekuwa wakiimba mahakama hizi kipindi chote cha kampeni hadi baada ya matokeo kutangazwa.
4.Nakubaliana na wewe kwamba mtapata mbadala ila naweka akiba ya maneno.
5.Siasa ni sayansi dogo...Mbowe anaelewa ninayosema wewe itakuchukuwa zaidi ya miaka 10 japo utakuwa umechanganyikiwa hadi upate ukweli.

Sasa kama anayeelewa ni mbowe tu wengine hatuelewi...Ungemwandikia barua mbowe basi sio kuweka hapa

Nimekuambia uweke specific habari ambayo siku hizi Tanzania daima linamchafua slaa ....umeshindwa kuweka...walau hata link

Dr slaa hakusema amefukuzwa alisema amejiuzulu baada ya kutoridhishwa na kupokewa kwa Lowasa...hayo ya kufukuzwa unayatoa wapi?

Kwani ni Uongo kwamba endapo wanasiasa watahamasisha mauaji ya wananchi hawatapelekwa ICC? Tanzania imesaini Rome Convention....

Akiba ya maneno ipi unataka niweke...Kwani slaa angekuwa amekufa leo ungeenda kumfufua aje aongoze chadema? si chama kingeendelea tu...Hatuabudu mtu

siasa ni sayansi....Ila hio sayansi hauelewi wewe na mbowe tu...hata na sisi tunaelewa
 
Back
Top Bottom