Mbowe: Lowassa ni dhaifu, ni bubu

Status
Not open for further replies.
Mh.Mbowe amenukuliwa na Tanzania Daima akimchana Mh.Lowasa kuwa ni mgombea dhaifu na bubu wa kukemea ufisadi.

Amesema UKAWA hawawezi kuwa nae,hivyo asiwatishe CCM kuwa ana nafasi UKAWA.

Source:Tanzania Daima page no.5

Tanzania Daima ni gazeti la ccm.. unategemea wamseje lowassa?
 
Eddo wa Miaka kumi iliyopita, Mwenye speech machachari bungeni, mwenye kupiga utani, vijembe na mikogo mbalimbali ya kisiasa hivi sasa Siyo kama yule.
Huyu mtu ana fundo moyoni na anadhani dawa yake ni apate power zaidi ili awaprove wrong mahasimu wake wa kisiasa, Angejisafisha tu tuhuma zake kisha akajipumzikia kwa amani!
 
KENYA PIA AMERICA KUNA KITU KWENYE TV KIITWACHO TRUTH METER.
mm nimeamua kumpitisha kwenye truth meter.
. LOWASA NI UKWELI HAWEZI KUJIELEZA. mara nyingi anapenda kusoma prepared speech,believe me lini ulimuona LOWASA akichangia bungeni tuseme ukweli.
LOWASA HAWEZI KUJENGA HOJA. LOWASA atapigwa sana kama atashiriki presidential debate. ukiwa mgombea halafu ukoweak katika kujenga hoja lazima utapwaya.
LOWASA PHYSICALLY YUKO WEAK. kwa wale waliofatilia mkutanowake kule aruscha msaidizi wake alimwambia acheze kidogo na tukio lilikua live so tuliona. pia juzi wakati wanashuka jukwaa juu alionekana anashuka kwa uangalifu ili asijedondoka
.LOWASA HAJUI SLOGAN ZA UPINZANI mfano anatumia maneno WATAISOMA NAMBA msemo wa CCM. kiongozi makini angejikita na slogan za upinzani l
ntaleta zingine baadae.......

Na bado,
Mtanyooka tu.
 
"Wanajidanganya, Lowassa ni dhaifu sana. Amekaa serikalini zaidi ya miaka 30 na hakuna maendeleo yanayoonekana ndani ya serikali zaidi ya kila siku wizi na ubadhirifu kuongezeka,"

Yuko ndani ya UKAWA sasa..Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi..Sasa naanza kuuelewa uamuzi wa Dr. Slaa.
 
Kama kawaida ya watanzania kila kunapotokea jambo nilalotulazimu kujikumbusha wosia wa mpenwa wetu Nyerere hatuna budi kujikumbusha baadhi ya maneno yake ya busara kwa sababu ni kiongozi wa kitaifa anayeheshimika hapa Tanzania.

Pia kwa sasa hatuna budi kujikumbusha wosia wa Ndugu Mbowe kwa watanzania ili kuchagua kiongozi mzuri kwa maana ya utendaji, maadili na mwadilifu

Quotes;


"Wanajidanganya, Lowassa ni dhaifu sana. Amekaa serikalini zaidi ya miaka 30 na hakuna maendeleo yanayoonekana ndani ya serikali zaidi ya kila siku wizi na ubadhirifu kuongezeka," Freeman Mbowe.


"Hao wanaomtaka Lowassa ni wale wanaojua kuwa watanufaika binafsi akipita kwenye urais lakini kimsingi huyu jamaa ni dhaifu sana na hafai kuongoza Tanzania ya sasa yenye changamoto lukuki. Wapambe wake wanasema si msemaji bali mtendaji, hivi nani atakubali porojo hizo wakati tunajua akiwa Waziri Mkuu hakufanya lolote kukemea wizi, ubadhirifu na ufisadi? Richmond ilikuja akiwa wapi?," Mbowe.

"Sina ugomvi wala simchukii Lowassa binafsi, lakini ni vema hawa wanaosema ni mtu wa maamuzi magumu wakaueleza umma wakati watendaji wa serikali wakitafuna mabilioni ya fedha, CCM wakipitisha Katiba inayopendekezwa ya hovyo pale Dodoma wakitetea kwa wizi...yeye alisema au kufanya nini?," Mbowe.

"Huyu mtu yumo ndani ya mfumo wa ufisadi ulioiharibu nchi kwa takriban miaka 50 halafu mnataka kutuaminisha ni mchapakazi, tuwe serious jamani, nchi inahitaji mabadiliko ambayo yanapatikana UKAWA," Mbowe.

"Msipate shida, UKAWA ni kiboko ya Lowassa na CCM yake, ikifika Oktoba wananchi watuchague tuwakwamue kutoka hapa tulipo, haiwezekani miaka 50 sisi tungali maskini wa kutupwa ilhali tuna rasilimali lukuki," Mbowe.

"Sasa tutapambana na CCM jino kwa jino mpaka kieleweke, wao walikuwa wakishinda kirahisi kwa sababu walikuwa na wenyeviti wa vijiji, lakini sasa wataonja nguvu yetu,"

Mkuu big up, waje sasa waseme hapo kuwa hayo yote yalikuwa uongo, asee jamaa hawapaswi hata kuongoza mtaa.
 
"Huyu mtu yumo ndani ya mfumo wa ufisadi ulioiharibu nchi kwa takribani miaka 50" Hapa mbowe ana kila sababu ya kujitetea kwa sababu kauli yake inaonyesha wazi kuwa udhaifu wa Lowassa akiwa katika mfumo ule wa tawala chama ulikuwa umemuathiri kwa kiasi kikubwa..
 
"Sina ugomvi wala simchukii Lowassa binafsi" Hapa mbowe anaonyesha chuki yake dhidi ya chama na si Lowassa bali alimlaumu Lowassa kwa kutokutoa kauli yoyote juu ya madudu ya tawala chama ikiwemo kupitisha katiba mbovu.Na Lowassa hakuwa na uwezo wa kufanya mabadiliko akiwa ndani ya tawala chama sawa na mtu anayelizuia gari katika mwendo wake huku akiwa ndani ya hilo gari.
 
Hao wanaomtaka Lowassa ni wale wanaojua watanufaika binafsi..Kwa hapo inaonesha hata Lowassa angekuwa shujaa vipi,angefuata mfumo.Kwa sababu yeye ni sehemu ndogo ya mfumo basi ilikuwa ni lazima agonge mwamba.Kwa kumalizia ni kwamba,Lowassa aliye nje ya CCM ni mpya kwa sababu sasa hivi anaaimamia miguu yake miwili bila kutegemea mfumo na msukumo wa awali uliokuwa wakimfumo ndani ya tawala chama unatoka kwa wananchi wenye kutaka mabadiliko.Hapa ndipo kazi ilipo...yangu macho
 
"Huyu mtu yumo ndani ya mfumo wa ufisadi ulioiharibu nchi kwa takribani miaka 50" Hapa mbowe ana kila sababu ya kujitetea kwa sababu kauli yake inaonyesha wazi kuwa udhaifu wa Lowassa akiwa katika mfumo ule wa tawala chama ulikuwa umemuathiri kwa kiasi kikubwa..

Kuna ule usemi wa pwani, "Kila apendae huwa kipofu. Hata chongo ataita kengeza."
Naona ndg umehemkwa na kupenda
 
Ingekuwa nchi nyingine Mbowe alitakiwa kujiuzulu mara moja. MAANA hata wavuta bangi na walevi wasingemsikiliza. Nyerere alilazimika kujiuzulu maana ilikuwa kwake vigumu kukumbatia vyama vingi wakati siku zote alishabikia chama kimoja. SLAA kaamua kukaa pembeni maana alitueleza bayana Lowasa ni fisadi na ushahidi anao.
Hawa akina mbowe, lema, tundulisu ni wahuni kwa historia ndio maana wako tayari kusema kinyume na waliyoyasema mwanzo.
 
Wakuu nimepitia kumbukumbu zangu zote sijaona sehemu hata moja Mh.Mowe mweyekiti wa CDM akimtaja Mh. Lowasa kuwa ni fisadi. waliokuwa wakisimama hadharani bila woga walikuwa ni Katibu mkuu na viongozi wengine wa chama. kuna nini nyuma ya pazia?
 
Wakuu nimepitia kumbukumbu zangu zote sijaona sehemu hata moja Mh.Mowe mweyekiti wa CDM akimtaja Mh. Lowasa kuwa ni fisadi. waliokuwa wakisimama hadharani bila woga walikuwa ni Katibu mkuu na viongozi wengine wa chama. kuna nini nyuma ya pazia?

Nyuma ya pazia kuna Mlango
 
Alishasema hili,,, tena video zipo akiwaambia watanzania wanachoma moto wezi wa simu halafu wanamuacha lowassa anapita,, nikiipata hii video nitaiweka hapa...
 
Wakuu nimepitia kumbukumbu zangu zote sijaona sehemu hata moja Mh.Mowe mweyekiti wa CDM akimtaja Mh. Lowasa kuwa ni fisadi. waliokuwa wakisimama hadharani bila woga walikuwa ni Katibu mkuu na viongozi wengine wa chama. kuna nini nyuma ya pazia?

Mh. Mowe ni yupi tena huyo?? Kwani wewe umeshawahi kusimama hadharani na kumtaja Lowassa kuwa ni fisadi, ilikuwa wapi na lini na ni ufisadi upi uliuzungumzia?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom