Mbowe, Jipime kwa mustakabali wa CHADEMA, Kinusuru Chama

Nilidhani ni mchango toka kwa mwanachama mwenzetu, nadhani ingekuwa na maana zaidi ungesema "tumpe Profesa Safari uongozi"

Sasa shida ipo wapi? jamaa uwezo wake umefikia hapo,hamuwezi fanya mambo kwa namna ile ile kwa miaka zaidi ya 20 mkitegemea mabadiriko.
 
Siasa si kama unavyo bashiri maana hata zitto wakati anahojiwa alijitamba kusimamisha wabunge karibu majimbo yote lakini Mahimbo 264 kawa mbunge peke yake. Huko kubadilishia ndege angani ni kupigi?Lowasa kaleta hamasa kubwa kwa upinzani pia wazo la UKAWA limeonyesha mafanikio. Tumeona kwamba watu wakiamua mabadiliko yatatokea. Bunge likianza naamini mtasahau ya kampeni kama wengi waliopokea rushwa za wagombea na kusahau kuwa miaka 5 ilopita walifanya hivyo pia..
 
Upinzani utashamiri tu ikiwa katiba mpya itapatikana yenye kuondoa umungu mtu na tume huru ya uchaguzi na muungano ufumuliwe na kusukwa upya ikiwa bado twauhitaji anyway. Dola iongezewe watu wenye fahamu kwa kufanya intake zao zipate watu wenye pass za hali ya juu na siyo failures. Hapo ndiyo ubabe utakoma na uchaguzi utakuwa huru na haki..

Sioni kitufe cha "LIKE" pokea like za kutosha rafiki
 
Tatizo la muono mwembamba na mawazo finyu! Huna faida

Wewe kweli ni fyatu; tatizo la upinzani wa tanzania na ambao unauota wewe ni ule wa kwenda Ikulu mengine kwenu sio mafanikio. Mimi nahitaji upinzani wa kuanzia chini mashinani kwenye mizizi hadi kata hadi vijiji hadi jimbo hapo ndipo mikakati ya kuingia Ikulu ipikwe; naona hata watawala wa sasa wanasita kuiacha nchi mikononi mwa upinzani ambao haujajijenga madhubuti kushika dola. Hivi leo hii hao CDM wangeshinda wangepata wapi uongozi mzima wa taifa anzia wakuu wa wilaya, mikoa, wakurugenzi, mabalozi, makatibu wakuu mawaziri, manaibu, watendajiji ngazi mbali mbali nk? si ingekuwa kichekesho tungewekewa hata wanafunzi wa vyuo au wajumbe wa nyumba kumi kuwa wakuu wa wilaya? hebu upinzani ujijenge kama taasisi kwanza ipate hazina kubwa ya viongozi kisha itake kupewa dola; kutawala watu na maisha yao sio lelemama na wanaoondoka madarakani wanatafakari kwanza wamwachie nani nchi kwa maana moto wake wanaujua. Hivyo hoja hii kuhusu Mbowe ni ya kupuuzwa kwa kuwa inapapara za kuingiza upinzani Ikulu ilihali haujajijenga.
 
Baada ya uchaguzi huu Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe anapaswa kujiuzulu wadhifa wake kwani matarajio ya chama baada ya kubadili gia angani hayajafikiwa badala yake tumeambulia kupata wabunge na siyo kushinda; ni wakati sasa wa chadema kuwa na viongozi wapya
 
Kwa hiyo una maana ajiuzulu kwa sababu CDM haikushinda? Sababu za kutoshinda ni Mbowe? Hujui kuwa Lubuva alitangaza matokeo feki? Hilo huna imani nalo? Muache kuvuruga chama, tukae chini tujipange upya, si kufukuzana, kama vipi ondoka wewe.
 
Kwa hiyo una maana ajiuzulu kwa sababu CDM haikushinda? Sababu za kutoshinda ni Mbowe? Hujui kuwa Lubuva alitangaza matokeo feki? Hilo huna imani nalo? Muache kuvuruga chama, tukae chini tujipange upya, si kufukuzana, kama vipi ondoka wewe.

Kwanini aendelee kubaki na wakati ameshindwa kutuletea matumaini na mabadiliko tuliyotegemea?
 
haya ni maneno yako ama ulikopi na kupaste?
Ushauri wangu kwa viongozi wangu wa UKAWA ni kwamba wakae chini watafakari wakae na serikali ijayo wahakikishe kabla ya uchaguzi mkuu ujao wanapata tume huru ya uchaguzi na uwanja sawa wa uchaguzi ikiwamo matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani, zaidi wapiganie katiba mpya ya wananchi ili siku za mbeleni kusiwepo na kelele za kura kuibiwa maana kweli zinaibiwa sababu tume siyo huru wapinzani tuungane katika hili!
 
Baada ya uchaguzi huu Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe anapaswa kujiuzulu wadhifa wake kwani matarajio ya chama baada ya kubadili gia angani hayajafikiwa badala yake tumeambulia kupata wabunge na siyo kushinda; ni wakati sasa wa chadema kuwa na viongozi wapya

siyo kumwambia lubuva ajuzulu maaana ile pia ni kamati ya ushindi wa ccm ikiongozw na mwenyekiti wake lubuva
 
Kwanini aendelee kubaki na wakati ameshindwa kutuletea matumaini na mabadiliko tuliyotegemea?

kuna kitu katika hesabu za logic kinaitwa premise halafu kingine kinaitwa conclusion
huwezi kuwa na false premise then ukawa na conclusion ambayo ni true.
kwahiyo msingi wa hoja yako ni false halafu unalazimisha conclusion yako iwe true haiwezekani.
moja kwa moja mpaka ccm wenyewe wanajua kuwa matokeo ya urais ni ya kupikwa wazi halafu unataka mtu haukumiwe kwa kutumia matokeo ya kupikwa haiwezekani kutumia fraudulent results kumuhukumu mtu humtendei haki
 
Back
Top Bottom