Mbowe awapa somo wananchi jinsi ya kulinda kura zisiibiwe

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amewataka wapiga kura nchini kuanza kujiandaa na jinsi ya kulinda kura zisiibiwe siku ya kupiga kura.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Daraja Mbili Manispaa ya Arusha, alisema ni kila mmoja atambue umuhimu wa kulinda kura, kwa kuwataka kutokwenda umbali wa zaidi ya mita 102 toka kwenye kituo cha kupigia kura na kupiga kambi.

"Nawaomba akina baba ila wamama mkipiga kura nendeni nyumbani ngoma hii mtuachie wanaume, tutapiga kura tunahesabu hatua mia moja na tunaongeza mbili za ziada na kulinda kura na akijitokeza mwizi tunamkamata,'alisema.

Mbowe alisema mahali ilipofikia Tanzania bila ulinzi wa kura hakuna ushindi kwa upinzani kwani watu wanapiga kura lakini zinachakachuliwa kwa kutumia nguvu ya dola.

Mwenyekiti huyo alisema ana uhakika chama chake kitaibuka na ushindi katika kata zote zinazorudia uchaguzi kwa sababu wananchi walishachoka na propaganda za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aliongeza kuwa kwa sasa hakuna jipya CCM kwa sababu mbinu zao zote za kutenganisha watu kwa misingi ya ukabila na dini, imeshindikana na watanzania hawawezi kugawanywa kwa misingi hiyo.

Pia alilaani kitendo cha uongozi wa Arusha kufunga maeneo ya wazi na matokeo yake wanakosa maeneo ya kufanyia mikutano na kulazimika kuziba njia kwa ajili ya kuendesha kampeni hizo za udiwani Daraja mbili.

Kwa upande wake Meneja kampeni wa mgombea wa udiwani kata ya Daraja Mbili, ambaye amejiunga Chadema hivi karibuni akitokea CCM, Mzee Zakaria, alisema kinachoiondoa CCM madarakani siyo watu, bali ni kilio cha Watanzania kilichomfikia Mungu ambaye ameamua sasa kushughulika nao.

"Hiki Chama nilitaka kujiunga siku nyingi, lakini nikawa natafakari uwongo wa CCM kuwa kina udini, lakini nikaangalia bendera ya Chadema sikuona alama ya udini ya msalaba wala nyota na mwezi, nikagundua hizi
ni siasa chafu," alisema.

Zakaria alitumia mkutano huo, kunadai mgombea wa chama hicho kwa kuwataka watu kubadilika kama yeye, kwa kumpigia kura mgombea wa Chadema Prospere Msofe.

SOURCE: NIPASHE
 
Ili kudhibiti wizi wa kura inabidi ujue techniques za wizi wa kura.Magamba wanawatumia mawakala wa CDM kupika matokeo.Njaa na usaliti ni kitu kibaya sana.
Cha msingi ni kuwa na mawakala waadilifu,wazalendo,wasioendekeza njaa.
 
Ili kudhibiti wizi wa kura inabidi ujue techniques za wizi wa kura.Magamba wanawatumia mawakala wa CDM kupika matokeo.Njaa na usaliti ni kitu kibaya sana.
Cha msingi ni kuwa na mawakala waadilifu,wazalendo,wasioendekeza njaa.
mkuu nakuunga mkono asilimia zote
 
Ifanywe kama Arumeru Mashariki.

Kulinda sio wakati wa hesabu tu. Hata wakati wa upigaji, wakati wa ukusanyaji pia.

1. Toyo ziwe tayari
2. Hardtops pia kwa ajili ya sehemu korofi
3. Wananchi pia wakae tayari tayari
Kwa lolote ama chochote saa yoyote.
 
Ili kudhibiti wizi wa kura inabidi ujue techniques za wizi wa kura.Magamba wanawatumia mawakala wa CDM kupika matokeo.Njaa na usaliti ni kitu kibaya sana.
Cha msingi ni kuwa na mawakala waadilifu,wazalendo,wasioendekeza njaa.

MGOMBA; hujasema uongo! kitu kinachoikwamisha chadema ni kupeleka mawakala njaa. Inabidi kutumia muda wa kutosha kuangalia ni wakala gani ambaye yupo kwa maslahi ya chama na wala si kwa maslahi yake mwenyewe.
 
Sawa amefanya vizuri sana na nampongeza lakini angeanza na za chaguzi za ndani ya chama chake maana nakumbuka viti maalumu uchaguzi ulipofanyika baada ya kuona wanaowataka wameshindwa waliamua kuuvuruga na kutouitisha tena na kuamua kukaa yeye na mkwewe kuchagua majina ya ndugu na marafiki na kuwapa viti maalumu vya ubunge.
 
Back
Top Bottom