Hata upinzani nao ni wadhaifu, maana wasingekuwa dhaifu, hiyo serikali dhaifu ya kikwete isingekuwa madarakani.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
Kwahiyo ushauri wako nini, gari kwa ajili ya kiongozi wa kambi ya upinzani lipo kisheria na alichokataa ni gari la kifahari na sio gari la kumwezesha yeye kufanya kazi kama kiongozi wa kambi ya upinzani
Kuhusu posho wanachukua hawachukui mimi sioni shida hapo, suala je hoja haikutolewa kuwa posho ziondolewe ? unataka wafanye nini watu wanaambiwa hii ni sheria ukuisha saini lazima tunaingiza kwenye akaunti yako , alafu wewe ukitaka zichukue zipeleke kwa wapiga kura, sisi hatuwezi kuzirudisha , kosa lao ni lipi, try to think critically !
Wanabodi.
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, anawahadaa Watanzania.
Mbowe aliwahadaa Watanzania kwa kukataa gari la Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB), Lakini akageuka kwa mlango wa nyuma na kuchukuwa jipya.
Mbowe alisema ni kweli kuwa hivi sasa analitumia gari la KUB ambalo alilikataa kwa kipindi cha miezi sita.
Kuhusu kugomea posho ya Sh80,000 ya bunge na kuchukuwa posho ya Sh 2 milioni kwa mwezi kama KUB, Mbowe alisema ni stahili zake ambazo zimepangwa na Bunge.
SOURCE: MWANANCHI JUN 21 2012
source please! hatutaki majungu hapa.Mbowe wewe mwenyewe dhaifu ulisema unarudisha gari la bunge baadae ukalichukuwa kimya kimya.
Utendaji mbovu CCM hauwezi kukerebishwa kwa mgongo wa Mbowe. Bado mfumko wa bei uko juu, madaktari wanapanga kugoma, walimu nao wanapanga kugoma, deni la taifa linazidi kupaa, miradi ya barabari inanuka madeni, makampuni ya madini wanaendelea kuzoa madini na kupeleka utajiri kwao, wakulima wa pamba wako njia panda, korosho nako si shwari na kama haitoshi IPTL bado inatafuna TANESCO!
Hii kadhia/fedheha haitoondoka kwa Mbowe kukataa/kukubali gari.
Hivi wewe mtoa mada, umekosa kitu cha kuleta hapa jamvini Kinacholeta mvuto kwa wasomaji,halafu unatoa matapishi tu? Hatuhitaji mawazo mfu hapa.