Mbowe asita kususia posho

aziz_ally

Member
Dec 20, 2008
10
0
Kizitto Noya, Dodoma
KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema licha ya kurejesha kwa hiari gari alilopewa na serikali ataendelea kuchukua posho za ubunge nyinginezo anazopewa kutokana na nafasi hiyo ya uongozi.

Mbowe alisema hayo jana wakati alipotakiwa kujibu hoja zilizotolewa kwa nyakati tofauti na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ofisi ya Bunge zikimtaka aeleze kama ameamua kurejesha gari, basi aache pia kuchukua posho mbalimbali anazozipata kama mbunge na nafasi yake ya uongozi wa kambi ya upinzani.

Katika mahojiano na gazeti hili, Mbowe alingaka na kusema kuwa hayuko tayari kuacha posho anazopewa kwa vile zipo kisheria na ni muhimu katika kufanikisha majukumu yake."Naweza kusema kuwa huu ni upuuzi! Alingaka Mbowe alipoulizwa kama yuko tayari kufuata ushauri wa CCM na ofisi ya bunge.

Lakini, akaongeza: Kuna mambo mengi ya msingi tunaendeleaa kuyafanya. Unaposema niache na huduma zingine, ofisi ile inaendeshwaje?

"Mambo hayo (kuacha gari) tunayafanya kwa sababu tunaangalia pia ni kwa namna gani hayaathiri shughuli za kiofisi. Ukisema nisichukue Sh2 milioni kwa mfano, unataka ofisi hii iendeshweje?"

Alieleza kuwa ataendelea kupata huduma hizo kwa kuwa ni haki yake, hivyo kuzikubali au kuzikataa ni uamuzi wake na hashurutishwi na mtu.Wiki hii, Mbowe alitangaza kuacha kulitumia gari alilopewa na serikali kwa ajili ya shughuli zake kama kiongozi wa upinzani ikiwa ni mkakati wake wa kutekeleza kwa vitendo ushauri wa chama, CHADEMA wa kuitaka serikali itekeleze sera ya kuondoa malipo mbalimbali na posho zisizo na tija kwa watumishi wa serikali.

Tangazo hilo la Mbowe lilipokewa kwa kebehi na CCM pamoja na ofisi ya bunge juzi, wakimtaka asisusie gari tu bali pia na posho anazopata ili kuonyesha nia yake ya dhati ya kutekeleza mkakakti wa chama chake.

CCM ilimwita Mbowe kuwa ni mnafiki na mwongo anayetafuta sifa zisizo na msingi kwa ajili ya kuudanganya umma.Chama hicho tawala kilieleza kuwa kitendo cha Mbowe kukataa gari, mafuta na dereva wakati akiendelea kupokea huduma zingine ni unafiki uliovuka mipaka.

Nayo ofisi ya bunge nayo ilisema huduma zote anazopewa kiongozi huo wa upinzani zipo kisheria, hivyo hawezi kuikubali nusu na sehemu nyingine asiikubali.Juzi, Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Mashariki alisema kama kweli Mbowe anataka kubana matumizi, akubali na kurudisha posho za Sh 2milioni ambazo hupewa na serikali kila mwezi kwa ajili ya viburudisho pajoma na na Sh45 milioni alizopewa kwa ajili ya kununua gari.

"Mwezi huu amepokea Sh2 milioni kwa ajli ya viburudisho kwenye ofisi yake kama kiongozi wa kambi ya upinzani. Ninamwuliza na hizo nazo atazirudisha? na je, ataendelea kupokea au hatapokea?" alihoji Nchemba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Naye Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel kwenye mahojiano na gazeti hili alisema:"Haya ni mambo ya kisiasa na sisi kama watendaji hatutaki kujiingiza kwenye siasa. Lakini, niseme tu kwamba lile gari hakupewa kufanyia shughuli za kisiasa ni la serikali kwa ajili ya kazi zake kama kiongozi wa upinzani." "Wabunge wote wanaongozwa kwa masharti, Spika anayo yake, Kiongozi wa Upinzani Bungeni kadhalika na hata wabunge wengine nao wanayo masharti yao.

"Sasa, mtu hawezi kukubali masharti fulani na kukataa mengine. Huku ni kuvunja sheria."

Kwa mujibu wa Joel, moja ya masharti aliyopewa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Oktoba 25 mwaka 2010 ni kupokea gari la serikali, dereva na kuwekewa mafuta kwenye gari hilo wakati wa shughuli za bunge.

"Sasa pamoja na kupewa gari, ofisi ya bunge pia inawajibika kisheria kumpa kiongozi huyo nyumba mbili; Dar es Salaam na Dodoma na mlinzi Ili kuhakikisha usalama wake wa kila siku," alisema Joel.

Aliongeza,"Sasa akisema gari sitaki, huu ni utashi wake, lakini kwa nini akatae gari pekee wakati kuna huduma zingine anazopewa?"

Jumanne, baada ya kupitishwa kwa bajeti ya serikali, kambi ya upinzani ilitangaza mgogoro na bunge wa kutochukua posho za vikao kuanzia jana. Lakini, hilo lingefanyika baada ya kuwasilisha rasmi taarifa bungeni jana.

Hata hivyo, wakati kambi hiyo ikitoa msimamo huo wa pamoja, Mbowe alitangaza kurejesha gari alilopewa na serikali, dereva na kutochukua mafuta.Hatua hiyo ilielezwa pia ni sehemu ya uamuzi wa kuonyesha kutoridhishwa na hatua ya serikali kudharau mapendekezo yaliyotolewa na kambi hiyo katika kuiboresha bajeti ya mwaka huu wa fedha.

"Msimamo wetu kama kambi ya upinzani baada ya serikali kuyakataa baadhi ya mapendekezo yetu Kwa kukataa kuondoa sitting allowances (posho za vikao)," alisema Mbowe na kuongeza:

" Serikali haikukubaliana nasi pia kuuza magari ya anasa (mashangingi), kuondoa misamaha ya kodi kwenye kampuni za madini na kupunguza gharama za kuwasafirisha viongozi wa umma daraja la kwanza."

"Sisi tunaamini kuwa viongozi wanaopaswa kusafirishwa kwa ndege katika daraja la kwanza ni rais na mke wake, makamu wa rais na mkewe, waziri mkuu na mke wake, Spika wa Bunge na mwenza wake.

Halafu mawaziri wanapaswa kusafiri kwa busines class (daraja la kati) na wabunge wote, economy (daraja la watu wa kawaida)."

Kwa sababu hiyo, Mbowe alisema atawasilisha barua ofisi ya Bunge kuijulisha kuwa wabunge wote wa kambi rasmi ya upinzani hawataachukua posho.

Alisema ataitaka ofisi hiyo iandae fomu mbili bungeni; ya mahudhurio ya wabunge na fomu za malipo ya posho ili wao wasaini hiyo ya mahudhurio.Alisema pia kuwa kuanzia siku hiyo ahlitaki tena gari alilopewa na serikali kwa kuwa mkakati wa upinzani ni magari yote ya kifahari, likiwepo alilopewa, kuuzwa na fedha zitumike kwa ajili ya kupambana na kero za wananchi.

Hata hivyo, pamoja na ahadi hiyo, Joel alithibitisha kwamba Ofisi ya Bungte haijapokea barua yoyote kutoka kwa kambi hiyo ya upinzani katika kutekeleza ahadi yao.Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya upinzani Bungeni, Tundu Lissu alidai kuwa tayari Mbowe amerejesha gari tangu Jumatatu lakini akakiri kuwa bado hawajaandika barua kama walivyoahidi.

"Ni kweli barua hatujapeleka ila itapelekwa kesho, lakini tayari Mbowe amerudisha gari hilo tangu juzi (Jumatatu) na ameanza kutumia usafiri binafsi," alisema Lissu

Source: Mwananchi
 
Mbowe kweli ni mnafiki na muongo sana, kama kweli anayo dhamira ya kweli mbona anachagua posho kama umeamua kususia posho usichukue posho yoyote Wachagga kwa pesa!! Endelea kuwadanganya Pro-Chadema-JF, ndio wengi wana upofu wa fikra
 
Ccm wendawazimu wote, hapa hoja ni kubana matumizi na si kuacha matumizi, matumizi hayakwepeki.
 
akili ya kitoto hiyo kujadili makabila, huyu Membe naye ni Mchaga? Huo upofu wako ni hatari, hoja hapa ni alichokifanya, ni kibaya au kizuri? Bora huyu aliyethubutu kuliko nyie mnaokula kwa kutumia mikono na miguu, mnakula kuku mnafakamia mpaka miguu na utumbo.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Ccm wendawazimu wote, hapa hoja ni kubana matumizi na si kuacha matumizi, matumizi hayakwepeki.

Soda na chai kwa wageni wa KUB ni Tshs. 2,000,000.00 kwa mwezi na kwa mwaka Tshs. 24,000,000.00!! Wakati kima cha chini ni Tshs. 120,000.00 kwa mwezi na mwaka ni Tshs. 1,440,000.00 kwa Mtanzania wa kawaida! Jamani jamani kama kweli Mbowe ana huruma kwa Watanzania akatae hii pesa ya viburudisho ofisini kwake. Hii ni kufuru kabisa tena dhihaka kwa watanzania wanaopata kima cha chini! Yaani Kiongozi wetu anatumia mara mbili ya pesa unayopata kwa mwaka kwa ajili ya kuwanunulia wageni wake soda kwa mwezi mmoja tu!!
 
Mbowe kweli ni mnafiki na muongo sana, kama kweli anayo dhamira ya kweli mbona anachagua posho kama umeamua kususia posho usichukue posho yoyote Wachagga kwa pesa!! Endelea kuwadanganya Pro-Chadema-JF, ndio wengi wana upofu wa fikra

'WaChagga kwa pesa' ina maana kabila nyingine wote hawatafuti pesa? Wabunge waliotetea kuendelea kulipwa posho na wengine kudai iongezwe wote ni waChagga?! I bet you look exactly like your avatar...because that face really suits you!
 
Watu wenye magamba hujulikana tuu. Mbowe anastahili sifa na heshima kwa dhamira yake ya kutaka kupunguza matumizi ya serikali. Huyo katibu wa bunge mnafiki. Mbona hakumkashifu Pinda alipokataa shangingi? Au shangingi la Pinda halikutolewa kisheria kama la Pinda? Mbona Pinda huduma zingine anazitumia ila gari amekataa?
 
..mbona Mwalimu Nyerere alihama Ikulu kwenda kuishi kwenye nyumba yake msasani?

..mbona Salim Salim alipoteuliwa Waziri Mkuu hakuhamia kwenye nyumba ya serikali bali aliendelea kuishi nyumbani kwake masaki?

..kama Mbowe ameamua hataki kutumia gari la serikali sidhani kama ni kitu kibaya. watendaji wa bunge wanakosea wanapomlazimisha aachie na mafao mengine kama ofisi, na posho.
 
mkubwa kashikwa pabaya...... ngoja tuone utetezi!
alianza vizuri nami nilimsapoti, ila hili "VIBURUDISHO" hapana
 
Mbowe kweli ni mnafiki na muongo sana, kama kweli anayo dhamira ya kweli mbona anachagua posho kama umeamua kususia posho usichukue posho yoyote Wachagga kwa pesa!! Endelea kuwadanganya Pro-Chadema-JF, ndio wengi wana upofu wa fikra
wewe ndio una upofu wa fikra. Ndio maana unaleta habari za ukabila. Upuuzi!
 
mkubwa kashikwa pabaya...... ngoja tuone utetezi! alianza vizuri nami nilimsapoti, ila hili "VIBURUDISHO" hapana
Acha Unafiki kijana acha kutaka kuonyesha kwamba kitendo cha Mbowe kuacha Shangingi ni jambo jepesi,Waambie Magamba nao waachie mashangingi kwanza halafu ndiyo tuanze kuhoji fedha za viburudisho vya ofisi ya Mbowe!!! Uamuzi huo ni wa kizalendo,Ofisi zinaweza kuendeshwa bila magari ya kifahari!!! That is a patriotic decision,Wajibu hilo kwanza Ccm kama wana ubavu!!!!
 
Dhana nzima ya matumizi ya magari na posho inapotoshwa. Kimsingi Mbowe hajakataa kutumia gari la serikari kwa matumizi ya ofisi ya kiongozi wa upinzani, na pia dhana siyo kukaata mawaziri au viongozi kutotumia magari. Swala hapa ni aina ya magari ambayo viongozi wanapenda kuyatumia, magari ya gharama kubwa ukilinganisha na hali halisi ya uchumi wa nchi. Kama unasema wewe ni nchi masikini, huna pesa, kwa nini ununue au uendekeze matumizi ya anasa? Kuna ulazima gani kiongozi anayeishi Dar-es-Salaam kutumia gari la sh. 200m. Hivi viongozi wakipewa magari ya gharama nafuu kama RAV4 ambayo gharama yake haizidi 50m kuna ubaya gani. Hadhi ya nchi kiuchumi ni maskini lakini viongozo wake wanajishebedua kuwa na hadhi ya kitajiri. Ndio maana kila mkubwa serikalini na kwenye mashirika ya umma mpaka mameya wa kwenye halmashauri eti wanataka magari yenye hadhi kama VX8 n.k yenye kugharimu mamilioni ya shilingi. Mbona wanapoachia madaraka au kustaafu hawendelezi hizo hadhi walizokuwanazo walipokuwa wanashikilia ofisi za umma, badala yake wananunua Mark II na magari mengine ya bei ndogo?

Suala la posho kwa kiongozi wa kambi ya upinzani ni kwa ajili ya uendeshaji wa hiyo ofisi kama stationaries, printing n.k. Sasa asipochukua hizo ofisi itaendeshwaje?
 
Mbowe kweli ni mnafiki na muongo sana, kama kweli anayo dhamira ya kweli mbona anachagua posho kama umeamua kususia posho usichukue posho yoyote Wachagga kwa pesa!! Endelea kuwadanganya Pro-Chadema-JF, ndio wengi wana upofu wa fikra

Una maana mamayake ndo alikuambia Mbowe ni mchagga.
 
Naanza kupata masha juu ya mpiganaji wetu kumbe mambo yenyewe yako hivi?
Kwanini watu mnakosa msimamo kiasi hiki?
Ishu ni Mbowe au kuipunguzia serikali mzigo wa gharama?
Hamuoni kuwa mbowe ni mzalendo wa juu sana kwa kitendo alichofanya?...tungekuwa msitari mmoja katika uelewa hii thread isingwekuwa subject-matter!
 
Jamani tuwe waelewa: CDM wanaposema kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima maana yake siyo kufuta kila kitu. Amerudisha gari kwa sababu haoni haja ya kuwa na magari mawili, moja la Ubunge na jingine la KUB ambalo gharama zake zote zinalipwa na kodi za walala hoi. Ndo maana kaamua alirudishe lipigwe mnada. Angalau amefanya hilo.

Sasa hao wanaosema ni mnafiki wanataka aifunge na hiyo ofisi au? Maana yeye kaanzisha, tena kwa mfano, sasa na nyie onyesheni kwa mfano ni eneo gani la kupunguza matumizi ya serikali.

Kwa mfano Mawaziri wote wana Magari mawili mawili, la ubunge na la uwaziri, wateme moja wapo kama kweli wana uzalendo. Pinda alilikataa VX lake yeye hakuitwa mnafiki. Hatujaambiwa kama PM alifuta posho ya ofisi yake ya chai na viburudisho vya wageni. Sasa mnataka Mbowe akatae na posho ya ofisi ya KUB!! Nyie mmefanya lipi??
 
NINANUKUU...... "Soda na chai kwa wageni wa KUB ni Tshs. 2,000,000.00 kwa mwezi na kwa mwaka Tshs. 24,000,000.00!! Wakati kima cha chini ni Tshs. 120,000.00 kwa mwezi na mwaka ni Tshs. 1,440,000" MWISHO WA KUNUKUU
 
Dhana nzima ya matumizi ya magari na posho inapotoshwa. Kimsingi Mbowe hajakataa kutumia gari la serikari kwa matumizi ya ofisi ya kiongozi wa upinzani, na pia dhana siyo kukaata mawaziri au viongozi kutotumia magari. Swala hapa ni aina ya magari ambayo viongozi wanapenda kuyatumia, magari ya gharama kubwa ukilinganisha na hali halisi ya uchumi wa nchi. Kama unasema wewe ni nchi masikini, huna pesa, kwa nini ununue au uendekeze matumizi ya anasa? Kuna ulazima gani kiongozi anayeishi Dar-es-Salaam kutumia gari la sh. 200m. Hivi viongozi wakipewa magari ya gharama nafuu kama RAV4 ambayo gharama yake haizidi 50m kuna ubaya gani. Hadhi ya nchi kiuchumi ni maskini lakini viongozo wake wanajishebedua kuwa na hadhi ya kitajiri. Ndio maana kila mkubwa serikalini na kwenye mashirika ya umma mpaka mameya wa kwenye halmashauri eti wanataka magari yenye hadhi kama VX8 n.k yenye kugharimu mamilioni ya shilingi. Mbona wanapoachia madaraka au kustaafu hawendelezi hizo hadhi walizokuwanazo walipokuwa wanashikilia ofisi za umma, badala yake wananunua Mark II na magari mengine ya bei ndogo?

Suala la posho kwa kiongozi wa kambi ya upinzani ni kwa ajili ya uendeshaji wa hiyo ofisi kama stationaries, printing n.k. Sasa asipochukua hizo ofisi itaendeshwaje?

Mkuu labda watoa habari wametudanganya. Mimi nilimsikia Lukuvi akisema ni entertainment allowance na mwingine ametuambia hapo kwamba ni pesa ya viburudisho (entertainment). Kwa mantiki hiyo unataka kutuambia hapa kwamba stationeries, printing, n.k ni viburudisho? Ingekuwa wamesema Office Running Cost ningeelewa lakini viburudisho? kwangu stationeries, printing, n.k siyo viburudisho.
 
Uellewa mdogo kwa magamba,kupunguza posho zisizokuwa na tija.zile za msingi ni muhimu kufanikisha maendeleo au ufanisi.mlitaka atumiemshahara wake kuendesha shughuli za ofisi kama kiongozi wa kambi ya upinzani?
 
NINANUKUU...... "Soda na chai kwa wageni wa KUB ni Tshs. 2,000,000.00 kwa mwezi na kwa mwaka Tshs. 24,000,000.00!! Wakati kima cha chini ni Tshs. 120,000.00 kwa mwezi na mwaka ni Tshs. 1,440,000" MWISHO WA KUNUKUU

Mkuu kuna makosa hapo nini? Tuambiane tu ndio uungwana. Au unashangaa au unasisitiza?
 
Back
Top Bottom