nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
[h=2][/h]JUMATATU, APRILI 16, 2012 05:42 NA BAKARI KIMWANGA, DAR ES SALAAM
Atishia Chadema kwenda mahakamani
Mrema alia wapinzani kupewa kiti kimoja
WAKATI Bunge likitarajia kuwachagua wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kesho, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe amemvaa Spika wa Bunge, Anne Makinda akimtaka atumie busara katika suala zima la mgawanyo wa viti hivyo.
Mbali na hatua hiyo, Mbowe amesema kama haki haitatendeka, Chadema kitakwenda katika Mahakama ya Afrika Mashariki, kudai haki zaidi.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Mbowe alimtaka Spika Makinda kutumia busara katika jambo hilo, kuliko kutumia ubabe ambao utakuwa hauna tija na maslahi kwa taifa.
Alisema ni vema ikaeleweka, uwakilishi katika Bunge la Afrika Mashariki huendana sawa na vyama vilivyo na wabunge na si vinginevyo.
Tuamini jambo hili ni la kutumia busara na imani yangu, kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, tutalizungumza kupitia vikao vyetu vya ndani ili kufikia muafaka. Itakuwa hakuna tija kama wakingangania kufanya uchaguzi huu, huku vyama vya upinzani vikipewa kiti kimoja cha uwakilishi.
Hii si haki hasa kwa nchi kama Tanzania ambayo viongozi wake wa taifa, wamekuwa wakitumia muda mwingi kuhubiri kukua kwa demokrasia, lakini yanapofika masuala ya kitaifa, wanashindwa kutoa haki.
Ikiwa wataendelea na uchaguzi huu, bila kulipatia ufumbuzi sakata hili, basi kwa uongozi wetu CHADEMA, tutatumia vyombo vya nje ikiwemo Mahakama ya Afrika Mashariki kudai haki hii ya msingi vya vyama vyetu vya upinzani.
Pale Uganda, Chama cha DP kilingangania jambo hili na kufanikiwa kwenda kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki na kufungua kesi, siku ya mwisho kikashinda, sasa iweje sisi tufumbie macho,
MREMA NAYE AIBUKA
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Dk. Agustine Mrema, alisema sasa umefika wakati kwa Spika Makinda, kutumia nafasi yake walau kutoa nafsi mbili kwa kambi ya upinzani, kuliko kuwa na nafasi moja kama ilivyo sasa.
Hili suala limefikishwa kwake Spika, nianachojua Mama Makinda ni mtu ambaye anaamini katika demokrasia, acha tusubiri busara zake katika hili kwanza. Ila kwa maoni yangu ingekuwa vizuri kambi ya upinzani, ikapewa nafasi mbili, badala ya moja kama ilivyo sasa.
Hili linawezekana, ila ninaomba tumuachie yeye kwa sababu ni kiongozi imara na anayezingatia demokrasia ndani na nje ya Bunge letu, alisema Mrema.
Wiki iliyopita,Chadema ilitangaza kupinga uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutokana na mchakato unaoendelea kutokuwa huru na haki.
Kutokana na hali hiyo, chama hicho kilimtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda, Katibu wake, Dk. Kashilillah na Serikali kuchukua hatua za haraka kurekebisha kasoro zilizojitokeza, ili kuhakikisha uchaguzi huo unawezesha wabunge kupatikana kidemokrasia na kwa kuzingatia maslahi ya umma.
Katika uchaguzi huo, CCM ina nafasi ya wagombea nane na vyama vya upinzani mgombea mmoja.
CHADEMA kilidai kulingana na idadi ya wabunge wa CCM kuwa 258, chama hicho kilistahili kupata viti visivyozidi saba, lakini wamepewa viti nane, huku vyama vya upinzani kwa ujumla wake vimepewa kiti kimoja.
CHADEMA, ilisema kwa kuzingatia ibara ya 50 ya mkataba wa Afrika Mashariki na uwakilishi wa vyama vyenye wabunge, CCM ilistahili kupata viti visivyoziti saba, Chadema chenye wabunge 48, kilistajili kupata kiti kimoja na chama cha CUF chenye wabunge 36 kilistahili kupata kiti kimoja.
.kule kuna vyama kama hapa Tanzania, walipunjwa viti kama tunavyofanyiwa, ninapenda ieleweke lengo si kwenda mahakamani, Spika pamoja na katibu wake, watatumia busara ili kulimaliza jambo hili bila kuadhirisha uchaguzi baada ya kuonekana una doa. Ni vema walau kati ya viti tisa, tungepewa viwili kutokana na uwiano wa vyama vyenye wabunge ili kuleta usawa na taswira sahihi, alisema Mbowe.
SURA ZA HABARI HII |
---|
Mbowe amvaa Spika Makinda |
MREMA NAYE AIBUKA |
Habari Yote |
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe
Spika wa Bunge, Anna Makinda
Amlalamikia uchaguzi wa ubunge Afrika MasharikiAtishia Chadema kwenda mahakamani