Mbowe akamatwa na polisi

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
Mbowe1(8).jpg

Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe

Polisi wamkamata Mbowe, ahaojiwa na kuachiwa

Mbunge wa Hai (Chadema), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, jana alishikiliwa na jeshi la polisi kwa takribani robo saa kwa mahojiano baada ya kupiga fataki katika maadhimisho ya miaka 50 ya kuzaliwa kwake bila kuwa na kibali cha kupiga fataki hizo.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa nne usiku katika ofisi za Hai Kilimanjaro Development Initiative ambapo alifanya tafrija ya kujipongeza kwa kutimiza miaka hiyo ya kuzaliwa kwake na ndipo askari walipofika na kumchukua kwa ajili ya mahojiano.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi, ni kwamba mbunge huyo alifanya hivyo kinyume na taratibu na pasipokuwa na kibali kutoka kwa jeshi hilo.

Taarifa hizo zilieleza kwamba baada ya kuhojiwa kwa muda, Polisi walimwachia. Kwa upande wao, wananchi waliozungumza na NIPASHE, walilaani kitendo cha polisi kumkamata mbunge huyo na kusema kuwa ni kumnyanyasa kisisasa na kumyima uhuru wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

John Mbowe na Mama Salama, waliliambia gazeti hili kuwa kitendo hicho ni cha kumdhalilisha na kulidhalilisha jeshi hilo kutokana na ukweli kuwa kupiga fataki tena katika maeneo ya wazi si kosa na kuongeza kuwa wapo watu wengine wamekuwa wakipiga fataki na hawakamatwi.

Kwa upande wake, Mbowe hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo kutokana na kuwa na shughuli nyingi ambapo alikuwa akielekea kwenye harambee ya kuchangia upanuzi wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), usharika wa Nshara.

Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi wilaya ya Hai, Revocatus Malin ili azungumzie tukio hilo, ziligonga mwamba kutokana na kutokuwepo ofisini wakati Kamanda wa polisi mkoani hapa, Absalom Mwakyoma hakupatikana kwenye simu yake ya mkononi.

Nipashe
 
Ni Tanzania tu ambapo watu wanajifanyia mambo ovyo ovyo. Si haki kwa mtu kukupigia fataki saa nne usiku bila taarifa
 
Lol! Serikali hii kwa visa utadhani mama mkwe! Wale wahindi walikuwa na sikukuu sijui ya nani huko wakapiga fataki hadi watu wakadhani imekua zamu ya mabomu ya kigamboni kulipuka; walichukuliwa hatua gani? Double stds at work,lol
 
Ni kweli ilitakiwa awe na kibali........hamna kudhalilishana wala nini kibali muhimu.
 
Ndiyo maana Pol ISI hupewa jina wao na wale wanaowafuga (rafiki ya mwindaji na kitoweo cha watu wa Iringa).
Mbona wale waliopiga fataki siku ya diwali bila kibari hawakuhojiwa? Mbona wale wahindi wanaopiga fataki beach usiku hawakamatwi?
 
Polisi wamkamata Mbowe, ahaojiwa na kuachiwa

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi, ni kwamba mbunge huyo alifanya hivyo kinyume na taratibu na pasipokuwa na kibali kutoka kwa jeshi hilo.

Nipashe

Hivi kinyume na taratibu ni uvunjaji wa sheria.. nilitegemea wangesema amevunja sheria no. flani sio kuja na hija zisizo za msingi.
Ukweli nikwamba jeshi la polisi limejisahau, kama kupiga fataki ni kosa mbona zinauzwa madukani kiholela na kila mwenye uwezo anajinunulia na kuzipiga atakavyo?? Siku mambo yatabadilika nchi hii ndio watajua jukumu lao kwa raia.
 
Ni Tanzania tu ambapo watu wanajifanyia mambo ovyo ovyo. Si haki kwa mtu kukupigia fataki saa nne usiku bila taarifa
Taratibu zinasema kwamba ukitaka kupiga fataki ni lazima kutoa taarifa polisi ili upewe kibali.
Hazisemi ukawaambie majirani.

Stuka.
 
Lol! Serikali hii kwa visa utadhani mama mkwe! Wale wahindi walikuwa na sikukuu sijui ya nani huko wakapiga fataki hadi watu wakadhani imekua zamu ya mabomu ya kigamboni kulipuka; walichukuliwa hatua gani? Double stds at work,lol

Sheria za nchi zinataka kuomba kibali serikalini, una uhakika hao Wahindi hawakuwa na kibali?

Hatua zilizochukuliwa kwa Mbowe zinaweza kuwa ni extreme lakini naye alikiuka sheria za nchi pamoja na kanuni za kibinaadamu tu. Huwezi kuwafanyia watu ghasia saa nne usiku bila ya taarifa
 
Taratibu zinasema kwamba ukitaka kupiga fataki ni lazima kutoa taarifa polisi ili upewe kibali.
Hazisemi ukawaambie majirani.

Stuka.

Kimsingi ni kuwa, anaekupa kibali ndie anaetakiwa kutoa taarifa kwa majirani kuwa kutakuwa na jambo kadha wa kadha
 
Hivi kinyume na taratibu ni uvunjaji wa sheria.. nilitegemea wangesema amevunja sheria no. flani sio kuja na hija zisizo za msingi.
Ukweli nikwamba jeshi la polisi limejisahau, kama kupiga fataki ni kosa mbona zinauzwa madukani kiholela na kila mwenye uwezo anajinunulia na kuzipiga atakavyo?? Siku mambo yatabadilika nchi hii ndio watajua jukumu lao kwa raia.

Nimekupata sana hapa una point. Kama fataka haziruhusiwi ila kwa kibali cha polisi basi hata kuzinunua ingetakiwa kwa vibali kama ilivyo kwa silaha. Kwa mtazamo huo polisi hawajui nini maana ya tofauti ya sheria na taratibu.
 
Kimsingi ni kuwa, anaekupa kibali ndie anaetakiwa kutoa taarifa kwa majirani kuwa kutakuwa na jambo kadha wa kadha
Taarifa polisi inasaidia nini kama watakaosumbuliwa hawatapewa taarifa ya usumbufu tarajiwa?
hizi sheria na taratibu zisizo na maana hazitakiwi, polisi wanaotaka watu wafuate sheria wakati wao hawatimizi wajibu wao ni upuuzi.
 
Back
Top Bottom