Mbowe ajisalimisha polisi; ahojiwa na kuachiwa

kwa nini wabunge wote wa chadema wasiende arusha wawekwe magereza ili dunia nzima ijue nini kinatokea waone namna yakutusaidia

ni wabunge wachache toka cdm wenye roho kama ya lema usifikiri ni rahisi kulala sakafuni na kunyea kwenye ndoo halafu nyumbani kwenu kuna kila aina ya starehe..mungu ibariki arusha mungu ibariki tanzania.
 
Wanazidi kuchochea mgogoro kuwa mkubwa badala ya kuupunguza,mahakama ya Arusha itabadilika kuwa ndio mahakama rasmi ya kesi za Chadema maana mpaka sasa wana kesi nyingi sana na hakuna hata moja ambayo imeisha, na kwa utaratibu wa mahakama na polisi kwa ujumla kesi hizi hazitakwisha na zitachukua kipindi kirefu sana na kuufanya mkoa wa Arusha kuwa na vuguvugu wakati wote wa kesi hizi.

Nenda Mbowe nawe wakupe kesi yako maana inawezekana wakaja na yako mpya ya kukimbia mkono halali wa Polisi.
Akifika watamfungulia kesi ya kuzungumza redioni bila kibali cha police. Tehe, hao ndio police wa magamba bana!
 
Ameendelea kusema kuwa,hao wanaosema ametoroka na hapatikani wanamtafutia nini?mbona juzi walivyotaka akawaondoe watu polisi walimpgia simu?mbona simu yake iko hewani na hawajasema wanamtafuta sasa hivi?kasema huyu mkuu wa mkoa mpya arusha magesa anajua nini kuhusu arusha?kwani wananchi wangapi wamemchagua na kwa kura ngapi?au ni kwa kupewa kazi tu na kikwete?amesema yeye hategemei kupewa kazi na mtu yeyote serikalini na kwamba anajiamini
Kweli jamaa ni mazuzu hasa, ni kweli kabisa baada ya kuona hali mbaya pale mahakamani walimwita Mbowe na kumsihi awaombe watu waondoke pale Mahakamani. Na kama vile wanatii amri ya Rais, watu wale waliondoka kwa nidhamu ya hali ya juu.
Hii inaonyesha nini? Polisi kwa watu wa Arusha sii mamlaka halali tena.
 
samahani mbona sijawahi kusikia radio Arusha tangu nizaliwe ?

Kwa kile kilichosemekana,kwamba mh.mbowe amekimbia viwanja vya nmc wakati polisi walipovamia.Mbowe mwenye amekanusha kauli hiyo anasema hawezi kujificha wala kukimbia polisi, kwa sababu yeye haogopi polisi wala magereza,bali alitoka kwenda kufanya kazi aliotakiwa kufanya kwa muda ule.Ameendelea kusema kuwa mgogoro unaondelea arusha unatokana na uchaguzi wa meya uliofanyika november mwaka jana!anaendelea kuzungumza
Source radio arusha 94.8 fm
 
Anaendelea kusema atafanya maamuzi magumu,na sasa anaelekea polisi.
My Gosh...anataka kuamua nini tena?
Kweli serikali hii ya ccm inataka kutuweka roho juu kila wakati!
Mi nadhani wanaharibu equilibrium ya wabunge wa cdm ili wapitishe mambo FULANI kule BUNGENI bila ya upinzani wowote!..ndio hasa nia yao!
 
Huyu jamaa bure kabisa, kwanini asingejitokeza jana ile ile.
 
Au Sun Rise Radio siku hizi imebadilisha jina inaitwa radio Arusha?

Kwa kile kilichosemekana,kwamba mh.mbowe amekimbia viwanja vya nmc wakati polisi walipovamia.Mbowe mwenye amekanusha kauli hiyo anasema hawezi kujificha wala kukimbia polisi, kwa sababu yeye haogopi polisi wala magereza,bali alitoka kwenda kufanya kazi aliotakiwa kufanya kwa muda ule.Ameendelea kusema kuwa mgogoro unaondelea arusha unatokana na uchaguzi wa meya uliofanyika november mwaka jana!anaendelea kuzungumza
Source radio arusha 94.8 fm
 
My Gosh...anataka kuamua nini tena?
Kweli serikali hii ya ccm inataka kutuweka roho juu kila wakati!
Mi nadhani wanaharibu equilibrium ya wabunge wa cdm ili wapitishe mambo FULANI kule BUNGENI bila ya upinzani wowote!..ndio hasa nia yao!

usiwe na wasiwasi, hana uwezo wa kuchukua uamuzi wowote mgumu. Jeshi limejipanga kikamilifu. Wajaribu tena waone.
 
Kuna jamaa zangu wapo Arusha nimeongea nao jana kwa njia ya simu, anasema wana Arusha wamesema "HAWADANGANYIKI TENA".
 
Kashajisalimisha sasa anahojiwa na Kamanda Simon Siro...Ila katika mkutano wake amesema yeye ahofi wala haogopi polisi kaahidi kufanya maamuzi magumu na mazito pindi atakapofikishwa mahakamani
 
samahani mbona sijawahi kusikia radio Arusha tangu nizaliwe ?

Kama upo Arusha Tune 94.8 utajua ni Station gani. Hoja siyo radio gani hoja ni mbowe kuzungumza na waandishi wa habari ikiwepo hiyo radio.
 
Hili lako naona ni suala la msingi sana kinachotakiwa ni kwamba sasa dunia ielewe CDM wanachokifanya kwa wakati huu na sio tena zile siasa uchwara za kila siku.
 
Hivi hawa wakuu wa mikoa wana tofauti gani na vibaraka enzi za ukoloni au hawa viongozi vilaza wa Africa wa zama hizi? Huu mfumo ni wa kikoloni na wa kishenzi sana.................

Vijana hima tudai katiba mpya na tuondoe vijana wenzetu kuendelea kuwa tegemezi kwa kuwa walamba viatu kwa wanaojiita watawala.. Mkuu wa Mkoa anaenda mahakamani kabla ya kesi??

Huu ni ujinga kabisa halafu bado anatoa mikwara......... najaribu kupima ushawishi wa mkuu huyo na Mbowe et al nagundua akili zake hazina tofauti na vilaza wengine .............
 
Back
Top Bottom