Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

ila ukiangalaia toka Mwaka 1996 wameombwa walipe deni ila hawajaonesha ushirikiano.Na kama ni hivyo basi na watu waliochukua za EPA warudishe bila kushtakiwa kama mtakavyo Mbowe asishitakiwe.

Suala la pili tunata kujua mazingira ya Mbowe kupewa mkopo NSSF,Je kulikuwa na Fair Game au ??hili ni suala ambalo tunahitaji kulijua.

though Mwandishi hakuupa upande wapili utoe Maelezo,ila tunahitaji kufahamu vizuri suala hili.tuseianza kuupanda Upinzani kumbe ndio hao hao!!

watu watasema apewe muda wa kulipa, wakati hii ishu ni tokea 1996 ! hadi sasa anasubiri nini ?? hii ishu itaexpand kwenye magazeti, kibanda kitawaka moto !
 
Ulimwenguni kote matajiri wanakopa.Hukusoma hata H CLINTON kakopa? Hii si hoja.Tunataka tuambiwe kachota kinanma ya ufisadi.Mbowe amekopa ,akaahidi kulipa.A VERY open and transparent busines deal.Unalinganishaje na ufisadi wa RICH-MONDULI ah sorry RICHMOND.You are not serious. Tuwe makini na deception kama hizi,they are just decoys to divert agenda ya UFISAAADI !!
SORRY TUNAFAHAMU KUSOMA NA KANDIKA.Unayejaribu kutuyumbisha ulaaniwe.

ni kweli kabisa alaaniwe ! Maana mbowe hadi leo anatufanya hatujui kusoma na kuandika namba especially hayo mabilioni !
 
Asante sana mkuu CHUMA,
Mimi naona hilo ndio suala la msingi kabisa kulijadili na pengine kugoma kulipa MPAKA KIELEWEKE alikofanya Bw.Mbowe ndio kutatuzindua juu ya ukweli kama viwango vya RIBA katika mabenki ya Bongo na hiyo mifuko yetu ya jamii kweli vinaweza kufanya mikopo hiyo ikawasaidia wananchi kujiinua kiuchumi au ni wizi wa mchanamchana?
Mbowe hastahili kutetewa kama hana sababu za kutolipa deni hilo.Lakini narudia tena ,kumwita Fisadi mtu aliyefuata utaratibu wa wazikabisa kukopa fedha na aka chelewa kulipa ni upotoshaji wa maana ya neno lenyewe, Au ni kujiridhisha tuu kwa baadhi ya watu kuwa "Tunajibu mapigo"
Mafisadi ni wale wanaotumbua fedha zetu kwa siri wakiulizwa wanakataa katakata, mpaka serikali iunde tume na kutumia fedha zingine nyingi kufichua yale waliyokataa ndio kwa shingo upande wanajiuzulu au kuingia mitini.
Tukubali ukweli.

Lakini kama alitia saini na kukubaliana na maelezo ikiwemo riba, tatizo liko upande wa nani ??
 
Huyu anadaiwa kihalali na alikopa mchana kweupe 1990.
Wale waliokopa miaka iliyofuatia bila interest na hawalipi mbona majina yao hayapo hapa?

Hivi hili deni lilikuwa linasubiri aseme ndipo litolewe?

Naona kuna kila aina ya Hila za Mzee fisi kwenye hili.

Mimi kwngu sioni shida kuhusu hilo deni.

Club ya Bilicanas ipo pale na makaratasi yote ya mkataba wanayo sasa wanasubiri nini?

Hiyo kitu ni Ufisadi kweli au imelazimishwa?

Utashangaa atakachosema Mbowe ! asingekumbushwa nafikiri asingelipa ! fisadi mwingine kumbe tokea longi !
 
ni kweli kabisa alaaniwe ! Maana mbowe hadi leo anatufanya hatujui kusoma na kuandika namba especially hayo mabilioni !

Pesa aliyokopa Mbowe haina uhusiano wowote na utendaji wa Serikali. Hata NSSF kama wangekuwa wanaihitaji haraka na sio kuwa wanataka aendelee kukaa nayo ili wavune faida, wangekuwa wameshalinadi jengo la Bilcanas.

MAFISADI NI WALE WANAOIBA PESA YA SERIKALI KUPITIA BOT MAANA HUKU KWENGINE HAKUKWEPEKI KULIPA.
 
Kutokana na hali hiyo, ni wazi NSSF inaendelea kupoteza mapato yake yanayokaliwa na wakopaji wa aina hiyo, ambapo mwenendo usipodhibitiwa shirika linaweza kufilisika sawa na ilivyotokea kwa mashirika mengi nchini.

Haya ni maoni ya kiupendeleo ya mwandishi asiyetaka kujua kwa nini NSSF wanakopesha. Mkopo wa Mbowe una rehani, hiyo hoteli. Kama NSSF wakichoka kumdai Mbowe, watanadi hoteli yake na kupata pesa yao. Kwa hiyo Mbowe kukaa na pesa ya NSSF, ndio biashara wanayotaka NSSF ili waendelee kuvuna riba, otherwise pesa yao itakuwa tasa bila kuzaa chochote.
 
Hizi mahakama zinamwogopa Mbowe au ni kitu gani? Au naye ni miongoni mwao mafisadi aliyejificha katika ngozi ya buluu? Maana Mzee Mapesa Cheyo alikuwa na kadeni kadogo tu ukilinganisha na hili, lakini tulishuhudia madalali wakiipiga bei nyumba yake ya kuishi kwa amri ya mahakama hiyohiyo ya biashara. Sasa kwa Mbowe tunasikia habari za kuzungushana tu ati ooh akamatwe afungwe, mara kakata rufaa, nini? Deni linamfunga mtu kivipi, kwani mali yake haitoshi kulipia hilo deni? Kuna nini hapo? Alipokopa hiyo hela hakuweka rehani kitu chochote? Sasa kuna shida gani kuchukua hicho alichokiweka rehani? Na kama hakuweka rehani, basi yeye na Mustafa Mkullo kwa pamoja walifanya njama za kuibia umma wakijua mambo yatazungushwa mahakamani weeeeh! Tukimbilie wapi walalahoi?
 
Maelezo ya mchakato wa deni hilo yanaonyesha wazi kwamba mkopo huo ulifuata taratibu zote na kuna mikataba ya namna fedha zitakavyolipwa na riba yake. Pia na riba juu ya riba iwapo malipo hayatafanyika kama makubaliano yalivyo, imetajwa. Mkataba ni kati ya Mbowe hotels na NSSF n siyo kati ya Mr. Freeman Mbowe na NSSF.
Mkopo huu si ufisadi; Mtu yeyote anayefuatilia ufisadi katika sakata la EPA atagundua hilo kwa sababu zifuatazo:
-Hiyo si mikopo maana mikopo huwa na mikataba inayoonyesha lengo la mkopo(KATIKA EPA HILO LIPO?)
-Hakuna makubaliano/mikataba ya namna ya kulipa, riba, na faini au riba juu ya riba iwapo mkopo hautalipwa katika muda uliokubaliwa(KATIKA EPA HILO LIPO?)
-Hakuna makubaliano ya lini wataanza na kumaliza kulipa.Na makubaliano hayo hufanyika kabla ya kuchukua mkopo (Ya EPA wanafanya makubaliano miaka 2 baada ya kuchukua)
_Katika mikopo kuna suala la dhamana,na hapa dhamana ni Hotel yenyewe.(KATIKA EPA HILO LIPO?)
Wanaotaka mkopo huu nao uwe wa kifisadi, kwanza wachunguze hayo ya EPA kuona kama mazingira ya kuchukua fedha hizo yanafanana na hii ya Mbowe Hotels?
Si tunaona pia kuwa Mbowe hotels aliposhindwa kulipa alifikishwa mahakamani? Na Mbowe Hotel si ipo mpaka leo? Ikishindikana si itauzwa kufidia deni?
Hawa wa EPA walitumia kampuni hewa za ujanja ujanja na hawana dhamana ndiyo maana inakuwa vigumu kuwabana. Si mmesikia AG anasema wanahangaika kujua mali zilizonunuliwa kutokana na hela hizo ili wazikamate? Kwa Mbowe Hotels hakuna hilo - inaweza kukamatwa Hotel.
Kuhusu kulipa, mkataba uko wazi, lazima deni lilipwe na huu ujanja ujanja wa kuchelewesha kulipa hausaidii badala yake unakuza deni. (tofauti na EPA ambapo Waziri alisema kati ya 133bn/= zitarudi 106bn/=!!yaani zinapungua wakati za Mbowe hotels zilikopwa 15m sasa zimefikia 1.2bn)
Wakishindwa kulipa hotel inauzwa, kama fedha bado haitoshi, tunakamata mali za wakurugenzi. Niliwahi kuandika juu ya kipengele cha Lifting of the veil wakati namshauri AG alift veil ya makampuni ya EPA ili awakamate wakurugenzi. Similarly kwa Mbowe Hotels, hela isipotosha, we lift the veil na kukamata mali za wakurugenzi, Period.
KAMWE MIKOPO HALALI HAIWEZI KUWA UFISADI NA WALA MKOPAJI KUSHINDWA KULIPA HAKUMFANYI AWE FISADI. WANA JF TUWE MAKINI WA HOJA.
 
Kweli mkuki kwa nguruwe...Hapa mafisadi waaina zote, awe wa CCM au Chadema hatuchagui...Wewe huo mkataba wa Mbowe umeuona? Upatikanaji wake je? Je kulikua na uhusiano wowote na Huyu mwana Mkullo ?Tusichulie hili jambo kirahisi rahisi kwa sababu zetu binafsi,kwa mtindo huu habari za EPA na Richmond leo zingekua wapi? Soma habari iliyowekwe na mwanahabari JF siku za nyuma

Mwanahabari
SECTION: ECONOMICS; No. 656

LENGTH: 400 words

HEADLINE: TANZANIA: Dubious loan for CCM

BODY:
About fifty contributors of Tanzania's National Provident Fund (NPF), a parastatal social security system, are considering whether to sue Horace Kolimba, the minister of state in the presidential office, and Mustafa Mkullo, NPF director general for mismanaging 250 million Tanzanian shillings (US$ 470,000). Plaintiffs allege the sum was released contrary to NPF regulations and paid to Kolimba, the secretary general of the government party Chama cha Mapinduzi (CCM), which was the intended beneficiary of the funds. Mkullo is alleged to have taken the decision without consulting the NPF board of directors. Sources claim that only 10 million shillings ever reached the CCM bank account.

Kolimba counterclaims that NPF released 240 million shillings ($ 450,000) to SUKITA, a trading company which is linked with CCM, in the form of a six-month loan. Until recently, SUKITA operated with special tax-exemption facilities which the CCM government granted it, but when the procedure became "uncomfortable", the company turned to NPF for a "loan" and used it to import Kenyan beer for end-of-year festivities. However, SUKITA is coming under increasing market competition and it does not appear at all certain that it will be able to repay the loan and interest due to NPF. In that case, SUKITA executive director John Kapinga is likely to find himself joining the list of suspects possibly being interrogated by a judge on their role in the affair.

I.O.N.- The fifty plaintiffs who have threatened to sue have expressed their "astonishment" that the Organization of Tanzanian Trade Unions (whose secretary general, Bruno Mpangala, is a member of the NPF board of trustees) has not seen fit to intervene in this case of misappropriation of National Provident Fund assets from members' salaries.

LOAD-DATE: January 27, 1995
 
Moderator Mbona uemweka hii habari vibweka vya wakubwa??ina maana ufisadi wa Mbowe nao ni kibweka
 
Mapambano nakushukuru kwa ukali wako, ila yaonekana hukunielewa na habari yenyewe(thread) hujaielewa. Muweka thread ameeleza mchakato wote ulivyokuwa na makubaliano yao (mkataba) Hivyo mkataba upo na ndiyo huo NSSF inaousimamia mahakamani. Ungekuwa haupo NSSF wasingeshtaki ili kudai walipwe. Kwa kuwa muweka thread amesema wamekwenda mahakamani kudai walipwe, ni wazi hiyo ni civil suit,. Kama isingekuwa hivyo, wangefungua criminal kama tunayotaka wafunguliwe wa EPA.
Hivu kweli Ndugu Mapambano wataka kutueleza kuwa mkopo huo wa NSSF kama ulivyoelezwa ni Ufisadi kama wa EPA na Richmond?
Hapa hatetewi mtu na ndiyo maana mwishoni nimeeleza kuwa kama Mbowe Hotel ikiuzwa na hela isitoshe, basi tuna-lift veil ya hotel na kukamata wamiliki wake ili walipe. period; na hata kufungwa ikionekana walikopa kitu wasichokuwa na uwezo wa kukilipa (utapeli)
 
Hapa naona kuna haja ya Mh. Mbowe kusafisha jina lake. Hata kama akidai kuwa ni kampuni na wala si yeye, lakini sote twajua kuwa hakuna kampuni isiyo na mwenyewe! Asituletee za hao jamaa wa EPA ambao wanasema pesa inarudishwa, lakini hajulikani nani anayeirudisha!

Tusaidiane kuikomboa nchi yetu kwa kukosa hata PANADOL.
 
Hii MIKOPO ya BENK, NSSF itatuuwa!!! Riba 31% mbona hatari?

Samahani hivi Riba NSSF bado ni hiyohiyo au imepungua sasa?

Nini Tofauti ya MKOPO wa BENK na MKOPO wa NSSF.
Duh!hii riba nayo ni aina fulani ya wizi.jamani wenye kipato cha chini kama mwalimu ,polisi wataweza kweli kupata mkopo?ndio maana nchi haiendelei kumbe
 
mahali penye mkataba ambao pande zote mbili zimewekeana saini haiwezi kuuita moja kwa moja utapeli au ufisadi.(Lazima tujue maana halisi ya maneno haya) Pale upande mmoja unaposhindwa kutekeleza wajibu wa kamkataba kunakuwa na taratibu za kufuata ikiwa ni pamoja na arbitration au mahakamani kuendana na mkataba huo. Kushindwa kulipa kunatafsiriwa vipi na huo mkataba? Surety, au collateral ilikuwa nini? Na hiyo interest ni ya aina gani hiyo? 31% compounded? NSSF inaweza kuwa na weak analysts wa mikopo .Kumbuka alikwa Mkulo. Je mwamfahamu huyu?

Simtetei asilipe. Lakini ana arguements , pengine NSFF wanataka kumfisadi yeye kwa kubambikiza interest juu ya interest? Tofautisha kati ya mkataba wa RDC na Tanesco.mkopo ni dimension nyingine kwani ukishindwa kulipa kuna remedy.tena kuna muda maalum .Isitoshe collateral inauzwa kuricover loan. Labda tujiulize kwa nini NSSF hawakuuza colateral iliyowekwa hadi leo.
 
Maelezo ya mchakato wa deni hilo yanaonyesha wazi kwamba mkopo huo ulifuata taratibu zote na kuna mikataba ya namna fedha zitakavyolipwa na riba yake. Pia na riba juu ya riba iwapo malipo hayatafanyika kama makubaliano yalivyo, imetajwa. Mkataba ni kati ya Mbowe hotels na NSSF n siyo kati ya Mr. Freeman Mbowe na NSSF.
Mkopo huu si ufisadi; Mtu yeyote anayefuatilia ufisadi katika sakata la EPA atagundua hilo kwa sababu zifuatazo:
-Hiyo si mikopo maana mikopo huwa na mikataba inayoonyesha lengo la mkopo(KATIKA EPA HILO LIPO?)
-Hakuna makubaliano/mikataba ya namna ya kulipa, riba, na faini au riba juu ya riba iwapo mkopo hautalipwa katika muda uliokubaliwa(KATIKA EPA HILO LIPO?)
-Hakuna makubaliano ya lini wataanza na kumaliza kulipa.Na makubaliano hayo hufanyika kabla ya kuchukua mkopo (Ya EPA wanafanya makubaliano miaka 2 baada ya kuchukua)
_Katika mikopo kuna suala la dhamana,na hapa dhamana ni Hotel yenyewe.(KATIKA EPA HILO LIPO?)
Wanaotaka mkopo huu nao uwe wa kifisadi, kwanza wachunguze hayo ya EPA kuona kama mazingira ya kuchukua fedha hizo yanafanana na hii ya Mbowe Hotels?
Si tunaona pia kuwa Mbowe hotels aliposhindwa kulipa alifikishwa mahakamani? Na Mbowe Hotel si ipo mpaka leo? Ikishindikana si itauzwa kufidia deni?
Hawa wa EPA walitumia kampuni hewa za ujanja ujanja na hawana dhamana ndiyo maana inakuwa vigumu kuwabana. Si mmesikia AG anasema wanahangaika kujua mali zilizonunuliwa kutokana na hela hizo ili wazikamate? Kwa Mbowe Hotels hakuna hilo - inaweza kukamatwa Hotel.
Kuhusu kulipa, mkataba uko wazi, lazima deni lilipwe na huu ujanja ujanja wa kuchelewesha kulipa hausaidii badala yake unakuza deni. (tofauti na EPA ambapo Waziri alisema kati ya 133bn/= zitarudi 106bn/=!!yaani zinapungua wakati za Mbowe hotels zilikopwa 15m sasa zimefikia 1.2bn)
Wakishindwa kulipa hotel inauzwa, kama fedha bado haitoshi, tunakamata mali za wakurugenzi. Niliwahi kuandika juu ya kipengele cha Lifting of the veil wakati namshauri AG alift veil ya makampuni ya EPA ili awakamate wakurugenzi. Similarly kwa Mbowe Hotels, hela isipotosha, we lift the veil na kukamata mali za wakurugenzi, Period.
KAMWE MIKOPO HALALI HAIWEZI KUWA UFISADI NA WALA MKOPAJI KUSHINDWA KULIPA HAKUMFANYI AWE FISADI. WANA JF TUWE MAKINI WA HOJA.
Nakubaliana na wewe mkuu.naona hapa watu wameshindwa kutofautisha ufisadi na mkopo wenye makubaliano ya kweli tofauti na waLE wa EPA.
 
Mimi naona Mbowe afunge vilago vyake aondoke. Hafai kuiongoza CHADEMA kabisaa. Huyu akiingia tu madalakani kwanza ni kutumia madaraka kulipia madeni yake. Tusimchague mwizi ashike madaraka.
 
Back
Top Bottom