Mbowe: Kesi zimeniletea msongo wa mawazo
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe, ameliambia Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kuwa, ameshindwa kujaza fomu za kutangaza mali zake kutokana na msongo wa mawazo.
Akihojiwa kwenye baraza hilo jana, Mbowe alisema tangu umalizike Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, amekumbwa na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kesi mbalimbali ambazo zimemsababishia msongo wa mawazo na kumwathiri kifamilia.Alisema alifikishwa katika mahakama tatu tofauti, zikiwamo Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Hai kwa tuhuma mbalimbali ambazo zimemsababishia msongo wa mawazo.
Katika kipindi chote hicho nimekuwa kwenye mahakama tatu tofauti nikituhumiwa kwa mambo mbambali ambayo ni matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na matokeo ya kazi yangu,alisema Mbowe na kuongeza:
Siilaumu Tume kwa lolote, naiheshimu sana na naheshimu kazi yao, niliona kuliko kujaza kwa makosa ni bora nichelewe kuileta,alisema.
Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema pia kutokana na mali na biashara alizonazo alishindwa kujaza fomu hizo kwa wakati kwa sababu ana makazi sehemu tatu na kote huko kuna mali zake.
Naliomba radhi Baraza, ratiba yangu imekumbwa na mambo mengi sana. Mimi ni mbunge na ni kiongozi wa chama cha siasa hivyo, nilikosa utulivu wa kujaza fomu kwa wakati,alisema.
Kapteni Komba adai jina lake limekatwa
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba amesema ameshangazwa kuitwa katika baraza hilo wakati yeye alijaza fomu na kuirejesha kwenye Ofisi ya Bunge.
Sina mali za kutisha hadi niogope kujaza fomu, mimi nina vijihela tu kidogo kama Mtanzania mwingine wa kawaida,alisema Komba na kuongeza kuwa:
Nina marafiki wengi kama kina Bakili Muluzi wamenipa mahela sasa ningeyafanyia nini,:
Komba pia alilalamikia jina lake kukatwa katika orodha ya wabunge wengine ambao walikuwa wamerejesha fomu na kudai kuwa hiyo ni hujuma.
Wana lao jambo haiwezekani jina langu liwemo kwenye orodha ya wabunge waliorejesha fomu halafu lionekane limekatwa,alisema.
Mbunge huyo aliitaka tume hiyo iwasiliane na viongozi husika moja kwa moja badala ya kupitia kwa spika kwa sababu katika suala la kutangaza mali hawawajibiki kwa spika. Mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Damian Lubuva alisema baada ya kusikiliza utetezi wa viongozi hao watatoa uamuzi na mapendekezo yao kwenye mamlaka zinazohusika.
Aingizwe kenye list ya mafisadi, kumbe list haikukamilika!"nimeshindwa kujaza fomu zakutangaza mali zangu kwasababu ya msongo wa mawazo" jamani huyu Aluatani hapa kaniboa siasa imemlewesha au ndo woga umemuingia baada ya kuwekwa kizuizini? Au anaumwa Zittophibiasis? Maana nae alianza hivihivi.
ndugu wanajf suala la mbowe kushindwa kuijaza fomu kuelezea utajiri wake si suala la kuwa na msongo wa mawazo bali ni maelezo ya wapi alizipata mali hizo na hofu ya namna hii inadhihirisha kuwa kuna mali alizopata kimagendo kama si hivyo kwanini ahofie wakati ni suala lakuchukua mwanasheria wake nakujaza fomu fasta.
polisiii kamata mwizi huyoooooooooooo
Ndugu wanaJF Suala la Mbowe kushindwa kuijaza fomu kuelezea utajiri wake si suala la kuwa NA MSONGO WA MAWAZO BALI NI MAELEZO YA WAPI ALIZIPATA MALI HIZO NA HOFU YA NAMNA HII INADHIHIRISHA KUWA KUNA MALI ALIZOPATA KIMAGENDO Kama si hivyo kwanini ahofie wakati ni suala lakuchukua mwanasheria wake nakujaza fomu fasta.
polisiii kamata mwizi huyoooooooooooo
Nadhani ilikuwa ni mbinu ya Mbowe kujinasua kwa yule Mzee (jaji) mind you it was the second time for him to stand before Pilato kwa makosa tofauti.Nimekubali mbinu yake ya mbaazi kukosa maua kwa kisingizio cha jua.Hapa labda Jaji awe "Mechanical" ndio atashughulika nae lakini "organical" lazima huruma itaingia tu japo sheria inatizamwa.
My friend Mbowe,jipange na kuwa makini na system iliyopo usije ukachizika muda si mrefu maake Magamba na miundo mbinu yake inaweza kukufanya "ukaranduka" badala ya "kubanjuka".Am talking as a human being,jamaa mpaka anatia huruma utadhani SOWETO.
gazeti la mwananchi la leo limeandika kuwa mhe freeman mbowe atasimamishwa katika baraza la maadili kesho 16 june 2011 ili kujibu tuhuma za kutowasilisha fomu zinazoonesha mali na madeni yake.
Huyu mheshimiwa ni siku chache tu zilizopita aliionesha dharau kubwa kwa mahakama mpaka ikabidi aswekwe polisi. Serikali ililazimika kumpeleka mahakamani chini ya ulinzi makali kama mhalifu asiye wa kawaida.
Watanzania wanajiuliza;
a. Tunastahili kuwa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni mtovu wa nidhamu kiasi hiki?
B. Kwa nini mbowe anaogopa kutaja mali zake?? Anaficha nini??
C. Chama chake kilikosa mtu mwingine wa kushika wadhifa huu wa heshma? ...mbona mhe zitto kabwe alitaka kugombea nafasi hiyo akakatazwa na ndugu zake mbowe?
D. Wanaomzunguka kama mhe g. Lema wanachangia katika kudidimiza nidhamu ya kiongozi huyu?
Dunia inaendelea kutucheka kwani kiongozi wa upinzani hatakiwi kuwa mhuni.
Hata akirudi shule haitasaidia maana hataelewa huyo. Dalili zote zinaonesha ubongo umesinyaa.mada ya kipuuzi hii , fomu wanazojaza za maadili ni kwa ajili kuweka wazi mali zako na si utajiri , rudi shule kajaribu kujifunza mali na utajiri tofauti yake ni nini
Huyu Mbowe hafai kabisa kuwa ktk kambi ya upinzani. Ni aibu kwa kubwa Chedema kuwa na kiongozi asiyeheshimu sheria za nchi. Huyu Mbowe inabidi ajibu mashitaka yote yanayomkabili, na atolewe haraka ktk kambi ya upinzani.
Gazeti la Mwananchi la leo limeandika kuwa Mhe Freeman Mbowe atasimamishwa katika Baraza la Maadili kesho 16 June 2011 ili kujibu tuhuma za kutowasilisha fomu zinazoonesha mali na madeni yake.
Huyu Mheshimiwa ni siku chache tu zilizopita aliionesha dharau kubwa kwa mahakama mpaka ikabidi aswekwe polisi. Serikali ililazimika kumpeleka mahakamani chini ya ulinzi makali kama mhalifu asiye wa kawaida.
Watanzania wanajiuliza;
a. Tunastahili kuwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni mtovu wa nidhamu kiasi hiki?
b. Kwa nini Mbowe anaogopa kutaja mali zake?? anaficha nini??
c. Chama chake kilikosa mtu mwingine wa kushika wadhifa huu wa heshma? ...Mbona Mhe Zitto Kabwe alitaka kugombea nafasi hiyo akakatazwa na ndugu zake Mbowe?
d. Wanaomzunguka kama Mhe G. Lema wanachangia katika kudidimiza nidhamu ya kiongozi huyu?
Dunia inaendelea kutucheka kwani kiongozi wa upinzani hatakiwi kuwa mhuni.