Mbowe admits failure to declare assets

Ni kweli ameshindwa kujaza form kila siku ccm wanamtafuta aende mahakamani aende polisi aende bungeni awasilishe bajati bado ajaze form za kulist mali cant u see he was too bize?
 
Jana aliandikwa mama Lwakatare mbona haikuwa issue? Mbowe kwanini asiandikwe si na yeye kiongozi? tena kiongozi wa upinzani bungeni anayetoka chama ambacho kipo mstari wa mbele kupiga kelele za ufisadi.Yes anatakiwa awajibishwe accordingly yeye ndio angekuwa mfano kwa wenzake.
 
Mbowe: Kesi zimeniletea msongo wa mawazo

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe, ameliambia Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kuwa, ameshindwa kujaza fomu za kutangaza mali zake kutokana na msongo wa mawazo.

Akihojiwa kwenye baraza hilo jana, Mbowe alisema tangu umalizike Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, amekumbwa na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kesi mbalimbali ambazo zimemsababishia msongo wa mawazo na kumwathiri kifamilia.Alisema alifikishwa katika mahakama tatu tofauti, zikiwamo Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Hai kwa tuhuma mbalimbali ambazo zimemsababishia msongo wa mawazo.

“Katika kipindi chote hicho nimekuwa kwenye mahakama tatu tofauti nikituhumiwa kwa mambo mbambali ambayo ni matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na matokeo ya kazi yangu,”alisema Mbowe na kuongeza:
“Siilaumu Tume kwa lolote, naiheshimu sana na naheshimu kazi yao, niliona kuliko kujaza kwa makosa ni bora nichelewe kuileta,”alisema.

Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema pia kutokana na mali na biashara alizonazo alishindwa kujaza fomu hizo kwa wakati kwa sababu ana makazi sehemu tatu na kote huko kuna mali zake.
“Naliomba radhi Baraza, ratiba yangu imekumbwa na mambo mengi sana. Mimi ni mbunge na ni kiongozi wa chama cha siasa hivyo, nilikosa utulivu wa kujaza fomu kwa wakati,”alisema.

Kapteni Komba adai jina lake limekatwa
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba amesema ameshangazwa kuitwa katika baraza hilo wakati yeye alijaza fomu na kuirejesha kwenye Ofisi ya Bunge.

“Sina mali za kutisha hadi niogope kujaza fomu, mimi nina vijihela tu kidogo kama Mtanzania mwingine wa kawaida,”alisema Komba na kuongeza kuwa:
“Nina marafiki wengi kama kina Bakili Muluzi wamenipa mahela sasa ningeyafanyia nini,”:
Komba pia alilalamikia jina lake kukatwa katika orodha ya wabunge wengine ambao walikuwa wamerejesha fomu na kudai kuwa hiyo ni hujuma.

“Wana lao jambo haiwezekani jina langu liwemo kwenye orodha ya wabunge waliorejesha fomu halafu lionekane limekatwa,”alisema.
Mbunge huyo aliitaka tume hiyo iwasiliane na viongozi husika moja kwa moja badala ya kupitia kwa spika kwa sababu katika suala la kutangaza mali hawawajibiki kwa spika. Mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Damian Lubuva alisema baada ya kusikiliza utetezi wa viongozi hao watatoa uamuzi na mapendekezo yao kwenye mamlaka zinazohusika.



 
Hii ni janja ya nyani, hivi kweli mtu angekuwa na nia ya kuijaza hii fomu si angeshaijaza? Utetezi wa msongo wa mawazo ni majibu ya ki-CCM CCM na sitegemei yatoke kwa kiongozi mkuu wa chama tawala 2015, uongozi ni pressure na ni pamoja na kufanya vitu vingi kwa wakati. Sasa haya majibu marahisi namna hii ni kutuonyesha in future haya tuyategemee auu?

Badilikeni.
 
Jogoo hafi kwa utitiri kinachompa mawazo nini, si achukulie pouwa aendeleze harakati.
If he can't make a choice the choice will make him.
 
kwani mlitaka asemeje sasa,hayo ni mjibu sahihi na atapewa muda wa kuzijaza,angalia ya majibu ya komba kama yanafaa basi
 
"nimeshindwa kujaza fomu zakutangaza mali zangu kwasababu ya msongo wa mawazo" jamani huyu Aluatani hapa kaniboa siasa imemlewesha au ndo woga umemuingia baada ya kuwekwa kizuizini? Au anaumwa Zittophibiasis? Maana nae alianza hivihivi.

Bwahahahahahahhhahahhahah! Mnafiki mkubwa huyo, tatizo hazijui hata mali zake, zilivokua nyingi halafau zote magumashi!
 
"nimeshindwa kujaza fomu zakutangaza mali zangu kwasababu ya msongo wa mawazo" jamani huyu Aluatani hapa kaniboa siasa imemlewesha au ndo woga umemuingia baada ya kuwekwa kizuizini? Au anaumwa Zittophibiasis? Maana nae alianza hivihivi.


hahaaaa ....au na yeye fomu imeibiwa na shetani?
 
Komba naye kaingia kwenye kauli za "Vijihela" ndo wale wale na mzee wa Vijisenti. Pole pole tutawajua tu. Kwa hiyo Mh Komba tutakapogundua kwamba ana vijisenti utetezi wake ni kwamba kapewa na Bakili Muluzi, si ndiyo??
 
"nimeshindwa kujaza fomu zakutangaza mali zangu kwasababu ya msongo wa mawazo" jamani huyu Aluatani hapa kaniboa siasa imemlewesha au ndo woga umemuingia baada ya kuwekwa kizuizini? Au anaumwa Zittophibiasis? Maana nae alianza hivihivi.

Mbowe aache woga, kushitakiwa ni nafasi ya pekee ya kuonekana mbele ya jamii ana hatia au la, kama hakufanya yale aliyoshitakiwa nayo si atashinda kesi tu, ana wasiwasi gani? Endapo anayoshitakiwa nayo ni ya kweli lazima atapata msongo!
 
Siasa za Tanzania rahisi sana, yani mwenyekiti wa CHADEMA ana predicament ya kutojaza fomu za maadili halafu sio issue?
 
Mbowe anafanya tujiulize uwezo wake katika kusimamia sheria na kuzitekeleza. Hiyo sababu aliyotoa ni dhaifu hata kama watu wa maadili wataikubali!. Nimemuona mara nyingi akaitimiza wajibu wake ktk chama chake (kama kuhudhuria maandamano na mikutano) bila kusema kesi zinamzonga. Kujaza form ya mali ni kitu muhimu ili tupime uadilifu......!

Kiongozi anaangaliwa kwa haya mambo madogo madogo. Najiuliza; alipanga kuzipeleka akimaliza kesi zote????



 
WanaJF

Hivi ni kweli Mh. Mbowe ametamka mwenyewe kuwa ana msongo wa mawazo na ameathirika?

Kama hivyo, ndivyo kwa nini Mh. Mbowe asipumzike japo kidogo?

Kama hiyo ni kweli, Mh. Mbowe atawezaje kutoa mchango wako katika kipindi hichi nyeti kwa Bunge letu?

Pole sana kamanda wetu!
 
Back
Top Bottom