hovyohovyo
JF-Expert Member
- Jul 8, 2012
- 547
- 157
Mbongo mmoja akiwa london uingereza anaingia katika restaurant na anaagiza chipsi kuku. Kuku wenyewe wa kizungu laini kama nini. Anakula chipsi na ktutafuna kuku pamoja na mifupa yake. Jirani yake kuna mzungu anakula wali na samaki. Mzungu kwanza anamwangalia mbongo anavyotafuna mifupa, kisha anauliza: Kama unaweza kula kuku na kutafuna pamoja na mifupa yake, je mbwa wenu huwa mnawapa nini huko Afrika?? ..Mbongo akaangalia, kisha akasema kwa dharau " well, we give them a plateful of rice and fish". Mzungu akabaki hoi.