Mbona wanaume huwa na kigugumizi kutamka 'mke wangu'

Wakuu bila shaka mtakubaliana nami kuwa wanawake hutambulisha waume zao bila kuuma maneno yaani 'huyu ndiye mume wangu'. Kwa upande wa wanaume hali naona huwa tofauti kwani utawasikia 'huyu ndo shemeji yako' huyu ndo mama watoto' huyu ndo mamsap' huyu ndo mama polisi' n.k. Akijitahidi sana utasikia 'huyu ndo my wife'. Hivi tatizo ni nini wanandoa wenzangu?
Because I never trust anyone...
 
Suala ni ujumbe ufike kwa anayepokea utambulisho. Haya mengine ni majungu tu.
 
hii ya kuitana majina halisi, sina comment ila mimi siwezi. Kuna majina ya kuitana mbele za watu na yale mkiwa peke yenu. Sweet, honey kwa maongezi ya cm au mkiwa room. Huwezi kumwita honey njoo akiwa ktk kundi la watu

ni mapenzi yenu wenyewe muitanaje
mie naitwa Honey hata ktk kadamnasi
and i am loving it!!
 
and by the way
tukitambulishana tunakuwa specific huyu ndie mke/mume wangu
aitwa......

hakuna kigugumizi ktk hilo
 
Majina mazuri ni yle yasiyomkwaza yeyote, kwa mfano huyu ni mke wangu mpenzi anaitwa Dora, na wala sio huyu ni mama watoat wangu kwani unayemtambulisha anaweza kuwa na ke lakini mungu hajawapa zawadi au mtihani wa watoto na si ajabu ndoa yao ina umri mrefu. Keep it simple huyu ni mke wangu.... kwani ni mke wako kweli? na atoke kiheshima sio mtu kavaa vitu vya ajabu mpaka unahesabu makunyanzi ya tumbo....lazima mtu asite
 
Back
Top Bottom