Mbona baadhi ya askari wetu wanaona sifa kuvunja sheria?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wanaJF, mara kadhaa nimeshuhudia baadhi ya askari wetu wakiringa kwa kivunja sheria. Huwa najisikia vibaya sana kuona wale wenye wajibu wa kulinda sheria ndio wanaoona fahari kuzivunja:

1. Mara kadhaa naona 'traffic police' wakiendesha pikipiki bila kuvaa helmet au kubeba abiria bila helmet.
2. Baadhi ya askari wanatanua kwenye foleni kwa kuwasha 'emergency lights' na kupita pembeni mwa barabara hata kama hakuna sababu ya maana ya kufanya hivyo.
3. Mgambo wanaonea wafanyabiashara hasa wanapotumia ubabe kuwakamata na kuharibu mali zao na kuwapiga.
4. Baadhi ya watuhumiwa wamekuwa wakidai askari wakiwakamata wanawapiga kuwashinikza wakubali kosa kwa kuogopa kuumizwa vibaya au kubambikiwa kesi mbaya zaidi.
5. Askari wa JWTZ na hata wa JKT na Magereza wanadaiwa na baadhi ya raia kwa kuwapiga raia mtaani au kwenye vilabu vya pombe kukitokea kutoelewana kati yao na raia.
6. Nchi nyingine askari wana nidhamu sana na ndio msaada mkubwa raia anapohitaji msaada wao. Asilimia kubwa ya askari wetu hawana moyo wa namna hiyo.

Je, tatizo ni nini? Ikitokea raia anaonewa na askari afanye nini? Nauliza hivi kwa vile si rahisi raia ambaye anapigwa sehemu fulani kumkamata askari au kumpeleka popote. After all, baadhi ya askari wanasema: 'chukua jina na namba yangu na nenda ushtaki sehemu yoyote unayotaka'.

Tujadiliane na kushauri njia gani wenye jukumu la majeshi yetu wanaweza kuondoa kero za namna hii na kurudisha nidhamu na uwajibikaji katika majeshi yetu.
 
Tatizo hatujui haki zetu na hata tunapozijua na kuzifuatilia unakutana na vikwazo vingine huko ulikoenda dai haki yako,maana mtoto wa nyoka ni nyoka tu na kesi ya nyani huwezi mpelekea ngedere. Laiti tungekuwa na ushirikiano wa pamoja haya yasingetokea na haswa hao viongozi wetu katika vyombo hivyo vya sheria kujua wajibu wao. Taratibu tutafika ila it will take long.....route.
 
Back
Top Bottom