Ndoto ya kuwa askari inayonitesa hadi sasa

danieltz

Member
Feb 18, 2022
5
8
Wakuu kwema heri ya mwaka mpya 2024 naomba nirejee moja kwa moja kwenye mada hapo juu kama ilivojieleza.

Ikumbukwe kwamba kila mtu tangu kuzaliwa kwake amekuwa na ndoto ya kuwa mtu fulani kuna wengine walikuwa na ndoto za kuwa madaktari, Marubani, Manahodha, Walimu, mahakimu, mawakili, mainjinia n.k

Vivo hivo nami pia tangu kuzaliwa kwangu nimekuwa na ndoto za siku moja kuitwa askari haijalishi ni askari wa nini iwe JWTZ, Police, magereza, uhamiaji, Wanyamapori, Zimamoto au idara nyeti za usalama (intelligence Service).

Ndoto hii nimekuwa nikiishi nayo tangu nikiwa mdogo vitu vyangu vya michezo vilikuwa natengeneza udogo wa ufinyanzi silaha na askari movie zangu za kuangalia tangu udogoni hadi sasa ni movie za kivita tu hapo ndo naenjoy najiona kama ni sehem ya maaskari vitani.

Mara baada ya kumaliza kidato cha nne matokeo hayakuwa mazuri nilipata Four hapo hapo nikaaza kupambania ndoto zangu za kuwa askari nikaanza kuhangaika nafasi ya kwenda JKT ili iwe rahisi kuingia kwenye majeshi ya ulinzi na usalama lakini niliishia tu ngazi ya wilaya na kukosa nafasi sikukataa tamaa nikaendelea kupambana kila mwaka zinapotoka nafasi naomba lakini bado ikashindikana nililazimika kutafuta connection kwa mtu wa karibu alieahidi kunisaidie kwa vipande kadhaa vya fedha nilipambana kadri ya uwezi wangu nikampa lakini bado sikufua dafu nikaenda chuo kusoma lakini sikuacha kuomba kwa kila tangazo la kazi liwe na police,magereza, uhamiaji n.k nilikuwa naomba lakini nakuwa sina kigezo cha cheti cha JKT.

Baada ya miaka kwenda na kuona ndoto yangu kuwa askari inazidi kudidimia nilianza kushawishaka hata kuanza kutafuta connection za kwenda kujiunga na vikundi vya alshabab au m23 huko mradi nikashike silaha na kupata purukushaji za vita..Basi nikaanza kutafuta marafiki wale wa Masheikh wa itikadi kali nia yangu nikuchunguza kama wanajua njia zozote za kwenda huko...Nako sikufua dafu kwa kuwa kwanza dini ni tofaut hivo kuwa na urafiki na wao ni swala gumu unless ubadili uwe kama wao pili kuchunguza mambo hayo wanakuona kama Spy tu

Mwisho wa siku nilirudi home na kujutia sana uamuzi wangu huu wa kipuuzi sana nilijutia mno na tangu siku hiyo itakutulia sikuwa na mkazo sana kama miaka ya nyuma ila sikuacha kuomba kila kazi ya inayotoka inayohusu majeshi ya ulinzi.

Sasa mwaka huu nikiwa Kwa shemeji yangu UKONGA Magereza hapa ndoto hii ni kama imeanza kunisumbua tena maana naishi kota mwezi wa 12 tarehe 15 ilikuwa mahafali ya maaskari Nyota moja na nyota tatu nilikwenda kwenye mahafali mapema sana kushuhudia Gwaride mwanzo mwisho kitendo cha kushuhudia Gwaride kiu yangu ya kuwa askari ikarudi tena upyaa kabisa nikatamani hadi niwe sehem ya watu wa Parade vijana wadogo kabisa ambao ni kama mie tu au nimewazidi umri wakiwa kwenye parade na wengine kuimarisha ulinzi ni jambo ambalo limezidi kuamsha hisia zangu za kua afande

Hivi majuzi wamekuja dempo mpya kutoka kiwira wamemaliza mafunzo na sasa kutumikia kama maaskari wapya nimekaa nimeshuhudia walivoripoti huku mie nikiwa tu home hii kitu imeniumiza sana naishi kuumia kwanini nashindwa kutimiza ndoto hii nimekuwa nikiteseka miaka na miaka.

Wakuu 2024 nataka niepukane kabisa na ndoto hii ila sijui nitumie mbinu gani kuondoa kabisa mambo ya kuwa askari akili mwangu nawaza kumuona mwanasaikolojia labda anaweza kunisaidia ila kama kuna mtu anaweza kunipa mbinu niepukane kabisa na hii hali naomba msaada wetu kwa kifupi nateseka sana hasa nikisie neno ASKARI.

NIFANYEJE
 
Namimi nilikuwa na mawazo kama wewe lakini baada ya kuona makomandoo wa Israeli wanavyo binuliwa bila huruma na wagambo wa Hamasi ambao ni wahuni wa mtaani tu, basi kiu yangu imeishia hapo
 
tupo wengi wenye hali kama yako, hadi huwa nawaambia MARAFIKI zangu kuwa ASKARI wa kweli tupo mitaani atujapata tu nafasi ya kusajiliwa 😭😭😭😭

kwa hapa nyumbani kutoboa inazidi kuwa ngumu haswa ukizingatia kuwa wametuwekea kigezo cha umri😭😭😭

kama umesoma vyuo... jaribu kuomba kazi inayo endana na elimu yako achana na habari za majeshi yetu. hivi sasa nchi yetu hii bila kuwana connection huwezi kupata kazi😭😭😭😭

nimeteseka kuzisaka hizo nafasi kwa muda wa miaka 11 mfululizo bila mafanikio.

natafuta kibunda niame nchi najiona kama mkimbizi kwenye nchi yangu mwenyewe 😭😭😭

nchi ambayo unaweza kuomba
nafasi za kazi kwenye makampuni au Serikalini kwa watu ambao ni ndugu zetu wenye nyazfa na vyeo ambao wAngeweza kukusaidia na UKANYIMWA.​

unaweza kupata ahadi NZURI, za kusaidiwa kwa watu wanaotujua tuliosoma nao, tuliotoka kijiji kimoja ambao sio RAHISI wao kutukimbia... lakini UKAKOSA msaada kwao😭😭😭

Inauma sana kwa kweli hivi karibuni naikimbia hii nchi...! hii nchi nadhani wachache ndio wanao paswa kuifaidi wengine tusipo kuwa makini tutaishia kuwa watumwa... 😭😭😭😭​
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom