Fedha za mafunzo Askari Polisi zazua jambo, Msemaji wa Polisi atoa ufafanuzi

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,828
21,457
Hali si shwari ndani ya Jeshi la Polisi, baada ya askari wenye cheo cha kuanzia konstebo hadi mkaguzi wanaohudhuria mafunzo ya utayari nchi nzima, kulalamikia kujigharimia mafunzo hayo, licha ya Serikali kueleza kuwa inatoa fedha kwa ajili hiyo.

Vyanzo mbalimbali vimelidokeza gazeti hili kuwa baadhi ya askari na maofisa walioanzisha vuguvugu hilo kupitia makundi sogozi (Whatsapp) ndani ya jeshi hilo, wanashikiliwa mahabusu katika baadhi ya vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alipotafutwa na Mwananchi azungumzie suala hilo, alisema madai hayo hayana ukweli kwa sababu mafunzo hayo hayalipiwi bali “yanahudhuriwa eneo la kazi na hufanyika saa za kazi za kila siku”.

“Mafunzo ya nje ya nchi Serikali hugharimia na wakati mwingine wafadhili. Lakini yapo mafunzo kazini (on job training), ambapo askari huhudhuria, ambayo hujulikana kwa jina la utayari eneo lake la kazi kama vile wilaya anayofanyia kazi,” alisema Misime.

Aidha, Misime alisema katika mafunzo hayo, yapo yanayoendeshwa vyuoni na wanaoyahudhuria Serikali huwalipia gharama za mafunzo, tofauti na kipindi cha nyuma walipokuwa wanajilipia wenyewe.

Alisema askari wanatakiwa wawe na weledi mkubwa, afya njema, ukakamavu, watende haki kwa jamii, wawe na uadilifu na wawe na nidhamu ya hali ya juu kutokana na kiapo walichoapa walipojiunga na Jeshi la Polisi.

“Hivyo ili kuhakikisha wanakuwa na sifa hizo wanatakiwa wahudhurie mafunzo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi,” alisema.

Kulingana na taarifa zilizoifikia Mwananchi, askari hao wamekuwa wakitolewa katika vituo vyao vya kazi na kupelekwa makao makuu ya wilaya au mikoa kuhudhuria mafunzo hayo na kutokana na umbali, baadhi yao hulazimika kujigharimia malazi.

Malalamiko ya askari hao yamekolezwa na hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni iliyobainisha kuwa Serikali imegharimia mafunzo ya askari hao kwa asilimia 100.

Hotuba hiyo iliibua maswali kutoka kwa baadhi ya askari na kupitia kwenye makundi yao ya Whatsapp, walianza kuhoji kama Serikali inagharimia, inakuwaje wanajigharimia kuanzia nauli, chakula na malazi kwa wanaotoka mbali?

Katika makundi hayo, inaelezwa baadhi walitumia lugha kali inayotafsiriwa kuwa walikiuka mwenendo wa Jeshi hilo, wakitaka waelezwe fedha hizo ziko mikononi mwa nani?

Alichokisema waziri bungeni

Katika hotuba hiyo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Masauni aliliambia Bunge kuwa jumla ya maofisa, wakaguzi, askari na watumishi raia 7,282 wameendelea kupatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo.
“Kati ya hao, 69 ni wa makao makuu ya wizara, 5,041 ni wa Jeshi la Polisi, 662 wa Jeshi la Magereza, 764 ni wa Jeshi la Zimamoto na 751 kutoka idara ya Uhamiaji.

“Mafunzo hayo yamegharimiwa na Serikali kwa asilimia 100 bila kuwa na makato yoyote kutoka kwenye posho za askari. Lengo la mafunzo ni kuimarisha utendaji, kuwaongezea ujuzi, maarifa na stadi katika utekelezaji wa majukumu yao,” alisema.

Waziri aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wizara itaendelea kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji askari, maofisa na watumishi raia ambapo Jeshi la Polisi limetengewa Sh20.7 bilioni.
Polisi wafunguka

Baadhi ya askari waliozungumza na gazeti hili katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Mwanza, Mtwara, Dodoma, Mara na Tanga walithibitisha uwepo wa mafunzo hayo ya utayari na sintofahamu kuhusu nani anayegharimia mafunzo hayo.

“Hili jambo lilianzia kwenye hotuba ya waziri wetu (Mambo ya Ndani) bungeni kwamba Rais (Samia Suluhu) amekubali kutoa fedha na mafunzo haya yanagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100,” alidokeza askari mmoja jijini Dar es Salaam.

“Sasa hapo ndiyo tukaanza kujiuliza mbona tunajigharimia wenyewe kila kitu? Katika baadhi ya makundi ya Whatsapp askari wakaanza kuhoji, naona hili halikuwafurahisha wakubwa, naambiwa baadhi (askari) wako mahabusu,” alidai.

Ofisa mmoja jijini Arusha aliyehudhuria mafunzo hayo, alidai yeye anatoka wilaya ya mbali na makao makuu ya mkoa, hivyo hawezi kwenda na kurudi na inamlazimu kulala hotelini kwa siku zote 30 za mafunzo.

“Mwanzoni ilikuwa ukienda kozi ulikuwa hupewi ile ration allowance (posho ya chakula) ambayo ni Sh10,000 kwa siku, lakini sasa imerudishwa tunashukuru. Ila haya mafunzo ni kututia umaskini tu na tunaambiwa pesa zimetoka,” alidai.

Hata hivyo, ofisa mwingine kutoka Mwanza, alidai kilichowaponza wenzao ambao inadaiwa waliwekwa mahabusu kwa utovu wa nidhamu, ni matumizi ya lugha za kejeli dhidi ya Rais Samia na viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi.

“Sawa, hata kama una haki huwezi kwenda tu kwenye group (makundi) ya Whatsapp na kuanza kudai kwa kejeli. Jeshi la Polisi linaendeshwa kwa nidhamu na amri. Hili lingeweza kujadiliwa kwenye mabaraza ya askari,” alisema.

Ofisa mwingine kutoka mkoani Mtwara, alisema kwa hali ya kawaida kabisa, kuna mikoa ambayo umbali kutoka wilaya hadi makao makuu ya mkoa au wilaya ni mbali na inawalazimu wanaohudhuria mafunzo kulala kwa siku 30 za mafunzo.

“Kumbuka wengine tuna familia, unakuta kutoka kituo chako cha kazi hadi makao makuu ya wilaya ni zaidi ya kilomita 100, tena ni rough road (barabara za vumbi) huwezi kwenda na kurudi maana ni kuchoshana na kutesana tu,” alidai.

Ofisa huyo alidai kama Jeshi la Polisi na Serikali linaona umuhimu wa mafunzo hayo waandae bajeti badala ya kuwabebesha mzigo askari na kuitaka Serikali kufafanua kauli ya Waziri Masauni kuwa yamegharimiwa na Serikali kwa asilimia 100.
 
Ninashauri ili kuuenzi muungano Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi ateuliwe kutokea Tanganyika.
Upande wa Tanganyika kuna wananchi 60 milioni hivyo itakuwa rahisi kuudumia wananchi walio wengi.

Pili polisi wengi wako upande wa Tanganyika kuliko visiwani hivyo ni bora wapate kiongozi wao kutokea upande ulio na matatizo mengi.

Waziri wa mambo ya ndani awe amesomea mambo ya kijamii au utawala kuliko kuchukua waliosomea engineering .
 
Acha polisi waione ngondo. Huwa wanaisaidia ccm kuiba kura. Acha wavune walichopanda
 
Hali si shwari ndani ya Jeshi la Polisi, baada ya askari wenye cheo cha kuanzia konstebo hadi mkaguzi wanaohudhuria mafunzo ya utayari nchi nzima, kulalamikia kujigharimia mafunzo hayo, licha ya Serikali kueleza kuwa inatoa fedha kwa ajili hiyo.

Vyanzo mbalimbali vimelidokeza gazeti hili kuwa baadhi ya askari na maofisa walioanzisha vuguvugu hilo kupitia makundi sogozi (Whatsapp) ndani ya jeshi hilo, wanashikiliwa mahabusu katika baadhi ya vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alipotafutwa na Mwananchi azungumzie suala hilo, alisema madai hayo hayana ukweli kwa sababu mafunzo hayo hayalipiwi bali “yanahudhuriwa eneo la kazi na hufanyika saa za kazi za kila siku”.

Vyanzo mbalimbali vimelidokeza gazeti hili kuwa baadhi ya askari na maofisa walioanzisha vuguvugu hilo kupitia makundi sogozi (Whatsapp) ndani ya jeshi hilo, wanashikiliwa mahabusu katika baadhi ya vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alipotafutwa na Mwananchi azungumzie suala hilo, alisema madai hayo hayana ukweli kwa sababu mafunzo hayo hayalipiwi bali “yanahudhuriwa eneo la kazi na hufanyika saa za kazi za kila siku”.
Polisi.jpg

Hotuba hiyo iliibua maswali kutoka kwa baadhi ya askari na kupitia kwenye makundi yao ya Whatsapp, walianza kuhoji kama Serikali inagharimia, inakuwaje wanajigharimia kuanzia nauli, chakula na malazi kwa wanaotoka mbali?

Katika makundi hayo, inaelezwa baadhi walitumia lugha kali inayotafsiriwa kuwa walikiuka mwenendo wa Jeshi hilo, wakitaka waelezwe fedha hizo ziko mikononi mwa nani?

Alichokisema waziri bungeni
Katika hotuba hiyo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Masauni aliliambia Bunge kuwa jumla ya maofisa, wakaguzi, askari na watumishi raia 7,282 wameendelea kupatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo.

“Kati ya hao, 69 ni wa makao makuu ya wizara, 5,041 ni wa Jeshi la Polisi, 662 wa Jeshi la Magereza, 764 ni wa Jeshi la Zimamoto na 751 kutoka idara ya Uhamiaji.

“Mafunzo hayo yamegharimiwa na Serikali kwa asilimia 100 bila kuwa na makato yoyote kutoka kwenye posho za askari. Lengo la mafunzo ni kuimarisha utendaji, kuwaongezea ujuzi, maarifa na stadi katika utekelezaji wa majukumu yao,” alisema.

Waziri aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wizara itaendelea kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji askari, maofisa na watumishi raia ambapo Jeshi la Polisi limetengewa Sh20.7 bilioni.

Polisi wafunguka
Baadhi ya askari waliozungumza na gazeti hili katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Mwanza, Mtwara, Dodoma, Mara na Tanga walithibitisha uwepo wa mafunzo hayo ya utayari na sintofahamu kuhusu nani anayegharimia mafunzo hayo.

“Hili jambo lilianzia kwenye hotuba ya waziri wetu (Mambo ya Ndani) bungeni kwamba Rais (Samia Suluhu) amekubali kutoa fedha na mafunzo haya yanagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100,” alidokeza askari mmoja jijini Dar es Salaam.

“Sasa hapo ndiyo tukaanza kujiuliza mbona tunajigharimia wenyewe kila kitu? Katika baadhi ya makundi ya Whatsapp askari wakaanza kuhoji, naona hili halikuwafurahisha wakubwa, naambiwa baadhi (askari) wako mahabusu,” alidai.

Ofisa mmoja jijini Arusha aliyehudhuria mafunzo hayo, alidai yeye anatoka wilaya ya mbali na makao makuu ya mkoa, hivyo hawezi kwenda na kurudi na inamlazimu kulala hotelini kwa siku zote 30 za mafunzo.

“Mwanzoni ilikuwa ukienda kozi ulikuwa hupewi ile ration allowance (posho ya chakula) ambayo ni Sh10,000 kwa siku, lakini sasa imerudishwa tunashukuru. Ila haya mafunzo ni kututia umaskini tu na tunaambiwa pesa zimetoka,” alidai.

Hata hivyo, ofisa mwingine kutoka Mwanza, alidai kilichowaponza wenzao ambao inadaiwa waliwekwa mahabusu kwa utovu wa nidhamu, ni matumizi ya lugha za kejeli dhidi ya Rais Samia na viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi.

“Sawa, hata kama una haki huwezi kwenda tu kwenye group (makundi) ya Whatsapp na kuanza kudai kwa kejeli. Jeshi la Polisi linaendeshwa kwa nidhamu na amri. Hili lingeweza kujadiliwa kwenye mabaraza ya askari,” alisema.

Ofisa mwingine kutoka mkoani Mtwara, alisema kwa hali ya kawaida kabisa, kuna mikoa ambayo umbali kutoka wilaya hadi makao makuu ya mkoa au wilaya ni mbali na inawalazimu wanaohudhuria mafunzo kulala kwa siku 30 za mafunzo.

“Kumbuka wengine tuna familia, unakuta kutoka kituo chako cha kazi hadi makao makuu ya wilaya ni zaidi ya kilomita 100, tena ni rough road (barabara za vumbi) huwezi kwenda na kurudi maana ni kuchoshana na kutesana tu,” alidai.

Ofisa huyo alidai kama Jeshi la Polisi na Serikali linaona umuhimu wa mafunzo hayo waandae bajeti badala ya kuwabebesha mzigo askari na kuitaka Serikali kufafanua kauli ya Waziri Masauni kuwa yamegharimiwa na Serikali kwa asilimia 100.

CHANZO: Mwananchi
 
Back
Top Bottom