Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 5,820
- 15,343
KESI YA KIKATIBA NA.5/2023:
Majaji wameingia ukumbi Na. 04 muda huu saa 6:05
1. Mark Muluambo - Wakili wa Serikali mkuu
2. Edson Mweyunge
3. Alice Mkulo
4. Edwin MubiloWote watawakilisha Wajibu Maombi.
UPANDE WA WALETA MAOMBI
1. Adv. Boniface MWABUKUSI
2. Philip Mwakilima
3. Livino Ngalimitumba.
Wakili wa serikali SA: Waheshimu Majaji, tulipokutana tarehe 3.7.2023, Mahakama ilitoa amri mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwamba Wajibu Maombi waweze kuleta majibu yao tarehe 14.7.2023, na kwamba kama Waleta maombi watakuwa na majibu ya ziada, waweze kujibu tarehe 19.7.2023.
Waheshimu Majaji, sisi tulifanikiwa kutii amri ya mahakama na tulileta majibu yetu kwa muda uliopangwa.Wenzangu Mawakili wasomi upande wa Waleta Maombi hawakuwa na majibu ya ziada. Na hivyo Tumekubaliana kwamba pleadings are complete" yaani Nyaraka zote zimekamilika kama mahakama ilivyokuwa imeelekeza.Na pia Tumekubaliana kwamba shauri hili sasa linafaa kwaajili ya kusikilizwa.
Hivyo kama wenzetu hawatakuwa na mapingamizi, basi mahakama itamke kwamba shauri hili linafaa kuanza kusikilizwa.Naomba kuwasillisha.
Boniface Mwabukusi (Wakili mleta Maombi): Waheshimu Majaji, ni sahihi kama alivyosema Msomi Wakili Mkuu wa Serikali. Tumepokea majibu yao lakini katika majibu yao wameibua Mapingamizi Manne ya Kisheria.
Na ni taratibu za kisheria kwamba kunapokuwa na mapingamizi ya kisheria, Mahakama hii tukufu huanza na mapingamizi hayo kabla ya kwenda kwenye Shauri la msingi.
Kwa kuzingatia aina ya shauri lililoko mbele yenu na maslahi mapana ya jamii pamoja na mahakama kuweza kutenda haki; ni ombi letu kwenu Waheshimiwa majaji, muone kwamba inafaa kwamba, mapingamizi ya kisheria ya kisheria yaliyoibuliwa pamoja na shauri la msingi yasikilizwe yote kwa pamoja.
Na kwamba, wakati wa kutoa maamuzi; Mahakama hii tukufu ikiona kwamba mapingamizi yale yana mashiko, basi itaishia kutoa uamuzi hapo. Na kwamba kwama mahakama hii itaona mapingamizi yale hayana mashiko basi mahakama iweze kutoa uamuzi kwenye shauri la msingi.
Lengo la ombi letu, ni kuifanya mahakama kwama iweze kumaliza shauri la msingi kwa uharaka, na au kuweza kumaliza jambo hili kwa "Substantive justice." Ni hayo tu Waheshimiwa. I humbly submit.
Wakili wa Serikali: Iwapendeze Waheshimiwa Majaji, nimemsikia msomi mwenzangu. Ni kweli kwamba kwa kawaida kwamba Mahakama huwa inaanza na kumaliza kwanza mapingamizi ya kisheria.
Lakini kutokana na aina hii ya shauri, sina pingamizi kwamba shauri hili lisikilizwe kwa pamoja Mapingamizi na Shauri la Msingi. Hivyo, ikiwa mahakama itaruhusu, tunapendekeza kwamba siku ya Jumanne tarehe 25.07.2023, kama wenzetu hawana kipingamizi basi shauri hili liweze kusikilizwa Mfululizo.
Narudia tena, ni ikiwa wenzetu hawana kipingamizi na iwapo mahakama hii itaridhia. Ni hayo tu Waheshimiwa.
Jaji Ndunguru: Basi kwakuwa tumekubaliana kwamba Pleadings zimekamilika na kwamba shauri hili lipo tayari kwa kusikilizwa.Nasisi upande wa mahakama kwamba shauri hili litasikilizwe kwa pamoja shauri mama pamoja na mapingamizi.
Na kwamba shauri hili litasikilizwa mfululizo. Muda ni saa 3:00 Asubuhi.
Kesi imeahirishwa mpaka jumanne, Julai 25, 2023.
-------
Serikali imewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya kupinga makubaliano ya ushirikiano wa kijamii na kiuchumi baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai, yanayohusisha uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam, ikiiomba Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya isisikilize.
Kesi hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023 imefunguliwa na wanasheria wanne Alphonce Lusako, Emmanuel Kalikenya Changula, Raphael Japhet Ngonde na Frank John Nyalusi, wakipinga makubaliano hayo, wakidai kuwa baadhi ya ibara zina masharti mabovu ambayo hayana maslahi kwa taifa.
Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge la Tanzania.
Sambamba na kesi hiyo ya msingi, pia wanasheria hao wamefungua maombi madogo ya zuio, wakiomba Mahakama hiyo itoe amri ya zuio dhidi ya wadaiwa kuwazuia kuendelea na hatua zozote za utekelezaji wa makubaliano hayo mpaka kesi ya msingi itakapoamuriwa.
Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa leo Alhamis Julai 20, 2023 na jopo la majaji watatu linoloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji Mustafa Ismail na Abdi Kagomba.
Hata hivyo Serikali katika majibu yake ya maandishi iliyoawasilisha mahakamani hapo yakiungwa na kiapo kinzani kujibu madai ya wadai hao, kabla ya kusikilizwa pande zote kwa mdomo, imeibua pingamizi la awali ikiiomba mahakama hiyo iitupilie mbali kesi hiyo kabla ya kuisikiliza.
Katika pingamizi hilo la awali, Serikali imeibua hoja nne za kisheria inazolenga kuishawishi mahakama hiyo kuwa haipaswi kuisikiliza kesi hiyo na badala yake iitupilie mbali.
Kutokana na kuwepo kwa pingamizi hilo la awali, kiutaratibu mahakama inapaswa kuanza kulisikiliza kwanza pingamizi hilo na kulitolea uamuzi
Hata hivyo Lusako, mmoja wa wadai, amelieleza Mwananchi Digital kuwa licha ya kuwepo kwa pingamizi hilo, wataomba kwanza maombi yao ya zuio la muda yasikilizwe kabla ya kusikiliza pingamizi akidai kuwa tayari hatua za utekelezaji wa makubaliano hayo zimeshaanza.
"Makubaliano hayo yanawaruhusu kufanya amendment (marekebisho) ya sheria za ndani. Na tayari wameshaanza kufanya hivyo. Kwa hiyo tunataka kuiomba mahakama kwanza tusikilizwe maombi yetu ya zuio," amesema Lusako.
Amesema kuwa kama watasubiri kusikiliza kwanza pingamizi kama taratibu zinavyoelekeza wakati utekelezaji wa makubaliano hayo, basi kesi hiyo haitakuwa na maana.
Makubaliano hayo baina ya Serikali ya Tanzania yalisainiwa Oktoba 25, 2022.
Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania yalisainiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, kwa mamlaka aliyopewa na Rais Samia Suluhu Hassan yakishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania lilipitisha azimio la kuridhia makubaliano hayo.
Hata hivyo makubaliano hayo yaliibua mjadala mkali unaoendelea mpaka sasa katika mitandao ya kijamii na hata viijiweni, huku wengine wakiyapinga na wengine wakiyaunga mkono
Katikati ya mjadala huo ndipo jopo Mwanasheria Lusako na wenzake walipoamua kufungua kesi Mahakama Kuu Kanda Mbeya, chini ya hati ya dharura kupinga uhalali wa mkataba huo.
Kwa mujibu wa hati ya wadai hao, wanadai kuwa makubaliano hayo ni batili kwa kuwa yanakiuka sheria za nchi za ulinzi wa raslimali na maliasili za nchi na kwamba yaliridhiwa na Bunge kinyume cha utaratibu bila kuwapa nafasi ya kutosha wananchi kutoa maoni yao.
Hivi sasa watu wanaofuatilia kesi hiyo wameshafurika mahakamani wakisubiri kuanza kusikiliza baada ya taratibu kukamilika.
Mawakili wa pande zote wako katika kikao na jopo la majaji wanaoisikiliza kesi hiyo Kwa majadiliano mafupi namna ya kuziendesha kesi hiyo.
Pia soma: Mawakili wataka Serikali ieleze sababu ya 'Kusaini’ Mkataba wa Bandari bila kushirikisha Wananchi
Majaji wameingia ukumbi Na. 04 muda huu saa 6:05
MAWAKILI WANAJITAMBULISHA
UPANDE WA SERIKALI:1. Mark Muluambo - Wakili wa Serikali mkuu