Mbeya: Elias Mwaimse ashikiliwa kwa tuhuma za kuvunja ofisi na kuiba bastola aina ya Short Gun

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga ameeleza kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia Elias Obadia Mwaimse [30] Mkazi wa Mikoroshini Wilaya ya Kyela kwa tuhuma ya kuvunja ofisi mchana na kuiba silaha moja aina ya Short Gun yenye namba T.26444, TZ CAR NA.55089 na risasi zake 17.

Amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo, Aprili 16, 2023 mchana katika Mtaa wa Tacoshill, Kata ya Ndandalo baada ya kuvunja ofisi ya kampuni ya ulinzi iitwayo AB & ANN SECURITY SERVICE CO. LTD na kuiba silaha hiyo na risasi zake 18.

68a97bcb-2452-41bd-b70d-b816201fa414.jpg

Kutokana na tukio hilo, tulianza msako katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyela na mnamo Aprili 21, 2023 majira ya saa 12:00 asubuhi tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa na silaha hiyo na risasi 17 akiwa ameificha juu ya dari kwenye kibanda chake cha biashara. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani.

Pamoja na hayo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na misako dhidi ya wahalifu wa kuvunja nyumba na kuiba, kuvunja maduka na kuiba na kuvunja ofisi nyakati tofauti na kuiba.

Katika Misako iliyofanyika kuanzia Aprili 12 hadi 23, 2023, jumla ya watuhumiwa wa makosa ya uvunjaji 10 wamekamatwa, wapokeaji na wauzaji wa mali za wizi 04 wamekamatwa.

Aidha, watuhumiwa walikutwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni:-
  • TV Flat Screen 04 aina ya Samsung, Startimes, Sunda na Alitop
  • Jokofu aina ya Boss milango miwili
  • Speaker kubwa moja
  • Amplifier mbili
  • Monitor ya Computer aina ya Accer
  • Deck ya TV aina ya Hometec
  • Sub-Woofer Radio mbili
Baadhi ya mali zimetambuliwa na wamiliki.

Kamanda Kuzaga ameongeza kuwa “Sambamba na hayo, tumeendelea na misako dhidi ya dawa za kulevya bhangi na pombe haramu ya Moshi @ gongo. Jumla ya watuhumiwa wa dawa za kulevya 05 walikamatwa wakiwa na kiasi cha gramu 650. Pia watuhumiwa 07 wa pombe haramu ya moshi @ gongo walikamatwa wakiwa na lita 10.”

Akamatwa na kete 13

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ZUBERI MICHAEL [29] Mkazi wa Mama John Jijini Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na kete 13 zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya Heroine.

Mtuhumiwa alikamatwa Aprili 23, 2023 katika Misako iliyofanyika maeneo ya Mama John, Kata ya Ilomba, Jijini Mbeya. Sampuli ya dawa hizo imechukuliwa na kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na mara baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kutoa wito kwa jamii kuachana na vitendo vya uhalifu na badala yake watafute kazi za kufanya ili kujipatia kipato halali.
 
Back
Top Bottom