Mbeya: Askari wa JWTZ amuua Baba yake kikatili akimtuhumu ushirikina

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,105
3,619
Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limethibitisha kutokea mauaji ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Edward Ndonde anayedaiwa kuuawa kikatili kwa kuchomwa visu na mtoto wake, Mussa ambaye ni mtumishi wa Ruvu JKT.

Mussa anadaiwa kufanya mauaji hayo leo Jumatano Januari 12, 2022 nyumbani kwa baba yake mtaa wa Lumbira Kata ya Iwambi jijini Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, Christina Musyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa chanzo ni kutuhumiana kwa mambo ya kishirikina.

Amesema mtuhumiwa ambaye ni mtumishi wa Ruvu JKT amekamatwa baada ya kufanya mauaji hayo na kwamba uchunguzi unaendelea ili hatua za kisheria ziweze kushika mkondo wake.

"Ni kweli tukio lipo na limetokea leo, ambapo pia marehemu alikuwa mwalimu msitaafu, chanzo kinadaiwa kuwa mambo ya kishirikina, ambapo mtuhumiwa alikuwa anamtuhumu baba yake kuwa ni mchawi na Jeshi la Polisi limemshikiria kwa uchunguzi zaidi" amesema Christina.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya, Alhaji Saad Kusilawe amesema marehemu aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Taifa ambapo alikitumikia kwa muda wote kwa uadirifu na kwamba wanasubiri maelekezo kwa ajili ya taratibu za mazishi.

"Tumepoteza hazina ya kiongozi, kwani katika utumishi wake aliweza kumaliza vyema hadi anastaafu, ni pigo kubwa na ni masikitiko makubwa" amesema Kusilawe.

Naye Balozi wa mtaa huo, Hezron Thobias amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alianza kutamka maneno kuwa amemaliza kazi yake aliyoitiwa na baba yake ya kuchinja kuku, jambo lililowashtua na kwenda kuangalia waliposikia kelele zikitoka ndani.

"Alionekana kama ana ugoro na amelewa, akawa anatamka maneno kuwa amemaliza kuchinja kuku, tukamuona mama yake analia anasema njooni muone mtoto alichofanya akiwa anatokwa machozi, ile tunaingia ndani tukakuta amemuua, damu zimemwagika" amesema Thobias.

Mwananchi imefika nyumbani kwa marehemu huyo na kukuta vilio na simanzi vikitawala huku majirani na waombolezaji wakiendelea na taratibu msiba.

Chanzo: Mwananchi, 12 January 2022
 
Juzi ilitokea kaskazini ikatafsiriwa kama tabia ya kabila fulani, leo imetokea kwingine haya mambo hayafai kutafsiriwa kwa picha ya ukabila maana hasira, chuki, tamaa, ugomvi na wivu havina ukabila vinaweza kuwa katika moyo wa yeyote na ikasababisha madhara kama haya ya mauaji.
 
Nyie ndio wabaguzi wakubwa, hili tukio lingetokea kanda ya ziwa maneno yangekuwa mengi sana
Kanda ya ziwa huko hamna madhara, nyie furaha pekee mliyochagua kuwa nayo duniani ni kusonga ugali mkubwa, mkipata ugali mkubwa tu hayo ni mafanikio makubwa sana kwenu Sasa kwenye vita ya ktafuta mafanikio/mali nani atawazungumzia vibaya?
Kaskazini inatafutwa pesa asee had nchi nzima Hadi mihimili ya nchi inashiriki kuweka chuki, maana ukiona huna adui ujue hauna mafanikio.
 
Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limethibitisha kutokea mauaji ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Edward Ndonde anayedaiwa kuuawa kikatili kwa kuchomwa visu na mtoto wake, Mussa ambaye ni mtumishi wa Ruvu JKT.

Mussa anadaiwa kufanya mauaji hayo leo Jumatano Januari 12, 2022 nyumbani kwa baba yake mtaa wa Lumbira Kata ya Iwambi jijini Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, Christina Musyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa chanzo ni kutuhumiana kwa mambo ya kishirikina.

Amesema mtuhumiwa ambaye ni mtumishi wa Ruvu JKT amekamatwa baada ya kufanya mauaji hayo na kwamba uchunguzi unaendelea ili hatua za kisheria ziweze kushika mkondo wake.

"Ni kweli tukio lipo na limetokea leo, ambapo pia marehemu alikuwa mwalimu msitaafu, chanzo kinadaiwa kuwa mambo ya kishirikina, ambapo mtuhumiwa alikuwa anamtuhumu baba yake kuwa ni mchawi na Jeshi la Polisi limemshikiria kwa uchunguzi zaidi" amesema Christina.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya, Alhaji Saad Kusilawe amesema marehemu aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Taifa ambapo alikitumikia kwa muda wote kwa uadirifu na kwamba wanasubiri maelekezo kwa ajili ya taratibu za mazishi.

"Tumepoteza hazina ya kiongozi, kwani katika utumishi wake aliweza kumaliza vyema hadi anastaafu, ni pigo kubwa na ni masikitiko makubwa" amesema Kusilawe.

Naye Balozi wa mtaa huo, Hezron Thobias amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alianza kutamka maneno kuwa amemaliza kazi yake aliyoitiwa na baba yake ya kuchinja kuku, jambo lililowashtua na kwenda kuangalia waliposikia kelele zikitoka ndani.

"Alionekana kama ana ugoro na amelewa, akawa anatamka maneno kuwa amemaliza kuchinja kuku, tukamuona mama yake analia anasema njooni muone mtoto alichofanya akiwa anatokwa machozi, ile tunaingia ndani tukakuta amemuua, damu zimemwagika" amesema Thobias.

Mwananchi imefika nyumbani kwa marehemu huyo na kukuta vilio na simanzi vikitawala huku majirani na waombolezaji wakiendelea na taratibu msiba.

Chanzo: Mwananchi, 12 January 2022
Muuaji kapigwa sana na raia mguu wamemvunjac
 
Juzi ilitokea kaskazini ikatafsiriwa kama tabia ya kabila fulani, Leo imetokea kwingine haya mambo hayafai kutafsiriwa kwa picha ya ukabila maana hasira,chuki,tamaa,ugomvi na wivu havina ukabila vinaweza kuwa katika moyo wa yeyote na ikasababisha madhara kama haya ya mauaji.
Tufunge hesabu na hili tulihamishie kaskazini ili watu wazidi kufurahi kwamba watu wa huko wanauwa wazazi ili warithi mali kwa nguvu.

Pia waseme huyu alikuwa na bei gani au mali kiasi gani mpaka akauwawa.
 
Kanda ya ziwa huko hamna madhara, nyie furaha pekee mliyochagua kuwa nayo duniani ni kusonga ugali mkubwa, mkipata ugali mkubwa tu hayo ni mafanikio makubwa sana kwenu Sasa kwenye vita ya ktafuta mafanikio/mali nani atawazungumzia vibaya?
Kaskazini inatafutwa pesa asee had nchi nzima Hadi mihimili ya nchi inashiriki kuweka chuki, maana ukiona huna adui ujue hauna mafanikio.
Acha dharau boss
 
Back
Top Bottom