Mbatia ataka siasa za kibabe ziepukwe wakati wa uchaguzi

Pengo

JF-Expert Member
Oct 15, 2009
579
10
Habari zilizotangazwa muda huu(saa kumi na mbili) katika taarifa ya habari ya redio Clouds imemnukuu mwenyekeiti wa chama cha siasa cha NCCR mageuzi akiongea kuwa watanzania tujali zaidi utaifa badala ya ubabe kama unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wanaotaka uongozi wa nchi kwa kutoa vitisho vya kumwaga damu za watanzania baada ya uchaguzi.

Mbatia amekwenda mbali zaidi aliposema hao wapuuzi wanaotangaza kumwaga damu baada ya tarehe 31/10/10 ni wasio na fadhila kwa nchi yao na ni wahaini wanaopaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
Hapa Slaa anahusika vipi? Huyu si tunamjua ni ubwabwa jamani? Nashangaa anadhani hatujui ni mtigo
 
Habari zilizotangazwa muda huu(saa kumi na mbili) katika taarifa ya habari ya redio Clouds imemnukuu mwenyekeiti wa chama cha siasa cha NCCR mageuzi akiongea kuwa watanzania tujali zaidi utaifa badala ya ubabe kama unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wanaotaka uongozi wa nchi kwa kutoa vitisho vya kumwaga damu za watanzania baada ya uchaguzi.Mbatia amekwenda mbali zaidi aliposema hao wapuuzi wanaotangaza kumwaga damu baada ya tarehe 31/10/10 ni wasio na fadhila kwa nchi yao na ni wahaini wanaopaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.

HUYU MAMA nanii na yeye, haachi tu kutaka vidume, ameisha ona kuna sauti ya Zege kule roho inamuuma.
 
Mbati amepoteza mwelekeo, na hatapata hata diwani achilia mbali Mbunge au uraisi.. NCCR

Unajua unapokosa mwelekeo hiyo ndiyo madhara yake, Unatapatapa tu. Mbatia toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utaona na utoe banzi kwenye jicho la nduguyo...

Hivi kawe watampa Ubunge kweli, nashauri akikosa 2015 agombe uenYekiti wa kitongoji.. labda atapata..

Slaa aluta kontinua, mapambano yanaendelea.
 
Habari zilizotangazwa muda huu(saa kumi na mbili) katika taarifa ya habari ya redio Clouds imemnukuu mwenyekeiti wa chama cha siasa cha NCCR mageuzi akiongea kuwa watanzania tujali zaidi utaifa badala ya ubabe kama unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wanaotaka uongozi wa nchi kwa kutoa vitisho vya kumwaga damu za watanzania baada ya uchaguzi.Mbatia amekwenda mbali zaidi aliposema hao wapuuzi wanaotangaza kumwaga damu baada ya tarehe 31/10/10 ni wasio na fadhila kwa nchi yao na ni wahaini wanaopaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.
Awe jasiri - awataje wanasiasa hao! Dr Slaa mwenzake alitaja fisadi mmoja hadi mwingine. Tumechoka na siasa nyepesi, tunataka majina ya wanasiasa hai ili tuwashughulikie.
 
Sasa nani wa kuangaliwa Dr slaa au ccm na shimbo? Wao ndio wanawaza kumwaga damu ya watu watakao hoji matokeo hata kama yame chakachuliwa! Mambo mengine ni uwezo wa kuchambua. Kichwa cha habari hakiendani na content! Hoja za kipuuzi ni za kupuuza. Tunaomba hoja za msingi tutadili. Sio hoja za kuhadaa watanzania zilizojaa ukibaraka!
 
alichozungumza kina ukweli asilimia 100.

tanzania imetahidi sana kuweka uwanja mzuri wa kupambana kwenye siasa, sasa iweje baadhi ya viongozi waanze kuimba wimbo mbaya kuwa patamwaika damu.

kauli hizi tuzilaani sote wapenda amani ktk nchi yetu bila ya kujali chama

taratibu zipo na tumejiwekea wenyewe wakiwemo chadema aidha kule dungeni, au kamati ya vyama na maadili au kwa kupitia wadau wa siasa

mifano ipo CHADEMA wagombea wao waliekewa pingamizi na kuzuiwa wasigombee hawakuridhika na wameenda vyombo vya juu na ilipoonekana haki haikutendeka maaamuzi ya awali yalifutwa

sasa huku kuhatarisha amani ya nchi ina maana gani? ni uhaini, tena ni aibu kwa chama ambacho kinadai kutaka kuwasimamia wanyonge wa nchi hii kiko tayari kuwaangamiza

kauli hizo na viongozi wanaozitoa walaaniwe
 
HON Mbatia is quite right. Hatutamfumbia macho mtu yeyote anayetaka kuhatarisha amani ya nchi yetu hata kama ni mwenzetu. Hon Dr Slaa alihamsisha utumiaji wa nguvu hata ikibidi kumwaga damu iwapo hatashinda na ndo maana Vyombo vya Usalama vikatoa onyo ambalo wasioitakia mema tz wamelitafsiri walivyotaka.


Let's think wisely in line with the following from RAIA MWEMA.




ONYO la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vyombo vingine vya usalama limeibua mjadala mpana na mzito nchini. Ni mjadala unaohusu weledi wa mijeledi. Wengine katika vyombo vya habari wanapigia kelele wakisema si weledi kumbe wanaogopa mijeledi!

Baada ya Luteni Jenerali Abdulraham Shimbo kutoa onyo, wapo waliostuka na wakidhani JWTZ imetangaza hali ya hatari, wengine wakidiriki kusema imedhamiria kuinusuru CCM huku wengine wakisema ilikuwa ni kazi ya jeshi la polisi.

Niliposikia hayo wakati nikiwa katika ndege, niliogopa nikidhani wajomba wamechukua hatamu sasa. Hawataki upuuzi na wanataka Jakaya Kikwete aongoze nchi vyema hadi matokeo ya uchaguzi mkuu yatakapotangazwa.

Lakini baada ya kukaa na kutulia, nilitafuta kauli sahihi iliyorekodiwa na kisha nilipata taarifa sahihi kwamba kumbe JWTZ haijatoka kambini kama ilivyokuwa imeripotiwa na wanasiasa na wadau wengine!

Kumbe ilichokuwa imekifanya JWTZ ni kujaribu kuonya vyama (ikiwemo CCM) kwamba hakuna damu itakayomwagika; kwani uchaguzi utafanyika katika mazingira ya amani na utulivu.

Ila, kilichonistua na kuonyesha watu hawajaelewa mantiki ya onyo la JWTZ ambalo ni jeshi lenye historia ya utiifu, ni pale wanasiasa wa Upinzani walipoibuka na nadharia kwamba jeshi limelenga kuinusuru CCM.

Nilipaswa kurejea onyo la Luteni Jenerali Shimbo, lakini bado nilipata ukakasi kuoanisha na kile kilichozungumzwa na Upinzani asubuhi yake. Wapinzani ambao baadhi tunafikiri ni wanasiasa wasomi, wakajikuta katika lindi la ujinga.

JWTZ ilisema, kwa niaba ya vyombo vya ulinzi na usalama: "Hakuna umwagaji damu utakaofanyika. Uchaguzi utafanyika kwa amani na kwamba vyombo hivyo viko tayari kupambana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani."

Hapa ukifanya uchambuzi wa kimaduhui, huoni hata sehemu moja ambayo JWTZ inasema imepanga kuibebea mbereko CCM kama ilivyodaiwa na vyama vingine vya Upinzani.

Jambo la ajabu kabisa ni kwamba, hata mwanangu wa chekechea alimwelewa Shimbo. Alichokisema ni kwamba, wao wa vyombo vya ulinzi na usalama watakabiliana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani ya nchi.

Lakini, nilistuka kusikia eti JWTZ imepanga kuinusuru CCM! JWTZ haikusema kwamba vyama vya Upinzani vikubali matokeo yoyote ambayo yatatangazwa kwamba CCM imeshinda. Ilichosema ni kwamba vyama vya siasa, ikiwemo CCM, vikubali matokeo yoyote.

Sasa unaweza kuona jinsi uwezo wa kufikiri wa baadhi ya wanasiasa wetu ulivyo mdogo au kuchanganyikiwa na mambo mengi ya maisha. Ni wanasiasa wenye migogoro ya kinafsia.

Wanasiasa wenye migogoro ya kinafsia, kifamilia na jamii, ndiyo ambao huweza kutamka na kurupoka kile walichoota jana usiku kwamba, kuna njama za kutaka kumuua. Inawezekana jana usiku mwanasiasa aliota kakabwa na jinamizi la usingizini, basi, anaamka asubuhi na kuambia umma yuko tayari kuuawa!

Huu ndiyo ujumbe tuliopata baada ya JWTZ kutoa onyo. Jeshi lina dhima ya kulinda nchi kutoka maadui wa ndani na nje, Jeshi lina intelejensi yake (Military Intelligence), kwa mantiki hiyo, linapozungumza kuna njama za watu kuvuruga amani, huwa halikurupuki.

Nilitegemea wananchi walipongeze jeshi kwa kuonyesha msimamo mapema na kutoa onyo kwa watu wanaotaka kuivuruga nchi. Unashangaa unaona wanasiasa wenye kuangalia madaraka badala ya Tanzania wanakurupuka na kulihusisha jeshi na mbeleko kwa CCM.

Wapo wanaosema JWTZ imeenda mbali zaidi kwani hilo lilikuwa jukumu la jeshi la polisi, lakini wamesahau kwamba hatua ya jeshi kuchelewa kuchukua hatua ndiko kunakofanya nchi kuvurugika na damu kumwagika.

Leo hii, watu wanalalamika uzembe katika kudhibiti mauaji ya halaiki ya Rwanda, kwa sababu Dk. Kofi Annan akiwa mkuu wa Ulinzi na Usalama wa UN, alishindwa kushauri umoja huo haraka kuzuia mauaji nchini humo.

Kwa mantiki hiyo, JWTZ iko sahihi kuhakikisha amani ya nchi haivurugwi na maadui wa ndani au nje. Jeshi limekuwa sahihi kutoa onyo mapema kwa sababu hatuwezi kuruhusu umwagaji damu wa kutisha ndipo tuombe nguvu za jeshi.

Amani na usalama wa nchi haufanyiwi majaribio. Amani, uhuru na umoja wa kitaifa unalindwa kwa nguvu. JWTZ imekaa katika nafasi yake husika.

Nimestushwa kusikia kauli ya JWTZ ikihusishwa na mbereko dhidi ya CCM. Hili ni jambo la kipumbavu. Kwa nini CCM ikae kando wakati nacho ni chama cha siasa kinachopaswa kutii matokeo kama kikishindwa?

Uropokaji huu wa wapinzani umezidi kuifanya CCM ionekane kama ni chama makini, kilichobobea katika siasa na kisichokurupuka. Ndiyo maana, ingawa chenyewe ni chama cha siasa, hakikutaka kukurupuka na kuirukia JWTZ.

Kwani kinajua jeshi letu lina nidhamu ya hali ya juu, halijihusishi na mambo ya siasa za majitaka, lina nidhamu, utiifu na uzalendo.

Hivyo, kudhani kauli ya JWTZ ni mbereko kwa CCM ni mawazo yasiyosadikika, na ni dhana tu isiyo na mashiko. Ni vema vyama vikaiga ukimya wa CCM.







 
Habari zilizotangazwa muda huu(saa kumi na mbili) katika taarifa ya habari ya redio Clouds imemnukuu mwenyekeiti wa chama cha siasa cha NCCR mageuzi akiongea kuwa watanzania tujali zaidi utaifa badala ya ubabe kama unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wanaotaka uongozi wa nchi kwa kutoa vitisho vya kumwaga damu za watanzania baada ya uchaguzi.

Mbatia amekwenda mbali zaidi aliposema hao wapuuzi wanaotangaza kumwaga damu baada ya tarehe 31/10/10 ni wasio na fadhila kwa nchi yao na ni wahaini wanaopaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.

nimepita bagamoyo road leo naona mabango/picha za Halima Mdee karibu zote zimetiwa X kwa wino mwekundu na sehemu zingine wamepaint red...jamaa haamini anayoyaona hapa Kawe,amekuwa mpinzani wa upinzani sana. Kama anahuisika na uhuni wa kuchezea picha za wagombea wenzake atakuwa amepoteza dira kabisa.....arudi CHICHIEMU wakampe cheo cha propaganda kama wenzake. kazi ya upinzani inataka ugangamale.
 
..JK aliposema wafanyakazi wakiandamana, wanaweza kuuwawa na kuanza kutolea mifano ya Kilombero, nani alimkanya?

..hizi habari za kutokea vurugu ni kwasababu wananchi wanaamini kwamba CCM siko zote huwa inacheza rafu.

..sasa labda Lt.Gen.Shimbo angetumia demokrasia kwa kuwahakikishia wananchi kwamba jeshi litahakikisha hakuna uwizi wa kura, na kwamba watahakikisha uchaguzi unakuwa free and fair.
 
Back
Top Bottom