Mbadala wa matumizi ya "shikamoo" wenye heshima ile ile

Unaiogopa Salaam ya Yesu Alayhi Salaam?
Mkuu hapa tofauti ni lugha iliyotumika tu, maana ni moja..sholom ni amani..vivyo hivyo na hiyo ya asalam al..
Ni lugha na dini tulizoletewa ambazo pia hazipaswi kututenganisha mimi na wewe..au wasemaje faiza
 
Kipi bora utoe salamu ya kitumwa shikamoo au utoe salama ya kawaida ambayo itamjulia hali mtu wa rika lolote lile
Mim sion utafauti kimantiki kati ya asalam aleykum na habari yako... mtamo tu ndugu

Hiyo explanation yako ya kuwa shikamoo ni salaam ya kitumwa haiingii akilini hata chembe, mimi naona ni uzushi tu.

Halafu, Asalaam Alaikum na habari yako ni vitu tofauti kabisa.

Halafu, wakati nyinyi akina juliasi mnahangaika kutafuta mbadala sisi tayari kwa enzi na enzi tunatumia salaam aliyoitumia pia Yesu Alayhi Salaam, Asalaam Alaikum. Haina walakin, haina gender haina mkubwa wala mdogo.

Mmechelewa jamvini karamu imeshaliwa.
 
Bwana asifiwe, naona imetulia?
 
ila kwa kweli shkamoo ni salamu ya kitumwa sana yn. mi napendekeza zitumike (za asubuh,za mchana, za jioni, za sa hz. mambo, niaje, mzima, )
 
Heshima yako Mkuu,ni salamu nayopenda sana kuitumia kuliko Shikamoo
 
Mimi hutoa shkamoo kama ishara ya heshima tu na wala si kujitumikisha...

Sijali na sitojali watu waitafsirivyo lakini kwangu itabakia kuwa ishara ya heshima tu....

Kufaa na kutokufaa kwa kitu huendeshwa na akili yako......mbona hata mama huitwa nyoko kwa kihaya na wala haiwasumbui

Utamu wa peremende ni mate yako
 
binafsi huwa sipendi kusalimiwa au kusalimia SHIKAMOO. sababu kubwa ni historia ya neno lenyewe kuwa la enzi za utumwa "NIKO CHINI YA MIGUU YAKO" lakin ningependa kumsalimia kwa adabu anayestahili. sasa wataalam wa lugha na maadili mnisaidie mbadala wa matumizi ya neno hilo na maana na adabu ibaki palepale. nilipokuwa Pemba nilifurahia matumizi ya asalaam aleikhum kwa rika zote. lakin kwa huku mikoani ni salaam yenye tafsiri ya dini ya uislam. huwez kuitumia pote ukaeleweka.
KIDUNIA SIO KWELI, wapo wakristo wengi tu huko Egypt, Israel,Palestina, na kuna jimbo lipo uingereza lenye waislam wengi huwa wanatumia salam hiyo ya "Asalaam Aleykyum" Hii ni kutokana adoption kwa waislam wengi walioispread lugha ya kiarabu maeneo hayo.

Kwa Tanzania salamu hiyo inatumika zaidi Zanzibar na mikoa ya pwani,ila pia kuna maeneo ya bara sehemu flan flan inatumika hiyo,mfano kwa Arusha kuna maeneo ya ndani kama Kaloleni,Ngarenaro n..k

The same to some parts za Mwanza,Dodoma,Singida etc.

Ni salamu yenye maana nzuri kama ilivyo Shaloom.

Then pia usicomplicate vitu vidoogo hivyo hata ukisema habari yako...au vipi...poa. baasi.
 
Bwana asifiwe, naona imetulia?

Naam hakuna wakusifuwa zaidi ya Bwana wa mabwana asiyezaa wala kuzaliwa, Muumba wa Ardhi na mbingu aliyemtuma Yesu Alayhi Salaam kama alivyowatuma Mitume wake wengine wote kuja kutufundisha mema na kutukataza mabaya.

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar.
 
Yote haya ya nin?
 
Hakuna kweli wa kusifiwa zaidi ya Yesu Kristo Mungu kutoka Kwa Mungu. Aliyejifanya MTU Kwa ajili yetu.

Kila mtu Na maoni yake though.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom