Maziwa ya kopo yanayofaa kwa mtoto mchanga

MDANGANYIKAJI

Member
Jan 27, 2011
77
59
Nina mtoto mchanga wa miezi 2 na nakaribia kurudi kazini sijajua ni maziwa gani bora ya kopo ya kumwanzishia naombeni msaada wadau
 
Miezi miwili umepe maziwa ya Ng'ombe/ kitimoto? Acha usharobaro wa kipuuzi huo. Kama ni kazi nenda nae panga chumba/nyumba utakuwa unachomoka mara1 moja unampa stahiki yake i:e Nyonyo. Mbwembwe zako zitampoteza huyo mwanao.
 
Ungejitahidi ukamnyonyesha nyonyesha. . .ila kama unalazimika jaribu Nestle. Wana formula za kila umri, zingatia sana hilo.
 
Nina mtoto mchanga wa miezi 2 na nakaribia kurudi kazini sijajua ni maziwa gani bora ya kopo ya kumwanzishia naombeni msaada wadau

Maziwa ya SMA gold, pale Namanga anza na number 1, Kama una maziwa mengi, nunua kile kimashine cha avent na uwe unaexpress maziwa yako asubuhi kabla ya kwenda kazini....hata sasa hivi anza kuexpress yanakaa maximum miezi 3 yakihifidhiwa vizuri,Mimi nimefanya hivyo kwa wanangu wote na SMA angalia nembo ya ubora gold.
 
Siku hizi tunakamua maziwa yetu wenyewe na kuyahifadhi kwa frizer,then watakuwa wanampa,at the same time na wewe unakuwa unarudi kumnyonyesha,ila kama upo dar na foleni hii.
 
nafikri njia nzuri tumia maziwa ya Ng'ombe.weka bill sehemu ya liter 5 au 10 ,weka kwenye fridge hawe anatumia taratibu,yakikalibia kuisha unaagaiza mengine hivyo hivyo..
 
Nina mtoto mchanga wa miezi 2 na nakaribia kurudi kazini sijajua ni maziwa gani bora ya kopo ya kumwanzishia naombeni msaada wadau
Achana na kuhangaika sana kuna madaktari bingwa wa watoto,Dk MASSAWE NA DK DULLA wapo hapo Morroco karibu kabisa na hilo ghorofa ya Zain(Airtel) na panaitwa Huruma Clinic.Nenda hapo wakushauri.Ila maziwa ya ng'ombe hayafai yatamletea mwanao pumu.
 
nafikri njia nzuri tumia maziwa ya Ng'ombe.weka bill sehemu ya liter 5 au 10 ,weka kwenye fridge hawe anatumia taratibu,yakikalibia kuisha unaagaiza mengine hivyo hivyo..

Wewe maziwa ya ng'ombe sio sahihi kwa watoto chini ya mwaka mmoja. Yana protein nyingi zaidi ya kiasi wanachohitaji.
 
Mtoto kwa kawaida anatakiwa kunyonya kwa miezi sita ukishindwa basi angalau miezi minne hadi mitano. Maziwa ya mama ndo chakula pekee yaliyojitosheleza kwa virutubisho.
Maziwa yako yanmsaidia kujenga kinga ya mwili lakini pia kujenga akili yaani iq ya mtoto. Zipo faida nyingi sana ila hizi ndo za mhimu ambazo maziwa ya ng'ombe au formular hayana. Maziwa ya mama yakikamuliwa yanaweza kukaa kwa masaa nane bila kuharibika na bila kuweka kwenye friji. Ninavyofahamu kama mfanyakazi unatakiwa kufanya masaa sita, kwa hiyo ukimkamulia 200mls kila siku zinamtosha sana kunywa mpaka utakapo rudi baada ya masaa 6. Kwa kawaida mtoto anatakiwa kunyonya angalau kila baada ya masaa matatu, mfano kama unatakiwa kazini saa 2 asub ukmnyonyesha saa 1, yale uliyokamua anywe saa tatu/nne baada ya masaa 3 yanayofuta utakuwa umesharudi.
Uzuri siku hizi kama huwezi kukamua vipo vifaa vya kukamulia siku hizi vipo unaweza kamua mpaka 500mls, sioni haja kumwazishia maziwa ya ng'ombe au formular.
Ushuhuda:
mimi ninamtoto wangu wa mwaka 1 na miezi 3, alinyonya mpaka miezi 5 bila kupewa kitu chochote cha ziada.
Alikuwa akiongezeka uzito kila mwenzi na kila mwenzi aliongezeka kwa 0.8kg hadi 1.8kg, hadi sasa anatembea. Baada ya miezi mitano alainza kupewa uji na maziwa ya ng'ombe na baadaye kila chakula anakula.
Hivyo acha kumexpose mtoto na artificial foods ataanza kukusumbua na fever zisizo za maana. Kwa mara ya kwanza aliiugua baada ya kuanzishiwa vyakula vinginne.
Note. Vyombo vya kukamulia hakikisha unaosha mwenyewe na mtoto akinywea chombo hicho asirudie tena kukitumia hicho kinaenda moja kwa moja kwa maandalizi ya kuoshwa kwa matumizi ya siku nyingine. Acheni tabia ya kuwaachia mahouse girls wanawafanyia kila kitu. Mimi kama Baba niliplay part kwa khakikisha kile kinashauriwa na madaktari kinafuatwa. Ingawa mimi mwenyewe na mama yake wote ni madaktari, bibi zake niligombana nao sana wakisema hataongezeka uzito lakini waliona tofauti. Binafsi namlea mwanangu kama kitabu kinavyoeleza na nimeona faida zake. Understanding capacity yake ni nzuri alianza kuelewa akiwa na miezi minne. Nikimwambia piga makofi aliweza. Na hili ndo lilikuwa neno la mwanzo klielewa. Tunzeni watoto wenu msiwaachie house girls.
Kama kuna sehemu sijaeleweka basi naomba maswali coz natumia simu.
Nawatakia siku njema kwa jina la Bwana.
 
kunyonya miezi mitano bila yeye kwenda kazini? ,mtoto ambaye hanyonyi fulltime huwa anakula sana kama ukiweza kamua na pia kama unampa ya ng'ombe yanatakiwa yachanganywe na maji ratio sawa na maziwa zingatia usafi wa vyombo vya kumlishia vinatakiwa vikae kwenye maji ya moto muda wote hakikisha una uhakikika wa hayo maziwa ya ng'ombe yanakotoka na kama ni ya kopo tumia lactogen 1 zingatia masharti
 
Maziwa ya SMA gold, pale Namanga anza na number 1, Kama una maziwa mengi, nunua kile kimashine cha avent na uwe unaexpress maziwa yako asubuhi kabla ya kwenda kazini....hata sasa hivi anza kuexpress yanakaa maximum miezi 3 yakihifidhiwa vizuri,Mimi nimefanya hivyo kwa wanangu wote na SMA angalia nembo ya ubora gold.
Nitakipata wapi kimashine cha avent cha kukamulia maziwa ya mama? na kwa shiling ngapi?
 
Fanya ufanyavyo ili uhakikishe mtoto ananyonya maziwa yako si chini ya miezi minne fululizo, la sivyo kila siku utampeleka hosptali, utasumbuana sana na walimu na hata tuisheni na ataendelea kuwa wa mwisho darasani.
Hizi njia za shotcut (za kurahisisha mambo) zinaligharimu taifa sana. Kumbuka maziwa ya ng'ombe, mbuzi n.k hayakuumbwa kwa ajili ya mtoto binadamu. Mtoto wa binadamu hukua zaidi ubongo (cognitive capacity) tofauti na mifugo, mifugo hukuwa zaidi misuli na viungo. Maziwa ya kopo ni feki au yapo chini ya viwango. Mbaya zadi, hayaendani na kasi ya ukuaji na uhitaji wa mwili wa mtoto.
Kama unampenda mwanao, mpe maziwa aliyopendekeza Mungu.
 
Nina mtoto mchanga wa miezi 2 na nakaribia kurudi kazini sijajua ni maziwa gani bora ya kopo ya kumwanzishia naombeni msaada wadau
mie pia namkamuliaga nikiwa natoka nilijua ni akili zangu mbovu kumbe niend6elee japo nampaja na lactojen 1 kama maziwa niliomkamulia yatakua yamekwisha,
mtoto anakua vizuri na mchangamfu na mwenye akili
 
Mtoto kwa kawaida anatakiwa kunyonya kwa miezi sita ukishindwa basi angalau miezi minne hadi mitano. Maziwa ya mama ndo chakula pekee yaliyojitosheleza kwa virutubisho.
Maziwa yako yanmsaidia kujenga kinga ya mwili lakini pia kujenga akili yaani iq ya mtoto. Zipo faida nyingi sana ila hizi ndo za mhimu ambazo maziwa ya ng'ombe au formular hayana. Maziwa ya mama yakikamuliwa yanaweza kukaa kwa masaa nane bila kuharibika na bila kuweka kwenye friji. Ninavyofahamu kama mfanyakazi unatakiwa kufanya masaa sita, kwa hiyo ukimkamulia 200mls kila siku zinamtosha sana kunywa mpaka utakapo rudi baada ya masaa 6. Kwa kawaida mtoto anatakiwa kunyonya angalau kila baada ya masaa matatu, mfano kama unatakiwa kazini saa 2 asub ukmnyonyesha saa 1, yale uliyokamua anywe saa tatu/nne baada ya masaa 3 yanayofuta utakuwa umesharudi.
Uzuri siku hizi kama huwezi kukamua vipo vifaa vya kukamulia siku hizi vipo unaweza kamua mpaka 500mls, sioni haja kumwazishia maziwa ya ng'ombe au formular.
Ushuhuda:
mimi ninamtoto wangu wa mwaka 1 na miezi 3, alinyonya mpaka miezi 5 bila kupewa kitu chochote cha ziada.
Alikuwa akiongezeka uzito kila mwenzi na kila mwenzi aliongezeka kwa 0.8kg hadi 1.8kg, hadi sasa anatembea. Baada ya miezi mitano alainza kupewa uji na maziwa ya ng'ombe na baadaye kila chakula anakula.
Hivyo acha kumexpose mtoto na artificial foods ataanza kukusumbua na fever zisizo za maana. Kwa mara ya kwanza aliiugua baada ya kuanzishiwa vyakula vinginne.
Note. Vyombo vya kukamulia hakikisha unaosha mwenyewe na mtoto akinywea chombo hicho asirudie tena kukitumia hicho kinaenda moja kwa moja kwa maandalizi ya kuoshwa kwa matumizi ya siku nyingine. Acheni tabia ya kuwaachia mahouse girls wanawafanyia kila kitu. Mimi kama Baba niliplay part kwa khakikisha kile kinashauriwa na madaktari kinafuatwa. Ingawa mimi mwenyewe na mama yake wote ni madaktari, bibi zake niligombana nao sana wakisema hataongezeka uzito lakini waliona tofauti. Binafsi namlea mwanangu kama kitabu kinavyoeleza na nimeona faida zake. Understanding capacity yake ni nzuri alianza kuelewa akiwa na miezi minne. Nikimwambia piga makofi aliweza. Na hili ndo lilikuwa neno la mwanzo klielewa. Tunzeni watoto wenu msiwaachie house girls.
Kama kuna sehemu sijaeleweka basi naomba maswali coz natumia simu.
Nawatakia siku njema kwa jina la Bwana.
asante. nami ninamtoto mchanga anamiezi miwili na nusu karibia ninanza kazi ivo vifa vya kukamulia maaziwa nitavipata wapi?nipo arusha. ninataka mwanangu hadi atimize miezi 6 ndipo anze kula vyakula vingine
 
nenda kwenye maduka ya vyombo vya nyumbani ulizia vifaa vya kukamulia,
 
Maziwa ya mama ni ya muhim sana ivo jitaidi umpatie mzaziwa yako mpaka miez 6. Kama ulivoelekezwa cha muhim sana ni kukamua maziwa yako mwenyewe, ukiwa na uwezo wa mashine ni sawa. Fanya hima kukamua maziwa pindi unapoanza kazi kwa kuwa usipokamua maziwa yatapungua ghafla sana na hatimae kukosa kabisa. Cha muhim zingatia usafi, na jins ya khifadhi. Hakikisha unamwelimisha anaemtunza mtoto jinsi ya kuongeza joto la hayo maziwa kabla ya kumpa mtoto. Si kuyapasha jikon bali weka chupa ya kumlishia ktk chombo chenye maji ya joto kwa muda ili maziwa yapate joto linalokaribia na la mwili
 
kama utataka maziwa ya kopo SMA yako vizuri na bei 50000 tu.mwanangu anatumia na yuko poa tangu nirudi kazini.
 
Back
Top Bottom