Mazishi ya Wapigania Uhuru wa TZ huko Arusha waliouawa kidhalimu 5 January 2011

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Waungwana,

Napenda kutoa ombi kwenu ili tufanye mchango wa nguvu kuwasaidia katika gharama za mazishi ndugu, jamaa na marafiki wa wale ambao wamepoteza maisha yao katika mauaji yaliyotokea Arusha na pia kuwasaidia wale waliojeruhiwa pesa za matibabu.

Invisible, Maxence na Mods tafadhali nawaomba muandae utaratibu wa kukusanya pesa toka ndani na nje ya nchi ili kufanikisha jambo hili na kututaarifu rasmi wapi tupeleke michango yetu.

Natanguliza shukrani.

UPDATE: Soma pendekezo la mkuu Gurudumu hapa

Ndugu wananchi wenzangu tunaopigania uhuru wa kweli wa nchi yetu ya Tanganyika, poleni sana. Serikali haramu ya CCM katika jiji la Arusha imeua waajiri wake (wananchi), imewajeruhi, kuwadhalilisha, kuwatesa, kuwapiga mabomu ya machozi, kuwarushia maji washawasha, kuwakera, kuwakimbiza hovyohovyo, kuwafarakanisha na familia na ndugu zao, kuwasababisha wasiendelee na kazi zao za kujipatia kipato, na kuwadharau. Imewaweka korokoroni viongozi halali wa wananch, na leo nasikia itawafikisha mahakamani.

Wakati kwenye thread nyingine tunahabarishana kinachojiri na kujieleza hisia zetu, nimeona nianzishe hii thread kuomba na kuelekeza yafuatayo;

1. Tuoneshe heshima yetu ya dhati kwa kuwaenzi wale waliokufa katika harakati hizi za siku ya kwanza ya kudai uhuru na ukombozi wa kweli wa nchi yetu Tanganyika (hata kama ni polisi alikufa). Ndugu, jamaa na marafiki zao watafarijika sana kuona kwamba wamepoteza ndugu zao ambao wanathaminiwa na wananchi wote. Kwanza walio arusha wafuatilie kwa kina details za waliokufa watupatie. Pili, watutangazie tarehe za mazishi kwa kila mmoja wao na eneo/mkoa ambapo maziko yatafanyika. Tatu, chadema wafungue bank account ili tupitishe michango yetu humo kuwafariji waliofiwa. Hii ina maana kama aliyekufa ni bread earner wa familia basi watoto wake wapelekwe shule na mambo kama hayo.

2. Waliojeruhiwa na kulazwa hospitali watambuliwe na kuorodheshwa kwenye tovuti maalumu ya uhuru wa kweli wa Tanganyika (ianzishwe). Kisha walio arusha na wale wanaoweza kusafiri kuelekea huko wawatembelee hawa majeruhi na kuwafariji. Michango yetu pia itumike kugharamia matibabu yao. Wapewe cheti maalumu cha kutambua mchango wao katika kudai uhuru wa kweli ya nchi yetu Tanganyika, ili hata vitukuu vyao viwe na ushahidi wa kujivunia.

3. Kwenye picha za jana, niliona baadhi ya wakina mama wachache sana pale uwanjani. Nilisisimka! Naomba watafutwe nao waorodheshwe na kutambuliwa kwa namna ya pekee. Hawa ndio wanawake wanaojua uwezo wao, siyo wale wanaosubiri kuwezeshwa ndipo waweze. Pia kwenye picha niliona wabunge wanawake wa Chadema na Mke wa Rais wa Ukweli wa Tanganyika, itafurahisha kama watatambuliwa kwa namna ya pekee pia

4. Wapinganaji wenzetu wamekamatwa na polisi na watafikishwa katika mahakama. Tunaomba pia tuchangie gharama za kesi na kujikimu kwao na wale wanaoshuhulikia hili tatizo

5. Tuanzishe kalenda ya ukombozi na kudai uhuru wa Tanganyika, ikianzia tarehe 5 January 2011. Chadema waanzishe kitengo cha kurekodi kumbukumbu za matukio na vitendo vyote kila siku ili vije kutumika kuandika historia ya kweli ya ukombozi wa nchi yetu. Taarifa hizi ziwe wazi kwenye tovuti ili kuepusha kuchakachuliwa kama ccm walivyochakachua histori ya tanzania

6. Kila mmoja wetu katika eneo alilopo, achangie na kugharamia harakati za wananchi wanaounga mkono mapambano ya kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye mikono ya hawa makuwadi, matapeli, majambazi, na wauaji. Eneza habari mtaani kwako, kazini kwako na hata mahali popote unapotembelea. Watu wengi bado wana imani kwamba serikali yetu ni tukufu na hawajui matatizo makubwa ya utawala huu uliopo madarakani sasa hivi.

Sina mamlaka wala wadhifa wa kutoa tamko, bali ni mawazo yangu tu
 
is that all you can say BAK. Kwa hiyo JF itakuwa kuchanga michango ya mazishi tu. Leo ya waliokufa Arusha, kesho watakaokufa Moshi, Mwanza, Mbeya, Kigoma, etc? Vipi kuhusu familia na watoto walioachwa na wazazi wao, nao tutawachangia vile vile au ndio bye bye do, sie tunaendelea na mapambano?

We have to think twice on how we go about police and wanachama wetu. Something is wrong somewhere.

Life is so precious as live only once.
 
Mazishi na matibabu ni vitu ambavyo ni lazima vifanyike sasa hivyo hiyo michango inahitajika haraka sana ili kusaidia ndugu, jamaa na marafiki wa wahusika. Kuwasaidia wote walioachwa na marehemu (kama ni wake, waume, watoto n.k) kunaweza kujadiliwa na kutafuta namna ya kuwasaidia.

Miye kwa maoni yangu kuandamana ni haki mojawapo ya msingi kwa Watanzania, polisi kama wana wasiwasi kwamba kunaweza kutokea machafuko basi watoe ulinzi wa kutosha kuhakikisha maandamano yanakuwa ya amani na si kuyazuia kwani hii ni kuwanyima haki Watanzania ambayo wanastahili kuwa nayo siku yoyote ile na pia bila kuingiliwa na mtu yeyote yule.
 
Analysis ifanywe kwa waathirika wote wa mauaji yaliyofanywa na mafisadi ikiwa ni pamoja na familia za waliouawa, kama wapo. Halafu tuhamasishane sisi kwa sisi namna ya kuchangia ili tuwasaidie ndugu zetu ambao jamaa zao wamepoteza maisha wakiipigania haki yao.
 
Waungwana,

Napenda kutoa ombi kwenu ili tufanye mchango wa nguvu kuwasaidia katika gharama za mazishi ndugu, jamaa na marafiki wa wale ambao wamepoteza maisha yao katika mauaji yaliyotokea Arusha na pia kuwasaidia wale waliojeruhiwa pesa za matibabu.

Invisible, Maxence na Mods tafadhali nawaomba muandae utaratibu wa kukusanya pesa toka ndani na nje ya nchi ili kufanikisha jambo hili na kututaarifu rasmi wapi tupeleke michango yetu.

Natanguliza shukrani.

Huu mchango unahusu mazishi ya wafuasi wa CDM tu au na Polisi wetu waliopoteza uhai wao wakiwa ktk utumishi wa umma?
 
Umeona kuna mahali hapo nimeandika CHADEMA au unataka kuanzisha longolongo lisilokuwepo!? Watu wengine bwana!!!!
 
mm sichangi na niko kinyume kutumia jamiiforums kuchanga kwa watu waliopingana na serikali

ss la kufanya ni kutuma ujumbe mkali na karipio kwa waliosababbisha haya, ambao ni uongozi wa chadema kuwatumia wananchi kwa maslahi yao
 
Jambo Zuri Tunaomba Utaratibu Hapa Kusaidia Mashujaa wa Nchi. Wamepigwa Risasi Kwa Ajili Yetu.
 
Ndugu wananchi wenzangu tunaopigania uhuru wa kweli wa nchi yetu ya Tanganyika, poleni sana. Serikali haramu ya CCM katika jiji la Arusha imeua waajiri wake (wananchi), imewajeruhi, kuwadhalilisha, kuwatesa, kuwapiga mabomu ya machozi, kuwarushia maji washawasha, kuwakera, kuwakimbiza hovyohovyo, kuwafarakanisha na familia na ndugu zao, kuwasababisha wasiendelee na kazi zao za kujipatia kipato, na kuwadharau. Imewaweka korokoroni viongozi halali wa wananch, na leo nasikia itawafikisha mahakamani.

Wakati kwenye thread nyingine tunahabarishana kinachojiri na kujieleza hisia zetu, nimeona nianzishe hii thread kuomba na kuelekeza yafuatayo;

1. Tuoneshe heshima yetu ya dhati kwa kuwaenzi wale waliokufa katika harakati hizi za siku ya kwanza ya kudai uhuru na ukombozi wa kweli wa nchi yetu Tanganyika (hata kama ni polisi alikufa). Ndugu, jamaa na marafiki zao watafarijika sana kuona kwamba wamepoteza ndugu zao ambao wanathaminiwa na wananchi wote. Kwanza walio arusha wafuatilie kwa kina details za waliokufa watupatie. Pili, watutangazie tarehe za mazishi kwa kila mmoja wao na eneo/mkoa ambapo maziko yatafanyika. Tatu, chadema wafungue bank account ili tupitishe michango yetu humo kuwafariji waliofiwa. Hii ina maana kama aliyekufa ni bread earner wa familia basi watoto wake wapelekwe shule na mambo kama hayo.

2. Waliojeruhiwa na kulazwa hospitali watambuliwe na kuorodheshwa kwenye tovuti maalumu ya uhuru wa kweli wa Tanganyika (ianzishwe). Kisha walio arusha na wale wanaoweza kusafiri kuelekea huko wawatembelee hawa majeruhi na kuwafariji. Michango yetu pia itumike kugharamia matibabu yao. Wapewe cheti maalumu cha kutambua mchango wao katika kudai uhuru wa kweli ya nchi yetu Tanganyika, ili hata vitukuu vyao viwe na ushahidi wa kujivunia.

3. Kwenye picha za jana, niliona baadhi ya wakina mama wachache sana pale uwanjani. Nilisisimka! Naomba watafutwe nao waorodheshwe na kutambuliwa kwa namna ya pekee. Hawa ndio wanawake wanaojua uwezo wao, siyo wale wanaosubiri kuwezeshwa ndipo waweze. Pia kwenye picha niliona wabunge wanawake wa Chadema na Mke wa Rais wa Ukweli wa Tanganyika, itafurahisha kama watatambuliwa kwa namna ya pekee pia

4. Wapinganaji wenzetu wamekamatwa na polisi na watafikishwa katika mahakama. Tunaomba pia tuchangie gharama za kesi na kujikimu kwao na wale wanaoshuhulikia hili tatizo

5. Tuanzishe kalenda ya ukombozi na kudai uhuru wa Tanganyika, ikianzia tarehe 5 January 2011. Chadema waanzishe kitengo cha kurekodi kumbukumbu za matukio na vitendo vyote kila siku ili vije kutumika kuandika historia ya kweli ya ukombozi wa nchi yetu. Taarifa hizi ziwe wazi kwenye tovuti ili kuepusha kuchakachuliwa kama ccm walivyochakachua histori ya tanzania

6. Kila mmoja wetu katika eneo alilopo, achangie na kugharamia harakati za wananchi wanaounga mkono mapambano ya kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye mikono ya hawa makuwadi, matapeli, majambazi, na wauaji. Eneza habari mtaani kwako, kazini kwako na hata mahali popote unapotembelea. Watu wengi bado wana imani kwamba serikali yetu ni tukufu na hawajui matatizo makubwa ya utawala huu uliopo madarakani sasa hivi.

Sina mamlaka wala wadhifa wa kutoa tamko, bali ni mawazo yangu tu
 
Mkuu yana umuhimu mkubwa chadema ni wasikivu watayafanyia kazi!
 
Naunga mkono, hoja, inasikitisha sana kuona tunavyonyanyasika katika nchi yetu wenyewe, Viongozi waliojipa madaraka wanatumia nguvu bila kujali maumivu ya watanzania.

Mungu tusaidie. sisi na kizazi chetu kinachokuja.

Wafariji waliofiwa na walioumizwa wapone haraka. Inauma sana
 
yana umuhimu ila bado hakuna uhakika kama kuna waliokufa, na kama wapo ni wangapi na wanaishi wapi na kadhalika... ingependeza zaidi kama watazikwa au kuagwa kwa heshima pamoja

Ngoja taarifa kamili ije, mipango iwe wazi and then the rest will follow
 
Back
Top Bottom