MAZISHI ya Hayati Mohamed Ali (Bob) Nyanga Makani, Juni 13,2012

Wakuu

Kesho Juni 13, 2012, Mpambanaji Kamanda Mohamed Ali (Bob) Nyanga Makani, atawekwa katika nyumba na makazi yake ya milele, katika Kijiji cha Negezi huko Kishapu, Shinyanga.

Atazikwa katika kiunga ambacho baba yake, Ali Makani alizikwa. Ni katika eneo hilo hilo pia, ndugu zake wengine kama Zwalo Makani walilazwa wapumzike milele. Atawekwa pembeni yao.

Heshima za mwisho kwa wakazi wa Mji wa Shinyanga na vitongoji vyake zilizoanza tangu saa 8 mchana hadi saa 11 jioni, zilihudhuriwa na maelfu ya watu. Wanashinyanga wamemuaga mpendwa wao, ambaye naye aliwapenda sana wakati wa uhai wake.

Kwa kweli njia nzima wakati tukitoka Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli baada ya msafara uliosindikiza mwili wa Hayati Mohamed Ali (Bob) Nyanga Makani ukijumuisha wanafamilia, ndugu, jamaa, marafiki na viongozi na watendaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutua, ungeweza kuona wananchi kandokando ya barabara walivyokuwa wakishuhudia safari ya mwisho ya mpendwa Bob.

Msafara wa CHADEMA uliongozwa na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Said Arfi (MB), pamoja naye walikuwa ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Musa Yusuf, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika, Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Siale, Ofisa wa Habari Tumaini Makene.

Viongozi wengine, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Tanzania Visiwani, Said Issa Mohamed, Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylivester Kasulumbayi, Ofisa wa Uenezi, Erasto Tumbo walifika baadae wakati tayari mwili wa marehemu ukiwa Uwanja wa Shycom ambako kabla ya heshima kutolewa, zilitangulia dua kwa marehemu kutoka dini za madhehebu mbalimbali, ambapo Shehe wa Mkoa wa Shinyanga alitangulia kuwafungulia mlango wenzake wa dini zingine.

Kesho viongozi wakuu wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti Kamanda Freeman Mbowe (MB na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni), Katibu Mkuu, Dkt. Wilibrod Slaa, Naibu Katibu Mkuu Bara (Naibu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni), wajumbe wa Kamati Kuu, Grace Kiwelu, Ezekia Wenje, Peter Msigwa na wengine watajumuika na wnaanchi wa Shinyanga katika maziko ya Bob.
Hii ni taarifa ya Masiba au ya Chadema?
jiheshimu.
 
bwna ametoa na bwna ametwaa jina la bwna lihimidiwe vile vile innallilah waina illah rjiooun pumzike kwa amamai Kamanda Makani na si dhanio la kifisadi kuhusisha kaika kipindi kigumu kwa wanafamilia na makamanda wote
 
Hivi hakuna mtu wa kuleta updates toka huko inakera sana kupata taarifa za magazetini!
 
Huyu ata sisi wasukuma wenzie hatutaki kumsikia wala kumuona wasukuma sisi si wapuuzi kama huyu bwana amechukua akili ya yule aliyesema atakuwa kampeni meneja wake.

Huyu anafikiri wasukuma tuta-side nae. Huyu Magare shibuda akili yake kweli inafanana fanana na kampeni meneja wake. Nadhani ndio watakaopigiana kura pia.
 
Tunashukukuru kwa taarifa hizi ni vizuri pia hawa wanabodi wenzetu wazipate pia. VUTA-NKUVUTE, Ng'wanangwa, Kiganyi, sain Ivuga, SMU, Matola, Bazazi, zaleo, zomba, Barubaru.

nimezipata mufti.

mwanaye mbalu ananitonya kuwa alibadili dini ili apewe kiwanja cha kujenga pale buguruni kwa waswahili, vinginevyo asingekaa ule mtaa. hizi dini za kulazimishana inabidi ifike wakati zikome sasa. dini ni hiari ya mtu, siyo kulazimishana kama wanavofanya Boko Haramu na Uamsho.
 
R.i.p bob.
eh pasco wa jf mwana bodi wa lowasa P.A leo katoa nani? Tujuze mkuu.
 
Back
Top Bottom