Mawazo na makamanda wengine wamewakurupusha ccm wakigawa chumvi usiku -sengrema.

OMUSILANGA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
384
227
Ndiyo Wakuu , heshima kwenu ! Awali ya yote naomba nianze na nukuu ifuatayo :- " TAIFA LETU,TAIFA LOLOTE NI ZURI NA MAHALI PAZURI PA KUISHI KAMA RAIA WAKE WATALIFANYA LIWE HIVYO .UONGOZI WAKE UNAWEZA KUWA MZURI,MBAYA AU USIOJALI LAKINI KAMA WATU WAKE WAMEAMKA KIELIMU NA WANAJITAMBUA, HAITACHUKUA MUDA MREFU KUWAKILISHA MTAZAMO WA JAMII NA KUBADILI MAWAZO NA MATUMAINI YA TAIFA ." BY MWL NYERERE 1922-1999 . Baada ya nukuu hiyo , naomba turejee kwenye mada yetu. Katika kuelekea hitimisho la kampeini za uchaguzi wa madiwani i.e kesho tarehe 16.6.2013 hapa wilayani Sengerema ,hali si nzuri upande wa ccm. Ikumbukwe kuwa kuna jumla ya kata mbili ambazo ni Nyampulukano na Lugata ambapo madiwani wake walijivua magamba chini ya kamanda Lema na kuamua kujiunga na jeshi la ukombozi cdm . Siku za mwanzo alifika Nape Mnauye ambapo ali ambulia aibu kubwa sana baada ya kuzomewa na umati wa wananchi hapa sengerema wakati akiendeleza siasa zake za maji taka. Baadae pia alifika Ngereja ambaye ni mbunge wa jimbo hili, nae vilevile tangu amefika hapa sengerema amekuwa akizomewa na wapiga kura wake ambapo hali hii imewafanya washindwe kufanya mikutano ya kumunadi mgombea wao. Jana mchana ccm wamekurupushwa maeneo ya uwanja wa ndege wakigawa chumvi na kununua shahada ambapo ktk purukushani hiyo kioo cha gari la cdm kilipasuliwa kwa mawe huku kamanda mmoja cdm akijeruhiwa. Kada wa ccm alikamatwa kwa kusababisha uharibifu huo na hatimae kupelekwa polisi. Kama hiyo haitoshi, usiku wa kuamkia leo makamanda cdm chini ya Mawazo walipata taarifa za kugawa chumvi na kununua shahada maeneo ya Nyamazugo road na Migombani ambapo waliweza kuwakurupusha na kutokomea mbali. Kwa ufupi, hiyo ndo njia sahihi ccm wameamua kutumia ili kuendelea kutawala huku wakivunja ahadi ya 4 ya MwanaTANU inayosomeka "RUSHWA NI ADUI WA HAKI.SITAPOKEA WALA KUTOA RUSHWA." Leo Wenje, Dkt Mbasa na Mawazo watahitimisha wakati Waziri Wasira atahitimisha upande wa ccm . My take :- " SIKU MJINGA AKIJITAMBUA ,MWEREVU YUPO MATATANI ."
 
Nimependa hii
"siku mjinga akijitambua mwerevu yuko matatani"
 
aibu kwa ccm. imemfanya mtanzania awe maskini kiasi cha kupewa chumvi kwa kugawa haki yake msingi!
 
"Usiombwe kupendwa na maskini tajiri atakuchukia" cdm inapendwa na watu wa kipato cha chini<masikini> na ndiyo walikuwa mtaji wa ccm kwa miaka yote,sasa mapenzi yao wameamua kuyapeleka chadema na ccm wamechukia na matokea yake tutazidi kuona mambo mabaya yakijitokeza kadiri siku zinavyozidi kwenda........kesho ni siku nzuri sana kwa vyama vyote pia ni siku mbaya sana kwa vyama vikuu viwili,lolote,kokote linaweza tokea ndani ya chaguzi 26 zinazofanyika 16/06/2013...

"Ombi kwa vyama hasa cdm na ccm,hatutaki damu ya raia wa Tanzania imwagike kwa njia yoyote ile tafadahali sana"
 
Mbinu ya kizamani sana,kugawa chumvi labda wazee.Kumbe umasikini wetu ni mtaji kwa baadhi ya watu?
 
Mkuu,jitahidini kuwahamasisha wapenda mabadiliko wote waende wakapige kura hiyo kesho na hiyo ndo siri ya ushindi!
 
Hii ni dharau mbaya sana,yaani utu wa binaadamu unabadilishwa kwa chumvi?ccm imefikia pabaya,wamekosa hata elfu elfu za kuwahonga mpaka wanawahonga chumvi??ccm inawaonaje wananchi? Roho inaniuma sana
 
Back
Top Bottom