Mkuu nliishawahi kuzungumzia haya. Mikataba unaingia kabla ya kuanza kazi ili ujue gharama halisi za mradi. Hauanzi kujenga mradi kama huu bila kuhakikishiwa KIMAANDISHI kuwa utapatiwa huduma. Inawezekana kabisa kuwa hayo mashirika kwa wakati huo watakuwa hawana uwezo wa kukupatia hizo huduma. Ukiona hivi, unaangalia njia mbadala. Kwa bahati mbaya technocrats badala ya kufanya kazi kitaaluma wamegeuka wanasiasa.
TCC wanamkataba na Tanesco ataipata. Ndiyo management inavyotakiwa. Si kutafuta visingizio. Nadhani Mkuu angeweza kuwa more effective kama angeita press conference na kutoa lawama zake badala ya kutumia platform ya siasa. Wengine (nakiri sio wengi) tukiona hivyo tunastuka!
Yaani hayo MAANDISHI Tanzania hayaheshimiki na wala hayamshtui mtu, ni lazima uwe nayo ofcourse maana usipokuwa nayo kisheria unakuwa hauna base yoyote. Lakini Tanzania ukitaka mambo yako yawe safi unatakiwa mambo unayapigia debe vile vile hata kama unayo kimaandishi, maana watu wajibu wao hawataki kuutimiza.
Tanzania unaweza ukapewa Scholarship kila kitu mikataba halafu ukienda shule jamaa hizo hela za scholarship hawakupi wala nini, Tanzania unaweza ukawa muajiriwa wa serikali unafundisha shule sijui wapi huko na mishahara usipewe wala nini, Tanzania unaweza ukapanga mipango yako sijui unataka kwenda kuhiji huko Macca jamaa ukaingia nao mkataba kimaandishi na Fwedha taslimu ukawapa na wala wasikusafirishe kwenda macca, watakwambia ooh ndege hatuna, Yaani tanzania ni nchi ya ajabu sana wakati mwingine unakuwa na mkataba wa kupata umeme jamaa hawakuletei na kana kwamba hiyo haitoshi watakuletea bili na kukulazimisha ulipe wakati wewe umeme hujawahi kuona, yaani nyie acheni tu, mwacheni jamaa awapashe.