Mawaziri waanza kuumbuana mchana kweupe!

Naona watu wana mis-interpret the whole thing about collective responsibility.Collective responsibility siyo kulindana, wala siyo kuficha uovu.

Collective responsibility ni baraza zima la mawaziri kufanya kazi kama kitu kimoja.It is more about waziri ambaye hajafanya makosa kukubali makosa yaliyofanya na waziri mwingine kwa sababu yeye ni member wa cabinet than waziri asiyefanya makosa kumlinda waziri aliyefanya makosa.Kwa hiyo kwa msingi huu utaona "collective responsibility" haina chembe ya kulindana.Ina lengo ya kupalilia efficiency ya baraza zima la mawaziri as opposed to the fragmented farce we currently have.

On the other hand, collective responsibility ina demand integrity ya hali ya juu kiasi kwamba ukiona baraza la mawaziri hali respond kwako, na jinsi wewe unavyoona sawa, unajiuzulu ili upate uwezo wa kusema vizuri maana kuna mambo mengi utashindwa kusema kutokana na kubanwa na hii collective responsibility.

Kwa hiyo Magufuli aache siasa za populism, afuatishe utaratibu na kutatua matatizo au kama anataka kublast ajiuzulu uwaziri abakie mbunge backbencher ataweza kusema vizuri sana.Maana kama nilivyosema mwanzo, kwenye moshi panafuka moto.Inaonekana hii ni tip of the iceberg tu, kwa hiyo muheshimiwa kama kweli ana nia ya kupasua jipu aondoe uvivu na uoga wa kupoteza privileges za uwaziri.Ajiuzulu, ajiunge na ma backbenchers na hapo anaweza kusema bila kufungwa na collective responsibility ya cabinet, maana atakuwa nje ya cabinet.
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia ukitaka maadui Tanzania wewe nenda na uwe mchapa kazi. Utatafutiwa kila sababu ilimradi tu aidha upunguze spidi na ujiunge na wenzio kulaza kazi au utoke kazini.

Sasa hapo Magufuli hakuna kujiuzulu, tuliona hiyo "collective responsibility" kule bungeni ya kumfanya Karamagi apete na kumfanyia mchapa kazi Zitto mizengwe na kumsimamisha ubunge.

Ni kubanana hapo unless raisi aseme Mze Magufuli wewe unachapa kazi sana na kuwajali sana Wananchi na mtu wa namna hii hafai serikalini, kwa sababu serikalini wananchi ni adui zetu.
 
Pundit:
Hiyo "Collective Irresponsibility" haikubaliki; na Magufuli kama amekwamishwa kufaniisha kazi zake na hiyo 'irresponsibility' ni bora kufukuzwa kwa kuikataa; kuliko kujiuzulu.
Kujiuzuzulu na kuacha uozo? Akheri ya kupambana na uozo humo humo; na wtu wajue. Atakuwa amefanya la maanazaidi kubaki humo humo kuliko kujiuzulu.
 
Sasa hapo Magufuli hakuna kujiuzulu, tuliona hiyo "collective responsibility" kule bungeni ya kumfanya Karamagi apete na kumfanyia mchapa kazi Zitto mizengwe na kumsimamisha ubunge.

Again,

Kama Karamagi alikosea na wenzake wakamtetea hiyo si "collective responsibility" hiyo ni nepotism.

"Collective Responsibility" is more about saying "if one minister does wrong, all ministers are in the wrong" kuliko "kulindana".Again, lengo ni kutafuta efficiency kwa baraza zima la mawaziri akam alivyosema Mwalimu Kithuku na mfano wake maridadi hapo juu.

Tatizo tunatafuta majawabu rahisi kwa matatizo complex.Inaonekana kuna uwezekano kabisa kwamba baraza letu la mawaziri linanuka na Magufuli ni mchapakazi, sawa, kama ni hivyo mimi naona kwa yeye kung'ang'ania kukaa kwenye hilo baraza basi anaweza kukosa nguvu ya kusema na hatimaye kuambukizwa uzembe huu.

Instead of kushabikia factions katika baraza la mawaziri, mimi niko interested na kuona baraza zima la mawaziri linafanya kazi in a systematic way.This is a bigger challenge I agree but there is no reason why we should set low standards for our cabinet.

To me this populism and kupayuka business is just cheap shots.This could be another Mrema in the making.Just as many people did not recognize Mrema for what he is in 1995 Magufuli bado ana nguvu ya soda na watu hawajamshtukia his cravings for popularity na colloquial strategies.

Kukaa humo humo maana yake ni kuwa in principle unakubaliana na cabinet.Kama hukubaliani na cabinet halafu umo humo humo then hiyo ndiyo tamaa ya "I eat my cake but still want it to be there too"
 
Ama kweli watu tuna mitazamo tofauti sana!

Yaani Magufuri ajiuzuru kwa vile hawezi fanya kazi na wazembe?? halafu akisha jiuzuru?? ama kwa lugha nyingine awazirie nchi yetu waendelee kufanya mauzembe na mauzo yao?? no, a big No!

Hapo Magufuri ni kukaza buti.. chapa kazi, anaye sema unajipendekeza naye achape kazi ajipendekeze tumuone! Hatuwezi kuendelea kuwa mandondocha watanzania wote eti tumulaumu kiongozi shupavu anaye kuwa mkweli! kwamba anawaibisha wenzake!.. kama wangekuwa timiza sehemu yao ya kazi angepata wapi pa kuwasemea? watimize wajibu wao mambo yote yatakuwa shwari.

Lililo muhimu kwao wote, kuanzia na mkuu wao wajue mwajiri wao ni sisi wanachi! wote tunaona na tunasikia!
 
...Inaonekana kuna uwezekano kabisa kwamba baraza letu la mawaziri linanuka na Magufuli ni mchapakazi, sawa, kama ni hivyo mimi naona kwa yeye kung'ang'ania kukaa kwenye hilo baraza basi anaweza kukosa nguvu ya kusema na hatimaye kuambukizwa uzembe huu.

Hapo ninatofautiana na wewe moja kwa moja, kwanza hawezi kukosa nguvu ya kusema, nguvu ya kusema anayo na ndio maana tunajadili hapa kuhusu kitu alichokisema wazi wazi. Badala ya kuambukizwa uzembe yeye ataweza kuwaambukiza uchapa kazi na nchi nzima tukafaidi.

Kubaki barazani hapo ni Pai, kwa utaratibu huo hatabakia kusema akiwa nje, bali atasema ndani na kuwa chachu ya kuleta maendeleo na kuwahamasisha wazembe waache uzembe tena kwa kuonyesha mfano.
 
Let's agree to disagree.

Wewe unasema kunaweza kuwa na Mkatoliki asiyeamini katika papa, mimi nasema by definition Mkatoliki anaamini papa, asipoamini katika papa huyo kajitenga na siyo Mkatoliki.

Likewise, cabinet ya CCM ni moja na inabidi kuongea kwa sauti moja.Kama mtu anaona yuko sawa na cabinet haimsikilizi inabidi ajiuzulu ili apate nafasi ya kueleza mawazo yake vizuri zaidi.Pengine hata kukishawishi chama (au kuingia upinzani) na kuwania urais ambapo anaweza kufanya vizuri zaidi ya cabinet iliyopo.

Tatizo watu wanaona kujiuzulu ni defeat wakati is one of the best thing an honest politician in Magufuli's position can do.Si unajiondoa kutoka uozo usiotibika?
 
Jamani hapa tukumbuke the most important ni maslahi ya nchi na wananchi, kujiuzulu itakuwa very personal, vile vile itawafurahisha sana wazembe na watu wasiojali wananchi.

Na kama cabinet ya CCM sauti yake moja ni kuufuga uzembe, basi lazima wana-CCM wanayoipenda CCM wawe ndani ya kabinet na kuubadili huo msimamo wa kizembe, watu wanaoipenda CCM ndio hao kina Magufuli, msimamo wake unaipamba CCM, wasioipenda CCM watawashangilia wazembe na kushabikia uzembe.

Hajiuzulu mtu hapo, unless jina lake Karamagi.
 
mi sioni kujiuzulu hatari.Mtu yeyote ambaye hawezi kujiuzulu kazi yake kutokana na principle hajiamini utendaji wake.

Hahaaa, unamshupalia Karamagi, si ndiyo "Ari Mpya" hiyo.

Word is alifadhili sana kampeni ya mkulu kwa hiyo hawezi kumtupa.
 
mi sioni kujiuzulu hatari.Mtu yeyote ambaye hawezi kujiuzulu kazi yake kutokana na principle hajiamini utendaji wake.

Hahaaa, unamshupalia Karamagi, si ndiyo "Ari Mpya" hiyo.

Word is alifadhili sana kampeni ya mkulu kwa hiyo hawezi kumtupa.


Pundit, there you come now!

nayo hiyo ni collective responsibility! Karamagi kasaini mkataba mbovu mbovu, madini yetu wachotaji wanazoa kwa kasi mpya, hawalipi kodi ya mafuta mile na milele.. lakini collective responsibility, karamagi kafanya vyema!!! Kwa mwendo huu huoni tunajimaliza??

Magufuri angekuwa ndo JK kwa ujasiri alo nao asinge mkingia kifua hata kidogo!! hata haya mambo ya Kiwira.. hawa wezi Kina yona wangeisha itema siku nyingi!! lakini unamuona JK mzee wa collective resp anatia tumuache mzee apumzike!!

Ee Mungu tunusuru!
 
Hiyo ya Karamagi ni nepotism.Just because watu wana act in unison it does not qualify that as "collective responsibility".Collective responsibility inakataa kunyoosheana vidole, kama kuna kitu kinaharibika mnakifanyia kazi wote pamoja mpaka kinakuwa sawa, kama kuna sehemu mmoja kakosea basi wote muwe tayari kuchukua lawama JKT style.Utaona gradually discipline ya cabinet nzima itapanda.

Lakini hii habari ya kunyoosheana vidole matokeo yake zitatokea spin hapo hata tutakuwa hatujui issue imeanzia wapi na kuishia wapi.

Katika system ya collective responsibility huwezi kumshutumu waziri mwenzako hadharani kwa sababu yeye na wewe ni kitu kimoja, cabinet, you can argue and fight all you want in cabinet meetings lakini hadharani discipline kama baba na mama wasiopatana lakini hawagombani mbele ya watoto.
 
There is such a thing as "collective responsibility". Naelewa alichosema ni kweli na kinahitaji kusemwa but not in such a fashion.Serikali lazima i present a united front hata kama kuna tofauti.Hii inaonyesha jinsi tatizo lilivyo kubwa, incompetence mpaka kufikia mawaziri kulumbana hadharani.

Hapana, sidhani kama walilumbana, mkuu. Kinyume cha hapo, ina maana Magufuli asingeelezea matatizo ya mradi wake. Hii tabia ni ya kuficha ficha matatizo na kujifanya kila kitu shwari. Ni usiri usio na tija hata kidogo. INgewasaidia nini hasa wapiga kura kama angefanya collective responsibility pale? Siamini kama kabla ya hapo hawakukutana na Magufuli kujadili tatizo hilo.

Juzi tu JK kamtoa nishai Magufuli juu ya msamaha wa kodi aliouomba ili HNC ipunguze gharama za ujenzi...kamshushua mble ya hadhara kwamba haiwezekani. That was ok, and nobody complained juu ya collective responsibility!

Kuna utamaduni ambao hauna maana sasa ambapo maendeleo yamechelwa na inabidi kukumbia wakti wenzetu wanatembea.
 
Pudit:
Usidhani hatukuelewi na hiyo 'collective responsibility' unayoizungumzia. Tunakubaliana kabisa, hivyo ndivyo inavyotakiwa iwe katika hali ya kawaida, yenye baraza la mawaziri linalofanya kazi ipasavyo. Hapa, hilo baraza la mawaziri halipo; lililopo ni la kukwamishana. Wanaopenda kupiga hatua moja mbele, kama kina Magufuli, wanakwamishwa na wazembe. Hata mpigiane kelele vipi huko kwenye mikutano yenu, hakuna linalotendeka, matokeo yake yankuwa kuvurugana hadharani kama alivyofanya Magufuli, kutokana na frustrations.
 
Sasa wewe unamuangalia huyu colloquial president ndiye awe mfano wa "collective responsibility"? Yaani mpaka Magufuli kufika hapa kazi si mchezo, mi ndiyo maana namshangaa anavyojaribu kutwanga maji ndani ya kinu.

Inaelekea JK hampendi sana Magufuli ila alishindwa kumtosa kutokana na popularity yake.Sasa inawezekana Magufuli naye anapalilia kibarua katika competition ya politiksi za kibongo.
 
Hivi karibuni wakati wa sakata la Tanesco na TCC iliposemekana kuwa pengine Waziri wa nishati ndiye aliyeamuru umeme urudishwe TCC na kumpelekea Mkuu wa Tanesco kujiuzuru wengi mlilani mlichokiita kuingiza siasa kwenye utendaji. Hapa mwenye nyumba ni shirika la NHC, mtoa umeme ni Tanesco na mtoa maji ni Dawasco, yote mashirika yanayotakiwa kujiendesha kibiashara, imekuwaje hawa mawaziri ndio wamekuwa wahusika wakuu? Tangu lini waziri amekuwa mtendaji mkuu? Kama uzembe umefanyika ni NHC kutoingia mikataba na hizo utility companies. Kama mikataba ipo, dawa ni kuwashitaki mahakami ili arejeshewe gharama za ziada alizoingia. Huku kusemana kwenye majukwaa hakutasaidia kitu kama mikataba haipo. Au waheshimiwa mlitaka Karamagi amwagize Idris apeleke umeme mara moja?
 
Instead of kushabikia factions katika baraza la mawaziri, mimi niko interested na kuona baraza zima la mawaziri linafanya kazi in a systematic way.This is a bigger challenge I agree but there is no reason why we should set low standards for our cabinet.

To me this populism and kupayuka business is just cheap shots.This could be another Mrema in the making.Just as many people did not recognize Mrema for what he is in 1995 Magufuli bado ana nguvu ya soda na watu hawajamshtukia his cravings for popularity na colloquial strategies.

Mkuu, hapo naona unachanganya mambo.
"mimi niko interested na kuona baraza zima la mawaziri linafanya kazi in a systematic way." so what was Magufuli supposed to do in case others do nothing? Kukaa kimya? Pangekosekana umeme na maji pale Chalinze. Nchi ingekuwa imafaidika na nini? Collective responsibility? Let us be realistic please. Kama baraza zima halifanyi kazi systematically, as you put it, is this his fault?

"To me this populism and kupayuka business is just cheap shots."Lets be fair kwa watu wetu wanaochapa kazi. Hivi anapayuka kweli? Ni nani asiyepayuka basi na tumsifu? Daudi Balali anayeamua kuwa kimya? Karamagi anayesaini contracts kimyakimya?

Nahisi hata wewe unaweka siasa mno kuliko realistic kwenye hoja hizi mkuu.
 
Sasa wewe unamuangalia huyu colloquial president ndiye awe mfano wa "collective responsibility"? Yaani mpaka Magufuli kufika hapa kazi si mchezo, mi ndiyo maana namshangaa anavyojaribu kutwanga maji ndani ya kinu.

Inaelekea JK hampendi sana Magufuli ila alishindwa kumtosa kutokana na popularity yake.Sasa inawezekana Magufuli naye anapalilia kibarua katika competition ya politiksi za kibongo.

Now, you're up to something concrete. Keep going my friend......
 
Fundi:
Very good reasoning. However, it is beyond belief to think that Magufuli hajui taratibu na wajibu wa mashirika hayo. Afterall, tunazungumzia mashirika - NHC, Tanesco, Dawasco, n.k. Yote haya yana wizara mama, yumkini ni huko huko palipona matatizo; ndio maana Magufuli kaingia - kwenye ngazi yake.
 
Hapa mwenye nyumba ni shirika la NHC, mtoa umeme ni Tanesco na mtoa maji ni Dawasco, yote mashirika yanayotakiwa kujiendesha kibiashara, imekuwaje hawa mawaziri ndio wamekuwa wahusika wakuu? Tangu lini waziri amekuwa mtendaji mkuu?

Fundi, kwa level ya uzembe na urasimu usiokuwa na maana, sidhani kama nguvu ya Madekwe (MD, NHC) ilitosha. Kuna mambo ya ajabu huwezi kuamini. Kama kaingilia kati waziri,na kashindwa, unadhani MD angefika wapi?

Hili la mkataba silifahamu, lakini kama ulivyosema, TCC wanamkataba unaosema umeme hauwezi kukatwa bila ya notice ya 48 hrs...na Tanesco wakakata bila ya notice hata ya dk 10!
 
Fundi, kwa level ya uzembe na urasimu usiokuwa na maana, sidhani kama nguvu ya Madekwe (MD, NHC) ilitosha. Kuna mambo ya ajabu huwezi kuamini. Kama kaingilia kati waziri,na kashindwa, unadhani MD angefika wapi?

Hili la mkataba silifahamu, lakini kama ulivyosema, TCC wanamkataba unaosema umeme hauwezi kukatwa bila ya notice ya 48 hrs...na Tanesco wakakata bila ya notice hata ya dk 10!

Mkuu nliishawahi kuzungumzia haya. Mikataba unaingia kabla ya kuanza kazi ili ujue gharama halisi za mradi. Hauanzi kujenga mradi kama huu bila kuhakikishiwa KIMAANDISHI kuwa utapatiwa huduma. Inawezekana kabisa kuwa hayo mashirika kwa wakati huo watakuwa hawana uwezo wa kukupatia hizo huduma. Ukiona hivi, unaangalia njia mbadala. Kwa bahati mbaya technocrats badala ya kufanya kazi kitaaluma wamegeuka wanasiasa.
TCC wanamkataba na Tanesco ataipata. Ndiyo management inavyotakiwa. Si kutafuta visingizio. Nadhani Mkuu angeweza kuwa more effective kama angeita press conference na kutoa lawama zake badala ya kutumia platform ya siasa. Wengine (nakiri sio wengi) tukiona hivyo tunastuka!
 
Back
Top Bottom