Mawaziri 6 sasa mikononi mwa TAKUKURU!

Kwa mwendo huu hata JK akiondoka madarakani anapaswa kushtakiwa, maana Richmond ni mzigo wake
 
Wakuu JF heshima mbele sana,

- Well, kitendo cha Rais kuwabadili mawaziri waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na upotevu wa hela za wananchi na ripoti ya CAG, kina maana moja tu kwamba hata na yeye ameridhika kwamba kuna ukweli au FACTS katika tuhuma walizokuwa wakituhumiwa nazo, ninasema great second day kwa Taifa, kwanza ilikuwa kuweka ripoti wazi to the public na kuruhusu mjadala wa public!

- Sasa ifike mahali pa kufanya kweli, yaani Watuhumiwa wote kufikishwa kwenye mkondo wa Sheria, haki itakua imetendeka na sio otherwise, kwanza haki kwao mawaziri maana wanahitaji kuwa wasafi mbele ya public na pili Serikali kulinda heshima yake kwamba sasa ipo serious, ama sivyo kuitoa ripoti ya CAG to the public itakuwa ni kazi ya bure, I mean mawaziri na viongozi wetu wakijua kwamba madhara ya kuiba ni kujiuzulu tu na kuachiwa ukale mihela ya wananchi tutakua tunajenga taifa la kusadikika, na itakuwa kazi kubwa kumpitisha Rais wa CCM 2015!

- MHESHIMIWA RAIS, UBARIKIWE KWA KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI, SASA TWENDE MBELE ZAIDI TUFIKE KWENYE SHERIA NA WOTE WENGINE HAO MAKATIBU NA WAKURUGENZI ULIOSEMA KWENYE HOTUBA YAKO KUWA WANAHUSIKA NA WAO PIA UWE MWENDO WA KUELEKEA KWENYE SHERIA!, NI SHERIA TU NDIO INAWEZA KUTUSAFISHA WOTE, SERIKALI NA MAWAZIRI WALIOACHWA!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!



Hakuna kitu hapo TAKUKURU ni bogus. Hawana uwezo huo waache wakamate rushwa za ngono na za Matrafiki barabarani
Mkuu ni ombi zuri sana lakini unaijua Bongo vizuri sana kwa sasa. Mpango ni Chukua Chako Mapema na ndio sheria ya utekelezaji sera, sasa tunapoomba mawaziri watiwe mbaroni wakati ni ruksa sijui tuna ushahidi gani?..Maana inavyosemekana hizo fedha zimepotea ktk idara zao na sii wao wamehusika na ufisadi huo. Hivyo maadam makosa yamepatikana ndani ya wizara zao imelazimika wajiuzuru lakini haina maana wao ndio wahusika...

Tunarudi palepale kwamba mfumo wa utawala wetu haukujenga kuwafanya viongozi wetu wawe responsible moja kwa moja na maamuzi ya wizara ktk matumizi. Tuna Waziri mkuu, Waziri, Naibu waziri na Katibu mkuu wote waajiriwa wa rais na wana uwezo wa maamuzi yoyote ktk wizara moja, tena Katibu mkuu ndiye anayeidhinisha matumizi ya wizara bado hujagusa kwenye idara zake pia kuna utararibu mwingine. Hivyo waziri anaweza kabisa kutojua kimefanyika nini hadi siku ya ukaguzi na report itatolewa kuihsisha wizara yake.

Wee umeona jinsi Omar Nundu na Naibu na katibu wake walivyokuwa wakishindana juu ya ujenzi wa gati za bandari na kila mmoja akijiona yeye ndiye kiranja. Na ndio maana husema hatuna sababu ya kuwa na waziri msomi ktk wizara husika wakati kazi kubwa ya utekelezaji ni ya Katibu mkuu,, hatuhitaji kabisa kuwa na watu watatu wizara moja wote wamechaguliwa na rais kuifanya kazi moja.
 
Na kama Yona na Mramba bado hakijaeleweka hata hao ni bure tu kuwafikisha huko kwani mahakama bado ziko chini ya udhalimi na kwamba anasaidia sana kuwapeleka huko. Mfano mzuri, mahanga aliiba kura machana kweupe na ushaidi wa kutosha upo lakini kapewa tena ubunge na uwaziri wake ukaendelea nao. Hakuna mahama kwa mafisadi nchi hii ziko kwa ajili ya walalahoi wanaoiba kuku n.k
 
Hakuna lolote, labda yy Jk ajipeleke mahakamani kwanza ! Mbona bado kaweka walaji wengine kulinda maslahi yake ktk sekta flan flan ? Katibu mkuu km yule Komba alimpa zawadi ya ubalozi Uganda baada ya kufanikisha kuuza wale wanyama sasa kama kweli yy hausiki basi amtimue yule haraka na kumrudisha ajibu mashtaka !

What about Jahiro ? Blandina Nyoni anajulikana tangu zamani, hao akina Mapunjo wanajulikana madili yao na yy mwenyewe tangu wakiwa wizara kibao mpaka alipmvuta Ikulu, na then kumpeleka viwanda na biashara ambako yy ni mmoja wa hao wenye makampuni feki na JK anajua siku nyingi.

WTF, mnampa sifa kuwa yy ndiyo aliamua report ijadiliwe, kwani hii ni report ya CAG ya kwanza ? Ni upinzani ndiyo umesababisha haya yote na baadhi ya wabunge wa CCM baada ya kufuatilia wakagundua ni kweli wenzao wanakomba bila huruma na JK anajua na kuhusika thru mtandao plus RZ1. Mbona yule DED aliyetafuna mahela akiwa Bagamoyo, rafiki yake mkubwa ndiyo kampa u RC Arusha ?

So wewe acha hizi sifa hewa unless sasa unavizia nafasi iliyobaki ya kuteuliwa ubunge !! Vp anakuja lini kufungua tawi lako la CCM...lol

ukweli mtupu, hizo ni sanaa za kila siku.. kama mahakamani kwa uabadhirifu wangapi watabaki ktk serikali ya ccm ya kisasa?
 
William hoja kama hoja si mbaya, maana machoni mwa wapiga kura wa CCM inaonekana JK anachapa kazi, anawawajibisha wezi na ambo mengine kama hayo. Mimi nakuhakikishia William, tatizo la wizi serikalini si la watu kama watu, bali ni mfumo, kwa hiyo mabadiliko amefanya lakini mchwa hawataacha kutafuna, watakula tu!!

Pili kuwapeleka mahakamani na kuhumiwa ni vitu tofauti, si kama ianvyoonekana, na ushahidi kwenye hili upo. JK aliwapeleka Mramba na Yona mahakamni, akapiga kelel kila kona kuonyesha jinsi serikali yake isvyokuwa na huruma na wachafu, well, naamini unatambua kuwa hadi leo hawa jamaa hawajahukumiwa na kesi zao zimekosa muelekeo, na tunaelewa maana ya kutotajwa tena, waaachiwa kwa kukosa substance ya kuwashitaki, na hili si kwa sababu nyingine yeyota zaidi ya mfumo!

Hawa sita unaosema wako mikononi mwa TAKUKURU, ni mazingaombwe mapya mnayotaka yatawale midomo yetu kwa muda mrefu tu ujao, na yatatumika kama mfano wa ku-revive imani ya wananchi kwa CCM na serikali yake!! Wengine tulishagoma kuwaamini na tutaendelea kuwatazama tu, tunajua mwisho umefika, hakuna dawa zaidi ya kusafisha nyumba nzima, risk ambayo hakuna aliye tayari kuichukua maana mnajua haitambakiza mtu!! Mansubiri kufa kiume tu...

Umesema huamini kupambana kulikomboa taifa ukiwa nje ya CCM, naheshimu sana maamuzi yako na misimamo yako. I am just saying wait and see...
 
- Hakuna lislowezekana kama wamesoma ripoti kwa taifa na yanayofuata wananchi tukiyataka tayafuata, ila kama wananchi wamekata tamaa hivi then inakuwa ni kazi sana, ila ninaamini wananchi tukidai itafanyika kama wananchi walivyodai waondolewe!

William.
Mkuu hebu nieleweshe namna ambavyo wananchi watataka haya yatimie kama serikali haijataka kuyatimiza.
 
Alishasema wanawajibika kisiasa kwa makosa ambayo walifanya wengine wala sio wao directly, what do you expect next?
 
Nasubiri hiyo saga kwa hamu. But Tza ni zaidi ya uijuavyo!!! Mimi nataka wakamatwe na nina hakika katika statements za ungamo watasema angalao walikuwa wanashirikiana na nani ili haki ipate kutendeka!!!!!!! sasa utashangaa watakaotajwa na kama kweli kuna haki itakayotendeka!!!!!! Hivi unafikiri hadi leo ni kwa nini Malegese hajakamatwa kuhusiana na skendo ya EPA? Ni kwa nini ikubalike kuwa Balali alikufa ili tu asiwepo asije akakamatwa ili atoe maelezo ya EPA? Hivi kwa nini Rostam na Manji hawakukamatwa kuhusiana na Kagoda? Iweje Manji arejeshe fedha za Kagoda ilihaji hajazichukua? Kwa mantiki hii mtasubiri uchunguzi hadi nje ya nchi kama walivyodanganya watanzania kwa makampuni yale yalyosalia hadi mwisho wa dunia na hakuna majibu.
 
kitendo cha kuwakabidhi takukuru tayari hawana kesi maana kimsingi hawa wengi hawakula hela hizi bali ni wazembe hawasimamii wizara zao. ushahidi wa kutafutwa na takukuru sioni bali wao ni uzembe na ripoti bila shaka ripoti ilisema kwa kila upotevu mhusika ni nani.

binafsi nimesikitika kwa waziri nundu kwani nimemsikliza akitoa hoja bungeni kwa mfano kuhusu kuruhusu kununua vifaa vilivyotumika alijenga hoja za kitaalamu, pili nilimsikia akiwasilisha bajeti akaulizwa kuhusu kutotenga fedha kwa shirika la ndege msimamo wake ulikuwa hawezi kuweka fedha katika shirika lililo kufa.

katika utetezi wake amelaum mfumo inakuwaje shirika kama bandari linambishia waziri, inakuwaje naibu waziri anaenda kumshitaki waziri ikulu. mifumo hii ndiyo inawaondoa watendaji wazuri wa kupeleka taifa mbele na kuwaacha ambao sijui niwaite ni mawaziri au maana waziri unakagua shule moja baada ya nyingine sasa ni waziri au mkaguzi na wakaguzi wako wapi wanafanya nini? maafisa elimu wako wapi? kazi ako waziri ni kuagiza tangu sasa hakuna shule kufanya kazi miaka miwili bila kusajiliwa na watendaji wa chini wanafanya kazi lakini hawa ndi tunawaona mashujaa kwetu.
tunayo kazi kubwa ya kufanya katika katiba mpya
 
Hii ngonjera haina msikilizaji wajameni,serikali hii ya magamba ipeleke mtu mahakani?labda house boi wake ama mjomba wake aliyechoka,zile za kina mramba ndo kwanza wataibuka kidedea tu,JK mwenyewe alimnadi Mramba kuwa 'Mgombea makini"huku akijua ana kesi mahakamani,Rostam hivyo hivyo,ndugu baharia mi naona kama unajiliwaza tu na machungu ya kukosa ubunge,Mzee tingatinga anafahamu sana jinsi ilivyo vigumu kumshugulia fisadi tz kuliko kwenda mwezini kwa ungo!
na uangalie wasikushughulike mapema usije ukawa unatoka ulezi kichwani,bado tunakuhitaji sana kwa story hapa Jf, teh!
 
- Kuja upande wa pili ni lazima nipaamini huko, so far bado sijafikia hilo kutokana na kujua mengi sana yanayoendelea within na hizi siasa, lakini mimi nimesema hivi na wakati wote kwamba siwezi hata siku moja kukosa kuweka wazi msimamo wangu on any ishus hapa bongo, kwenye hili la mawaziri ninasema sasa tumewaondoa kwenye nafasi kwa sababu ya kuamini sio wasafi, basi wakasafishwe na Sheria!

- Upande wa pili bado sijaamini kwamba huku niliko kumeshindwa, siku nitakapoaamini hivyo utaniona nikiwa wa kwanza kuja huko, sio sasa!

William.

mpaka uone CDM wamechukua nchi ndio utaamini?au ndio sizitaki mbichi hizi?na siku muda ukifika itakua too late kuwa na mwanachama kama wewe maana unaonekana uko kimaslahi zaidi
 
mpaka uone CDM wamechukua nchi ndio utaamini?au ndio sizitaki mbichi hizi?na siku muda ukifika itakua too late kuwa na mwanachama kama wewe maana unaonekana uko kimaslahi zaidi

- CDM watachukua nchi only kama CCM itaacha kusikiliza mawaidha ya wananchi, kwa mfano hoja ya Zitto kwa sasa imekufa kifo cha mende, simply kwa sababu CCM imesikiliza wananchi, ni kweli nipo kimasilahi zaidi ya Taifa na wananchi kuliko yangu binafsi!

William.
 
i am appalled and frustrated that bw malecela, despite being educated and exposed to the outside world, you still bear the rudimentary thinking that we see in our semi literate, feeble minded politicians!!!

yaani tumpe uongozi mwandosya ili atibiwe na nchi!!!!!
khaaaa this is the most stupid notion ever, utter nonsense and complete BS!!! kwani hana bima ya afya?? je mababu zetu nao tuwape uongozi ili watibiwe pia na serikali si ndio jamani cz wagonjwa ni wengi.

i have nothing against waziri mwandosya na i would have supported him being treated kwa fedha za kodi yetu but sio kwa namna hii jamani!! utter and complete BS!! na new generation ya CCM kama malecela anasupport!!!! yaani am disappointed , totally.

- Umeonyesha tu uwezo wako finyu wa kufikiri unapoanzia na kuishia, Mwandosya ni Kiongozi wa juu sana wa Taifa na kwa muda mrefu sana, sasa unasema nini wakifikia mahali wanaugua wakiwa kwenye power dawa ni kuwatupa?

- Halafu tizama your contradictions, unasema hutaki Mwandosya atibiwe halafu unarudia tena kwamba ni afadhali atibiwe na hela zetu walipa kodi, pure confusion unataka nini na hutaki nini bro?

William.
 
mkulu alimeshasema wamepozwa na watu wao wa chini , sasa nani atapingana na mkulu, kuna wakubwa wengi wanaingilia utendaji wa vyombo vyetu vya sheria, hapo ndipo kwenye ugumu
 
- CDM watachukua nchi only kama CCM itaacha kusikiliza mawaidha ya wananchi, kwa mfano hoja ya Zitto kwa sasa imekufa kifo cha mende, simply kwa sababu CCM imesikiliza wananchi, ni kweli nipo kimasilahi zaidi ya Taifa na wananchi kuliko yangu binafsi!

William.

We mwananchi, inaonekana unajitahidi kujaribu kutumia akili ili utoe hoja zenye mashiko, lakini unachotoa hakina uzito wowote kwani ni lugha ile ile ya ccm ya uongo uongo. BILA PRESSURE YA ZITTO BUNGENI KUTAKA KUMWAJIBISHA WAZIRI MKUU, KUSINGETOKEA MABADILIKO YOYOTE. UNASIKITISHA KUMBE ULIKUWA HUFATILII HOJA YA ZITTO NA MADHUMUNI YAKE HASA HUKO BUNGENI, HIVYO WACHA KUPOTOSHA UMA KWAMBA CCM IMEWASIKILIZA WANANCHI, KWA HILO SIDHANI KAMA UNAFAA KUWA HATA KATIBU KATA, SABABU UNAGEUZA MAMBO. ZILEZILE PERSONAL QUALITY ZA WANA CCM.
 
We mwananchi, inaonekana unajitahidi kujaribu kutumia akili ili utoe hoja zenye mashiko, lakini unachotoa hakina uzito wowote kwani ni lugha ile ile ya ccm ya uongo uongo. BILA PRESSURE YA ZITTO BUNGENI KUTAKA KUMWAJIBISHA WAZIRI MKUU, KUSINGETOKEA MABADILIKO YOYOTE. UNASIKITISHA KUMBE ULIKUWA HUFATILII HOJA YA ZITTO NA MADHUMUNI YAKE HASA HUKO BUNGENI, HIVYO WACHA KUPOTOSHA UMA KWAMBA CCM IMEWASIKILIZA WANANCHI, KWA HILO SIDHANI KAMA UNAFAA KUWA HATA KATIBU KATA, SABABU UNAGEUZA MAMBO. ZILEZILE PERSONAL QUALITY ZA WANA CCM.

- Nothing to do na ishu at hand, the ishu hapa ni wananchi tuamue kuililia Serikali mawaziri waende kwenye Sheria, what is your point on that? au unataka Zitto ndio apigane peke yake?

- Hayo mengine ni kelele za mlango! keep them to yourself! ha! ha! ha! ha!

William.
 
Hakuna lolote, labda yy Jk ajipeleke mahakamani kwanza ! Mbona bado kaweka walaji wengine kulinda maslahi yake ktk sekta flan flan ? Katibu mkuu km yule Komba alimpa zawadi ya ubalozi Uganda baada ya kufanikisha kuuza wale wanyama sasa kama kweli yy hausiki basi amtimue yule haraka na kumrudisha ajibu mashtaka !

What about Jahiro ? Blandina Nyoni anajulikana tangu zamani, hao akina Mapunjo wanajulikana madili yao na yy mwenyewe tangu wakiwa wizara kibao mpaka alipmvuta Ikulu, na then kumpeleka viwanda na biashara ambako yy ni mmoja wa hao wenye makampuni feki na JK anajua siku nyingi.

WTF, mnampa sifa kuwa yy ndiyo aliamua report ijadiliwe, kwani hii ni report ya CAG ya kwanza ? Ni upinzani ndiyo umesababisha haya yote na baadhi ya wabunge wa CCM baada ya kufuatilia wakagundua ni kweli wenzao wanakomba bila huruma na JK anajua na kuhusika thru mtandao plus RZ1. Mbona yule DED aliyetafuna mahela akiwa Bagamoyo, rafiki yake mkubwa ndiyo kampa u RC Arusha ?

So wewe acha hizi sifa hewa unless sasa unavizia nafasi iliyobaki ya kuteuliwa ubunge !! Vp anakuja lini kufungua tawi lako la CCM...lol

Hapo kwenye red sio kweli ulichoandika, Magessa alikuwa ni DC Bagamoyo na wala hakuwa DED kama ulivyoandika. Vilevile jaribu kufuatilia Magessa aliingia lini Bagamoyo na alikaa muda gani. Huo uizi ulifichuliwa kwa kipindi kifupi alichokuwapo Magessa na inasadikika alitumwa kwa kazi Maalum baada ya DC aliyekuwepo mwanzo kuonekana wazi kumkingia kifua DED wakati wa uchunguzi wa ndani kabla uozo haujawa public. Huyo DED unayemsema alikuwa ni mama mmoja na mpaka sasa yuko Bagamoyo anaendelea na kesi zake

Source mimi mwenyewe!
 
- Kwa mfano ni Viongozi wapi wa level ya uwaziri unaowakumbuka waliowahi kwenda Jela hizo enzi, please naomba majina ili tuongee na FACTS!

William.

Hizo enzi unazoziongelea hakukuwa na wizi/ufisadi wa level tuliyo nayo. Haya yote ni baada ya kuua Azimio la Arusha na kuleta Azimio la Zbr! Ndipo ushenzi mwingi umeanzia hapo pamoja na kulindana. Kwa mtindo huo nani ataenda jela kaka?
 
Kaka William, kama kumbukumbu zangu ziko sawa nakumbuka uliwahi kuulizwa hapa kama ungeunga mkono mapinduzi dhidi ya mawaziri watuhumiwa ukasema unataka legal facts.

Do u really need facts besides a professional auditor's report?
 
Back
Top Bottom