Mawaziri 6 sasa mikononi mwa TAKUKURU!

hakuna lolote hapa..hivi ni siasa tu
Itaanza kwa mbwembwe nyingi! na magazeti yao yakipamba "Mawaziri sita ndani ya mahakama ya Kisutu" na Udaku kibao. JK awapa.............!
Mwisho wa siku utasikia "mahakama imeona hawana hatia hivyo inawaachia huru"
Na kama watakuwa na hatia utasikia "Mahakama imewakuta na hatia hivyo inawahukumu kwenda jela miaka miwili...."

Hivi ni kwamba CAG hatakiwi kumchunguza raisi
au raisi ni msafi sana?
Maana kila taarifa ya uchunguzi anayo toa sioni Ikulu ikiguswa
hata kidogo,lakini tunaona jinsi wanavo kula kodi kwa kutalii
ulimwenguni kote.

Kwa nchi za kiafrika rais ni mtukufu
 
Iundwe independent elimination squad.

Inachunguza, inahukumu, ina eliminate kila afanyae madudu awe ni waziri au tarishi. Siku anayokuwa eliminated, anawekewa na hukumu yake na ushahidi kamili wa madudu aliyofanya.

Wakifika watano tu! ukimpa mtu hata soda atakataa! wacha "takrima" na "ten percent".

Haya ndio huwa nayaita MAWAZO MAKUBWA......

Hi nchi tutaendelea kama tukianza kuwaza namna hii
 
Iundwe independent elimination squad.

Inachunguza, inahukumu, ina eliminate kila afanyae madudu awe ni waziri au tarishi. Siku anayokuwa eliminated, anawekewa na hukumu yake na ushahidi kamili wa madudu aliyofanya.

Wakifika watano tu! ukimpa mtu hata soda atakataa! wacha "takrima" na "ten percent".
Halafu tangu jana unaongea pointi kumbe unaakili...Hongera sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
kama ni sheria zetu ndizo zitakazo tumika basi bado tunasafari ndefu sana,maana mpaka juzi ndio nimesikia kuwa kesi ya akina mramba itatajwa tena ili kuangalia kama watakuwa na kujibu ama la na baada ya hapo kesi yao iendelee tena

kwa mtindo huu kesi yao yaweza isha labda mwaka 2020 wakati tayari tumesha poteza pesa nyingi kwa ajili yao

napendekeza

kama tunaweza kuazima sheria za uchina ili zitumike kwa mawaziri hawa basi na tufanye hivyo,kwani wenzetu kesi zao huwa hazichukui muda mrefu kama za kina mramba na majibu yake huishia ktk kunyongwa kama walivyo mnyonga mwanasheria wao mkuu kwa kosa la rushwa.

nadhani baada ya kuazima sheria za uchina na tukazitumia pasi kuwatilia maanani akina HAKI ZA BINADAMU twaweza songa mbele kwa kutengeneza sheria zetu zitakazo endana na sheria za uchina

lakini kwa sheria zetu zinazohitaji upembuzi yakinifu,na mchakato usiokamilika ukienda sambamba na upelelezi usio kamilika daima kwa kesi kubwa ila hukamilika mapema kwa kesi za bangi,kuku na kuibiana wake ,hakika nawaeleza hatuwezi fika popote pale.
 
- Hakuna lislowezekana kama wamesoma ripoti kwa taifa na yanayofuata wananchi tukiyataka tayafuata, ila kama wananchi wamekata tamaa hivi then inakuwa ni kazi sana, ila ninaamini wananchi tukidai itafanyika kama wananchi walivyodai waondolewe!

William.

Mkuu.. Hebu nisaidie hapo kwenye red.. Tudaije ili ifanyike..? Maana tukiandamana ili ifanyike tunaambiwa ni wahuni na wanachama wa chama cha maandamano na fujo.. Tunaishia kupigwa risasi na marungu na kesi kupewa..! Tumepiga kelele mpaka sauti zimekauka.. Hakuna wa kutucikiliza na ndio kwanza tunadhihakiwa na kudharauliwa.. Tukiamua kutowachagua wanalazimisha iwe kwa kuiba na kununua kura ili waendelee kubaki madarakani..!
 
- Tumedai waondolewe wameondoka, sasa tudai next step! SHERIA!

William.
 
Mdogo wa Rostam Aziz aachiliwa huru

na Happiness Katabazi

amka2.gif
Mahakama Kuu Kanda ya Tanga imemwachilia huru mdogo wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga (CCM), Rostam Aziz, Assad Aziz Abdulrasul, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kula njama na kuingiza dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 92. 2 ambazo zina thamani ya sh bilioni 2.4 baada ya kumuona hana kesi ya kujibu.
Abdulrasul katika kesi namba 19B ya mwaka 2011 alikuwa akikabiliwa na makosa mawili ya kula njama na kusafirisha kiasi hicho cha dawa za kulevya aina ya heroine na alikuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza. Washtakiwa wengine ni Kileo Bakari Kileo, Yahaya Zumo Makame, Mohammadal Gholamghader Pourdad na Saidi Ibrahim Hamis.
Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Kipenka Mussa, aliyesema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, ushahidi ulitolewa na mashahidi 200 na vielelezo 25 vya upande wa jamhuri, mahakama hiyo imeona ushahidi na vielelezo hivyo havithibitishi mshtakiwa wa saba (Abdulrasul) kuwa alitenda makosa hayo mawili aliyoshtakiwa nayo.
Jaji Kipenka alisema ushahidi na vielelezo vyote umeweza kuishawishi mahakama iwaone washtakiwa waliosalia kuwa wana kesi ya kujibu.
"Kwa sababu hiyo mahakama hii inamuachilia huru mshtakiwa wa saba (Abdulrasul) kwa sababu upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi yake ila kwa washtakiwa wengine waliobakia katika mahakama hii imewaona wana kesi ya kujibu hivyo watatakiwa wapande kizimbani wajitetee katika tarehe itakayopangwa na mahakama hii," alisema Jaji Kipenka.
Mapema 2011 ilidaiwa kuwa mshtakiwa alikula njama kusafirisha dawa za kulevya kinyume na kifungu cha 384 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 pamoja na kifungu cha 22(a) and 25 cha Sheria ya Dawa za Kulevya.
Kuwa washtakiwa wote kwa pamoja kati ya Aprili Mosi na Machi 8 mwaka 2009 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, Tanga na Jamhuri ya Iran ,washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama kusafirisha dawa hizo na kosa la pili ni ni la kukutwa na dawa hizo Machi 8, 2010 huko kijiji cha Kabuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga, kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 16(1)(b)(1) cha Sheria ya Dawa za Kulevya.
Polisi yakamata wawili Dar
Polisi wakishirikiana na watumishi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wamewakamata watu wawili akiwemo raia wa Ghana, Emanuella Adom (51), wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam jana.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ambaye ni mkuu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya Tanzania Godfrey Nzowa alisema Adom alikamatwa jana saa kumi usiku akitaka kuelekea Accra Ghana kwa kutumia ndege aina ya KQ akiwa na hati ya kusafiria namba G0084666 iliyotolewa February 8, 2011.
Nzowa alisema walipata taarifa kutoka kwa wananchi na kumfuatilia na kumkuta na paketi 2 zenye uzito wa kilo 3 za heroin ambazo alikuwa amezihifadhi katika mabegi yake mawili ya kuhifadhia nguo.
Nzowa alisema kuwa Mei 2, mwaka huu, polisi walimkamata mtuhumiwa mwanamke Mary Mvula, raia wa Zambia akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin akitokea Pakistan kupitia Dubai, Addis Ababa na hatimaye kukamatwa uwanja wa ndege wa hapa nchini.
Alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa amemeza dawa hizo na kujisingizia kuwa ana ujauzito, lakini baada ya uchunguzi ilibainika kuwa ni dawa na kufanikiwa kutoa kete 49 za dawa hizo.
Nzowa alisema jeshi la polisi limejipanga vyema katika mipaka yote, bandarini pamoja na viwanja vyote vya ndege kuhakikisha wanadhibiti uingizwaji na utoaji wa dawa hizi haramu.
Hata hivyo jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa vituo vyote vya polisi vilivyopo karibu nao kama wanafahamu viongozi, watu mbalimbali wanaojihusisha na biashara haramu ili waweze kuchukuliwa hatua.

Mkuu.. Hebu nisaidie hapo kwenye red.. Tudaije ili ifanyike..? Maana tukiandamana ili ifanyike tunaambiwa ni wahuni na wanachama wa chama cha maandamano na fujo.. Tunaishia kupigwa risasi na marungu na kesi kupewa..! Tumepiga kelele mpaka sauti zimekauka.. Hakuna wa kutucikiliza na ndio kwanza tunadhihakiwa na kudharauliwa.. Tukiamua kutowachagua wanalazimisha iwe kwa kuiba na kununua kura ili waendelee kubaki madarakani..!

Umesahau mkuu sosoliso!
Ni hao hao watakuja hapa jukwaani na kulaani kuwa "watanzania tuache ushabiki" "tutii mamlaka" "Jamani Tz nchi ya amani".......... bla blah
 
Last edited by a moderator:
:A S thumbs_up:
Iundwe independent elimination squad.

Inachunguza, inahukumu, ina eliminate kila afanyae madudu awe ni waziri au tarishi. Siku anayokuwa eliminated, anawekewa na hukumu yake na ushahidi kamili wa madudu aliyofanya.

Wakifika watano tu! ukimpa mtu hata soda atakataa! wacha "takrima" na "ten percent".

Kwa mara ya kwanza toka nipate kuyaona maandiko yako hapa JF.. Umeandika point Mkuu..! Kama kweli tukifanya hivyo kucingekuwa na hata haja ya kulumbana maana ufanisi ungekuwa juu.. Na uchumi wa Tanzania ungalipaa.. Salute Mkuu Ribosome.. :A S thumbs_up:
 
Basi sisi watanzania tukiona taarifa hii tunafurahi sana but kulingana na takwimu hakuna watuhumiwa wowote waliopita ambao wamechukuliwa hatua thabiti wapi YONA, MRAMBA. ni kudanganywa tu, wacha tupende SIMBA tu achana na siasa
 
Wakuu JF heshima mbele sana,

- Well, kitendo cha Rais kuwabadili mawaziri waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na upotevu wa hela za wananchi na ripoti ya CAG, kina maana moja tu kwamba hata na yeye ameridhika kwamba kuna ukweli au FACTS katika tuhuma walizokuwa wakituhumiwa nazo, ninasema great second day kwa Taifa, kwanza ilikuwa kuweka ripoti wazi to the public na kuruhusu mjadala wa public!

- Sasa ifike mahali pa kufanya kweli, yaani Watuhumiwa wote kufikishwa kwenye mkondo wa Sheria, haki itakua imetendeka na sio otherwise, kwanza haki kwao mawaziri maana wanahitaji kuwa wasafi mbele ya public na pili Serikali kulinda heshima yake kwamba sasa ipo serious, ama sivyo kuitoa ripoti ya CAG to the public itakuwa ni kazi ya bure, I mean mawaziri na viongozi wetu wakijua kwamba madhara ya kuiba ni kujiuzulu tu na kuachiwa ukale mihela ya wananchi tutakua tunajenga taifa la kusadikika, na itakuwa kazi kubwa kumpitisha Rais wa CCM 2015!

- MHESHIMIWA RAIS, UBARIKIWE KWA KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI, SASA TWENDE MBELE ZAIDI TUFIKE KWENYE SHERIA NA WOTE WENGINE HAO MAKATIBU NA WAKURUGENZI ULIOSEMA KWENYE HOTUBA YAKO KUWA WANAHUSIKA NA WAO PIA UWE MWENDO WA KUELEKEA KWENYE SHERIA!, NI SHERIA TU NDIO INAWEZA KUTUSAFISHA WOTE, SERIKALI NA MAWAZIRI WALIOACHWA!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William @DSM CITY!

Mkuu umeongea vizuri na ni mategemeo ya watanzania wote wangependa iwe hivyo,lakini kwa tanzania hii yetu ya leo sidhani kama kuna litakalofanyika maana tuna mifano mingi iliyopita na watu wameachiwa tuu wanaendelea kula inji hii mpaka leo na kesho.
 
Huu mchezo/wimbo tushauzoea...Magamba hawana ubavu wa kuwawajibisha viongozi wa juu,hata kwa mahakama .Tena ningeshauri waache coz ni matumizi mabaya ya rasilimali za uma kuwapeleka watu mahakamani halafu hakuna matokeo inabaki usanii
 
Mkuu umeongea vizuri na ni mategemeo ya watanzania wote wangependa iwe hivyo,lakini kwa tanzania hii yetu ya leo sidhani kama kuna litakalofanyika maana tuna mifano mingi iliyopita na watu wameachiwa tuu wanaendelea kula inji hii mpaka leo na kesho.

- Ni kwa sababu tunalia lia sana bila vitendo na kusubiri wengine na kuanza kuwatukana tu, lakini matendo hakuna! Tumedai waondoke wameondoka, sasa tudai Sheria maneno mengi off course ndicho watwala wanachokitaka kwenye maneno haya mengi watapitisha agenda zao na kubadili subject, kama wanavyojaribu sana kwa kukomalia Mbowe aeme majina by kesho media nzima itakuwa kwenye hiyo ishu, huku la mawaziri na Sheria hakuna!

- Haya tunayataka wenyewe, kwa sababu ni very clear kwamba Rais aemwaondoa kwa sababu ya CAG, sasa kwa nini tusidaai aende mbele zaidi? No wengi tunafurahia kuwaona wapo nje tu as if watapanda dala dala na sisi hata siku moja, never!

William.
 
Wakuu JF heshima mbele sana,

- Well, kitendo cha Rais kuwabadili mawaziri waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na upotevu wa hela za wananchi na ripoti ya CAG, kina maana moja tu kwamba hata na yeye ameridhika kwamba kuna ukweli au FACTS katika tuhuma walizokuwa wakituhumiwa nazo, ninasema great second day kwa Taifa, kwanza ilikuwa kuweka ripoti wazi to the public na kuruhusu mjadala wa public!

- Sasa ifike mahali pa kufanya kweli, yaani Watuhumiwa wote kufikishwa kwenye mkondo wa Sheria, haki itakua imetendeka na sio otherwise, kwanza haki kwao mawaziri maana wanahitaji kuwa wasafi mbele ya public na pili Serikali kulinda heshima yake kwamba sasa ipo serious, ama sivyo kuitoa ripoti ya CAG to the public itakuwa ni kazi ya bure, I mean mawaziri na viongozi wetu wakijua kwamba madhara ya kuiba ni kujiuzulu tu na kuachiwa ukale mihela ya wananchi tutakua tunajenga taifa la kusadikika, na itakuwa kazi kubwa kumpitisha Rais wa CCM 2015!

- MHESHIMIWA RAIS, UBARIKIWE KWA KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI, SASA TWENDE MBELE ZAIDI TUFIKE KWENYE SHERIA NA WOTE WENGINE HAO MAKATIBU NA WAKURUGENZI ULIOSEMA KWENYE HOTUBA YAKO KUWA WANAHUSIKA NA WAO PIA UWE MWENDO WA KUELEKEA KWENYE SHERIA!, NI SHERIA TU NDIO INAWEZA KUTUSAFISHA WOTE, SERIKALI NA MAWAZIRI WALIOACHWA!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William @DSM CITY!

mateso ya prezidaa msanii tumekomaje? maana epa, rada, richmond, ticks watu wanakula bata mtaani tu lakini wacha tukione maana mkwer kaiba kura tukawa makondoo kuacha kupigania haki zetu. mzee wa mahhatan karibu bongo darisalaama
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom