Mavazi ya kikahaba yanikosesha kupata mume

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,921
14,821
Kwani mavazi ya kikahaba ni yapi jamani, mbona mnanichanganya?

Je ni kweli mavazi ya kikahaba yanamfanya msichana kutopata mume?

Mbona wanawake wanaokaa uchi wameolewa sana mpaka na kuacha na kuolewa mara ya pili? Je, kupata ndoa ni lazima uvae mavazi kama staha?

Skia hii:
Shouger: Money Penny, nimeenda kuombewa kanisani nikaambiwa kupata mume nibadilishe mavazi nayovaa!

Money Penny: Kwani unavaa mavazi gani?

Shouger: Navaa suruali, skirt fupi, gauni za kuni shape, skirt ndefu, leggings, nikaambiwa nivue hayo mavazi ni ya kikahaba ndio maana wanaume wanaonifuata kama mvua, lakini hawako serious wanakuja kunichezea na kukimbia na mimi nataka kuingia kwenye ndoa sasa!

Lakini money penny mbona kuna makahaba wanavaa ovyo zaidi yangu lakini waliolewa, wakaolewa, na kuolewa na wameolewa hata zaidi ya mara 4? kwani shida ni nini wakati mimi sivai kama wao?

Kwani mavazi ya kikahaba ni yapi? ina maana mavazi ya kikahaba ndio yananikosesha kupata mume?

Haya njooni mumjibu mwenzenu na kumuongezea akili.
 
Msitudanganye hapa, huko kanisani si ndiyo mnafundishwa kuwa kahaba ndiyo wa kwanza kwenda mbinguni?

Mathayo 21:31
..Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.



Sasa kwa mafunzo hayo ya kwenye biblia nani akukataze ukahaba kanisani? Kwani hatuwaoni mnavyovaa mkienda makanisani?

Msitudhani hapa JF sote tu wajinga kama nyinyi mnaofanya ukahaba eti mtatangulia ufalme wa Mungu!

Au biblia ilimaanisha kwa ukahaba mtakufa mapema? Maana utaendaje kwenye ufalme wa Mungu kabla hujafa? Fikiri.
 
Back
Top Bottom