Mauzauza ya usiku, nitamuua huyu mama

Aliyeleta matatizo kwenye familia yenu sio uchawi ni mama yako, ndio maana mzee akaona bora ajuvutie kitu kingine atulize mawazo, baada ya kuona mama yako amezidiwa na bi mdogo kila dingi wako nao akiangalia kuanzia mapishi, mwendo wa maringo, kauli safi na usafi ndani ya nyumba kageuzia mapenzi kwa bi mdogo, nyie mnaona limbwata.

Hakuna Limbwata ni mapenzi tu. Hakuna mwanamme anaependa mwanamke mchafu, mwenye maneno ya kukera, asiyetulia kwake, asiyejua kupika. ena mzee mstaarabu angetoa talaka kabisa ajilie vyake kwa amani.

Una uhakika kuwa baba yake amechukua mke mwingine kwa kuw mama yake jamaa hana hayo usemayo…? Waislam wanapoa wake zaid ya mmoja ina maana wote waalio nao wamekosa hayo…?
Inatakiwa ifike muda utumie akili zako binfsi na sio kuangalia upepo na kutoa hoja zinazo kosa heshima wala staha kwa mzazi wa mtu. Wanaume tuna hulka zetu, sometimes tunaamua kufanya vitu na si kwamba tuna sababu za msingi, selfinshnes tunayo. Umeshowa dharau kwa mama wa mwenzio, umesem pumba.
 
Kila kitu kinaanzia chini. Hapo kuna mambo mawili
1.Usalama wako na maendeleo yako.
2. Usalama wa mama yako, familia na ndoa yake.

Hapo kwenye hali uliyopo kwa sasa, unataka solve mambo yote mawili kwa wakati mmoja ni jambo ambalo haliwezekani.
Anza na jambo la kwanza,
Tafuta mbinu ya kukuinua kiuchumi na kimaisha, na hiyo si nyingine zaid ya kufanya kazi na kuweza kujitegemea, ukiweza hilo utaweza kupata akili na njia ya kumuinua mama yako.
 
Usiku huu wa saa nane kasoro nipo macho sina hata usingizi na huko nje ya nyumba nasikia vishindo ila watu hawaonekani. Ni hivi baba yangu ana wake wawili ambao ni mama yangu na ma mdogo na wote anaishi nao nyumba moja (na mi naishi hapa nyumbani maana sijaanza kujitegemea.

Sasa tatizo kubwa ni mauzauza ya nyumba hii 90% ya watu mtaani kwetu wanajua kabisa huyu mama yangu mdogo ni mchawi. Kuna watu hapa mtaani washawahi kugombana nae wakimwambia aache kuwawangia.Mi mwenyewe alishawahi kunitokea ndotoni na wenzake wakiwa wamevaa kaniki, nilishtuka usingizini na kupiga kelele sana, but nikaamua kupotezea tu sikuwahi kumwambia mtu.

Baba nae kahisi karogwa na kapewa limbwata juu maana yupo ka zuzu, inshort katekwa sana akili. Ukimwambia mkewe mchawi ugomvi unaanzia hapo.Maelewano ya familia ya mama mdogo na familia yetu ni madogo sana maana tunajua dhahiri pasi na shaka kuwa huyo maza anaturoga na kutufanyia mauzauza na shida yake kubwa sie tupotee hapa ili ye atawale. Kiukweli maisha haya ya kurogana na kuwangiana daily mimi binafsi nimeyachoka sana.

Natamani nihame hapa home ila tatizo sina kazi itayoniwezesha kujitegemea.Yaani sasa hivi akili ishachanganyikiwa kabisa, natamani hata kumuua huyu mama ili tuishi kwa amani. Nipeni mawazo maana nahisi nishadata na nitapoelekea nitakuja kumtoa roho huyu mtu. Au kama kuna mtu anajua dawa ya kukomesha uchawi (apart from maombi au kwenda kwa waganga) anisaidie jamani.

NB: Nishaomba na kusali sana ila mauzazuza ya usiku yapo vile vile.

Msaada wenu wakuu
Ukitaka kumkamata Mama yako mdogo uchawi fanya hivi ikifika saa 9 usiku muamshe baba yako mzazi utoke nae nje ya nyumba ukae nae huko nje kama dakika 10 nzima zungumza mazungumza ya kawaida bila yeye kujuwa kuwa umemuamshia kitu gani huyo Mama yako Mdogo kama alitoka kwenda uchawini atakamatwa huko aliko na mutamuona nyinyi wote jaribu kufanya hivyo kisha utakuja kunipa feedback mkali wao;
 
Last edited by a moderator:
uchawi haupo mkuu hivyo ni kweli huna haja ya maombi sababu hayafanyi kazi unachotakiwa wewe kufanya tafuta shughuli ya kuku keep busy kidogo hizo shutuma anazopewa mama yako ni mambo tu ya wanawake wivu tu na jambo unalofikiria sana mara nyingi ubongo unakupa ndoto kuhusu hilo jamb ndio maana unapata mauzauza hayo.
 
Kama husomi hama hapo kwa baba yako, nenda kajitegemee hayo mambo ya wake za baba yako mwachie mwenyewe , wewe hayakuhusu.

Tafuta chumba cha bei rahisi panga Anza kujitegemea mambo ya kukaa kwa wazazi utakuwa unakosoa kila kitu,kila kitu utakuwa unaona hakiendi sawa.

Nilikua napata wakati mgumu sana kujua ni kwanini watu wanafeli mtihani. Ila kadiri siku zilivyokua zinaenda na kuona baadhi ya hoja zinazojengwa humu Jf juu ya Uzi fulani ndio nikaanza kupata mwangaza ka kilichokua kinanitaza. Na kamwe tupunguze kusingizia eti ni lugha ndio chanzo cha watu kufeli.
 
nicheki 0787987160 nitakusaidia ushauri ununue dawa za kisunah na uhakika hivo vituko vitaisha inshaallah.WALLAHU AALLAM.
 
Hata mi kupanga natamani hata leo... tatizo mkwanja wa kulipia kodi sina

Mkwanja sio tatizo wewe ni mwanaume kazibue hata mitalo mbona mimi nilibaki yatima ndugu ote wakanitenga nikiwa na umri wa miaka 15 nilipanga namshukuru mungu mpaka leo maisha yanaendelea tatizo uko nyumbani na mzazi wako amejenga ila angekua amepanga ote mnaishi chumba kimoja ungeenda kupanga .

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom