Mauzauza ya usiku, nitamuua huyu mama

Kama ni Muislam, hakikisha sala zako za faradhi (tano kwa siku) hazikupiti na hakikisha unakuwa udhu saa zote na unapoingia kulala hakikisha una udhu na unasoma Qur'an japo sura tatu ndogo za mwisho kila moja mara tatu.

Mashallaah!!! Huu ni ushauri mzuri wenye busara!! Ila mbona ucku wa manane ulikua unachat tu? Shemeji kasafiri au?
 
Aliyeleta matatizo kwenye familia yenu sio uchawi ni mama yako, ndio maana mzee akaona bora ajuvutie kitu kingine atulize mawazo, baada ya kuona mama yako amezidiwa na bi mdogo kila dingi wako nao akiangalia kuanzia mapishi, mwendo wa maringo, kauli safi na usafi ndani ya nyumba kageuzia mapenzi kwa bi mdogo, nyie mnaona limbwata.

Hakuna Limbwata ni mapenzi tu. Hakuna mwanamme anaependa mwanamke mchafu, mwenye maneno ya kukera, asiyetulia kwake, asiyejua kupika. ena mzee mstaarabu angetoa talaka kabisa ajilie vyake kwa amani.
 
Naomba Mungu asiwatoe hapo nyumbani.... Ila awakingeni na huyo mwovu shetani..( sio mama yako Mdogo)
 
Siku nyingine matatizo yanayomhusu mama yako usiyaongelee hadharani, kuna wenzio wanatafuta weakness halafu wanapenyea hapo hapo kwenye weakness kesho unaumbuka
 
Sasa hivi mtu akimtaka mama yako atakuja na kujifanya mganga wa kugangua limbwata, mama akishangia laini unajua kitakachoendelea. Achaneni na imani potofu za kishirikina. jiulize MBONA WACHAWI AU WAGANGA WAKIKAMATWA NA POLISI HAWAJIONDOI MIKONONI MWA DOLA KIUCHAWI.
 
Yaani kama ningepata dawa ya kumuona na kumgandiha akiwa anafanya mambo yake hiyo ingekua evidence kubwa sana...

Chunga, muda si mrefu utaanza kwenda kwa waganga na hapo utakuwa umekwisha habari yako maana utakuwa umeshaingia kwenye uchawi.

Vv
 
ukwe wenza wa mama ako na mama ako wa kambo wewe haukuhusu. mama ako na gurupu lake la marafiki majirani muachie wamsaidie kulilia wivu sio wewe mtoto wa kiume wa kutegemewa kuitwa baba unamsaidia mama ako na marafiki zake kuwa na wivu.

aisee hiyo ni aibu kwa mtoto wa kiume sio siri, yaani umetiwa kasumba chuki barabara ya kumchukia mke wa baba ako na wewe kwa akili zako fupi umeyabeba na ukayajaza tele akilini, na kumwita mama ako wa kambo mchawi.

Acha kuwa na akili changa zako na za kuchangiwa.possibility kubwa kuwa wewe hufanyi kazi kabisaa, kwa hiyo kijana fikiria maisha yako yatakuwaje na vipi utaweza kupata pesa za halali kwa ajili ya maisha yako mwenyewe kuliko kuendelea kukaa nyumbani mpaka saivi wakati ullitakiwa uwe na maisha yako na mkeo na wanao.Fikra potofu za uke wenza achana nazo na umwambie mama " wivu utakuja kukutia maradhi hii baba ni haki yake kisheria najua inauma lakini VUMILIA"

umenena vema,mchawi ni yeye na akili yake mbovu.Mtoto wa kiume inatakiwa uingie mtaani kusaha noti si kuendeleza chuki za marafiki wa mama yako na mama yako mdogo.Yaonesha bado ni mbumbumbu wa mambo mengi hapa duniani hususani ndoa.

Acha ubwege wa kukaa kwa babako halafu utegemee maisha bora.Ingia kitaa,beba mizigo,uza machungwa piga debe kisha tofauti chumba ujitegemee huo ndo utakuwa mwisho wa akili ya kijinga inayoona mauzauza.

CHANGAMKA ANZA SASA
 
Usiku huu wa saa nane kasoro nipo macho sina hata usingizi na huko nje ya nyumba nasikia vishindo ila watu hawaonekani...

Ni hivi... baba yangu ana wake wawili ambao ni mama yangu na ma mdogo na wote anaishi nao nyumba moja (na mi naishi hapa nyumbani maana sijaanza kujitegemea)

Sasa tatizo kubwa ni mauzauza ya nyumba hii... 90% ya watu mtaani kwetu wanajua kabisa huyu mama yangu mdogo ni mchawi. Kuna watu hapa mtaani washawahi kugombana nae wakimwambia aache kuwawangia.

Mi mwenyewe alishawahi kunitokea ndotoni na wenzake wakiwa wamevaa kaniki, nilishtuka usingizini na kupiga kelele sana, but nkaamua kupotezea tu sikuwahi kumwambia mtu.

Baba nae kahisi karogwa na kapewa limbwata juu maana yupo ka zuzu, inshort katekwa sana akili. Ukimwambia mkewe mchawi ugomvi unaanzia hapo..

Maelewano ya familia ya mama mdogo na familia yetu ni madogo sana maana tunajua dhahiri pasi na shaka kuwa huyo maza anaturoga na kutufanyia mauzauza na shida yake kubwa sie tupotee hapa ili ye atawale.

Kiukweli maisha haya ya kurogana na kuwangiana daily mimi binafsi nimeyachoka sana. Natamani nihame hapa home ila tatizo sina kazi itayoniwezesha kujitegemea.

Yaani sasa hivi akili ishachanganyikiwa kabisa, natamani hata kumuua huyu mama ili tuishi kwa amani.

Nipeni mawazo maana nahisi nishadata na ntapoelekea ntakuja kumtoa roho huyu mtu. Au kama kuna mtu anajua dawa ya kukomesha uchawi (apart from maombi au kwenda kwa waganga) anisaidie jamani

NB: Nishaomba na kusali sana ila mauzazuza ya usiku yapo vile vile.

Msaada wenu wakuu
Paw please,mada hii ni ya mmu!
 
Last edited by a moderator:
Uchawi upo na nguvu za kuushinda uchawi zinatrofautiana kati ya mtu na mtu.
FaizaFoxy kashauri vzr sana.
Kama ni mkristo fanya maombi ya kubomoa ufalme kwa kufunga, hapa ni uache kazi ufanye kazi manake sio kazi ndogo na sio mchezo ata kidogo.

kama ni wa anga za juu kusin basi nenda na wewe mlingotini kammalize manake akuanzae mmalize
 
Last edited by a moderator:
Ndugu mi nshaomba sana... ila huyu mama ni kiboko,kila siku afadhali ya jana

Hakuna kiboko zaidi ya YESU, omba na uamini, Mungu hapendezwi na mtu anaye omba huku bado ana mashaka moyonin mwake. Sio unaomba halafu kuingia kitandani unaogopa au unaingia halafu unalala kimachale, ukijigusa tu wewe mwenyewe unaruka. Mchawi unamjua tena upo nae ndani, hiyo ni fursa ya kuomba na kumuombea kwelikweli tena usiku simama na uombe bila uoga.

Pata picha mchawi angekuwa mtu wa nje na usiyemjua?? unayo sababu nzuri zaidi ya kutokuogopa na kumuomba Mungu, lakini tambua hivi vitu vinahitaji uwe THABITI mbele za Mungu. Mungu wetu na awasaidie. "LUKA 10:19"

Pia lijue neno litakupa Imani na nguvu zaidi.
 
eti apart from maombi... sasa Bila kumuomba Mungu unategemea mauza yanaishaje tatizo uliomba bila imani na hauamini ndo maana hakuna kunachoshindikana ukiliitilizia jina la Yesu..... kama unategemea ushauri wa kumuua mamako mdogo hiyo dhambi itakutafuna milele muombe Mungu
 
Kama ni Muislam, hakikisha sala zako za faradhi (tano kwa siku) hazikupiti na hakikisha unakuwa udhu saa zote na unapoingia kulala hakikisha una udhu na unasoma Qur'an japo sura tatu ndogo za mwisho kila moja mara tatu.
Faiza Foxy nakukubali. somo tosha kwa sisi wote. ulipitia madrasa ya baba ake Sheikh Yahya Hussein pale Kinondoni nn??!!
Mashallah motto weye
 
Kama husomi hama hapo kwa baba yako, nenda kajitegemee hayo mambo ya wake za baba yako mwachie mwenyewe , wewe hayakuhusu.

Tafuta chumba cha bei rahisi panga Anza kujitegemea mambo ya kukaa kwa wazazi utakuwa unakosoa kila kitu,kila kitu utakuwa unaona hakiendi sawa.

Pamoja mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom