Mauzauza nyumba ya kupanga sio uchawi wala wezi, ni wenge langu tu!

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Jun 20, 2022
1,215
2,995
habari zenu wana JF,

I hope ni wazima wa afya kabisa na wenye matatizo mbalimbali mungu awapone, ameen.

Kuna kisa kimoja kuhusu hizi nyumba za kupanga, tunaishi bila kuyaelewa vizuri mazingira na kupelekea kuwa na hofu na kuwaza vitu vibaya.

Nakumbuka niliahamia kwenye nyumba moja mtaa X ile nyumba ina vyumba 2 self, sebule, jiko na stoo ndogo mazingira ya ile nyumba ilikuwa ipo mwishoni baada ya nyumba kuna kama hekta 2 za pori halafu unakutana na mto mdogo (niliyapenda mazingira hayo sababu napenda sehemu iliyotulia).

Kisa: Baada ya kuhamia wiki moja niliishi safi tu ila ghafla mida ya usiku hasa dirisha la chumbani ambalo limeangalia kwenye lile pori nikawa nasikia vishindo, nikitulia kidogo nasikia kama kioo kinavunjika cha dirisha hii hali iliendelea kwa wiki kadhaa nikawa na hofu wachawi au wezi wanataka kuniotea.

Ila niliendelea kuamini ni hali ya kawaida mpaka nikaizoea nilichogundua kuwa haya madirisha ya alluminium baada ya kupigwa jua mchana usiku yanatabia ya kujitanua lazima usikie kama mlio fulani hivi kama kioo kinavunjika au kishindo fulani kidogo.

Unakuta mtu amehamia kwenye nyumba akisikia kishindo au mlio fulani usiku wazo linalokuja kichwani ni wachawi au wezi kumbe ni hali ya kawaida tu.

Niliishi pale mwaka 1 nikahama na niliishi kwa amani na starehe sana.

NB: Mauzauza yapo kwenye nyumba za kupanga lakini sio kila nyumba iko hivo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom