Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Atengwa kwa kuoa albino

Mkazi wa Dodoma mjini, Bw. Peter Msangi, amejikuta katika wakati mgumu baada ya familia yake kumtenga kutokana na kuoa mwanamke albino, Bi. Mariam Simon.

Ndugu wa Bw. Harusi huyo walisusia sherehe ya kijana wao baada ya kumtaka amwache albino huyo, lakini bila mafanikio.

Kutokana na hali hiyo, wazazi walimfukuza kwa madai kuwa
amewapelekea nuksi katika familia, kwani tangu ukoo huo umekuwapo duniani haujawahi kuzaa mtoto albino wala kuozesha mtu wa jinsi hiyo.

Katika utaratibu mzima wa kuhakikisha anapata jiko, aliwapa taarifa wazazi wake, lakini ilikuwa vigumu kueleweka kwa wazazi wake jambo ambalo lilimfanya ajishughulikie katika suala zima la mahari.

Pamoja na kuendelea na hatua hizo zote, wazazi wake waliendelea kumchukia na kumwona kama amechanganyikiwa lakini msimamo wake ulizidi kuwa madhubuti na kutaka kumaliza mahari, ili aweze kupata fursa ya kupangiwa muda wa kuoa.

Hata hivyo, juhudi za kuhakikisha anakamilisha hatua zote zilizidi kuwapa hasira wazazi wake ambao waliamua kutotaka kumwona hata kwa sura, kwa madai amewafanyia kitu kibaya.

Baada ya wazazi kususia harusi hiyo na kuamua kumfuta katika ukoo, Kanisa liliamua kumtafuta mzazi wa bandia ili kuweza kuondoa maswali mengi kwa watu walioalikwa kufika katika sherehe ambayo ilikuwa ya kufa mtu.

Akizungumzia suala hilo Bwana Harusi juu ya uamuzi wake na wa wazazi, alisema amempenda binti huyo ambaye ni albino kwani ana sifa zote za kuitwa mke mwema.

Bw. Msangi alisema kuwa anachotambua ni kila mtu ana kasoro zake na kila mtu ni mlemavu, hivyo suala la ngozi haliwezi kuwa kigezo cha kumfanya asimwoe binti huyo ambaye anajua wazi kuwa hakuna binti mzuri kama yeye.

“Albino ni mwanadamu kama mwanadamu mwingine na rangi yake
imenivutia zaidi kwani hana tofauti na Wazungu," alisema Bw.

Msangi ambaye sherehe yake ilikuwa kubwa kuliko kawaida.
Juu ya uamuzi wa wazazi kumtenga, alisema anachoshukuru wazazi wake ni kumlea vizuri na kumfundisha mema na mabaya, hivyo kwa kuwa ameishakua amechagua kumwoa mke huyo ambaye ni chaguo la moyo wake.

Alisema anachosubiri sasa ni kuona kama wazazi wake watamchukia yeye pekee au watawachukia pia wajukuu kama Mungu atawajalia kupata watoto hapo baadaye.

Kwa upande wake, Bibi Harusi, Mariam Saimoni alisema mpango wake na wa Mungu, ni kuona kila mwanamke anaolewa na yeye ameolewa kama walivyo wanawake wengine na kuhusu suala la yeye kuzaliwa albino si lake ni mpango wa Mungu.

Alisema kuwa albino si tiketi ya kukosa haki zake, bali anastahili kupata haki zake kama watu wengine na anawashukuru wazazi waliomsomesha na kumfanya aishi maisha mazuri kama watu wengine.

Pia alimsifu mumewe kwa ujasiri wa kumchumbia na kufuata taratibu zote kwa uaminifu, mpaka kufikia hatua ya kufunga pingu za maisha ingawa wamekuwa na mapito mengi, kwani alionekana kama anaoa mtu ambaye hastahili kuwa katika jamii.
 
Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Na alichokiunganisha Mungu mwanadamu asitenganishe.

Ndugu Msangi, hongera sana kwa kumuona binti Mariam. Mungu Mwenyezi aliyewaumba alijua kuwa siku moja mtakuwa mke na mume. Mwenyezi Mungu awabariki awape maisha marefu (awajalie muone watoto, wajukuu, watoto wa wajukuu na wajukuu wa wajukuu wenu), pamoja na utajiri (Fedha na Dhahabu ni Mali ya Mungu) ili hata hao waliowatenga waje kukopa na kuomba kwenu. Amen.
 
Albino Tanzania wafikiria kuomba hifadhi nchi za je
Burhani Yakub, Tanga

WATU wenye ulemavu wa ngozi, Albino, wamehoji sababu za serikali kushindwa kuwapatia ulinzi na kufikia hatua ya kufikiria ama kulala barabarani au kuomba hifadhi nchi nyingine.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa maandamano yatakayofanyika Oktoba 18 mwaka huu jijini Dar es salaam kupinga mauaji ya albino yanayoendelea nchini, hasa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Josephat Torner.

Torner mwenye ulemavu huo alisema kadili siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo hali inakuwa tete kwa maisha yao na kwamba hawajui wafanye nini au waende wapi.

“Hivi serikalini kuna ajenda ya siri? Mbona haionyeshi kuwa imepania kukomosha mauaji ya albino au inaona kama sisi siyo sehemu ya jamii?” alihoji Torner .

Kiongozi huyo alisema kama serikali imeshindwa kuwalinda basi waamue kulala barabarani au kuomba hifadhi nchi nyingine.

“Hatujui sasa tuende wapi miili yetu imegeuka kuwa mitaji ya kuwatajirisha baadhi ya watu wanaoaumua kutufanyia ukatili wa kutuua na kututesa kwa kunyofoa viungo na nywele zetu,” alisema Torner.

Mratibu huyo alisisitiza maneno yake ya ambayo amaekuwa akiyasema mara kwa mara anapozungumza na Mwananchi kuwa anaamini serikali haijaamua kutumia nguvu zake kukomesha mauaji hayo

Kikwete amealikwa kuwa mgeni rasmi katika maandamano ya kitaifa ya kupinga ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ya Oktoba 18, mwaka huu na kwa mujibu wa Torner maandalizi yamefikia hatua nzuri.

Alisema kulingana na uzito wa maandamano hayo, kamati ya maandalizi iimeomba Raisa Kikwete ndiye awe mgeni rasmi ili kumpa nafasi kutoa tamko zito ambalo linaweza kusaidia kukomesha mauaji hayo.

“Barua ya kumuomba Rais ilishawasilishwa na kupokewa jana (Jumatatu) Ikulu Jijini Dar es salaam na tumehakikishiwa kuwa atahudhuria,” alisema Torner.

Maandamano hayo yaliyopangwa kuanza katika Ofisi za TGNP, Mabibo na kuelekea viwanja vya Jangwani yanaratibiwa na wajumbe 13 wanaowakilisha asasi na mashirika mbalimbali yakiwamo ya kimtaifa yanaojihusisha na watetezi wa haki za walemavu.

Mashirika hayo ni Chama cha Malabino Taifa, Mtandao wa Jinsia (TGNP), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Asasi ya Inayojihusisha na Ututezi wa Sheria (LHR), Site Save Us International, ICD, ADD, Shivyawata Taifa na TNIB.

MY TAKE: Ni aibu kubwa kwa serikali yetu pale inaposhindwa kulinda watu wake. Moja ya jukumu la serikali ni kulinda watu wake, lakini kibaya zaidi hapa ni kwamba wananchi hawa wasio na hatia, hawana usalama ndani ya nchi yao . Hivi hili nalo linahitaji misaada ya wafadhili ?

Ni aibu kwa serikali ya awamu ya nne kujivuna kuwa na viongozi wakati viongozi hao wanashindwa mambo ya msingi kabisa kama ulinzi wa wananchi wake, na tena wananchi hawa ambao hawafikii hata 5% ya jumla ya watanzania wote.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Polisi (IGP) wana jukumu katika ulinzi wa wananchi hawa, na kama wameshindwa kufanya kazi hii, WAJIUZULU.
 
Albino Burundi wauawa kwa ajili ya soko la Tanzania
BUJUMBURA, Burundi

BURUNDI imekumbwa na wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, kutokana na imani za kishirikina.


Kwa mujibu wa Polisi nchini Burundi hivi sasa maalbino wamelazimika kukimbilia katika hifadhi ya jeshi hilo baada ya kundi la watu kuua maalbino watatu na kuondoka na miguu yao.


Katika albino walionusurika, wanne wamelazimika kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Ruyigi na polisi sasa wanatoa ulinzi mkali kwa watu hao.


Tanzania imekumbwa na wimbi la mauaji ya albino na hadi sasa albino 26 wameshauawa katika kipindi cha mwaka mmoja kutokana na imani za kishirikina. Mauaji hayo yansababishwa na imani kwamba viungo vya albino husaidia bahati uchimbaji wa madini na kuwafanya watu watajirike.

Chanzo BBC
 
Disgusting!!!

The governments inability to stop this madness is inexcusable and unforgivable.
 
naona burundi wanatafuta sababu za kuingia tanzania kutumia suala hili la maalbino usishangae wanausalama wake wakasema wamelazimika kuvamia vijiji huko mpakani kutafuta wanaouwa maalbino
 
Albino Burundi wauawa kwa ajili ya soko la Tanzania
BUJUMBURA, Burundi

BURUNDI imekumbwa na wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, kutokana na imani za kishirikina.


Kwa mujibu wa Polisi nchini Burundi hivi sasa maalbino wamelazimika kukimbilia katika hifadhi ya jeshi hilo baada ya kundi la watu kuua maalbino watatu na kuondoka na miguu yao.


Katika albino walionusurika, wanne wamelazimika kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Ruyigi na polisi sasa wanatoa ulinzi mkali kwa watu hao.


Tanzania imekumbwa na wimbi la mauaji ya albino na hadi sasa albino 26 wameshauawa katika kipindi cha mwaka mmoja kutokana na imani za kishirikina. Mauaji hayo yansababishwa na imani kwamba viungo vya albino husaidia bahati uchimbaji wa madini na kuwafanya watu watajirike.

Chanzo BBC

Mama Mia na huyu Mr Dog alivalishwa bendera ya chama fulani ulikutana naye wapi? Ni mbwa wa polisi ya Tanzania nini? maana wanafanana fanana.
 
Albino Burundi wauawa kwa ajili ya soko la Tanzania
BUJUMBURA, Burundi

BURUNDI imekumbwa na wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, kutokana na imani za kishirikina.


Kwa mujibu wa Polisi nchini Burundi hivi sasa maalbino wamelazimika kukimbilia katika hifadhi ya jeshi hilo baada ya kundi la watu kuua maalbino watatu na kuondoka na miguu yao.


Katika albino walionusurika, wanne wamelazimika kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Ruyigi na polisi sasa wanatoa ulinzi mkali kwa watu hao.


Tanzania imekumbwa na wimbi la mauaji ya albino na hadi sasa albino 26 wameshauawa katika kipindi cha mwaka mmoja kutokana na imani za kishirikina. Mauaji hayo yansababishwa na imani kwamba viungo vya albino husaidia bahati uchimbaji wa madini na kuwafanya watu watajirike.

Chanzo BBC

Binadamu anayefanya unyama wa namna hii dhidi ya binadamu mwenziwe hata kama ni kwa kisingizio cha mafanikio, anaonyesha kiwango cha hali ya juu cha ushenzi maana hana tofauti na mnyama. Maana binadamu kaumbwa mwenye huruma si kwa binadamu mwenzie tu bali hata kwa viumbe wenzake
 
Habari zaidi!
Tushirikiane kupambana na unyama huu dhidi ya albino


Hakuna asiyefahamu uwapo wa tatizo la mauaji ya albino ambalo kwa sasa kasi yake inazidi kuongezeka, tatizo hilo pamoja na kutishia maisha ya jamii ya albino pia linatishia kuipotezea nchi yetu sifa yake ya amani na utulivu iliyojiwekea kwa muda mrefu.

Ukweli ni kwamba vitendo vya mauaji ya albino ni vya kinyama na vinakiuka si tu haki za binadamu bali hata Katiba ya nchi ambayo inasema kila mtu ana haki ya msingi ya kuishi na kulindwa.

Ingawa itaonekana suala hili limepigiwa kelele sana lakini bado mauaji yanazidi kutokea na kuongeza hofu katika jamii ya albino ambayo kwa mujibu wa Mratibu wa Maandamano ya kupinga mauaji ya Albino yaliyofanyika jana, wengi wao wana hofu, hasa watoto, kiasi cha kugoma kwenda shule.

Kama hiyo haitoshi wengine wamefikia kukimbia huko vijijini ambako vitendo hivyo vimeshamiri kutokana na dhana ya ushirikina na kukimbilia mjini na wengine kufikia hadi kulindwa na askari ili tu kuokoa maisha yao.

Wakati umefika kwa waganga wanaosambaza dhana hii potofu ambayo Rais wetu Jakaya Kikwete ameikemea vikali, kwamba viungo vya wenzetu hawa albino ni chanzo cha utajiri, watafutwe kwa udi na uvumba na kuchukuliwa hatua kali dhidi yao ili iwe fundisho.

Na katika hotuba yake aliyoitoa jana Kikwete aliahidi kuwa serikali yake itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tatizo hilo linapewa uzito ikiwa ni pamoja na kusambaza elimu kwa wananchi juu ya albino ili waweze kuondokana na dhana potofu dhidi ya jamii hiyo.

Rais Kikwete aliita dhana kwamba viungo vya albino huleta utajiri kuwa ni ujinga. Tunaunga mkono kauli hii kwani albino ni kama binadamu wa kawaida isipokuwa tu ukosefu wa vinasaba vya kutengeneza rangi ya mwili tuliyoizoea.

Sasa iweje tatizo la vinasaba vya kutengeneza rangi ya mwili iweze kumletea mtu utajiri? Na kama kweli kinachosababisha utajiri huo ni rangi yao, Wazungu, Wahindi na wengineo ambao wana rangi nyeupe wana nafasi gani katika hili? Ukweli ni kwamba hayo yote ni imani na dhana potofu ambazo zimejengwa na watu wachache kujipatia fedha na jambo la kuzingatia ni kwamba Watanzania wanapaswa kuwa makini na watu wa aina hiyo.

Ili kupambana na vitendo hivyo, itawezekana iwapo tu jamii nzima itashirikiana na serikali kupitia vyombo vyake vya dola katika kuwafichua waganga hawa ambao tuna imani wamo ndani ya jamii zetu na wanafahamika ili waweze kuchukuliwa hatua zinazostahili.

Suluhu la matatizo yanayowapata albino nchini mwetu kutokana na imani za kishirikina na mila potofu, inahitaji uangalizi na ufumbuzi mpana na wa kudumu utakaoshirikisha Watanzania kwa ujumla na siyo juhudi za zima moto.
 
Polisi wantia mbaroni kwa tuhuma za kumvamia albino


JESHI la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kushiriki katika tukio kumvamia na kumkata mapanga albino kwa lengo la kumuua na kuchukua viungo vyake.


Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Andrew Salewi alidai kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 17, mwaka huu ambapo kundi la watu waliokuwa na silaha za jadi walivamia na kuvunja nyumba alimokuwa akiishi albino huyo, Miriam Stanford (28), mkazi wa Kata ya Nyamiaga wilayani

Ngara saa 7.00 usiku na kuanza kumkata kwa mapanga.


Hata hivyo wavamizi hao hawakufanikiwa kumuua huyo baada ya albino kupiga kelele za kuomba msaada kwa majirani, lakini walimkata na kisha kimbia na mkono wake wa kulia.


Kamanda Salewi alisema kukamatwa kwa mtu huyo kulitokana na mtuhumiwa kutambuliwa na kutajwa na albino huyo kuwa ni miongoni mwa watu waliomvamia siku

hiyo.


Kamanda Salewi jeshi lake linawahoji watu wanne ambao ni jamaa wa albino huyo walikuwa wakiishi naye katika nyumba hiyo ili kujua kwa nini walishindwa kutoa msaada wa haraka kwa ngudu yao.


Alifahamisha kuwa kabla ya wavamizi hao kuondoka walitaka kumkata mkono wa pili, lakini walishindwa kutokana na kelele za kuomba msaada zilizokuwa zinapigwa na albino huyo na majirani kuanza kukusanyika kwa ajili ya kumsaidia.


Baada ya tukio hilo, albino huyo alipelekwa katika hospitali teule ya Murgwanza iliyoko wilayani Ngara ambako amelazwa kwa matatibabu kutokana na majeraha aliyopata baada ya kukatwa mkono wa kulia.


Kamanda huyo alidaikuwa kinachoshangaza ni kwamba albino huyo alikuwa akiishi na watu wanne ambao hakuwataja majina yao wakati wa tukio walikuwa ndani ya nyumba hiyo lakini hawakumsadia.


Jeshi hilo limetoa onyo kwa watu wanaojihusisha na matukio ya kuwajeruhi na kuwaua watu hao wenye ulemavu wa ngozi kwa imani za kishirikina na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria
 
Tume yampinga Rais Kikwete kuhusu hukumu ya kifo kwa mauaji ya albino
Na Furaha Kijingo

TUME ya Haki za Binadaamu imesema ina mpango wa kumwandikia barua Rais Jakaya Kikwete kumueleza sababu za mauaji ya albino na kupinga adhabu ya kifo.


Akihutubia mkutano wa hadhara kuhitimisha maandamano ya kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, Rais Kikwete alisema adhabu ya kuua bado haijabadilishwa na wala haibagui, hivyo anayeua albino anafanya kosa la mauaji ambalo adhabu yake ni ile ile ya kifo hadi hapo sheria itakapobadilishwa.


Akizungumza na Mwananchi jana, mwanasheria wa tume hiyo, Clarence Kipobota alisema kitendo cha Rais Kikwete kutamka kwamba atakayejihusisha na mauaji ya albino atakumbana na adhabu ya kifo kama sheria zinavyosema.


“Rais jana (juzi) alizungumza kisiasa kwa sababu adhabu ya kifo haiwezi kukomesha maujai ya albino,” alisema Kipobota.


Alisema kutokana na msimamo huo wa rais kuhusu adhabu ya kifo, wameamua kumuandikia ili kumueleza sababu za tume hiyo kupinga na jinsi ya kumaliza tatizo kubwa la mauaji ya albino.


Awali alifafanua kuwa kinachosababisha mauaji ya albino ni umasikini hivyo ni vema serikali ikaangalia jinsi gani itaondokana na tatizo la umaskini na ufahamu wa masuala mbalimbali.


''Kutokana na umasikini, hali ngumu ya maisha na ufahamu mdogo, mtu hana njia ya kujikwamua kimaisha. Anapoambiwa ukimuuwa albino utapata pesa, anaamua kufanya hivyo,'' alisema Kipobota.


Kipobota alisema adhabu hiyo inaweza ikawapata wasio na hatia kwani mauji hayo hufanyika kisiri na sehemu iliyojificha hivyo inawezekana kabisa mahakama ikamuona mtu ambaye hakuhusika kabisa na mauaji, kuwa ndiye aliyefanya tendo hilo na kuhukumiwa kifo, kitu ambacho alisema kinakuwa kibaya miaka michache baadaye inapobainika kuwa aliyeua ni mwingine.
Tume yampinga Rais Kikwete kuhusu hukumu ya kifo kwa mauaji ya albino
Source:Mwananchi
 
Hapo Kikwete hajazungumza kisiasa, amezungumza kama sheria inavyosema, kuwa adhabu ya muuaji kwa mujibu wa sheria hadi sasa ni kifo. Hapo Rais hajakosea chochote, anasimamia utawala wa sheria kwa mujibu wa kiapo chake. Ingekuwa sheria inasema tofauti na rais akasema wauaji wa albino wauawe, hapo kungekuwa na hoja ya kumpinga.Hadi sasa hivi huyu Kipobota hana hoja dhidi ya Rais, labda watafute hoja dhidi ya sheria iliyopo. Na wakija na hoja dhidi ya sheria ya adhabu ya kifo, tuko wengi tunaoiona inafaa sana kwa wauaji, na tutapambana kwenye hoja. Naamini serikali haitakurupuka kwenda kufuta adhabu hiyo bila kuhusiaha wadau. Kama kuna watu wanaofaidika na hela za NGO's za watu wanaotetea "haki" za wauaji, wanatakiwa wajue pia raia wema wana haki pia ya kutetewa, na kwa mtazamo wangu haki ya raia wema ni bora kuliko "haki" feki za wauaji.

Sheria iendelee kuchukua mkondo wake dhidi ya wanaofanya mauaji ya raia wetu (wakiwemo albino), na hukumu iliyopo iendelee kutumika na kutekelezwa. Namwomba JK kuwa iwapo wanakamatwa hao wauaji wa albino na kukutwa na hatia, hukumu ya kunyongwa ikipitishwa dhidi yao, namwomba sana JK aweke hizo saini tupunguziwe haya mabaradhuli.

Jaribio lolote la kutaka kufuta hukumu ya kifo dhidi ya wauaji litakutana na upinzani mkali kutoka kwa wanaharakati wa haki za raia wema. Na hapo tutataka tujue nchi hii inaheshimu haki za nani kati ya raia wema na majambazi wauaji.
 
Kithuku,

First of all, I am anti- death penalty and generally anti-Kikwete. But the truth must be told, Kikwete said nothing wrong according to my observation.

Hao majaji wa aina hii huku Marekani wanaitwa "activist judges".Huyu jaji inaonekana ni anti-death penalty, which is OK. Lakini to fault the president in the reported manner is not only irresponsible, but also can be interpreted as improper use of judiciary influence.

Kama hamna swala la misreporting the whole thing, judge anakuja across kama ana m lecture rais kwamba death penalty is not a determent of killing the albinos, but that is besides the point.If the existing law says the death penalty must apply to killers, the president is only reiterating and stressing the law.

Jaji anavyoongea it is as if Tanzania ilisha abolish the death penalty halafu Kikwete anataka kuirudisha kwa nguvu.
 
Kithuku,

First of all, I am anti- death penalty and generally anti-Kikwete. But the truth must be told, Kikwete said nothing wrong according to my observation.

Hao majaji wa aina hii huku Marekani wanaitwa "activist judges".Huyu jaji inaonekana ni anti-death penalty, which is OK. Lakini to fault the president in the reported manner is not only irresponsible, but also can be interpreted as improper use of judiciary influence.

Kama hamna swala la misreporting the whole thing, judge anakuja across kama ana m lecture rais kwamba death penalty is not a determent of killing the albinos, but that is besides the point.If the existing law says the death penalty must apply to killers, the president is only reiterating and stressing the law.

Jaji anavyoongea it is as if Tanzania ilisha abolish the death penalty halafu Kikwete anataka kuirudisha kwa nguvu.

Mkuu, ni kweli unachosema. Lakini pia Watanzania huru wana haki ya kutoa maoni yao hata kwa yale yanayosemwa na Rais. Kwa hapa Tanzania, kumeshakuwa na mjadala kuhusu kuondolewa kwa adhabu ya kifo na kama wanaharakati wengine wanvyosema, hata mimi sioni kama adhabu ya kifo inaweza kuondoa mauaji ya albino.

Kwanza kama hiyo ingekuwa dawa mauaji yanayotokea hapa Tanzania na si kwa albino tu bali hata kwa watu wengine yangekoma kabisa: mke kumwua mme au mme kumwua mke kwa sababu ya wivu wa kimapenzi, ujambazi wa kutumia silaha na nk.

Mauaji haya yataondoka tu iwapo jamii ya Watanzania itaondokana na umaskini na hasa vitendo vinavyokithiri vya rushwa vinavyowafanya baadhi ya watu na wao watumie njia zao za kufanya uhalifu kama huo wa kuwaua maalbino ili wapate utajiri (yaani waondokane na umasikini - wheather real au unreal).

Ukimwua mtu, hujamfunza chochote - umekatiri tu. Kuna mtu alishawahi kuuliza hivi: kwa vile mtu akiua na yeye auawe, je mtu akilawiti naye alawitiwe? Sasa ni nani atakuwa na haki ya huko kuua au kulawiti kwa vile watakaofanya hivyo si wale - aliyeuawa na kulawitiwa?

Nadhani unaweza kuona kitu gani najaribu kueleza: yaani kuwa 'revenge is never a solution to any problem, it only increases the problem - more revenge'. Na adhabu ya kifo iko kwenye kundi hili!
 
Last edited:
I'm just sitting here and it just hit me... familia zote zenye Albino zipewe leseni na bastola za kujihami nazo. Wapewe mafunzo ya kuzitumia. Hii ni kwa vile serikali imeshindwa kuwalinda na haki yao ya kujilinda na kulinda maisha yao itumiwe.

Wale maalbino watu wazima wapewe bunduki zao wao wenyewe na wale wenye wana familia basi wapewe silaha hizo ili kulinda familia zao.
 
isije ikawa ndio njia rahisi ya kuchukua ivo viungo kwani wataanza kuwaweka chini familia kwanza na silaha yao ikawa ndio kirahisisho cha kazi yao!
angalia tukio la juzi wamemvamia albino amepiga kelele familia imechelewa??????kutoka kumsaidia wakaondoka na mkono!
 
inaweza ikasaidia ,na pia kuwe na ulizzi wa kijiji au sehemu ,ingawaje kwa sasa maeneo mengi yameacha huo ulinzi (sungusungu),kwani mara nyingi matukio haya ya mauaji ,wizi ramani inachorwa na mtu anaefahamu vema hiyo sehemu,huenda hata akawa ni ndugu au jamaa wa karibu.
 
Back
Top Bottom