Mauaji Tarime: Daktari atishiwa kuuawa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
DAKTARI aliyesimamia uchunguzi wa miili ya watu wanne kati ya watano waliouawa na Polisi Mei 16, mwaka huu akiziwakilisha familia za wafiwa amedai kwamba ametumiwa ujumbe wa maandishi kwa simu kwamba atauawa.

Daktari huyo, Grayson Nyakarungu wa Mwanza alisimamia uchunguzi wa miili ya Chacha Ngoka, Emmanuel Magige, Bhoke Chawali na Mwikwabe Mwita katyika uchunguzi uliofanyika Mei 23, mwaka huu.

Alisema kwamba alipokea ujumbe wa simu mara mbili kwa nyakati tofauti Mei 26, mwaka huu akiwa safarini kuelekea Dar es Salaam uliojaa vitisho.

Alidai kwamba moja wa ujumbe huo unaosomeka, “Hizo ripoti siyo za kisiasa, acha kujiingiza kichwa kichwa utajutia, Tundu Lissu ndiye anakutumia ili yeye apate umaarufu, usipokoma kwa onyo hili, tutakushughulikia, subiri mahakamani ukatoe ushahidi, usidanganywe...”

Dk Nyakarungu alisema mara baada ya kupokea ujumbe huo, alipiga simu katika namba hiyo na kupokewa na mwanamke aliyedai kuwa yuko Mwanza ambaye hakutaka kujitambulisha. Alidai kwamba mara baada ya kukata simu hiyo, alipokea ujumbe mwingine uliosema:

“Hata ukitutambua utafanya nini, narudia mara ya mwisho, hizo ripoti haziwahusu wanahabari, funga domo lako.”Dk Nyakarungu alisema kwamba ametoa taarifa juu ya matukio hayo katika Kituo cha Polisi, Oystebay, Dar es Salaam na kufunguliwa jalada namba OB/RB/9214/11.

Hata hivyo, alisema licha ya vitisho hivyo hataogopa kwa kuwa alitumwa na familia na amelazimika kuwapa taarifa zote zilizojitokeza.Alisema inaelekea kuwa aliyetuma ujumbe huo amekuwa akimfuatilia kwa kuwa ametuma ujumbe huo katika namba zake mbili tofauti za simu.
 
Daktari Grayson Nyakarungu wa Mwanza aliyesimamia uchunguzi wa miili ya watu wanne kati ya watano waliouawa na Polisi Mei 16, mwaka huu akiziwakilisha familia za wafiwa amedai kwamba ametumiwa ujumbe wa maandishi kwa simu kwamba atauawa.

Amedai kupokea ujumbe wa simu mara mbili kwa nyakati tofauti Mei 26, mwaka huu akiwa safarini kuelekea Dar es Salaam uliojaa vitisho.

Moja wa ujumbe huo unaosomeka, “Hizo ripoti siyo za kisiasa, acha kujiingiza kichwa kichwa utajutia, Tundu Lissu ndiye anakutumia ili yeye apate umaarufu, usipokoma kwa onyo hili, tutakushughulikia, subiri mahakamani ukatoe ushahidi, usidanganywe...”

“Hata ukitutambua utafanya nini, narudia mara ya mwisho, hizo ripoti haziwahusu wanahabari, funga domo lako.” Dk Nyakarungu alisema kwamba ametoa taarifa juu ya matukio hayo katika Kituo cha Polisi, Oystebay, Dar es Salaam na kufunguliwa jalada namba OB/RB/9214/11.

Hata hivyo, alisema licha ya vitisho hivyo hataogopa kwa kuwa alitumwa na familia na amelazimika kuwapa taarifa zote zilizojitokeza. Alisema inaelekea kuwa aliyetuma ujumbe huo amekuwa akimfuatilia kwa kuwa ametuma ujumbe huo katika namba zake mbili tofauti za simu.

Mwananchi.
 
Binadamu kazaliwa siku moja atakufa siku moja.Kama wamesema ni mambo ya kisiasa kitakuwa chama fulani kilichozoea kuua wananchi.Tenda haki bila woga
 
DAKTARI aliyesimamia uchunguzi wa miili ya watu wanne kati ya watano waliouawa na Polisi Mei 16, mwaka huu akiziwakilisha familia za wafiwa amedai kwamba ametumiwa ujumbe wa maandishi kwa simu kwamba atauawa.

Daktari huyo, Grayson Nyakarungu wa Mwanza alisimamia uchunguzi wa miili ya Chacha Ngoka, Emmanuel Magige, Bhoke Chawali na Mwikwabe Mwita katyika uchunguzi uliofanyika Mei 23, mwaka huu.

Alisema kwamba alipokea ujumbe wa simu mara mbili kwa nyakati tofauti Mei 26, mwaka huu akiwa safarini kuelekea Dar es Salaam uliojaa vitisho.

Alidai kwamba moja wa ujumbe huo unaosomeka, "Hizo ripoti siyo za kisiasa, acha kujiingiza kichwa kichwa utajutia, Tundu Lissu ndiye anakutumia ili yeye apate umaarufu, usipokoma kwa onyo hili, tutakushughulikia, subiri mahakamani ukatoe ushahidi, usidanganywe..."

Dk Nyakarungu alisema mara baada ya kupokea ujumbe huo, alipiga simu katika namba hiyo na kupokewa na mwanamke aliyedai kuwa yuko Mwanza ambaye hakutaka kujitambulisha. Alidai kwamba mara baada ya kukata simu hiyo, alipokea ujumbe mwingine uliosema:

"Hata ukitutambua utafanya nini, narudia mara ya mwisho, hizo ripoti haziwahusu wanahabari, funga domo lako."Dk Nyakarungu alisema kwamba ametoa taarifa juu ya matukio hayo katika Kituo cha Polisi, Oystebay, Dar es Salaam na kufunguliwa jalada namba OB/RB/9214/11.

Hata hivyo, alisema licha ya vitisho hivyo hataogopa kwa kuwa alitumwa na familia na amelazimika kuwapa taarifa zote zilizojitokeza.Alisema inaelekea kuwa aliyetuma ujumbe huo amekuwa akimfuatilia kwa kuwa ametuma ujumbe huo katika namba zake mbili tofauti za simu.

Namshangaa sana huyo aliye mtumia Dr. ujumbe wa kusema anatumiwa je yeye tutasemaje afadhali ya Dr alifika na kuchunguza miili yeye je sindio katuma ujumbe nanani hapo anatumiwa sasa Dr au aliyetuma ujumbe?

Mmmh hii njii hii...saa ya ukombozi ni ndefu sana!! I doubt kwamba there is hiden secret to be reviewed in these scandal!!
 
Wataalamu wa IT ninaomba mumpe msaada Dr Nyakurungu kuwajua wahusika wa namba iliyotuma sms kama vile mlivyotusaidia kumjua Rashid Shamte na uhusika wake wa kutuma sms za udini na ubaguzi wa kikabila wakati kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010.
 
Daktari Grayson Nyakarungu wa Mwanza aliyesimamia uchunguzi wa miili ya watu wanne kati ya watano waliouawa na Polisi Mei 16, mwaka huu akiziwakilisha familia za wafiwa amedai kwamba ametumiwa ujumbe wa maandishi kwa simu kwamba atauawa.

Amedai kupokea ujumbe wa simu mara mbili kwa nyakati tofauti Mei 26, mwaka huu akiwa safarini kuelekea Dar es Salaam uliojaa vitisho.

Moja wa ujumbe huo unaosomeka, “Hizo ripoti siyo za kisiasa, acha kujiingiza kichwa kichwa utajutia, Tundu Lissu ndiye anakutumia ili yeye apate umaarufu, usipokoma kwa onyo hili, tutakushughulikia, subiri mahakamani ukatoe ushahidi, usidanganywe...”

Dk Nyakarungu alisema mara baada ya kupokea ujumbe huo, alipiga simu katika namba hiyo na kupokewa na mwanamke aliyedai kuwa yuko Mwanza ambaye hakutaka kujitambulisha. Alidai kwamba mara baada ya kukata simu hiyo, alipokea ujumbe mwingine uliosema:

“Hata ukitutambua utafanya nini, narudia mara ya mwisho, hizo ripoti haziwahusu wanahabari, funga domo lako.” Dk Nyakarungu alisema kwamba ametoa taarifa juu ya matukio hayo katika Kituo cha Polisi, Oystebay, Dar es Salaam na kufunguliwa jalada namba OB/RB/9214/11.

Hata hivyo, alisema licha ya vitisho hivyo hataogopa kwa kuwa alitumwa na familia na amelazimika kuwapa taarifa zote zilizojitokeza. Alisema inaelekea kuwa aliyetuma ujumbe huo amekuwa akimfuatilia kwa kuwa ametuma ujumbe huo katika namba zake mbili tofauti za simu.

Mwananchi.
Ina maana Polisi yetu haina ubavu wa kushughulikia watoa vitisho hao?????????? Kitengo cha IT si ni rahisi kuwafahamu na kuwabana, au ni wana maghamba wanatumia watu wao???? Nchi hii ipo hatarini kama ni hivyo, lazima ukweli uwekwe wazi na haki ipatikane, vinginevyo wananchi wanazidi kupandishiwa hasira!!!!!!!!!!
 
Una hakika kwamba vitisho hivyo havitoki kwa Polisi?
 
Ule usajili wa simu tulioelekezwa kusajili tuliambiwa ni kwa ajili ya shughuli za usalama. Sasa shughuli yenyewe ndio hiyo.
 
naomba aweke namba hizo kwenye hapa au kwenye pm yang na baada ya robo saa tutawajua ni kina nani hao......wanamtishia
 
ni-PM na kunipa hizo namba,in an hour nitakuwa nimeshakutajia mmiliki wa hiyo line. Alternatively weka public hiyo namba ukiona Polisi ndani ya wiki moja hawajakupa jibu la kueleweka!!
 
nyakarungu umebeba kazi ngumu na nzito, baada ya bavicha tu, kuna lingine tena, chadema msaidieni utulivu wa kisaikologia grayson.
 
Amtumie Ela kupitia huduma za Pesa Mtandao atapata majina yao.

Dr. Kasema aliipiga hiyo namba na ikapokelewa na mama to that case and if only if thy're smart enough for investigation mpaka hapa laziama jina hilo wanalo au wanayao hayo majina

Hivyo ni vitisho tu! wameanza kuogopa kivuli chao, mwisho wa yote siko zinakuja watafungwa tu.
 
Mauaji Tarime: Daktari atishiwa kuuawa Monday, 30 May 2011 21:17

Anthony Mayunga, Tarime

DAKTARI aliyesimamia uchunguzi wa miili ya watu wanne kati ya watano waliouawa na Polisi Mei 16, mwaka huu akiziwakilisha familia za wafiwa amedai kwamba ametumiwa ujumbe wa maandishi kwa simu kwamba atauawa.

Daktari huyo, Grayson Nyakarungu wa Mwanza alisimamia uchunguzi wa miili ya Chacha Ngoka, Emmanuel Magige, Bhoke Chawali na Mwikwabe Mwita katyika uchunguzi uliofanyika Mei 23, mwaka huu.

Alisema kwamba alipokea ujumbe wa simu mara mbili kwa nyakati tofauti Mei 26, mwaka huu akiwa safarini kuelekea Dar es Salaam uliojaa vitisho.

Alidai kwamba moja wa ujumbe huo unaosomeka, “Hizo ripoti siyo za kisiasa, acha kujiingiza kichwa kichwa utajutia, Tundu Lissu ndiye anakutumia ili yeye apate umaarufu, usipokoma kwa onyo hili, tutakushughulikia, subiri mahakamani ukatoe ushahidi, usidanganywe...”

Dk Nyakarungu alisema mara baada ya kupokea ujumbe huo, alipiga simu katika namba hiyo na kupokewa na mwanamke aliyedai kuwa yuko Mwanza ambaye hakutaka kujitambulisha. Alidai kwamba mara baada ya kukata simu hiyo, alipokea ujumbe mwingine uliosema:

“Hata ukitutambua utafanya nini, narudia mara ya mwisho, hizo ripoti haziwahusu wanahabari, funga domo lako.”Dk Nyakarungu alisema kwamba ametoa taarifa juu ya matukio hayo katika Kituo cha Polisi, Oystebay, Dar es Salaam na kufunguliwa jalada namba OB/RB/9214/11.

Hata hivyo, alisema licha ya vitisho hivyo hataogopa kwa kuwa alitumwa na familia na amelazimika kuwapa taarifa zote zilizojitokeza.Alisema inaelekea kuwa aliyetuma ujumbe huo amekuwa akimfuatilia kwa kuwa ametuma ujumbe huo katika namba zake mbili tofauti za simu.
 
Ndugu zangu,
Kuna faida gani kuishi miaka mingi iwapo hutatimiza malengo na ndoto yako?
Kuna hasara gani kuishi muda ulioishi iwapo utakufa kwa haki?
Na waishi milele watakao kuishi kwa dhambi, na furaha ya miili yao itageuka tindikali na nyongo kwao na vizazi vyao hata siku watapokufa.
Dr atambue kuwa WAOGA HUFA MARA NYINGI SANA KABLA YA SIKU YAO YA KIFO! ASIOGOPE.
 
Back
Top Bottom