Matumizi yasiyo Sahihi ya herufi ''L'' na ''R'' mitandaoni yananikera

nchi ya jirani, hatuna nne tuna ine, hao migration wa Tz hawadai pass, wao humtaka mtu ahesabu mpaka tano tu,? 1, 2,3,ine ..5 ;;
Afande pakia hili...
 
Sio mtandaoni tu...watangazaji wa radio na TV ...ilitakiwa moja ya kigezo cha kuwa mtangazaji ni kuweza kutamka harufi hizi ipasavyo
Wengine waimbaji wetu...unsmkuta muimbaji nae hata kutamka hizi harufi nad hajui basi npanapiga kelele tu na vinanda
 
Mimi nimejikuta nasahau herufi sahihi kwa baadhi ya maneno kutokana na watu wengi kukosea kosea
 
Yatakukera zaidi kwenye vibao vya anwani za makazi
 
Unakuta mtu badala aandike neno kwa usahihi analiandika katika matumizi ya herufi ambayo siyo na huku ni kuzuoesha wengine matamshi ambayo mwisho wa siku yatazidi kuharibu lugha ya kiswahili.

Mfano mtu anaandika neno ''kelo'' badala ya kero
''habali'' badala ya habari
''badara'' badala ya badala
''hasila'' badala ya hasira

Tujifunze matumizi sahihi ya herufi ndugu zangu, mazoea ni kilema. Hadi kwenye magazeti waliozoea kukosea matamshi haya huandika kwa kukosea pia.

Ahsanteni.
Sasa hawa watangazaji wa redio za mtaani ndio wanakera zaidi. Utasikia: "ulefu wa balabala....." Hahahahaja......ovyo.,.,
 
Tatizo nyinyi watoto wa ki dar es saraama mnajifanya mnajuwa sana kufanya critic, mmesaau kuwa watu utofautihana ufaamu na mda mwengine ni makaso ya kibinadamu na wengine kiswahili sio lugha yao.
Duh! Hiki Kiswahili chako!
Halafu tunajinasibu kuwa tujifunze kwa lugha ya Kiswahili hadi chuo kikuu!
Hao waalimu itabidi watoke Kenya au China!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom