Matumizi yasiyo Sahihi ya herufi ''L'' na ''R'' mitandaoni yananikera

Na mbaya zaid na huwa inanipa picha ya mwandishi jinsi alivyo kabisa ni pale badala ya kutumia neno ''SASA'' anatumia neno ''xaxa'' inakera mno..
 
Unakuta mtu badala aandike neno kwa usahihi analiandika katika matumizi ya herufi ambayo siyo na huku ni kuzuoesha wengine matamshi ambayo mwisho wa siku yatazidi kuharibu lugha ya kiswahili.

Mfano mtu anaandika neno ''kelo'' badala ya kero
''habali'' badala ya habari
''badara'' badala ya badala
''hasila'' badala ya hasira

Tujifunze matumizi sahihi ya herufi ndugu zangu, mazoea ni kilema. Hadi kwenye magazeti waliozoea kukosea matamshi haya huandika kwa kukosea pia.

Ahsanteni.
" Mfano mtu anaandika neno ''kelo'' badala ya kero
''habali'' badala ya habari
''badara'' badala ya badala
''hasila'' badala ya hasira"

Hii ni sendesi mmoja? Jifunzishage kuwekaga koma na nukta!
 
" Mfano mtu anaandika neno ''kelo'' badala ya kero
''habali'' badala ya habari
''badara'' badala ya badala
''hasila'' badala ya hasira"

Hii ni sendesi mmoja? Jifunzishage kuwekaga koma na nukta!
duh! This might be a wrong forum.
 
Tatizo nyinyi watoto wa ki dar es saraama mnajifanya mnajuwa sana kufanya critic, mmesaau kuwa watu utofautihana ufaamu na mda mwengine ni makaso ya kibinadamu na wengine kiswahili sio lugha yao.
Umekosea pia wakati sasahivi umetoka kurekebishwa...utofautiana=hutofautiana.
 
jamani mie nisaidieni huyu fundi samani (kapenta) herufi zake huandikwaje kwa usahihi: SEREMARA au SELEMARA au SEREMALA au SELEMALA?.hapa huwa nachemka kwelikweli.
 
sio wanaoandika tu kaa kwenye FM Radio zetu ndio utatapika,hizi fm za wilaya ndio balaa ,sijui hakuna usaili wa kabla,
maana unakuta mtu yuko chuo lakini akiandika hapa au akiongea ni mtihani
 
Ata mi wananikela sana wanatia hasila sana awa na hii ni asala kubwa
 
Labda mtoa maada yanakela nini, ivi ukikuta sms kwenyesimu yako imeandikwa "Umepokea SHIRINGI 1'000'000 utakuwa bado hujahelewa.
Watu kama nyie ndiyo hamtaki kujifunza. Ndicho tunacholalamikia matumizi mabaya ya herufi "l" na "r".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom