Matukio yaliyotawala vyombo vya habari katika kipindi cha miaka 50 ya Tanganyika

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,316
10,782
Salaam wakuu!

Katika kipindi chote cha kuzaliwa hadi sasa inapotimiza miaka 50, Tanganyika imekua ikipatwa na habari ambazo zinatawala kurasa za mbele za vyombo vya habari (hususani magazeti na radio).

Sasa katika kutafakari miaka 50 ya Tanganyika, nimeona ni vyema tukatakafari kwa kufahamishana na kukumbushana habari 50 za kisiasa ambazo zimetawala magazeti, radio na sasa televisheni katika kipindi chote cha miaka 50.

Mimi naanza kwa habari hizi: (mpangilio haumaanishi umuhimu/uzito wa habari husika; bali ni mpangilio mchanganyiko)

1. Kifo cha Edward Moringe Sokoine mwaka
2. Kesi dhidi ya akina Chipaka juu ya jaribio pili la kuipindua serikali ya Tanganyika.
3. Utekelezaji wa sera ya ujamaa; hususani villagilization
4. Mpango wa kwanza wa maendeleo wa Tanganyika (1961-1964)
5. Vifo vya Kolimba, Malima, Kambona na Kombe
6. Jaribio la kwanza la kuipindua serikali ya Tanganyika
7. Tofauti za kiidiolojia kati ya Mwalimu Nyerere na Kambona hadi mwisho wa maisha yao
8. Kujiuzulu kwa Edward Lowassa kutokana na kashfa ya Richmond
9. Kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa
10. Kung'atuka kwa Mwalimu kama rais wa Tanzania
11. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
12. Ofisa wa idara ya usalama wa taifa kujitokeza hadharani kwa mara ya kwanza kujibu tuhuma juu ya uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka 2010.
13. Kifo cha Mwalimu Nyerere
14. Ushindi wa mashaka wa rais Kikwete katika uchaguzi wa mwaka 2010; kususia kwa sherehe za uhapishwaji wake kulikofanywa na aliyekuwa mgombea wa urais kupitia kwa tiketi ya CHADEMA
15. Suala la Mwalimu kuwakataa waziwazi Kikwete na Lowassa kama wagombea urais wa Tanzania
16. Kugundulika kwa uwepo wa mabaki ya zamani kabisa ya binadamu wa kale (hii ilikua na some political implications)
17. Mlipuko wa mabomu katika ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam
18. Kujiuzulu kwa waziri Ali Hassan Mwinyi (akiwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi)
19. Uvamizi wa Nduli Idd Amin, vita kati ya Tanzania na Uganda na ushindi wa vita hivyo
20. Vifo vya watu 35 na majeruhi 600 kule Pemba kutokana na machafuko ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000
21. Wilbrord Slaa mgombea urais kwa mwaka 2010 kupitia CHADEMA
22. Skendo ya rais Mkapa na mkewe kuwa na kampuni binafsi yenye ofisi pale Ikulu
23. Kujificha kwa Mwalimu Nyerere na Kawawa kule Kigamboni katika kukwepa jaribio la kupinduliwa
24. Kusomwa kwa ripoti ya Kamati Teule ya Mwakyembe
25. Hotuba ya Mwalimu Nyerere pale Mbeya katika siku ya wafanyakazi
26. Tanzania kuwa kituo cha wapigania uhuru na ukombozi wa mataifa kusini mwa Afrika
27. Kuchaguliwa kwa Anna Makinda kuwa spika wa kwanza mwanamke wa bunge la JMT
28. Kuungana kwa TANU na ASP; kuzaliwa kwa CCM
29. Hotuba ya rais Kikwete kwa wazee wa Dar es Salaam pale Diamond Jubilee Hall (ya kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010)
30. Wabunge wa CHADEMA kuwalk out bungeni wakati wa hotuba ya rais Kikwete katika ufunguzi wa bunge Disemba, 2010
31. Mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2011-2016
32. Kupingwa kwa muswada wa matayarisho ya kutengenezwa kwa katiba ya kwanza ya wananchi kuanzia bara hadi visiwani
33. Sakata la Jairo na uundwaji wa kamati teule ya bunge
34. Kuruhusiwa kwa usafirishaji wa abiria/umma kwa kutumia vyombo vya usafiri vya binafsi (kuanza kutumika kwa daladala)
35. Ajali za meli ya M.V Bukoba, Spice Islander; ya basi ya Air Msae; na ya treni Dodoma.
36. Utoroshwaji wa wanyamapori walio hai mchana kweupe ndani ya ardhi ya Tanzania
37. Kurudi kwa Kambona kutoka uhamishoni; na kuchafuliwa kwa tuhuma za kwamba yeye si mtanzania.
38. Ujio wa Papa John Paulo II
39. Maadui watatu wa watanganyika baada ya kupata uhuru; ujinga, malazi na umaskini
40. Kufanikiwa kwa Kambona kuwatuliza wanajeshi wa Tanzania waliokua wana nia ya kuipindua serikali ya Mwalimu
41. Matamashi ya David Cameroon juu ya misaada kwa nchi zinazotegemea misaada kutoka Uingereza
42. Kusomwa kwa List of Shame (ya mafisadi) iliyotolewa na CHADEMA pale Mwembeyanga, Dar es Salaam
43. Skendo ya ufukiaji wa raia kule Bulyankhulu
44. Madai ya utengenezaji wa katiba mpya toka enzi za kamati ya wanamageuzi hadi muswada kuwa mikononi mwa rais Kikwete
45. Mpango wa kupunguza matumizi ya serikali na utekelezaji wa sera za uwekezaji na ubinafshaji wa mashirika ya umma
46. Augustine Mrema mgombea wa urais kwa mwaka 1995 kupitia NCCR-Mageuzi
47. Kufeli na mwisho wa sera ya ujamaa; azimio la Zanzibar
49. Kashfa ya sukari na kujiuzulu kwa waziri Idd Simba
50. Kuundwa kwa Azimio la Arusha na miiko ya viongozi

Wakuu hayo ndio matukio ambayo naona yameweza kutawala vichwa vya habari katika vyombo mbalimbali vya habari katika kipindi hiki cha miaka 50 ya Tanganyika.

Je, wewe una matukio gani ambayo unadhani yanastahili kuwepo katika matukio 50 yaliyotawala vyombo vya habari vya Tanganyika?
 
Aden rage kupanda jukwaani na kuhutubia watu na bastola kiunoni live watu wakiona,matumizi ya uhesabuji wa kura kwa kompyuta mwaka 2010,Rostam azizi kujiivua gamba,chama cha cuf kufunga ndoa na ccm zanzibar,mkuu wa mkoa kuuwawa kwa bunduki na mwananchi mh kleruu wa Iringa na mkuu wa mkoa tabora ukiwaona ditopile kumuua mwananchi kwa bunduki barabarani mbele ya umati wa watu,babu seya na familia yake kupelekwa ukonga kwa chuki za kuiba demu wa mtu!daaah na nyingineee kibaooo nikikumbuka ntazimwaga
 
Aden rage kupanda jukwaani na kuhutubia watu na bastola kiunoni live watu wakiona,matumizi ya uhesabuji wa kura kwa kompyuta mwaka 2010,Rostam azizi kujiivua gamba,chama cha cuf kufunga ndoa na ccm zanzibar,mkuu wa mkoa kuuwawa kwa bunduki na mwananchi mh kleruu wa Iringa na mkuu wa mkoa tabora ukiwaona ditopile kumuua mwananchi kwa bunduki barabarani mbele ya umati wa watu,babu seya na familia yake kupelekwa ukonga kwa chuki za kuiba demu wa mtu!daaah na nyingineee kibaooo nikikumbuka ntazimwaga

Pangalia basi mkuu ili iwe rahisi kusomeka!!
 
Kondoo mwenye maneno matakatifu ubavuni
kondoo.jpg
 
Back
Top Bottom