Matokeo ya Uchaguzi Uzini - Raza (CCM) aibuka kidedea!

Hivi mpinzani wa CDM ni CUF?
Nilifikiri strategy ya CDM ni kuitoa CCM madarakani, but nashangaa now wanashindana na CUF.
Hamuoni CCM inavyozidi kuchanja mbuga.

Hongera sana CCM...imani ya watanzania na mioyo ya watanzania ipo kwa CCM pekee!

mpinzani wa CDM ni CCM
mpinzani wa ccm ni cdm
mpinzani wa cuf ni cdm

Amini usiamini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa kweli watanzania wado hawajifunzi kutokana na makosa yao. Sijui kitokee nini ndio watakuja kujutia maamuzi yao, yaan mtu unapata nafasi ya kujirekebisha bado unarudia makosa tena! Mimi nadhani haya yote yanayotokea sasa haina haja ya kuilaumu serikali tena bali wananchi walioiweka hiyo serikali madarakani.

Jay Z aliwahi kusema "men lie, women lie, numbers dont". Kwa uwiano huo, utagundua Watanzania wengi bado wana walakini katika ufanyaji wa maamuzi sahihi. Binafsi sikutegemea CDM ishinde kirahisi huko Uzini but nilitegemea wanauzini wangetuma ujumbe mzito sana kwenye Ballot Box jumapili hii. Sasa kwa matokeo haya tegemeeni mkiwaona CCM na Serikali yake wakizidi kubweteka na kusherekea ushindi, wakati wananchi wanazidi kutaabika.

Uamuzi huo haujaikomoa CDM, bali tunajikomoa wananchi wenyewe

Mkuu hili jambo ndio linatuangusha hapa kwetu, sijui watu wapate shida kiasi gani ndio wajue kunahitajika mabadiliko. Hivi kwa kipindi toka uhuru nchi hii inaongozwa na chama hicho hicho na hakuna mabadiliko kwa raia lakini hao hao bado wanairudisha madarakani serekali hiyo hiyo.
 
kumbe tanzania tunaelekea kuendelea,kura za udiwani zinaweza kutngazwa kwa siku moja tujitahidi hata kwa ubunge tunaweza kuta ngaza kwa siku mbili.

nawatakia siku njema.
 
Pro-Chadema JF bana sasa mmeamua kujifariji kwa kuishambulia Cuf baada ya kuangukia pua Uzini.
 
Mungi.....Kwa matokeo haya naweza kusema CHADEMA wameteleza kidogo maana katika uchaguzi mkuu uliopita katika jimbo la Uzini CHADEMA pia walishika nafasi ya pili(kwa ubunge na uwakilishi),na walipata kura nyingi zaidi ya hizi walizopata safari hii........

So tusipotoshe hapa kusema kwamba CHADEMA wameibuka kutoka 0 hadi namba 2..........

Hongera kwa CCM,hongera kwa Razza...CHADEMA wajipange sasa kwa ajili ya 2015 badala ya kutegemea hizi by-elections kujijenga,na ni vema hata katika mikutano yao(mfano operesheni Sangara n.k) wawe wanaiweka na Zanzibar katika Ratiba

ni kweli ukiangalia uchaguzi uliopita mbunge wa CDM alipata 7.6% almost 8% na pia wa uwakilishi alipata kura nyingi zaidi ya hizi hivyo matokeo ya sasa yanaonyesha kuporomoka kwa siasa za upinzani, imagine 4%. hivyo badala ya kupongezana (kudanganyana) ni vyema kusahihishana makosa na kuangalia mbele. ukumbuke kuwa kulikuwa na ujumbe mzito sana wa CDM kule Uzini.
 
Mkuu hili jambo ndio linatuangusha hapa kwetu, sijui watu wapate shida kiasi gani ndio wajue kunahitajika mabadiliko. Hivi kwa kipindi toka uhuru nchi hii inaongozwa na chama hicho hicho na hakuna mabadiliko kwa raia lakini hao hao bado wanairudisha madarakani serekali hiyo hiyo.

Mkuu inategemea unavyotafsiri (au kuidefine) shida. Kila mtu ana namna yake ya tafsiri hiyo. Wewe unaweza kusema unashida lakini wengine katika mazingira hayo hayo wanafutahia maisha. Ukienda vijijiniutakutana na wazee wanalia shida lakini ukiwapa pesa wanaenda kwenye klabu yapombe na wakishakunywa watakwambia maisha mazuri sana.
 
Hizi story nilianza kuzisikia Segerea, ikaja Kibaha, halafu Shinyanga, mara Igunga (the list goes on). Tell me, CDM inafanya nini kuhusiana na hizi rafu? Nasi tunafanya nini ili zisijirudie?

Mkuu nimekua nikiuliza na kujiuliza hili swali siku zote.
CHA.DE.MA. kama kinaona mchezo hauko fair,kwanini kiingie uwanjani? Hii inaonyesha ukosefu wa dhamira ya kweli.

Maana malalamiko kama hayo yamekua yakisikika kila mara,na sijaona chama kimefanya jitahada zipi za dhati katika kukabiliana na hali hiyo.

Cha ajabu,hata chaguzi ndogo ya Arumeru,mazingira ya mchezo bado ni yale yale,lakini utasikia chama kinaingia uwanjani. Halafu baada ya mchezo,kinaanza kulalama foul plays zilizokuwepo!

CHA.DE.MA. kinapaswa kuanza kuwa na dhamira ya kweli na dhati katika kuonyesha hakikubaliani na mchezo husio huru na wa haki.
La sivyo,kelele kinazopiga kupitia malalamiko ya kila mara,ndio yanakipa kiburi C.C.M. cha kuendelea foul plays katika mchezo.
 
Tusubiri Arumeru...Tunakuja Arusha kuchukua kilicho chetu.
CCM ni kila kitu!!

Mkuu Rejao habari za uchakachuaji ha,haaaa naona CDM wanajifaraji badala ya kujiuliza include all team campiagner walikwenda kufanya nini Uzini? haya bana nasubiria Arumeru nimeshachoka na ngojera zao hapa JF
 
kwa matokeo haya,inaonyesha kuwa ccm ndio chama kinachokubalika katika siasa za tanzania
 
Mkuu Rejao habari za uchakachuaji ha,haaaa naona CDM wanajifaraji badala ya kujiuliza include all team campiagner walikwenda kufanya nini Uzini? haya bana nasubiria Arumeru nimeshachoka na ngojera zao hapa JF

Exactly.
Uwa najiuliza,ni kipi kinachokifanya CHA.DE.MA. kishindwe kusema kinasusia chaguzi zote mpaka pale,malalamiko na madai ya mchezo kutokua huru na wa haki,yatakapofanyiwa kazi?
 
Chadema inabidi wajitafakur kama watakuwa chama makini na viongozi makini.

Wasitafute mchawi kwa kushindwa kwao. Mchawi ni kauli zao Bungeni na nje ya bunge kuhusu Znz na waZnz. Vile vile walitakiwa wasome alama za nyakati kuhusu siasa za Znz.

Lakin la mwisho viongozi wawe na huruma na pesa za posho walizo zoa kule Uzini. Kwani walijua kabisa wanashindwa bali waliongopa kuwa wana nafasi kubwa ya kushukua jimbo hilo.

nafikiri sasa ni wakti wa kuwachukulia hatua kali viongozi walioweka kami Uzini na kuzoa posho bila kusema ukweli kuwa hakuna uwezekano wa kushinda. Chini ya 5% ni aibu kubwa sana ka Chadme na watendaji wakuu waliweka kambi huko.
 
Mkuu inategemea unavyotafsiri (au kuidefine) shida. Kila mtu ana namna yake ya tafsiri hiyo. Wewe unaweza kusema unashida lakini wengine katika mazingira hayo hayo wanafutahia maisha. Ukienda vijijiniutakutana na wazee wanalia shida lakini ukiwapa pesa wanaenda kwenye klabu yapombe na wakishakunywa watakwambia maisha mazuri sana.

Kumbe ni hivyo? Kweli Chadema ndani ya JF inapendwa mno, hadi inasikitisha
 
[h=3]CCM YASHINDA UZINI[/h]

Chama cha Mapinduzi5377
Chama cha Demokrasia na maendeleo281
Chama cha Wananchi223
TADEA14
FFP8
Kura zilizopigwa5902
Kura zilizoharibika28

Wasiopiga kura
2852
 
Chadema inabidi wajitafakur kama watakuwa chama makini na viongozi makini.

Wasitafute mchawi kwa kushindwa kwao. Mchawi ni kauli zao Bungeni na nje ya bunge kuhusu Znz na waZnz. Vile vile walitakiwa wasome alama za nyakati kuhusu siasa za Znz.

Lakin la mwisho viongozi wawe na huruma na pesa za posho walizo zoa kule Uzini. Kwani walijua kabisa wanashindwa bali waliongopa kuwa wana nafasi kubwa ya kushukua jimbo hilo.

nafikiri sasa ni wakti wa kuwachukulia hatua kali viongozi walioweka kami Uzini na kuzoa posho bila kusema ukweli kuwa hakuna uwezekano wa kushinda. Chini ya 5% ni aibu kubwa sana ka Chadme na watendaji wakuu waliweka kambi huko.

Mkuu kwenye posho hapo za campaign nakupinga kabisa ni lazma waende ili kugombania kiti sio kuacha, swala ni walijifunza Igunga hata hivyo takwimu za Igunga zinardhisha sana sana na mategemeo ya wengi kama kulikua na mbinu chafu wangezisawazisha kabla ya kwenda Uzini sasa na uzini wameshindwa kumbuka hapa tunajadili takwimu walizozipata na sio ushindi hizi takwimu azilingani na propaganda walizokuwa wanazimwaga hapa JF

Swala la kujiuliza ni nini kimetokea?
Team yote ya Campaign ilikua inafanya kazi gani uko?
Je kuna ombwe la kurekebisha hiyo team ili yasitokee yaliyowatokea?
4%? jamani ni aibu hapo akuna kutetea
Kuna chaguzi nyingine kule Arumeru je itakuwaje?
Fikiria na hapa wanatakiwa watoe majibu mazito na sio mepesi mepesi hizi ni chaguzi ndogo za jimbo moja moja na all team ya CDM imeshiriki include top leaders na ikawa ivi je ikija chaguzi za tz nzima na mgombea anatakiwa kujipima nguvu mwenyewe itakuje?

Haya ni maoni tuu nategemea CDM watakuja na jibu sahihi nawakilisha.
 
Swadakta.

Hayo ndio makusudio yangu.

Kwani wanahitaji viongozi wenye uzoefu sana katika chaguzi na uongozi. nafikiri katika top ten ya Chadema katika uongozi wao sioni mwenye uzoefu wa kutosha katika uongozi wa Kiserikali hata kisiasa. Wote wanajifunza humo humo.

kazi ipo.

Tusubiri majibu yao
 
Stay tuned nitawamwagia full data muda si mrefu.

Kwa CDM hii ni hasara kubwa sana, wametumia zaidi ya Tshs 167 million wamkwenda kuambulia kura hizo. Ambapo kwa hesabu za haraka haraka kwamba kwa kila aliyepiga kura gharama yake ni Tshs 590,000. Hii ni biashara kichaa CDM wamepata, ni watu wakuonea huruma sana
 
Back
Top Bottom