Matokeo ya Uchaguzi Uzini - Raza (CCM) aibuka kidedea!

Nadhani CUF wameibiwa kura ila hawawezi kulalamika kutokana na makubaliano ya mwafaka.Haiwezekani CHADEMA wawashinde CUF huko visiwani, labda kama hali ya hewa imewaharibikia sana ndugu zangu wa CUF; jambo linaloweza kuwa limeisadia sana CCM
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, kweli kichuguu ni nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila kwaruzo
 
Wauzini wamelala wameamua kuchagua pumba tuwaache waendelee kula pumba.
 
Raza hajashinda kafanya mauaji. Chadema msijipe moyo hapo hapo CUF wengi wamempigia kura Raza. Msikate tamaa.
 
Gerald,
JF ni jukwaa huru wapo vyama tofauti tofauti sio Chadema peke yenu tatizo la Pro-Chadema mnadhani wazalendo wa nchi lazima wawe Chadema..

Suala la data mbona hata mie uwa nawaletea data za Chadema humu JF mnanipinga baadae mnakubali kimya kimya.

JF imepoteza kichwa muhimu FaizaFoxy kapigwa ban ya maisha kukokosekana kwake hata nyie ni pigo kubwa mnakosa data muhimu.

Mkuu:

Nakupinga vikali hapo kwenye red. Mzalendo wa nchi hii hawezi kamwe kukumbatia chama kinachosimamia wizi, ufisadi, kulindana, kunyima haki za wafanyakazi wake etc. 'Mzalendo' wa aina hiyo unayemaananisha ni yule ambaye bado kajifunika blanketi nene la CCM.

Kazi kubwa ya CDM ni kujaribu kuliondoa blanketi hilo ingawa watu kama nyinyi mnaeona giza ni mwanga ndiyo mnajaribu kukwamisha jitihada hizo.
 
kweli tuko too far ....sasa hivi mjinga mjinga yoyote akinipiga mzinga namtosa live hawa watu wa chini hawa hawajui kitu wanateseka maisha magumu ila wakipewa t shirt au kofia wanaipa ccm ulaji. now i will not give a damn

Wakuu huyu Raza aliyeshinda ni yupi? Zanzibar kuna kina Raza wengi na kuna mmoja ni mfanyabiashara maarufi wa dawa za kulevya, ingekuwa vizuri kama huyu Raza akifahamishwa zaidi ya ushindi wake tu.
 
Wauzini wamelala wameamua kuchagua pumba tuwaache waendelee kula pumba.

Na kweli pumba wataendelea kuzila chini ya huyu Raza ambaye anaingia Barazani kusimamia masilahi yake tu. Kwani kabadilika tangu 'nanihii' wake aondoke madarakani mwaka 2000?
 
Mkuu najua azipo fair ila asilimia 4.8%? inasikitisha sana sana tuu usitetee kitu hapo ni failure mbaya sana believe or not

Hilo ni pigo kubwa sana, inaonesha ni baadhi tu ya ukoo wa candidate wa chadema ndio waliompigia kura. Sidhani kama yupo ambae si ukoo wake.

Siasa za Zanzibar ni ngumu sana kwa chama kama chadema.
 

Na kweli pumba wataendelea kuzila chini ya huyu Raza ambaye anaingia Barazani kusimamia masilahi yake tu. Kwani kabadilika tangu 'nanihii' wake aondoke madarakani mwaka 2000?


Fafanua, mbona unaongea kama unarusha roho.
 
Nadhani CUF wameibiwa kura ila hawawezi kulalamika kutokana na makubaliano ya mwafaka.Haiwezekani CHADEMA wawashinde CUF huko visiwani, labda kama hali ya hewa imewaharibikia sana ndugu zangu wa CUF; jambo linaloweza kuwa limeisadia sana CCM

CUF hawajaibiwa kura, Uzini ni jimbo la CCM, siasa za visiwani kama huzijui ni ngumu sana, halafu usisahau kuwa wengi wa CUF wamempigia Mheshimiwa Raza.
 
Wanabodi tujipongeze kwa nafasi tuliyopata kwa siasa za ZNZ zilivyo pamoja na uwezo wa kipesa na umaarufu wa mgombea wa ccm tumepata zaidi ya tulichostahili.
 
Ushindi wa Raza kwa asilimia zaidi ya tisini ni kutokana na msimamo wake mkali kuhusu haki za Zanzibar ndani ya muungano. Team imekamilika, Jussa na Raza expect fireworks mambo ya muungano, Keep in touch.
 
wanabodi tujipongeze kwa nafasi tuliyopata kwa siasa za znz zilivyo pamoja na uwezo wa kipesa na umaarufu wa mgombea wa ccm tumepata zaidi ya tulichostahili.

mlistahili ngapi?....lol!
 
Hivi mpinzani wa CDM ni CUF?
Nilifikiri strategy ya CDM ni kuitoa CCM madarakani, but nashangaa now wanashindana na CUF.
Hamuoni CCM inavyozidi kuchanja mbuga.

Hongera sana CCM...imani ya watanzania na mioyo ya watanzania ipo kwa CCM pekee!
 
kweli tuko too far ....sasa hivi mjinga mjinga yoyote akinipiga mzinga namtosa live hawa watu wa chini hawa hawajui kitu wanateseka maisha magumu ila wakipewa t shirt au kofia wanaipa ccm ulaji. now i will not give a damn

wakinyonywa vya kutosha watakumbuka na kuchagua mabadiliko
 
Kutoka 0 hadi namba mbili si mchezo.
Mungi.....Kwa matokeo haya naweza kusema CHADEMA wameteleza kidogo maana katika uchaguzi mkuu uliopita katika jimbo la Uzini CHADEMA pia walishika nafasi ya pili(kwa ubunge na uwakilishi),na walipata kura nyingi zaidi ya hizi walizopata safari hii........

So tusipotoshe hapa kusema kwamba CHADEMA wameibuka kutoka 0 hadi namba 2..........

Hongera kwa CCM,hongera kwa Razza...CHADEMA wajipange sasa kwa ajili ya 2015 badala ya kutegemea hizi by-elections kujijenga,na ni vema hata katika mikutano yao(mfano operesheni Sangara n.k) wawe wanaiweka na Zanzibar katika Ratiba
 
Zanzibar ya leo watu wanazaliwa na mambo makuu mawili:
-DINI yao;
-vyama vyao vya SIASA.
Kura zile alizopata mgombea wa CHADEMA ni za wanaCCM. CUF jimbo lile haipo kabisa kama ambavyo CCM haipo majimbo ya Pemba.
 
Back
Top Bottom