Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

Kuna watu wajanja duniani lakini hapa Maalim Seif safari hii kuudanganya umma wa waTanzania kuwa anaitambua serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Ni kichekesho cha karne.Sijui kama CCM imeelewa maana yake?Je Kikwete anajua shabaha hiyo inalenga wapi?Muafaka na mafanikio yake nini??Je kero za Muungano zimejibiwa kikamilifu? Utata wa serikali ya Zanzibar na kauli tata zake inakuwaje?Je nafasi ya Karume katika serikali ya Muungano iko sawa sawa ?Kwanini msifikirie jambo hili mapema zaidi ya miaka kumi iliyopita??Maalim Seif Hamad Sharif hafanyi makosa kila anapolenga jambo ana kusudi fulani,Hebu someni historia yake kwanza!!Hafanyi makosa huyu mtu jamani ana malengo yake tena ya muda mrefu sana.Leo hii ameiteka CCM VISIWANI NA WAMEMWAMINI ETI AMEITAMBUA SERIKALI YAO!!!Hii ni janja ya nyani mbona?Kwani chanzo na chokochoko za Zanzibar kuwa nchi HURU kilianzia wapi? Kwani hamkumbuki madai mbali mbali yaliyoelekezwa kuifanya Zanzibar kuwa Taifa linalojitegemea?Kuwa na wimbo wake,bendera yake,maamuzi yake,leo wanazungumza sarafu yake nk? Wana JF waelezeni watanzania hususani Kikwete kwamba shabaha ya Seif siyo hiyo!!!Wasichekelee!!!Waamke!
 
Kamatire, you are very right. Basically Seif na Karume wanakubaliana katika mambo ya Zanzibar ya kimsingi, kama vile vinavyohusu rasilimali za Zanzibar kwa ajili ya Zanzibar, Zanzibar ya Wazanzibar, kupungaza utegemezi wa Zanzaibar kwa bara, kuimarisha KMKM ili kuchukua nafasi endapo wataamua kwenda kivyao, n.k. Pia Karume anaondoka na anataka aondoke na kama CCM hawatamweka mtu anayekubalika Zanzibar kugombea basi yeye atampa shavu Seif. Zanzibar ina mambo jamani? Na mara zote wakitaka mapinduzi wanatumia mamluki hata ya 1964 hayakuongozwa na Karume na ndiyo maana si yeye wa kwanza kutangaza kuwa wamepindua serikali ya Kisultan bali yeye alitokea baadaye akawekwa kuwa rais, mambo ni mengi, historia ya Tanzania inatkiwa iandikwe upya na kwa usahihi mkubwa....
 
Kamatire, you are very right. Basically Seif na Karume wanakubaliana katika mambo ya Zanzibar ya kimsingi, kama vile vinavyohusu rasilimali za Zanzibar kwa ajili ya Zanzibar, Zanzibar ya Wazanzibar, kupungaza utegemezi wa Zanzaibar kwa bara, kuimarisha KMKM ili kuchukua nafasi endapo wataamua kwenda kivyao, n.k. Pia Karume anaondoka na anataka aondoke na kama CCM hawatamweka mtu anayekubalika Zanzibar kugombea basi yeye atampa shavu Seif. Zanzibar ina mambo jamani? Na mara zote wakitaka mapinduzi wanatumia mamluki hata ya 1964 hayakuongozwa na Karume na ndiyo maana si yeye wa kwanza kutangaza kuwa wamepindua serikali ya Kisultan bali yeye alitokea baadaye akawekwa kuwa rais, mambo ni mengi, historia ya Tanzania inatkiwa iandikwe upya na kwa usahihi mkubwa....

Ni dhahiri hatima ya Muungano iko mashakani,Hilo halina ubishi,Seif na Karume wana undugu hilo linajulikana.Hapa wazanzibar wasipoelewa hicho kitendawili wakakitegua wenyewe Wallahi nawaambia tena huko hakutatawalika kama ilivyo Somalia na kwingineko duniani!!
 
Nilishawahi sema mgogoro wa Zanzibar ulisababishwa na Maalim , na yeye analijua hivyo ndio maana alivyokubaliana tu na Abeid, akatangaza mgogoro umeisha...

"Narudia tena nilishawahi mfananisha huyu jamaa na Jonas Savimbi, ambaye alitulazimisha kuamini kwamba mgogoro ulikuwa wa chama chake na serikali, lakini alivyofariki ilichukua hardly 3 days, mgogoro ukaisha..""

Sasa Maalimu. furahia yote lakini kuna siku utaulizwa zile damu za watu wa Pemba.

Kwa hilu ndio utajua viongozi wetu wanatuona sisi mafala sana, yaani siku zote tunaambiwa mgogoro ni wa CUF na CCM, kumbe mgogoro ni wa Maalimu Seif na CCM...

Haya sasa tumewashitukia najua mnataka taifa lenu... kama ndivyo basi ombeni JK aendelee kuwa Rais maana yeye itakuwa rahisi kuwakubalia... lakini akija mjeuri kama alivyokuwa BWM, ole wenu.
 
Upinzani kati ya CAF na CCM Zanzibar unaelekea kufa kama bado upo ila kinachooneka kuzaliwa ni upinzani wa Zanzibar dhidi ya Tanzania bara na matunda ya huu upinzani ni kupatikana kwa Taifa lililo huru la Zanzibar na baada ya hapo ndipo U CAF na U CCM utarudi mahala pake.

Mkuu Mvina taratibu kidogo CAF haina upinzani wowote na CCM jitahid kutofautisha CUF na CAF though i like your comments
 
ukosefu wa kutojua chama ni watu na watu ndio wananguvu...kumemponza maalim seif kutoeleweka kwa wapiga kura wake....mwelekeo wake umeonekana si mzuri ndani ya wafuasi wake...sasa kajiweka pabaya kwa uchaguzi wa 2010 labda asigombee tena...waswahili wanasema hakuna marefu yasiyokuwa na nicha......sasa mwisho wa kusaminiwa umeisha...kibanda maiti hakuna atayeenda kumsikiliza tena....kapoteza mwelekeo....Anakazi ya kujisafisha.....
 
mojawapo ya mambo yaliyonishangaza nilipokua Zanzibar ni ukweli kwamba wana umoja wa kipekee ukilinganisha na bara...mtu atakwambia nikienda polisi kuna mjomba, jeshini kuna kaka, shamba kuna babu..n.k..na kiukweli wengi wamechoshwa na siasa za chuki, wanadai viongozi ndio wanaofaidi na wao wanaumia wakati kimsingi ni ndugu kabisa..jambo la msingi nililojifunza pale, muungano ni adui wao namba moja, wanawaita wabara wakoloni...wonderful enough, wanasema CUF na CCM ni walewale tu, hamna ambaye hajawahi kuwa upande wowote, especially wakikumbushia Maalim kama kada wa CCM na Waziri Kiongozi wa zamani...kwa hiyo basi, nachokiona hapa ni mkakatyi wa makusudi wa kuongez nguvu ya Zanzibar ktk muungano, with a view to separate at last(aisee).....CCM haijawahi kushinda Pemba na majimbo ya Unguja mjini...right now kuna mvutano wa nani atakuwa rais, na kumbukeni tofauti na Hayati Karume, marais wote waliofuatia wana mkono wa bara..hivyo basi, either Karume atampisha Seif mwakani, kuepusha pandikizi toka bara ambaye atatishia maslahi ya Zanzibar katika muungano, ama wanamkakati wa pamoja wa kumuweka mtu wanemuamini wote kwamba atakua na nguvu za kutikisa muungano...tuisubiri tuone....
 
Mkuu Zitto heshima mbele,

Hapo ndo tunasema hapa kuwa upinzani mlitakiwa kuseize hii opportunity na kumobilise umma tayari kwa 2010.

wakati CCM wakiparurana huko, hapa tulitegemea alternatives kama Chadema muwe mitaani mkiwaeleza watu kinagaubaga ni nini kinaendelea nchi hii na incompetence ya huu utawala uliopo. Maana si wananchi wengi wenye access ya habari/taarifa kama ilivyo hapa JF.


Lakini, ndio kwanza Maalim yupo Ikulu anaweka mambo yake sawa na mh Karume, huku mkuu kama wewe tunayekutegemea bungeni nasikia upo Jordan kwenye mkutano, sijasikia viongozi wengine wa Chadema wanasemaje kwenye hili!

Mi nilidhani hii ni a golden window of opportunity kwa upinzani Tanzania kuonyesha makali yake!

Nakupa five mkuu kwa ushauri wako uliotulia. Tatizo la wapizani hawana strategy, siasa ni mbinu.
 
all this its just a mind game of this stupid politicians with their politics... belive me nothing will change... zaidi tu ya maudhi zaidi... huwezi kuniambia kuwa CUF walikuwa hawamtambui karume wakati walikuwa ni sehem ya serikali yake... kama walikuwa na wawakilishi barazani(bungeni kwao) coz kama walikuwa hawaudhurii wangeshavulia coz sheria ilikuwa inawataka waapishwe na kuhudhuria.. na walikuwa wanahudhuria vikao.. utasemaje humtambui mtu ambaye unatumikia serikali yake.... thats bullshit... bado watanzania wanaamini kuwa kuna UPINZANI wa kweli hapa... poor tz....

sasa new chapter has been revealed mtaona maaupuuzi mengine yanayokuja..sijui mtamlilia nani.. na subirini ya chadema ndio mtajua kuwa.. we dont have truly politicians.. we have morons and monsters...

DAMN YOU CCM...CUF, CHADEMA and whomever is associated with these fuckin tramps

******************************
 
...Maalim Seif Hamad Sharif hafanyi makosa kila anapolenga jambo ana kusudi fulani,Hebu someni historia yake kwanza!!Hafanyi makosa huyu mtu jamani ana malengo yake tena ya muda mrefu sana....
MKUU WALA USENDE MBALI HAYA HAPA MAKUSUDIO YA WAZANZIBAR KUUTAFUTA UMOJA KWA GHARAMA YOYOTE...NA KWA TAARIFA YAKO TU HIVI NINAVYOZUNGUMZA MAALIM SEIF....IS PRICELESS DIAMOND IF HE IS NOT A GOLD...ANALINDWA KAMA RAIS VILE...



What are Karume and Seif up to in Zanzibar?
By Ray Naluyaga and Salma Said, Zanzibar

Leaders from across the political divide in Zanzibar have joined forces to counter what they see as Tanzania Mainland's undue influence in the isles, sources within the ruling CCM and opposition CUF told The Citizen yesterday.

The newfound camaraderie between President Amani Abeid Karume of CCM and his longtime political rival, Mr Seif Shariff Hamad of CUF, is said to be the outcome of behind-the-scenes efforts to chart a more independent future for Zanzibar.

More clues emerged yesterday when Mr Hamad addressed a rally in Pemba, where he defended CUF�s decision to recognise President Karume and work with his government to lay the ground for what his close associates described as "the rebirth of Zanzibar".

The reception accorded to Mr Hamad at Masota Village in Pemba, which is a CUF stronghold, contrasted sharply with the reaction of a boisterous crowd that jeered and heckled CUF officials when Mr Hamad announced at a public rally in Unguja on Saturday that the party had decided to recognise Mr Karume as the President of Zanzibar.

Mr Hamad and other top officials, including CUF national chairman Ibrahim Lipumba, were forced to cut short their speeches and leave the Kibanda Maiti grounds under tight security.

Mr Hamad told an attentive crowd in Pemba yesterday that Zanzibaris should trust him and President Karume and expect "better things" from the Union.

He vowed never to turn back despite Saturday�s debacle in Unguja.

In a hint that corroborated what sources told The Citizen, the CUF secretary-general said Zanzibaris would no longer depend on the Mainland to decide their political destiny and for their development.

He said past efforts to find a lasting solution to problems bedevilling the isles failed mainly because they were advanced by "outsiders"and other people "who were either not very keen or who simply ignored the realities on the ground while championing their own interests".

Zanzibari leaders had realised their mistakes and were now ready to find homegrown solution and secure the isles� future, he added.

Mr Hamad said former President Benjamin Mkapa and his successor, President Jakaya Kikwete, had both failed to live up to their promises to break the longstanding political stalemate in Zanzibar.

"We took time to ponder with Karume where we were heading. We came to the conclusion that we had fought one another for far too long.

We decided that nothing would come out of sabotaging one another, and that we need to work together to save our people from the suffering they have gone through all these years."

Sources told The Citizen that the general mood among Zanzibaris had changed since Mr Karume met Mr Hamad in Zanzibar last Thursday, and that the new partnership should be reflected by debates in the House of Representatives, where CCM and CUF have in recent months taken common stands on a number of issues.

Representatives from CCM and CUF have been unanimous that Zanzibar should not share oil revenues with the Mainland should the resource be discovered in the isles.

The Zanzibar legislature also recently decided that the Zanzibari national anthem, and not the Union one, should be played before sessions commence.

CCM and CUF representatives earlier this year assailed Prime Minister Mizengo Pinda when he told Parliament in Dodoma that Zanzibar could not be an independent and sovereign country outside the Union.

It is, however, still not clear what positions the two parties will take ahead of and during next year's Zanzibari presidential election.

President Karume is currently serving his second and final term, and a number of influential CCM members in Zanzibar are already lining up to succeed him. Mr Hamad unsuccessfully vied for the Zanzibar presidency in 1995, 2000 and 2005.

Yesterday, CUF director of foreign affairs and international cooperation Ismail Jussa told The Citizen from Pemba that Zanzibaris stood to benefit from the "painful" reconciliation between President Karume and Mr Hamad.

"Labour is painful to a woman, but in the end, when a new baby is born, everybody is happy. What we have done and are doing will have a happy ending," he said.

Mr Jussa attributed Saturday's near-riot during the rally in Zanzibar to people not being ready to receive such "earth-shaking" news.

"People were not prepared psychologically to receive the news. It�s not that they don't trust Maalim Seif. They trust him, and know that he has never and can never betray them."

Mr Jussa said CUF�s stance not to recognise Mr Karume as the President of Zanzibar was more theoretical than practical because CUF members in the House of Representatives were posing questions to ministers appointed by Mr Karume.

He said the cooperation would transform Zanzibar into the "Dubai of Africa" within a short time.

Respected CUF elder Chema Simai, 72, said the party had done the right thing by recognising Mr Karume, adding that it was the style of delivering the news to CUF supporters that was wrong, sparking Saturday's chaos.

SOURCE:THE CITIZEN NEWSPAPER
MSISITIZO NI WANGU
 
Pemba Day One: Wananchi Wajitokeza kwa Wingi.
Wakazi wa Pemba na vitongoji vyake, vyake, leo wamejitokeza kwa mamia, katika zoezi la kuboresha Daftari la Kudumu la Kupiga Kura, linaloendelea katika maeneo kadhaa kisiwani Pemba, ikiwa ni siku mbili tuu zimepita tangu Katibu Mkuu wa CUF kutangaza kumtambua Karume kama rais halali wa Zanzibar.

Ofisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar aliyeko Pemba, ameeleza tangu kufunguliwa kwa vituo vya uandikishaji asubuhi ya leo, wananchi wamejitokeza makumi kwa mamia kujiandikisha wakiwa na vitambulisho vyao vya ukaazi wa Zanzibar ili kujiandikisha.

Ofisa huyo amesema leo tangu asubuhi, makundi takriban 6 ya wakazi wa baadhi ya maeneo ambayo uboreshaji ulishamaliziki, walifika ofisi za ZEK zilizoko Chake Chake Pemba, na kuomba kujiandikisha vituo ambavyo siyo vyao, ama kuwaomba maofisa wa ZEK warejee katika vituo walivyoshamaliza ili wawaandikishe na wao.

Ofisa wa ZEK aliwakatalia kata kata kuandikishwa vituo ambavyo sio vyao, halikadhalika, ZEK imesisitiza hakuna kurudi nyuma kwa maeneo ambayo uboreshaji ulishamalizika, ZEK inasonga mbele kwa mbele kukamilisha ratiba ya vituo vilivyobakia.

Pemba Day Two
 
Ahsante Mkuu...lakini hapo juu tume ya uchaguzi ni ZEC,kwa kuweka kumbukumbu sawa
 
Kesho uboreshaji unaendelea katika Jimbo ya Wawi atokalo Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, nitatembelea kupata fursa ya kushuhudia ongezeka hili, sambamba na kutembelea ofisi za Vitambulisho vya Ukaazi kupima short time effects za utambuzi wa Karume ulofanywa na Maalim Seif. Pia nitatafuta muda wa kujichanganya na wananchi mitaani kupima wamemkubalia Seif kwa moyo mmoja, ama wanajitokeza kwa wingi tayari kumvote out, maana Wapemba kwa Misimamo, ni kama wakazi wa Tarime.
Heeee heeee heeh! Sidhani kama wana nia ya kumvote out! Hali hii inaonyesha kuanza kuamini kuwa hapakuwepo na mpango wa kuwaibia kura zao, kama ilivyokuwa ikitangazwa na wanasiasa wao.
 
Picha ya wiki

i138_KarumeSeif1023x682.jpg
 
  • Asema nia ni kufungua milango ya makubwa
  • Profesa Lipumba amtetea hajaisaliti CUF
  • Chiligati amkaribisha kwa mazungumzo
Seif_Sharrif-150x150.jpg

Katibu Mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.

Licha ya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kumpa kibano Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, kutokana na tamko lake la kumtambua rasmi Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kiongozi huyo amesisitiza msimamo wake wa kumtambua Rais Karume.

Maalim Seif alisisitiza msimamo huo jana mbele ya wananchi na wafuasi wa chama chake kwenye ngome kuu ya chama hicho Kisiwani Pemba, wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Masota mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alisema historia ya vyama vya siasa Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi imekuwa yenye mivutano ambayo haisaidii maendeleo ya Wazanzibari.

“Kumtambua Karume tutafungua milango ya makubwa zaidi… natoa kauli hapa (Pemba) kuwa namtambua Karume na tushirikiane naye,” alisema na kuongeza kuwa amepata silaha na baraka zote kwa Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho kuhusiana na uamuzi wa kumtambua Rais Karume.

Alisema kuwa watu wasioitakia mema Zanzibar wamekuwa wakichonganisha kuona siku zote haitulii huku wananchi wakirudi nyuma kimaendeleo, hivyo ni lazima Wazanzibari watambue kuwa suala la umoja na mshikamano ni muhimu kwao.

Maalim Seif alifafanua kuwa mazungumzo yake na Rais Karume wiki iliyopita yalilenga katika kuimarisha umoja miongoni mwa wananchi na kuiacha Zanzibar ikiwa nchi iliyotulia kwa faida ya kizazi hiki na kijacho kuondoka katika mifarakano.

Naye Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, aliwatoa hofu wanachama kwamba katibu mkuu wao amewasaliti na ni vyema wakamuamini kwani ana nia njema ya kuleta umoja na mshikamano wa Wazanzibar kwa kushirikiana na Rais Karume.

Hata hivyo, wanachama wa Pemba walitulia na kumsikiliza kwa makini wakati wote wa mkutano huo, tofauti na Unguja juzi, ambapo mkutano huo ulivunjika kutokana na wanachama kupinga tamko la Maalim Seif.

Wakati Seif akisisitiza msimamo wake, CUF kimetoa tamko kuwa msimamo wa Seif unabakia pale pale kwa madhumuni ya kulinda umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Zanzibar. Tamko hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasilaino ya Umma, Salum Bimani, kufuatia wanachama wa CUF kutaka kumpiga Seif baada ya kutangaza kumtambua Rais Karume juzi mjini Zanzibar.

Bimani alisema baada ya vurugu za juzi viongozi wa CUF walikutana usiku kutathmini hali iliyojitokeza na kuamua kuwa msimamo wa kumtambua Rais Karume uendelee kubakia kama ulivyo kwa maslahi ya nchi.

“Uamuzi wa kumtambuwa Rais Karume unaendelea kubakia pale pale na vurugu zilizojitokeza ni joto la kisiasa lililotokana na jazba,” alisema.

Hata hivyo, alisema kitendo hicho ni changamoto kubwa kwa viongozi wa Serikali kwa vile wananchi wanaonyesha hivi sasa wamechoshwa na matatizo ya kisiasa ya Zanzibar na kufikia kushindwa kuwasikiliza viongozi wao.

“Mwenye macho haambiwi tazama kitendo hiki kinatupa changamoto viongozi wa vyama na Serikali kuona kwamba wananchi wameshachoka na matatizo ya kisiasa ya Zanzibar,” alisema Bimani.

Alisema mazungumzo ya Rais Karume na Seif yanaonyesha njia nzuri ya kupita kuelekea uchaguzi mkuu, ingawa alisema wananchi wanataka mafanikio hayo yawe ya utekelezaji wa vitendo.

Kwa upande wake, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema imesikitishwa na kitendo cha wafuasi wa CUF kutaka kumpiga Maalim Seif kutokana na uamuzi wa kumtambua Rais Karume.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, alisema kitendo hicho kinakwenda kinyume cha misingi ya demokrasia na utawala bora.

Alisema SMZ imepokea kwa faraja kubwa uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF kutangaza kumtambua Rais Karume.

Alisema suala hilo lilikuwa likiwasumbua kwa muda mrefu na kutumia gharama kubwa katika masuala ya ulinzi na usalama, lakini sasa gharama hizo zitatumika katika kupambana na maadui wa nje na sio wa ndani.

“Serikali kwa upande wake tumepokea kwa furaha kubwa uamuzi wa Maalim Seif wa kutangaza kumtambua Rais Karume, kwa maslahi ya nchi yetu,” alisema. Hata hivyo, alisema kwamba katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu ni vyema wananchi wakapokea na kuyaheshimu maamuzi yaliyofikiwa na viongozi hao katika suala la kulinda umoja na mshikamano.

Jijini Dar es Salaam, CCM kimempongeza Maalim Seif, kwa kumtambua Rais Karume, lakini kimesema amechelewa kutoa tamko hilo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, John Chiligati, alisema kauli ya Maalim Seif italeta maelewano na kuondoa chuki na uhasama.

Alisema sasa ni wakati mzuri kwa chama hicho kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili kumalizia ngwe iliyokuwa imebaki katika mazungumzo ya mwafaka.

Alisema mazungumzo ya mwafaka yalikuwa yanakwenda vizuri na yalikuwa yakikaribia mwishoni ndipo CUF waliposusia.

“Sasa tumefungua ukusara mpya maana uhasama na chuki siku zote vinamalizwa kwa watu kukaa na kuzungumza, sasa baada ya kauli ya Seif tunatarajia watakuja tukae na kuzungumza nao,” alisema.

Wakati huo huo, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Zanzibar wamelaani kitendo cha baadhi ya wafuasi wa CUF kumfanyia fujo Maalim Seif kwa maelezo kuwa kitendo hicho kinakwenda kinyume cha misingi ya demokrasia na hakisaidii kumaliza tofauti za kisiasa.

Katibu Mkuu wa Tadea, Juma Ali Khatib, alisema wamepokea kwa mshutuko tukio hilo kwa vile wanachama wa CUF walipaswa kumkosoa kiongozi wao kupitia vikao vya faragha na sio hadharani.

“Kitendo cha Rais Karume na Hamad kukutana kumaliza matatizo ya Zanzibar ni jambo la kuungwa mkono kwa vile hakuna mtu anayetaka watu wapigane,” alisema. Khatib.

Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa CUF kutaka kumpiga kiongozi wao hakikuwa cha kiungwana kwa vile uamuzi wa kumtambua Rais Karume kinafaida kubwa katika kuimarisha misingi ya demokrasia na kuondoa tofauti za kisiasa.

Hata hivyo, alisema kwamba msimamo wa CUF kutomtambua Karume ulikuwa sawa na utani wa kisiasa kwa vile tayari katiba ya Zanzibar ilikuwa inamtambua baada ya kumalizika uchaguzi mkuu na ndio maana wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CUF wamekuwa wakishirikiana na Serikali kwa muda wote.

Alisema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walikubali kula kiapo cha kuitii Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati kiongozi mkuu wake ni Rais Amani Abeid Karume na kulipwa posho na mishahara na serikali. Hata hivyo, alisema tukio hilo ni fundisho kubwa kwa viongozi wa kisiasa kwa kuzingatia propaganda zenye ukweli badala ya kuahidi wanachama mafanikio ya kisiasa yasiyokuwa na ukweli.

“Sisi kama CCM tupo tayari kuendelea na mazungumzo ya mwafaka na ni vyema wakaunga mkono uamuzi wa viongozi wao badala ya kuendeleza ubishi wa jogoo sio kuku,” alisema Vuai.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Hamad Mussa Yussuf, alisema kitendo cha wanachama wa CUF kupinga uamuzi wa viongozi wao hadharani kinaonyesha wameshakata tamaa na maneno ya mwafaka.

Alisema wananchi wa Zanzibar hivi sasa wanahitaji kuona utekelezaji wa vitendo katika ushughulikiaji wa mpasuko wa kisiasa na sio propaganda za kisiasa.

“Viongozi wa CUF lazima wasome alama za nyakati, wananchi wamechoka na suala la mwafaka kugeuzwa propaganda za kisiasa,” alisema na kuongeza: “Maalim Seif lazima awe makini asije ingizwa katika mtego wa panya na paka katika mazungumzo yake na Rais Karume.” Alisema kitendo cha wanachama kutaka kumpiga Maalim Seif kinaonyesha viongozi wa CUF walikurupuka katika uamuzi huo kwa vile walitakiwa wafahamu msimamo wa wanachama katika suala hilo kabla ya kutangaza kumtambua Rais Karume.

Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Sau, Peter Magwila, alisema uamuzi wa CUF wa kumtambua Rais Karume umechelewa kwa vile hivi sasa kila chama kipo katika harakati za kujitayarisha na uchaguzi mkuu wa mwakani.

Alisema CUF walitakiwa kumtambua Rais Karume mapema ili wapate nafasi ya kutatua matatizo ya kisiasa na sheria mbaya zinazokandamiza ustawi wa demokrasia nchini na kutolea mfano sheria zinazotumika katika uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Juzi baada ya kuvunjika kwa mkutano wa CUF wafuasi wa CUF waliandamana kuelekea nyumbani kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, lakini walishindwa kufika katika eneo la nyumba yake baada ya kukuta ulinzi mkali wa askari FFU ulioimarishwa katika eneo hilo.

Imeandikwa na Juma Mohamed, Pemba; Mwinyi Sadallah, Zanzibar na Joseph Mwendapole Dar.


CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom